Keki ya Bethidei Kutimiza Miaka 130

Friday, July 09, 2010 / Posted by ishak /


Bibi Antisa Khvichava wa nchini Georgia ambaye alizaliwa mwaka 1880 alisherehekea siku yake ya kuzaliwa jana kwa kukata keki iliyokuwa na maandishi ya umri wake Miaka 130.
Bibi Antisa Khvichava anayeishi kwenye kijiji cha Sachire magharibi mwa Georgia, alizaliwa julai 8 mwaka 1880 na kwa mujibu wa maafisa wa Georgia, Antisa ndiye mtu ambaye ameishi miaka mingi kuliko watu wote duniani.

Maafisa wa Georgia walimtembelea bibi Antisa Khvichava ambaye alistaafu kazi yake ya kuvuna chai mwaka 1965 wakati huo akiwa na umri wa miaka 85.

Maafisa hao walimwonyesha bibi Antisa nyaraka mbili ambazo alizipoteza, moja ikionyesha tarehe yake ya kuzaliwa kama ilivyoandikwa kwenye cheti chake cha kuzaliwa ambacho amekipoteza.

Bibi Antisa alikata keki aliyoletewa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa na kutimiza miaka 130.

Bibi Antisa ambaye hutembea kwa kutumia mkongoja, ana mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Mikhail mwenye umri wa miaka 70. Mikhail alizaliwa wakati mama yake akiwa na umri wa miaka 60.

Bi Antisa ana wajukuu 10, vitukuu 12 na vilembwe sita.

source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment