Mwanamieleka wa Sumo Ainyofoa ATM na Kukimbia Nayo

Sunday, March 07, 2010 / Posted by ishak /


Mwanamieleka wa Sumo wa nchini Urusi ametiwa mbaroni baada ya kuinyofoa mashine ya kutolea fedha toka kwenye ukuta wa duka moja nchini humo na kisha kuibeba mabegani na kukimbia nayo.
Mwanamieleka wa mchezo wa Sumo wa nchini Urusi ametiwa mbaroni baada ya kuing'oa mashine ya kutolea fedha toka kwenye ukuta wa duka moja mjini Moscow na kisha kuanza kukimbia nayo.

Polisi wa nchini Urusi walisema kuwa mwanamieleka huyo baada ya kuing'oa mashine hiyo yenye uzito wa kilo 90, aliiweka mabegani na kuanza kukimbia nayo.

Polisi waliendelea kusema kuwa mwanamieleka huyo alifika kwenye eneo la tukio akiwa na wenzake wawili na kuing'oa mashine hiyo iliyokuwa na kiasi cha pesa za kirusi roubles 25,000 sawa na Tsh. Milioni 1.2.

Mfanyakazi wa duka hilo aliyeshuhudia tukio hilo alipiga simu kuwaita polisi ambao waliwahi kufika na kuwakamata washirika wawili wa mwanamieleka huyo.

Mwanamieleka huyo alikamatwa na kushikiliwa na polisi baada ya kukiri kosa lake

source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment