Vidume wazichapa ndani ya daladala

Monday, March 15, 2010 / Posted by ishak /

WANAUME wawili wamejikuta wakipeana dozi ya ngumi baada ya kukerwa na adha ya usafiri iliyofanya mmoja ashikwe na hasira baada ya mmoja kumuumiza mke wake.
Wanaume hao wamejikuta wakirushiana maneno na mmoja wao kushikwa na hasira kali na kujikuta akimrushia ngumi mwenzake baada ya kukerwa na kuumizwa kwa mke wake ndani ya dalalada hiyo.

Hali hiyo ilitokea mwishoni mwa wiki, maeneo ya Kariakoo katika mabasi yaendayo Mbezi.

Mtafaruku huo ulitokea baada ya mume wa dada huyo kuingia ndani ya daladala na kuwahi siti mbili ili nyingine aje kukalia mke wake ambaye hakuweza pulukushani ya kuingia mlangoni kuwahi siti.

Hivyo katika hali ya kawaida jijini Dares Salaam utaratibu huo wa kuwekeana siti ndani ya daladala huwa watu wengi watumiao usafiri huo huwa hawaukubali kutokana na shida ya usafiri na hasa nyakati zajioni kila mmoja huwa amechoka na kutaka kukalia siti.

Kwa kuwa dada huyo alichelewa kuingia ndani ya basi hilo na watu wengine waliona siti hiyo imewekwa handbag kumaanisha kuwa kuna mtu amewahi ilihali yuko chini baba mmoja alimtaka atoe handabag hiyo akalie hiyo siti.

Mume wa dada huyo alianza kumwambia kuwa alimuweke mkewe ambaye yuko chini atakuja kukalia, kutokana na jibu hilo mtu aliyetaka kukalia siti hiyo hakumuelewa na kumuona mpuuzi na kutoa handbag hiyo na kukalia siti hiyo.

Alianza kumwambia atoke na mke wake akalie siti hiyo mtu huyo aliendaelea kumuona mpuuzi na mume wa dada huyo kumuamrisha mke wake amkalie baba huyo hivyohivyo kwa kuwa alikuwa mbishi.

Kabla dada huyo hajafanya kama mumew ake alivyomwambia baba huyo aliyekalia hiyo siti alimsukumiza dada huyo na kuanguka upande mwingine.

Hivyo kutokana na hali hiyo mtafarufku ndipo ulipoianzia hapo na kuanza kutupiana maneno hali iliyofanya kuzuke kwa zaogo ndani ya basi hilo bila sababu za msingi.

BAadhi ya abiia walionekana kumsaidida mume wa dada huyo na baadhi walimsaidia aliyekalia siti hiyo na kumtetea kuwa utaratibu wa kuwekeana siti kikawaida hautumiki unatumika kwa mabasi yanedayo mikoani.

Kwa kuwa mtu aliyekalia siti hiyo aliendelea na msimamo wake wa kutotoka mume wa dada huyo alishikwa na jazba na kuanza kumpiga ngumi na Yule hakukubali na kuanza kuzichapa.

Hali hiyo ilitulia baada ya dereva kuamrisha kuwa akifika Magomeni ataingiza gari polisi awaache watu hao kwa kuleta adha ndani ya daladala.

Matukio hayo hutokea mara kwa mara katika mabasi ya usafiri wa daladala, na kadri siku zinavyozidi kusogea usafiri huo wa daladada unazidi kuwa washida na mgumu mno kwa kusemekana kila siku idadi ya watu wengi kuingia jijini Dar es Salaam wakitokea mikoani na kufanya usafiri huo kuzidi kuwa mgumu katika njia zote jijini.


source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment