George Bush Ajiunga na Facebook

Friday, June 04, 2010 / Posted by ishak /


Rais wa zamani wa Marekani, George Bush amejiunga na mtandao wa Facebook na kufanikiwa kuwavuta wanachama 65,000 katika muda mfupi, hata hivyo baadhi ya wanachama wake wanalalamika kuwa Bush anayafuta maoni yao wanapomkosoa.
Mtandao wa FACEBOOK umepata mwanachama mwingine ambaye ni rais wa zamani wa Marekani, George W Bush.

Bush alijiunga na mtandao wa Facebook jana na alifanikiwa kupata wanachama zaidi ya 2,000 ndani ya masaa machache. Hadi sasa jumla ya watu 65,000 wamejiunga na ukurasa wa Bush.

Ujumbe wa kwanza katika ukurasa wa Bush uliezea kazi alizofanya Bush tangu alipoondoka madarakani januari 2009.

"Rais Bush ameendelea kuchapa kazi, ametembelea majimbo 20, nchi 8 na ametoa jumla ya hotuba 65 na ameshiriki kikamilifu katika miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo mfuko wa kusaidia Haiti ambao aliuanzisha kwa kushirikiana na rais mstaafu Bill Clinton".

Meseji nyingi zilizoandikwa na wanachama wa Bush ni za kumsifia sana kwa kipindi chake cha urais.

"Mungu akubariki, ahsante kwa uongozi wako wa taifa hili kubwa, tutakumiss sana". alisema jamaa mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Matt Thullen.

Hata hivyo baadhi ya wanachama wake walilamika kuwa maoni yao ya kumkosoa Bush yalifutwa.

Ukurasa wa Facebook wa Bush unapatikana kwa linki hii:
facebook.com/georgewbush


source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment