Mtoto wa miaka miwili, mvuta sigara mdogo zaidi duniani

Wednesday, January 20, 2010 / Posted by ishak /


SOTE tunafahamu kwamba mvulana mwenye umri wa miaka miwili ni dhahiri atakuwa bado anakunywa maziwa au ameanza kula vyakula vya watu wazima. Lakini, mvulana mmoja wa Kichina ameanza kuvuta sigara wakati akiwa na umri wa miezi 18...Mtoto huyo huvuta paketi moja ya sigara kila siku na hushikwa na hamaki iwapo hapewi kiburudisho chake hicho.

Mtoto huyo, Tong Liangliang, alifundishwa jinsi ya kuwasha sigara na baba yake ambaye aliamini kwamba uvutaji ungempunguzia maumivu ya ugonjwa wa ngiri (hernia).

‘Baba-mtu hakujua jinsi tabia hiyo ingekolea kwa kitoto chake hicho hadi pale alipong’amua kwamba idadi ya sigara kilichokuwa kinavuta kila siku ilikuwa imeongezeka,” kilitangaza kituo cha China Radio International.

Tong alianza kuvuta sigara yake ya kwanza akiwa na umri wa miezi 18 katika jitihada za kupunguza maumivu ya ngiri yaliyokuwa yanamsumbua. Hili lilifanyika kwa kutambua kwamba mtoto huyo alikuwa ni mdogo mno kiasi cha kutoweza kufanyiwa opasuaji.

Hata hivyo, hii ni “rekodi ya dunia isiyokuwa rasmi” kwa vile kuingizwa kwake katika Kitabu cha Rekodi za Guiness (Guinness Book of Records) kama mvutaji mdogo zaidi wa sigara duniani, kutakataliwa kwa madai kwamba kitendo hicho kilichochea tabia yenye madhara kwa watoto.

source globalpublisher

0 comments:

Post a Comment