Mbunge ataka jina la fataki lisitumike, atoa ombi bunge

Wednesday, February 10, 2010 / Posted by ishak /

MBUNGE wa Jimbo la Sumbawanga Mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Kimiti ameiomba Serikali kulifuta jina la fataki linalotumika kwa jamii kwa kuwa jina hilo ni jina la babu yake na kudai anadhalilishwa.
Mbunge huyo aliwasilisha ombi hilo jana wakati akiuliza swali bungeni katika kipindi cha maswali na majibu bungeni Dodoma.

Mbunge huyo aliiomba wizara husika kufanya utaratibu wa kufuta jina hilo na kutafuta jina mbadala la Fataki kwakuwa linalotumika vibaya hivi sasa na ni jina la babu yake.

" Naomba wahusika muangalie uwezekano wa kutumia jina lingine kwani hilo la Fataki ni la babu yangu na roho inauma sana ninaposikia linatumika sasa,"alisema mbunge huyo bungeni akiwasilisha hoja hiyo kwa masikitiko.

Baada ya kuwasilisha ombi lake hilo baadhi ya wabunge waliangua vicheko cha nguvu huku ukumbi wote wa bunge ukizizima kwa vicheko, huku Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bi. Mwantumu Mahiza akiahidi kulishughulikia suala hilo baada ya kumalizika kwa vikao vya bunge.

Jina hili la fataki linatumika hivi sasa kwenye matangazo kuwaelimisha wanafunzi na jamii kwa ujumla kuachana na kutodanganywa na wanaume watu wazima wanaowadanganya wanafunzi na mabinti wadogo kwa kuwahonga vitu vya thamani na hata fedha ili wawarubuni.

Jina hili limejipatia umaarufu mkubwa kuelimsha jamii ya kitanzania hasa katyika kumaliza janga zima la gonjwa hatari la ukimwi.


source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment