Wachina ni NOMA kwa Kukopi - Wavumbua Goojle Badala ya Google

Friday, January 29, 2010 / Posted by ishak /


Wachina wamedhihirisha kwa mara nyingine kuwa wao ni wakali wa kukopi kwa kuikopi tovuti ya google na kutoa tovuti yao inayoitwa Goojle na pia kwa kuikopi YouTube na kutoa YouTubecn.
Wachina katika kuendeleza mpambano na tovuti za kampuni ya Google ya Marekani wameziigiza tovuti za Google na YouTube.com na kutoa tovuti zao za Goojle na YouTubecn.com.

Hivi karibuni Google walitishia kusimamisha shughuli zao nchini China kutokana na mashambulizi toka kwa hackers wa nchini China.

Katika kuendeleza vita hivyo, Wachina wametoa tovuti ya Goojle ambayo imetengenezwa kwa kuigiza kila kitu kutoka kwenye Google. Kuanzia rangi mpaka mpangilio wa ukurasa wa Google.

Herufi "jle" katika Goojle zinamaanisha dada kwa lugha ya taifa ya China, Mandarin wakati herufi "gle" katika Google zinamaanisha kaka katika lugha ya Kichina.

Tovuti ya Goojle imeambatanisha meseji ambayo inasema "Dada alikuwa na furaha sana baada ya kaka kuutupilia mbali uamuzi wake wa kuondoka na kuamua kukaa na dada yake". Meseji hiyo ilikuwa ni kijembe kwa Google ambao wanatishia kusimamisha shughuli zao nchini China.

Nayo YouTube ya Kichina YouTubecn.com video zake zote zinatoka kwenye YouTube original inayomilikiwa na Google ambayo imepigwa marufuku nchini China.

Tovuti hizo mbili ziliwekwa online kuanzia katikati ya mwezi huu punde baada ya google kutishia kusimamisha shughuli zake nchini China.

Kampuni ya Google yenye makazi yake mjini California ilifungua matawi yake nchini China mwaka 2006 na ilisema kuwa itaendelea kuwepo nchini China iwapo serikali ya China itasaidia kukomesha mashambulizi ya hackers wa China.

Wachina ni maarufu kwa kutoa bidhaa feki kuanzia kwenye magari mpaka kwenye madawa. Tovuti ya Goojle ni kithibitisho kuwa Wachina wanatisha kwa kutoa vitu vya kukopi.


source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment