Mtu wa Kwanza Duniani Ambaye Hana Jinsia

Thursday, March 18, 2010 / Posted by ishak /


Mlowezi wa kiingereza nchini Australia ameingia kwenye rekodi za dunia kwa kuwa mtu wa kwanza kutambulika kisheria kuwa hana jinsia yoyote si ya kiume wala ya kike.
Norrie May-Welby mwenye umri wa miaka 48, Muingereza anayeishi nchini Australia amekuwa mtu wa kwanza duniani kutambulika kisheria kuwa hana jinsia yoyote.

Madaktari nchini Australia walishindwa kumuweka Norrie kwenye fungu la wanawake au wanaume kutokana na hali yake ya kutokuwa na viungo vyovyote vya siri.

Norrie alizawaliwa kama mwanaume lakini alifanya operesheni ya kubadilisha jinsia yake kuwa mwanamke mwaka 1990 wakati huo akiwa na umri wa miaka 28.

Lakini baada ya kutokuwa na furaha katika hali yake mpya ya uanamke, Norrie aliamua kufanya operesheni nyingine na kuondoa uke alioupandikiza ili asiwe na jinsia yoyote.

Katika pasipoti yake mpya kama raia wa Australia, ilibidi maafisa wa serikali waongeze fungu jingine la watu wasio na jinsia baada ya madaktari kusema kuwa wanashindwa kuthibitisha Norrie ni jinsia gani.

"Mimi si mwanaume wala mwanamke, mimi nimeona bora nisiwe na jinsia yoyote", alisema Norrie.

Kutokana na uamuzi huo wa maafisa wa Australia, Norrie amekuwa mtu wa kwanza duniani kutambulika kisheria kuwa hana jinsia yoyote.

source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment