Marekani Yagundua Hazina ya Utajiri Afghanistan

Tuesday, June 15, 2010 / Posted by ishak /


Marekani imegundua hazina ya madini yenye thamani kubwa nchini Afghanistan ambayo yanakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya dola trilioni moja.
Msemaji wa Pentagon alisema kuwa utafiti wa wataalamu wa madini wa Marekani umeonyesha kuwa nchini Afghanistan kuna kiasi kikubwa sana cha madini ya thamani tofauti na ilivyokuwa ikijulikana awali.

Thamani ya madini kama vile niobium, lithium, chuma, dhahabu na kobalti ambayo yanapatikana kwa kiasi kikubwa nchini Afghanistan ni zaidi ya dola trilioni moja.

Maafisa wa Marekani waliliambia gazeti la New York Times la Marekani kuwa hazina ya madini yaliyopatikana nchini Afghanistan yanatosha kuubadilisha uchumi wa Afghanistan na kuigeuza Afghanistan kuwa mojawapo ya nchi zinazoongoza kwa uzalishaji wa madini duniani.

Rais wa Afghanistan, Hamid Karzai alisema mwanzoni mwa mwaka huu kuwa kiasi kikubwa cha madini kilichogunduliwa nchini humo kitaifanya Afghanistan itoke kwenye umaskini iwe miongoni mwa nchi tajiri duniani.

0 comments:

Post a Comment