Makahaba Kuvaa Vizibao Vya Njano Ili Waonekane Vizuri

Thursday, October 28, 2010 / Posted by ishak /


Makahaba wa nchini Hispania wanaowinda wanaume pembeni ya barabara wameanza kuvaa vizibao vya njano vinavyoakisi mwanga ili waweze kuonekana vizuri.
Ili kuepuka faini ya euro 40, makahaba katika mji wa Els Alamus kaskazini mwa Hispania wameanza kufuata masharti ya serikali ya kuvaa vizibao vya njano vinavyoakisi mwanga.

Meya wa mji huo aliamuru makahaba wote wanaosimama pembeni ya barabara kuwinda wanaume wavae vizibao hivyo ili kuwafanya waonekane vizuri na hivyo kuepusha kutokea kwa ajali.

Taarifa ya meya wa mji huo ilisema kuwa baadhi ya makahaba wameanza kuvaa vizibao hivyo baada ya polisi kuanza kuwatoza faini ya euro 40 makahaba wanaosimama pembeni ya barabara kuu kuwinda wateja.

Nchini Hispania kuna jumla ya wanawake laki tatu wanaofanya biashara ya ukahaba. Mwanamke anaruhusiwa kisheria kufanya ukahaba nchini Hispania ingawa kujinufaisha kwa kuwatafutia makahaba wateja ni kinyume cha sheria.

Ni jambo la kawaida katika miji mbalimbali nchini Hispania kuwaona wanawake wanaovaa nguo fupi sana wakiwa wamesimama pembeni ya barabara wakitafuta wanaume.

Utafiti uliofanywa hivi karibuni nchini Hispania ulionyesha kuwa mwanaume mmoja kati ya wanne nchini Hispania ameishawahi kununua penzi toka kwa kahaba.

source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment