Mji wa Luanda Angola Ndio Mji Wenye Maisha Ghali Afrika

Thursday, July 01, 2010 / Posted by ishak /


Mji wa Luanda nchini Angola ndio mji ambao gharama za maisha ni kubwa kuliko miji yote barani Afrika, kwa duniani mji huo unashika nafasi ya tatu baada ya miji ya Tokyo, Japan na Oslo, Norway.
Kwa mujibu wa takwimu za gharama za maisha katika miji mbalimbali duniani kwa mwaka huu wa 2010 zilizotolewa na ECA International, mji wa Luanda nchini Angola unashika nafasi ya tatu duniani kwa gharama za maisha.

Katika takwimu za mwaka jana, mji wa Luanda ndio uliokuwa ukishika nafasi ya kwanza mbele ya miji mingi mikubwa duniani.

Katika takwimu za mwaka huu, mji wa Tokyo Japan unashika nafasi ya kwanza ukifuatiwa na mji wa Oslo, Norway.

Mjini Luanda nchini Angola, chakula cha mchana katika mgahawa wa saizi ya kati, kinagharimu dola 47, kopo moja la bia ni dola 1.62, kilo moja ya mchele ni dola 4.73 na dazani moja ya mayai hugharimu dola 4.75. Ukitaka kwenda sinema na mpenzi wako basi jiandae kutoa dola 13 kwa kichwa kimoja.

ECA imetoa listi ya miji 65 duniani ambayo ndiyo inayoonekana ina gharama kubwa za maisha kwa kuangalia gharama za chakula, nguo, vifaa vya umeme na burudani.

Katika listi ya miji 65 iliyolewa mji wa New York unashika nafasi ya 29 wakati jiji la Dar es Salaam limeshindwa kuingia kwenye orodha hiyo.

Chini ni orodha ya miji iliyomo kwenye top 10.

1:Tokyo
2:Oslo
3:Luanda
4:Nagoya
5:Yokohama
6:Stavanger
7:Kobe
8:Copenhagen
9:Geneva
10:Zurich



source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment