Wabunge kupimwa Saratani

Thursday, June 10, 2010 / Posted by ishak /

NAIBU Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Aisha Kigoda alisema, wanajipanga kuwafanyia vipimo ya saratani wabunge kabla ya kumalizika kwa mkutano huo Julai 16, mwaka huu.


Hatua hiyo imekuja kwa kutaka kuonyesha mfano kwa wananchi wajitokeze kuangalia afaya zao kwa kuwa ugonjwa huo umekuwa ni hatari na kumaliza wananchi walio wengi.

Dk. Kigoda amesema serikali imeandaa mkakati wa kukabiliana na ongezeko la ugonjwa wa saratani nchini kwa kuwa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha kuwa ifikapo 2020, theluthi moja ya vifo vyote vitasababishwa na saratani duniani, na zaidi vifo hivyo vitatokea katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.

Amesema hii inatakiwa iwe mfano kwa kuwa wananchi wengi zaidi ya asilimia 80 wamekuwa wakienda hospitalini wakati saratani imewashawatafuna na inakuwa ngumu kutibika.

Amesema saratani ni ugonjwa unaouwa wananchi walio wengi nchini na inaua kuliko ugonjwa wa ukimwi mbao wengi wameonekana kuuogopa kuliko hata saratani ambayo ni hatari zaidi.

source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment