Mashindano ya Maimamu 'Imamu star' Yaanza Malaysia

Saturday, June 26, 2010 / Posted by ishak /


Kuna mashindano mengi yameibuka duniani kutafuta vipaji kama vile Pop Star, Bongo Star Search na mengineyo lakini huko nchini Malaysia yameanza mashindano ya aina yake kutafuta imamu bora.
aada ya mashindano ya Popstar, American Idol, The X Factor na mengineyo kuibuka sehemu mbalimbali duniani, mashindano ya kwanza ya aina yake yameanza nchini Malaysia yakienda kwa jina la "Imam Star".

Mashindano hayo ambayo nchini Malaysia yanajulikana kwa jina la "Imam Muda", yanawashindanisha vijana wa kiislamu ili kumpata imamu bora kati yao.

Vijana wenye umri kati ya miaka 19-27 wamewekwa nyumba moja ambapo kwa kipindi cha miezi mitatu na watakuwa wakishindana kumpata imamu bora kati yao.

Vijana hao watashindana kusoma azana, kusalisha, kutoa khutba, kuosha maiti na kuongoza mazishi.

Maiti zitakazotumika katika mashindano hayo ni maiti zilizopo monchwari ambazo hazijatambuliwa na ndugu zao.

Mshindi wa mashindano hayo hatapewa zawadi ya pesa kama yalivyo mashindano mengine. Atapewa schorlaship ya kusoma mambo ya dini katika chuo kikuu cha al-Madinah University cha nchini Saudi Arabia. Mshindi pia atapewa kazi ya kusalisha misikiti mikubwa ya mjini Kuala Lumpur na pia atakuwa akilipiwa gharama zote za kuhiji Makka.

Mashindano hayo yamekuwa gumzo nchini Malaysia yakivunja rekodi ya watazamaji. Yamebakiza mwezi mmoja kuisha.

source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment