http://www.nifahamishe.com/NewsImages/4193402.jpg

Monday, March 08, 2010 / Posted by ishak /


Mtoto aliyezaliwa kabla ya muda wake ambaye alikuwa mwepesi sana kiasi cha kwamba kopo dogo la cocacola lilikuwa zito kulinganisha na uzito wake, amemaliza minane akiwa hai pamoja na hofu ya madaktari kuwa asingeweza kuishi siku nyingi.
Mtoto huyo alizaliwa nchini Ujerumani akiwa na umbile dogo sana na uzito wa gramu 275 tu kiasi cha kwamba aliingia kwenye rekodi za kuwa mtoto wa kiume aliyezaliwa akiwa na uzito mdogo kuliko wote.

Kwa jinsi alivyokuwa na umbile dogo karatasi ya daftari yenye ukubwa wa A4 iliweza kumfunika kuanzia kichwani hadi miguuni.

Uzito wake ulikuwa ni robo tatu ya uzito wa kopo la Cocacola ambalo huwa na uzito wa gramu 350.

Awali madaktari walisema kuwa ni vigumu sana kwa mtoto anayezaliwa akiwa na uzito chini ya gramu 350 kuishi muda mrefu.

Lakini mtoto huyu amefanikiwa kumaliza miezi kadhaa akiwa hai kutokana na matunzo ya kitaalamu aliyokuwa akipewa.

Habari za kuzaliwa kwa mtoto huyo hazikutangazwa kutokana na hali mbaya ya kiafya aliyokuwa nayo wakati alipozaliwa.

Madaktari wameamua kutoa taarifa za kuzaliwa kwa mtoto huyo baada ya kuthibisha sasa kuwa afya yake imekuwa njema na maisha yake hayako hatarini tena.

Mtoto huyo alizaliwa mwezi juni mwaka jana wakati mimba ya mama yake ilipokuwa imetimiza wiki 25.

Alitumia miezi sita akipewa huduma maalumu hospitalini kabla ya wazazi wake kuruhusiwa kuondoka naye mwezi disemba mwaka jana wakati uzito wake ulipoongezeka na kufikia kilo 3.7.

Taarifa ilisema kuwa madaktari wa Ujerumani walizipitia rekodi za watoto wa kiume waliozaliwa kabla ya muda wao katika nchi mbali mbali duniani lakini hakupatikana mtoto hata mmoja aliyezaliwa akiwa na uzito mdogo kama wa mtoto huyo.

source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment