Babu wa Miaka 96 Amuoa Mwanamke wa Miaka 30

Saturday, March 27, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Babu mwenye umri wa miaka 96 wa nchini Taiwan amekuwa gumzo nchini humo baada ya kufunga ndoa na mwanamke aliyemzidi miaka 66.
Babu Lin Chung ameweka rekodi ya kuwa bwana harusi mwenye umri mkubwa kuliko wote nchini Taiwan baada ya kufunga ndoa na mwanamke mwenye umri wa miaka 30.

Chung amekuwa gumzo kwenye kitongoji cha Tainan baada ya kumuoa mwanamke huyo anayetoka maeneo ya ukanda wa kati nchini China katika jimbo la Hunan.

Chung ambaye hakuwahi kuoa katika ujana wake, ana watoto wawili aliojitolea kuwalea tangia walipokuwa wadogo ambao hivi sasa mmoja kati ya watoto hao ana umri wa miaka 68.

Chung anadai kwamba miaka mitatu iliyopita, alipewa maelezo na Mungu aende kwenye jimbo la Hunan nchini China ili kumtafuta mwanamke anayekuja kuwa mke wake.

Chung alifunga ndoa na mwanamke huyo hivi karibuni pamoja na upinzani mkali toka kwa mwanae huyo wa kujitolea ambaye alikuwa akimuona babu huyo kama amelaghaiwa.

"Inanibidi niwe na mwenza katika uzee wangu... sikuwahi kuwa na mke, kwanini hivi sasa hataki mimi nioe", alisema Mzee Chung.

Chung hivi sasa anashughulikia taratibu za kisheria kumwezesha mkewe ahamie Taiwan toka China ili waishi pamoja.

source nifahamishe

Ili Kuzuia Watu Kufanya Mapenzi, Miti 6,000 Yakatwa Uingereza

Wednesday, March 24, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Miti ipatayo 6,000 iliyopo pembeni mwa barabara moja kuu nchini Uingereza imekatwa ili kuwazuia watu kupeana huduma za chap chap.
Miti zaidi ya 6,000 iliyopo pembeni barabara namba A666 katika mji wa Darwen kaskazini masharibi mwa Uingereza imeteketezwa ili kuwazuia watu kufanya mapenzi chini ya miti hiyo.

Miti hiyo iliyochukua eneo la hekta 12 ilikuwa ni maarufu kama kituo cha watu wanaopeana huduma za mapenzi za chap chap.

Miti hiyo iliyopandwa baada ya vita vya pili vya dunia, ilikatwa baada ya maafisa wa manispaa ya mji huo kudai kuwa miti hiyo imezeeka na inaweza ikayaangukia magari yanayopita kwenye barabara hiyo.

Lakini sajenti wa polisi Mark Wilson alisema kuwa miti hiyo ilikatwa kutokana na kuwa kero kwa wapitanjia kutokana na baadhi ya watu kupenda kufanya mapenzi kwenye maeneo ya miti hiyo huku wakionekana wazi.

"Lilikuwa ni tatizo la muda mrefu lililoleta kero kero kubwa sana kwa jamii", alisema sajenti Wilson.

Haijajulikana kama kukatwa kwa miti hiyo kutaleta ufumbuzi wa tatizo hilo la watu kujisevia pembeni mwa barabara hiyo.

source nifahamishe

Akataa Zawadi ya Tsh. Bilioni 1.3

Wednesday, March 24, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanaume wa nchini Urusi ambaye anaishi maisha ya kifukara katika nyumba yake iliyojaa mende kibao, amekataa zawadi ya dola milioni moja aliyopewa baada ya kulipatia jibu fumbo la hesabu lililowashinda wataalamu wa mahesabu kwa miaka 100.
"Nimetosheka na kile nilicho nacho", alisema Dr Grigory Perelman, 44, mwanaume anayesemekana kuwa yeye ndiye Genius wa hisabati kwani yeye ndiye mtu pekee aliyefanikiwa kulifumbua fumbo la hisabati linaloitwa "Poincare Conjecture" ambalo wanahisabati wote duniani kwa kushirikiana walishindwa kulifumbua fumbo hilo lenye miaka 100.

Dr Grigory Perelman anaishi mjini Petersburg katika nyumba yake ambayo imejaa mende wengi sana kiasi cha majirani zake kutoa malalamiko kuwa mende hawaishi kuingia kwenye nyumba zao toka kwenye nyumba ya mtaalamu huyo wa hisabati.

Dr. Perelman nyumbani kwake ana meza moja, stuli moja na kitanda chenye godoro chafu lililochakaa lililoachwa na wamiliki wa nyumba hiyo ambao walikuwa walevi kupindukia ambao ndio waliomuuzia Dr.Perelman nyumba hiyo.

Pamoja na maisha anayoishi, Dr. Perelman ameikataa zawadi ya dola milioni moja aliyopewa na taasisi ya hisabati ya Marekani akisema kuwa hana shida ya pesa ametosheka na alichonacho.

Miaka minne iliyopita, Dr. Perelman alikataa kwenda kuichukua tuzo maalumu aliyotunukiwa na umoja wa kimataifa wa wanahisabati kwa kulipatia jibu swali hilo gumu la hisabati.

Wakati huo Dr. Perelman alisema "Sina shida ya pesa wala umaarufu, sitaki nionyeshwe kwa watu kama vile wanyama kwenye bustani za wanyama".

"Mimi sio shujaa wa hisabati, sijafanikiwa kwa kiasi hicho ninachoongelewa, na hivyo sitaki watu wote wawe wananiangalia mimi", alisema Dr. Perelman.

Ilikuwa ni mwaka 2002 wakati Dr. Perelman alipokuwa akifanya kazi kwenye taasisi ya utafiti wa hisabati nchini Urusi wakati alipoanza kutuma majibu kwenye internet ya fumbo la Poincare Conjecture ambalo ni miongoni mwa mafumbo saba magumu ambayo kila fumbo moja limetengewa zawadi ya dola milioni moja kwa mtu atakayelipatia jibu.

Kupatikana kwa jibu la fumbo la Poincare Conjecture kutawawezesha wanasayansi kuweza kujua umbile la ulimwengu.

Mwaka 2003 Dr. Perelman aliacha kazi kwenye taasisi hiyo ya utafiti wa hisabati na inadaiwa na marafiki zake kuwa ameachana kabisa na masuala ya hisabati.

source nifahamishe

Mwanamke Afungwa Jela ya Wanaume Kwa Miezi Sita

Wednesday, March 24, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Skendo limeikumba kitengo cha kurekebisha tabia cha Afrika Kusini ambapo mwanamke aliyakamatwa kwa makosa ya ujambazi anadaiwa kufungwa kwenye jela ya wanaume kwa kipindi cha miezi sita na kupelekea mwanamke huyo abakwe na kulawitiwa na wafungwa wa kiume.
Denise Wilson au maarufu kwa jina la Abbah wa mji wa Isipingo nchini Afrika Kusini amekifungulia mashtaka kitengo cha kurekebisha tabia cha Afrika Kusini kwa kumweka kwenye jela ya wanaume kwa miezi sita wakati alipokuwa akisubiria kufikishwa mahakamani kwa makosa ya ujambazi, kujaribu kuua na kuteka watu.

Denise anadai fidia ya rand 100,000 kwa madhila aliyoyapata wakati alipokuwa kwenye jela ya wanaume.

Katika nyaraka za mahakama, Denise alisema kuwa alikamatwa septemba 24 mwaka 2002 na kupelekwa kwenye jela ya wanaume.

Alisema kuwa kitendo chake cha kupinga kuwekwa jela moja na wanaume kilisababisha avuliwe nguo mbele ya wanaume huku akizomewa na kuchekwa.

Wakati wa kipindi chake cha miezi sita kwenye jela ya wanaume, Denise anadai kuwa walinzi wa jela walikuwa wakimlazimisha afanye matendo ya ngono bila ya idhini yake.

Alidai pia kuwa wafungwa wa kiume walikuwa wakimpapasa mara kwa mara kwenye sehemu zake za siri bila ya idhini yake.

Denise pia hakusita kusema kuwa alibakwa na kulawitiwa katika kipindi cha miezi sita kwenye jela ya wanaume.

Alisema kuwa ingawa maafisa wa jela walikuwa wakijua kuwa yeye ni mwanamke, waliendelea kumweka jela moja pamoja na wanaume.

Alisema kuwa hata daktari wa wilaya alipomfanyia uchunguzi wa kuthibitisha jinsia yake, aliendelea kuwekwa kwenye jela hiyo.

Kitengo cha kurekebisha tabia cha Afrika Kusini kimeamua kukaa kimya kikisubiria kesi hiyo ianze kusikilizwa mahakamani.

source nifahamishe

Aibiwa Mumewe, Aenda Mahakamani, Alipwa Fidia Dola Milioni 9

Wednesday, March 24, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanamke wa nchini Marekani aliyemfikisha mahakamani mwanamke aliyempora mumewe, ameshinda kesi aliyomfungulia mwanamke huyo kwa kumuibia mumewe na atalipwa fidia ya dola milioni 9.
Cynthia Shackelford mwenye umri wa miaka 60 aliiambia mahakama ya North Carolina kuwa aliacha kazi yake ya ualimu ili kulea watoto na kumsaidia mumewe Allan katika kuziendeleza shughuli zake za kisheria.

Kwa kutumia kipengele cha sheria ambacho huwa hakitumiki sana, Bi Cynthia alisema kuwa mumwe alikuwa ni mtu mwenye furaha na mwenye kuonyesha mapenzi kwake kabla ya bi Anne Lundquist, 49, kuuingilia uhusiano wao na kuanza uhusiano na mumewe.

Baada ya siku mbili za kuisikiliza kesi hiyo, majaji waliamuru bi Cynthia alipwe fidia ya dola milioni 9 baada ya bi Cynthia kuithibitishia mahakama jinsi mapenzi yao yalivyokuwa motomoto kabla ya Anne kuanza uhusiano na mumewe.

Mahakama ilitaka bi Cynthia alipwe fidia kwa kitendo cha mumewe kutembea nje ya ndoa yao na kumuumiza kihisia bi Cynthia.

Anne ambaye hivi sasa anaishi na Allan, alisema kuwa atakata rufaa kupinga hukumu hiyo akidai kuwa alianza uhusiano na Allan baada ya ndoa ya Allan na mkewe kuvunjika.

Jimbo la North Carolina ni miongoni mwa majimbo machache ya Marekani ambayo yanaruhusu wanandoa kuwafikisha mahakamani wenzao wanaozisaliti ndoa zao.

source nifahamishe

Mnigeria Afariki Kwa Njaa Uswizi Akigoma Kurudishwa Kwao

Monday, March 22, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Raia wa Nigeria ambaye alianzisha mgomo wa kula akipinga kurudishwa Nigeria toka Uswizi amefariki kwenye uwanja wa ndege dakika chache kabla ya kupandishwa ndege kurudishwa kwao.
Raia huyo wa Nigeria mwenye umri wa miaka 29 alikuwa kwenye mgomo wa kula kwa siku kadhaa akipinga kurudishwa kwao Nigeria.

Raia huyo wa Nigeria ambaye alikuwa miongoni mwa wahamiaji 15 toka Nigeria waliokuwa waondoshwe kinguvu kutoka Uswizi baada ya kugoma kurudi kwenye nchi zao.

Mnigeria huyo alianza kuumwa ghafla baada ya kufungwa pingu kinguvu wakati akilazimishwa kupandishwa ndege maalumu iliyoandaliwa kuwarudisha wahamiaji makwao.

Maafisa wa Uswizi walimvua pingu walizomfunga na daktari alijaribu kunusuru maisha yake lakini jitihada za0 hazikuzaa matunda na Mnigeria huyo alifariki kwenye uwanja wa ndege wa Zurich Airport.

Wanigeria wawili ambao nao walikuwa wakirudiswa Nigeria walipohojiwa na tovuti ya habari ya Swissinfo walisema kuwa polisi walikuwa wakiwafanyia vitendo ambavyo havikuwa vya kibinadamu.

"Walitufanya kama wanyama vile, walitufunga pingu mikononi, miguuni, kwenye mapaja na kiunoni. Pia walituvalisha helmet kama za mabondia, ilikuwa ni vigumu mtu kujisogeza", alisema mmoja wa Wanigeria hao.

Mnigeria aliyefariki alikuwa akiishi nchini Uswizi tangia mwaka 2005 na alikuwa akikabiliwa na kesi ya kukamatwa na madawa ya kulevya.

Safari za kuwarudisha wahamiaji makwao zimesitishwa kwa muda huku uchunguzi wa kifo cha raia huyo wa Nigeria ukifanyika.

Mwaka jana jumla ya safari 43 za kuwarudisha makwao wahamiaji zilifanyika nchini Uswizi na jumla ya wahamiaji 360 walirudishwa makwao wengi wao wakiwa ni kutoka nchi za Afrika na nchi za kusini mashariki mwa bara la ulaya.

source nifahamishe

ontena za betri bandia zakamatwa

Monday, March 22, 2010 / Posted by ishak / comments (0)

SHEHENA ya kontena 20 za betri aina ya Tiger Head kutoka China zimekamatwa kutokana na kukosa ubora na viwango vya matumizi ya bidhaa hiyo.
Kontena hizo zimekamatwa katika operesheni ya Shirika la Viwango nchini (TBS) kayitka kukagua bnidhaa ziingiazo nchini ambazo hazina viwango vya matumizi.


Mkurugenzi Mkuu wa TBS Charles Ekerege alisema shehena waliyokamata ya betri hizo ilifika nchini Januari mwaka huu, lakini walipozikagua wakagundua kuwa hazina ubora uliowekwa na shirika hilo.

Alisema Betri hizo zinaingizwa nchini na wafanyabiashara wakubwa na wakati mwingine imedaiwa kuwa wanaziingiza kwa njia ya panya.

Alisema betri hizo huingizwa nchini na huuzwa kwa bei ya rejereja shilingi 350 na zinazotengenezwa hapa nchi huuzwa kwa shuilingi 45o kila moja, na watanzania wengi hukimbilia betri hizo kutokana na unafuuu wa bei.


source nifahamishe

Akamatwa akiwa katika zoezi la kuiba mtoto

Monday, March 22, 2010 / Posted by ishak / comments (0)

MWANAMKE mmoja amekamatwa akiwa anazungukazunguka mazingira katika nyumba moja huku akimemendea kuondoka na mtoto aliyelazwa barazani mwa nyumba hiyo .

Tukio hilo lilitokea jana huko maeneo ya Buguruni kwa Mnyamani, majira ya jioni, huku mama huyo alionekana kwa muda mrefu akizunguka nyumba hiyo bila ya wakazi hao kutambua dhumuni la mama huyo.

Ilidaiwa kuwa mama huyo alikuwa akipita njia hiyo mara kwa mara na wenyeji wa nyumba hiyo wakidhani kuwa alikuwa amepotea ramani ya alipotaka kuelekea bila kutambua dhumuni lake.

Kumbe mama huyo lengo na madhumuni yake alikuwa anasubiri watu waishio humo wazubae na kumuacha mtoto huyo nay eye amuibe na aondoke nae.

Bila kutambua mama wa mtoto huyo baada ya mtoto huyo kulala alichukua mto na kumlaza mtoto huyo barazani hapo na kuingia ndani na watu wengine waliendelea na shughuli zao bila kutambua kuwa mtoto huyo alikuwa anaviziwa.

Hivyo dakika chache mama huyo alpoach kisogo na kuingiga ndani mama huyo mwizi alisogea maeneo hayo na kutaka kumchukua huyo mtoto ghafla mama wa mtoto huyo alitoka na kumkuta mama huyo akwia barazani hapo na kumshangaa.

Mama huyo alitaka kukimbia kabla hajakimbia mama wa mtoto huyo alimdaka na kumuhoji alikuwa anahitaji nini kwa muda huo ili aweze kumsaidia na mama huyo kukosa jibu la uhakika na kumjibu kuwa alipita hapo na kuona mdudu alikuw anataka kumsogelea mtoto huyo na ndipo alisogea kumuondoa mdudu huyo.

Majibu hayo yalimtia mashaka mama wa mtoto huyo na kuita wenzake waliopanga katika nyumba hiyo na kumuhoji mama huyo bila majibu.

Ndipo mmoja wao alipopataw azo na kuwaambia wenzake huenda alikuwa anataka kumuiba mtoto huyo na wakashtuka na wakampeleka kituo cha polisi ili akaoe maelezo.

Kabla hajafika kituoni mama huyo aliwaomba wanawake wenzake hao wamsamehe kwa kuwa alikuwa na lengo l kuiba mtoto huyo na aliomb wasimpeleke kituo cha polisi.

NIFAHAMISHE ilibahatika kumuona watu wa mtaa huo walivyojazana mahali hapo na wakimpeleka kituoni mama huyo.

Mama wa mtoto huyo alipozungumza na nifahamishe alidai kuwa “ mimi na wenzangu tulikuwa tunamuona mama huyu akipita njia hii mara kwa mara na tulikuwa hatuelewi alikuwa na dhumuni gain, kumbe inaonekana anapitaga hapa na kumuona mtoto analazwa hapa nje na leo alikwu anamsalandia

“Ujue mimi kutokana na sasa hivi kuwa na joto kali sana ndani naamuaga kumlaza mwanangu hapa nje ili aweze kulala vizuri kwa kuwa kunakuwa na upepo hapa barazani'

Mama huyo alifikishwa kituo cha polisi ili aweze kusalimika huku baadhi ya watu wakiokuwa na jazba wangeweza kumjeruhi, hadi nifahamishe inondoka kituoni haikuweza kuongea na mkuu yoyote kituoni hapo na itafatilia kujua hatma ya mama huyo kituoni hapo leo.

source nifahamishe

Imani za Kishirikina Zapelekea Abanikwe Kichwa Chake

Monday, March 22, 2010 / Posted by ishak / comments (0)



Imani za kishirikina nchini Bangladesh zimepelekea wauzaji wa matofali ya kuchoma wamuue mtu na kisha kukibanika kichwa chake baada ya kuambiwa na mganga kuwa kufanya hivyo kutayafanya matofali yao yawe mekundu na hivyo kununuliwa kwa wingi.
Wafanyakazi wanne wa sehemu ya kutengeneza na kuuza matofali ya kuchoma nchini Bangladeshi wanashikiliwa na polisi kwa kumuua kibarua na kisha kukibanika kichwa chake kwenye jiko la kuchomea matofali.

Tukio hilo limetokea kwenye kijiji kimoja kaskazini mwa Bangladeshi baada ya mmiliki wa sehemu hiyo kuwapa maagizo wafanyakazi wake kuwa mganga ameagiza wamtoe kafara mtu mmoja ili kuyafanya matofali yao ya kuchoma yawe mekundu.

Mmiliki huyo alikuwa hana furaha na rangi ya matofali yake kutokuwa mekundu pamoja na kwamba walikuwa wakiyachoma sana matofali yao.

Matofali mekundu ni dili sana nchini Bangladeshi kutokana na kwamba watu wengi wanaamini kuwa matofali yaliyochomwa ipasavyo huwa na rangi nyekundu iliyokolea.

Wafanyakazi wa sehemu hiyo ya kutengeneza matofali walimuua mmoja wa kibarua wao na kisha kukibanika kichwa chake kwenye makaa ya moto kama mganga alivyoagiza.

Polisi wanawashikilia wafanyakazi wanne na wanamtafuta mmiliki wa sehemu hiyo pamoja na mganga wake ambao walitoroka baada ya tukio hilo kugundulika

source nifahamishe

Aibu Kubwa Baada ya Moto Kuzuka Kwenye Danguro

Monday, March 22, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Moto uliozuka kwenye danguro la mashoga nchini Uswizi ulisababisha wateja wa danguro hilo wakimbie uchi kunusuru maisha yao.
Mmoja wa wateja wa danguro hilo aliyetajwa na gazeti la Blick la Uswizi kuwa jina lake ni Memeth J, alilazimika kuning'inia kwenye dirisha akiwa uchi huku akificha sura yake wakati akisubiri zimamoto waje kumuokoa.

Tukio hilo lilitokea kwenye danguro moja mjini Basel nchini Uswizi ambapo mashoga hujiuza.

Memeth ambaye anakataa kuwa yeye pia alikuwa mteja wa danguro, alijitetea kuwa alienda kwenye danguro hilo kumtembelea rafiki yake wa miaka 10, Tamilo H ambaye ni shoga anayefanya kazi kwenye danguro hilo.

Memeth aliliambia gazeti la Blick kuwa alikuwa akijirusha na shoga huyo kwenye danguro hilo kabla ya kupitiwa na usingizi na kuzinduka danguro hilo likiwa limeshika moto.

Memeth alilazimika kukimbilia kwenye korido ya danguro hilo huko akiwa uchi lakini huko alikutana na kundi la waandishi wa habari na wapiga picha wakiwa pamoja na zimamoto.

Hali hiyo ilimfanya Memeth akimbilie kwenye dirisha na kuacha makalio yake nje huku akificha sura yake kwa kutumia pazia. Alikubali kuondoka kwenye dirisha hilo baada ya zimamoto kumhakikishia kuwa wataendelea kuificha sura yake.

"Nafikiri ndugu zangu hawatanitambua kwa kuangalia makalio yangu", alisema Memeth akiliambia gazeti hilo.

"Familia yangu haijui kuhusiana na tabia yangu hii ndio maana nimelazimika kuificha sura yangu", alisema Memeth ambaye alisema ana umri wa miaka 33.

source nifahamishe

Vijimambo vya Mapenzi

Monday, March 22, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanaume mmoja wa nchini Uingereza ambaye alitoswa mkewe wa ndoa ya miaka 14 ambaye alipata mwanaume mwingine nje, amefariki dunia kutokana na moto aliouanzisha ili kuichoma moto nyumba yake ili mkewe asiambulie kitu watakapoachana.
Wakati Timothy Flood alipoimiminia petroli nyumba yake ili ndoa yake na mkewe itakapovunjika, mkewe asiambulie kitu, hakungundua kuwa kuna kiasi kidogo cha petroli kilimwagikia kwenye nguo zake.

Na wakati alipoipiga kiberiti nyumba yake alishangaa kujikuta na yeye mwenyewe akiwaka moto.

Timothy ambaye ni baba wa watoto watatu alijaribu kuuzima moto uliokuwa ukimteketeza kwa kutumia maji ya mvua lakini hadi wakati anaokolewa alikuwa ameishangua asilimia 90 ya mwili wake na alifariki dunia siku mbili baadae hospitalini.

Timothy mwenye umri wa miaka 42, aliamua kuichoma moto nyumba yake baada ya mkewe kuamua kuivunja ndoa yao alipoanza uhusiano na mwanaume aliyesoma naye shule.

Ingawa Timothy na mkewe, Catherine, 39, walikuwa wakiendelea kuishi kwenye nyumba moja walikuwa hawazungumzi wala kujuliana hali.

Mgogoro mkubwa ulikuwa kwenye nyumba yao ambapo Catherine alimtaka Timothy aondoke amuachie yeye nyumba hiyo.

Timothy kwa kuhofia kuwa watakapoachana rasmi kisheria kutokana na sheria mkewe anaweza akapewa nyumba kwa sababu ya watoto wao,
aliamua kuichoma moto ili wakose wote.

Mahakama katika mji wa Newport, kusini mwa Wales iliambiwa kuwa Timothy ili kuichoma moto nyumba hiyo alinunua lita 51 za petroli na viberiti kadhaa ili kuhakikisha kuwa hakitoki kitu.

Siku ya tukio, alimpeleka mkewe kwa wazazi wake na ndipo aliporudi na kuipiga moto nyumba hiyo baada ya kumtumia meseji mkewe akimwambia "Nimeishapata suluhisho la kuishi bila wewe".

Moto mkubwa ulizuka ambao uliiteketeza sehemu kubwa ya nyumba hiyo.

Majirani wanasema kuwa Timothy alisikika akipiga kelele za kuomba msaada wakati moto aliouanzisha akitegemea kuiteketeza nyumba yake ulipokuwa ukimchoma yeye mwenyewe.

Timothy alifariki siku mbili baadae hospitalini baada ya ndugu zake kukubali kuzizima mashine zilizokuwa zikimsaidia aendelee kuishi.

source nifahamishe

Mtu Aliyeishi Mwaka Mzima Bila Kutumia Pesa

Monday, March 22, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Kutana na Mark Boyle, mwanaume wa nchini Ireland ambaye aliamua kuondokana na stress za maisha ya kutafuta pesa na kuamua kuishi mwaka mzima bila kutafuta pesa wala kutumia pesa kununua kitu chochote.
Mark Boyle mwenye umri wa miaka 30, ambaye ana shahada ya masuala ya uchumi anasema kwamba kwa mzima alioishi bila kuigusa pesa ulikuwa ni mwaka wenye furaha sana katika maisha yake na hakuwa na stress yoyote ile.

Mark kwa zaidi ya miezi 12 amekuwa akiishi kwenye gari lake aina ya caravan kwahiyo halipi pesa zozote za pango la nyumba, hanunui chakula, anaandaa chakula chake mwenyewe au kula vyakula vinavyotupwa na watu wengine.

Mark anasema kwa mwaka mzima hakutumia hata senti moja na amekuwa mtu mwenye furaha sana na anatarajia kuendelea kuishi bila pesa.

Usafiri wake ni wa kwa kutumia baiskeli aliyoiokota, simu yake inapokea tu yeye hampigii mtu simu, anatumia solar-power kuchemsha maji yake ya kuoga.

Dawa ya meno anayoitumia anaitengeneza mwenyewe kwa kutumia mifupa ya samaki. Analima chakula chake mwenyewe au anaokota vyakula majalalani. Nguo anazovaa anaziokota pia majalalani.

Mark anaendesha blogu yake ambayo anaelezea maisha yake ya kila siku. Anatumia laptop inayotumia umeme wa solar-power na hupewa muda wa kutumia wireless internet kwa malipo ya kufanya kazi za shambani.

"Umekuwa ni mwaka wenye furaha sana kuliko miaka yote ya maisha yangu, na natarajia kuendelea kuishi hivi, sioni sababu ya kurudi kwenye maisha ya dunia yanayotawaliwa na pesa", alisema Mark.

"Sina stress za kuchelewa kazini, sina stress za kulipa bili za umeme, maji au gesi na sihitaji kufanya kazi ili kuendeleza maisha yangu", alisema Mark.

Hata hivyo Mark anakiri kuwa anazikosa starehe za dunia kama vile kwenda disko au baa kwani huko pesa zinahitajika wakati yeye hatafuti wala kutumia pesa.

"Badala ya kwenda baa, huwa naweka kambi na kuwasha moto nikicheza muziki au wakati mwingine huwa nazurura mitaani", alimalizia kusema Mark Boyle.

source nifahamishe