Kahaba Aenda Mahakamani Kupinga Kufukuzwa Kazi

Monday, March 15, 2010 / Posted by ishak /


Ingawa ni kinyume cha sheria kufanya ukahaba, Kahaba mmoja nchini Afrika Kusini ameenda mahakamani kupinga kusimamishwa kazi isivyo halali kwenye danguro moja lililopo mjini Cape Town.
Kahaba huyo anayejulikana kwa jina la Kylie alisimamishwa kazi kutokana na tabia yake ya kuchagua wateja na kutumia muda mwingi na mpenzi wake ambaye alikuwa hataki kulipa kwa huduma ya ngono anayopewa.

Jaji wa kesi alishikwa na butwaa akisema kuwa haamini inakuwaje mtu anayefanya kazi haramu akaenda mahakamani kuitetea kazi haramu anayofanya.

Hata hivyo wanasheria wa Kylie wanasema kuwa kesi ya Kylie si kuhusiana na kufanya kwake ukhaba ambao ni kinyume cha sheria bali ni kufukuzwa kwake kazi isivyo halali.

Mahakama kadhaa za nchini Afrika Kusini zimekataa kuisikiliza kesi hiyo zikisema kuwa kufanya ukahaba ni kinyume cha sheria, vimeripoti vyombo vya habari vya Afrika Kusini.

Majaji watatu wa mahakama ya kazi wanakuna vichwa vyao kujua kama waisikilize kesi hiyo au la.

"Wakati unaposimamishwa kufanya kitu haramu.. haiingii akilini kusimama na kupigania watu wakurudishe kufanya kazi ya haramu", alisema rais wa majaji, Raymond Zondo.

Kylie amekuwa akipigania kurudishwa kwenye kazi yake haramu kwa miaka saba sasa tangia aliposimamishwa kazi mwaka 2003

source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment