Britney Spears Ashtakiwa Kwa Kumtesa Kingono Mlinzi Wake

Sunday, September 12, 2010 / Posted by ishak /


Mlinzi wa zamani wa nyota wa muziki wa Pop wa Marekani, Britney Spears amefungua kesi mahakamani akimshtaki nyota huyo wa muziki kwa kumnyanyasa kijinsia kwa kutembea uchi mbele yake na kufanya mapenzi na mpenzi wake mbele yake.
Mlinzi wa zamani wa nyota wa muziki wa Pop wa Marekani, Britney Spears, Fernando Flores amefungua kesi mahakamani akimtuhumu nyota huyo wa muziki kwa kumnyanyasa kijinsia.

Flores amedai kuwa nyota huyo wa muziki alikuwa akitembea uchi mara kwa mara mbele yake na wakati mwingine alikuwa akifanya mapenzi na mpenzi wake mbele yake.

Mlinzi huyo alisema katika hati alizowasilisha mahakamani mjini Los Angeles kwamba Britney Spears alijaribu mara kwa mara kumvuta kimapenzi na wakati mwingine alimvuta chumbani kwake na kujianika uchi mbele yake.

Mlinzi huyo alisema kuwa kitendo cha Britney Spears kugombana na mumewe wa zamani mbele ya watoto wao kilikuwa kikiumiza hisia zake.

Mlinzi huyo ambaye alifanya kazi kama mlinzi wa Britney Spears kuanzia mwezi february hadi julai mwaka huu, aliilalamikia pia kampuni yake ya ulinzi kwa kutoyatilia mkazo malalamiko yake aliyokuwa akiyapeleka kuhusiana na unyanyasaji wa kijinsia wa Britney Spears.

Wakili wa Britney Spears alikataa kusema chochote kuhusiana na kesi hiyo.

source nifahamishe