Nyota wa Muziki wa Pop wa Ujerumani Awaambukiza Ukimwi Wanaume Watatu

Saturday, February 13, 2010 / Posted by ishak /


Mahakama ya nchini Ujerumani imemuona nyota maarufu wa muziki wa Pop, Nadja Benaissa wa kundi la waimbaji wanawake la 'No Angels' ana hatia ya kuwaambukiza ukimwi wanaume watatu aliofanya nao mapenzi bila kinga huku akijijua kuwa yeye ni muathirika.
Waendesha mashtaka wa Ujerumani jana ijumaa walimuona msanii maarufu wa kundi la "No Angles" Nadja Benaissa mwenye umri wa miaka 27 ana hatia ya kuwaambukiza ukimwi wanaume watatu aliofanya nao mapenzi bila kinga.

Nadja anadaiwa kufanya mapenzi na wanaume hao kati ya mwaka 2000 na 2004 bila kuwataarifu kuwa yeye ni muathirika.

Nadja alikuwa akijitambua fika kuwa yeye ni muathirika tangia mwaka 1999, nyaraka za mahakama zilisema.

"Alikuwa akijua wazi kuwa kwa kufanya mapenzi bila kinga atawaambukiza maradhi yake wanaume hao", alisema mwendesha mashtaka katika mji wa Darmstadt ulio jirani na Frankfurt.

Mmoja wa wanaume hao watatu ameishathibitishwa kuwa ameambukizwa virusi vya HIV vinavyosababisha ukimwi.

Kundi la No Angeles liliibuliwa na mashindano ya vipaji kwenye luninga mwaka 2000 na baada ya kujipatia umaarufu mkubwa walifanya ziara nyingi sana barani ulaya kabla ya kundi hilo kuvunjika mwaka 2003.


source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment