Nyota wa Hip Hop Kugombea Urais

Thursday, August 05, 2010 / Posted by ishak /


Mwanamuziki maarufu duniani wa muziki wa Hip Hop, wa kundi la Fugees, Wycleaf Jean amejitosa kwenye siasa na atagombea urais wa Haiti katika uchaguzi utakaofanyika novemba.
Baada ya kutesa kwa muda mrefu katika anga ya muziki wa hip hop na miondoko reggae, nyota wa kundi la Fugees la Marekani, Wycleaf Jean ameamua kujitosa kwenye masuala ya siasa na atakuwa miongoni mwa wagombea urais.

Wycleaf ambaye alizaliwa nchini Haiti amesema kuwa atatangaza rasmi kugombea wa urais wa Haiti kesho alhamisi kupitia televisheni ya CNN kwenye kipindi cha Larry King Live.

Uchaguzi wa Haiti utafanyika novemba 28 mwaka huu na rais wa sasa wa Haiti, Rene Preval, hataweza kugombea tena urais kutokana na kumaliza miongo yake kisheria.

Ili aweze aweze kugombea urais Wycleaf anakabiliwa na changamoto ya kuthibitisha kuwa ameishi nchini Haiti kwa miaka mitano na hana uraia wa nchi nyingine yoyote.

Wycleaf alizaliwa nje kidogo ya mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince, lakini alilelewa Brooklyn, New York nchini Marekani.

Wycleaf ana historia ndefu ya kujihusisha na masuala ya kisiasa nchini Haiti na alikuwa miongoni mwa watu walioshiriki kuandaa tamasha la kusaidia wahanga wa tetemeko kubwa la ardhi lililotokea mwezi januari mwaka huu na kuua maelfu ya watu.

source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment