Ajiua Baada ya Video Akilawitiwa Kuwekwa Online

Friday, October 01, 2010 / Posted by ishak /


Mwanafunzi wa kiume wa nchini Marekani ambaye marafiki zake walirekodi kwa siri video wakati akiingiliwa kinyume cha maumbile na mwanaume mwenzie na kisha kuiweka video hiyo kwenye internet amejiua kwa kujirusha toka kwenye daraja.
Tyler Clementi, Mwanafunzi wa kiume wa mwaka wa kwanza wa chuo kikuu cha Rutgers University cha nchini Marekani mwenye umri wa miaka 18 ambaye alikuwa akifanya ushoga kwa siri, amejiua mwenyewe kwa kujirusha toka kwenye daraja baada ya video yake akiingiliwa kinyume cha maumbile na mwanaume mwingine kurushwa LIVE kwenye internet.

Clementi alijirusha wiki iliyopita toka kwenye daraja la George Washington na kuangukia kwenye mto mkubwa wa Hudson River, last week, maiti yake ilipatikana juzi kwenye mto huo.

Clementi alichukua uamuzi wa kujiua baada ya kugundua marafiki zake aliokuwa akikaa nao chumba kimoja walimrekodi kwa siri wakati akifanya mapenzi na mwanaume mwingine na VIDEO za tukio hilo zilirushwa LIVE kwenye internet kupitia Webcam.

"Kama angekuwa kitandani na mwanamke, haya yote yasingetokea", alisema mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho.

"Kama asingeanikwa LIVE kwenye internet, mambo yake ya ndani yasingeanikwa na leo tungekuwa naye hapa", aliongeza mwanafunzi huyo.

Wanafunzi wawili mmoja wa kiume Dhraun Ravi na mwingine wa kike Molly Wei, ambao wote wana umri wa miaka 18, wamefunguliwa mashtaka ya kuvunja haki za msingi za Clementi.

Mahakama iliambiwa kuwa webcam ilitumika kurusha LIVE tukio la Clementi akiingiliwa na mwanaume mwingine mnamo septemba 19 na Ravi alijaribu kulirusha LIVE tena tukio la pili lililofanyika septemba 21 ambayo ni siku moja kabla ya Clementi kujiua.

Taasisi za kutetea haki za mashoga zimeichachamalia kesi hii zikitaka Ravi na mwenzake wahukumiwe adhabu kali.

Taasisi hizo zimesema kuwa Ravi na mwenzake wameonyesha chuki waliyo nayo kwa mashoga na wasagaji na wameitaka mahakama itoe adhabu kali.

Ravi na mwenzake huenda wakahukumiwa kwenda jela miaka mitano iwapo watapatikana na hatia ya kuingilia undani wa mtu bila ya ridhaa yake.

source nfahamishe