Mama Afungwa Miaka 30 Jela Kwa Kufanya Mapenzi na Mwanae

Wednesday, July 14, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanamke wa nchini Marekani ambaye alifanya mapenzi na mwanae mwenye umri wa miaka 14 amehukumiwa kwenda jela miaka 30.
Aimee Sword, 36, atatumia miaka 30 jela kwa kufanya mapenzi na mtoto wake wa kiume wa kumzaa hotelini na nyumbani kwa rafiki yake katika jimbo la Michigan.

Sword alianza kufanya mapenzi na mwanae baada ya kuwasiliana naye kupitia Facebook mwezi mei mwaka 2008 wakati huo mwanae alikuwa na umri wa miaka 14.

Kabla ya hapo Sword hakuwa na mawasiliano na mwanae huyo ambaye alimtoa kwenye nyumba ya watoto yatima wakati mtoto wake huyo akiwa na umri wa miaka miwili.

Sword ambaye ni mama wa watoto sita, alikiri kosa moja la kufanya ngono na mtoto mwenye umri mdogo na aliwaomba msamaha watoto wake na dada yake.

"Najuta kwa yote yaliyotokea.... sielewi imekuwaje", Sword aliiambia mahakama.

Sword mbali ya kuhukumiwa kwenda jela miaka 30 amepigwa marufuku kuwasiliana na mtoto wake.


source nifahamishe

Mlevi Ampanda Mamba Mgongoni

Wednesday, July 14, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanaume mmoja wa nchini Australia aliyekuwa amelewa chakari amelazwa hospitali baada ya kujeruhiwa na mamba alipoamua kumfanya mamba kama farasi kwa kumdandia mgongoni.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 36 alifukuzwa baa baada ya kuonekana pombe zimemzidia ndipo alipoamua kwenda kwenye bustani ya wanyama ya mjini Broome nchini Australia.

Mwanaume huyo aliipanda fensi na kuingia kwenye bustani hiyo kabla ya kujisogeza kwenye sehemu ambayo wametengewa mamba.

Katika tukio hilo lililotokea kwenye majira ya saa nne usiku, mwanaume huyo alimsogelea mamba mwenye urefu wa mita 2.8 na kujaribu kumnyeshwa bia kabla ya kuamua kurukia kwenye mgongo wa mamba huyo aliyepewa jina la Fatso.

"Alitoka kwenye eneo hilo na kwenda kwenye eneo jingine ambalo lilikuwa na mamba mwenye urefu wa mita 5", alisema msemaji wa polisi na kuongeza "Aliona ni wazo zuri kukaa juu ya mamba huyo aendeshwe kama farasi".

"Mamba alijipindua na kuung'ata mguu wake", alisema msemaji huyo wa polisi.

Alifanikiwa kuchoropoka akiwa amejeruhiwa vibaya sana, aliwahishwa hospitali kwa matibabu zaidi.

"Ana bahati sana kuwa hai hadi leo, mtu mwenye akili timamu hawezi kukaa juu ya mamba mwenye urefu wa mita 5", alisema afisa mwingine wa polisi.

Taarifa zinasema kuwa mmiliki wa bustani hiyo hana mpango wa kumfungulia mashtaka mwanaume huyo.


source nifahamishe

Mabaki ya Binadamu Yakutwa Kwenye Tairi la Ndege

Sunday, July 11, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mabaki ya mwili wa binadamu yamekutwa kwenye matairi ya ndege ya Saudi Arabia iliyokuwa ikitoka Lebanon kuelekea Saudi Arabia.
Mabaki ya mwili wa binadamu yamekutwa kwenye matairi ya ndege ya shirika la ndege la Saudia, Nas Air wakati ndege hiyo ilipotua kwenye uwanja wa ndege wa Riyadh.

Maafisa wa Lebanon walisema kuwa mabaki hayo ni ya mwanaume aliyejaribu kusafiri bure toka Lebanon kwa kujificha kwenye sehemu ya matairi ya ndege.

"Mwanaume ambaye hakutambulika jina lake alifanikiwa kujificha kwenye sehemu ya matairi ya ndege bila ya waongozaji wa ndege mjini Beirut kumuona", alisema afisa mmoja wa Lebanon.

Ndege ya Nas Air namba XY 720 ilipaa toka uwanja wa ndege wa Beirut ijumaa usiku na ilitua Riyadh siku ya jumamosi asubuhi.

Mabaki ya mwili wa mwanaume huyo yalionekana wakati wa ndege hiyo ilipokuwa ikifanyiwa marekebisho baada ya kutua.

Shirika la habari la Lebanon NNA lilisema kuwa baadhi ya abiria walimuona mwanaume huyo aliyekuwa amebeba kibegi kidogo mgongoni akijificha kwenye sehemu ya matairi ya ndege wakati ndege hiyo ikijiandaa kuanza safari.

"Abiria walimpa taarifa rubani lakini hakuchukua hatua yoyote na alianza kuiendesha ndege kujiandaa kupaa bila ya kuwataarifu waongoza ndege", lilisema shirika hilo la habari.

Mwanaume huyo alipondwa pondwa na matairi ya ndege na mabaki ya mwili wake yalibaki yamegandia kwenye matairi ndege ilipotua.

Maafisa wa Nas Air walisema kuwa wanasubiri taarifa ya mamlaka ya anga ya Saudia kabla ya kusema chochote kuhusiana na suala hilo.

source nifahamishe