Ili Kumlinda Obama, Nazi Zaangushwa Toka Kwenye Minazi India

Saturday, November 06, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Ili kumlinda rais wa Marekani Barack Obama anayefanya ziara yake nchini India, serikali ya India imeamua kuangua nazi zote toka kwenye minazi iliyo karibu na majengo ambayo Obama atayatembelea.
Katika kujiandaa kumpokea kwa mara ya kwanza rais wa Marekani, Barack Obama, serikali ya India imeangua nazi zote toka kwenye minazi iliyopo karibu na majengo ambayo Obama atayatembelea mjini Mumbai.

Obama anawasili leo jumamosi nchini India katika hatua yake ya kwanza ya ziara zake katika bara la Asia.

Pamoja na ulinzi mkali kuwekwa kama ilivyotegemewa, maafisa wa serikali ya India wameamua pia kuchukua hatua zaidi kwa kumlinda rais huyo wa Marekani hata kwa hatari zitokenazo na mimea.

Nazi zote toka kwenye minazi yote inayolizunguka jengo la ukumbusho la Gandhi zimeangushwa chini ili kumlinda Obama.

Jengo hilo ni mojawapo ya sehemu tano ambazo Obama atazitembelea mjini Mumbai. Katika sehemu zote hizo hatua sawa za ulinzi zimechukuliwa.

"Kwanini tubahatishe?, tumewaagiza maafisa husika kuziangua nazi zote toka kwenye minazi iliyo karibu na jengo hili", alisema mkurugenzi wa jengo la Mani Bhavan ambalo Mahatma Gandhi aliishi wakati wa kupigania uhuru wa India toka kwa Uingereza.

Wiki iliyopita maafisa wa Marekani walilifanyia uchunguzi jengo la Mani Bhavan pamoja na sehemu zingine ambazo Obama atazitembelea.

Obama atazitembelea pia nchi za Indonesia, South Korea, Japan na China katika ziara yake ya siku 10 barani Asia.

source nifahamishe

Mwanamke wa Iran Aliyefanya Mapenzi Nje ya Ndoa Kuuliwa Leo Kwa Mawe

Wednesday, November 03, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mahakama ya nchini Iran imeruhusu adhabu ya kifo inayomkabili mama wa watoto wa wawili wa nchini Iran ambaye alikamatwa akifanya mapenzi na mwanaume aliyemuua mume wake.
Pamoja na shinikizo kubwa toka nchi za Magharibi na taasisi za kutetea haki za binadamu, Sakineh Mohammadi-Ashtiani huenda akauliwa leo kwa kupigwa mawe kwa mujibu wa vyanzo vya habari.

Mwanaharakati anayemtetea Sakineh alisema kuwa wamepokea taarifa toka kwa mtu anayefanya kazi ndani ya mahakama kuwa Sakineh atauliwa siku ya jumatano.

"Tumepokea taarifa siku tatu zilizopita kuwa Sakineh atauliwa siku ya jumatano", alisema Mina Ahadi, mwanaharakati anayemtetea Sakineh wakati akiongea na shirika la habari la AFP kuhusiana na barua aliyotumiwa na mtu ambaye hakutajwa jina lake.

Mahakama ya mji wa Tabriz ambako Sakineh ametupwa jela imeruhusu adhabu ya kifo inayomkabili Sakineh itekelezwe. Kwa kawaida adhabu za kifo nchini Iran hutekelezwa siku ya jumatano.

Tangu mwezi julai mwaka huu Iran ilikuwa ikisema kuwa adhabu ya kifo kwa kupigwa mawe inayomkabili Sakineh haitafanyika mpaka baada ya kuidhinishwa na mahakama kuu.

Sakine mwenye umri wa miaka 43 ambaye ni mama wa watoto wawili, alihukumiwa adhabu ya kifo na mahakama mbili tofauti mjini Tabriz mwaka 2006.

Adhabu yake ya kwanza ilikuwa ni adhabu ya kifo kwa kunyongwa ambayo baadae ilibadilishwa kuwa kifungo cha miaka 10 jela. Adhabu hiyo ilitokana na Sakineh kutuhumiwa kushiriki kwenye mauaji ya mumewe.

Adhabu ya pili ya kifo ilikuwa ni kuuliwa kwa kupigwa mawe kwa kosa la kufanya mapenzi nje ya ndoa na mwanaume aliyekamatwa kwa mauaji ya mumewe.

source nifahamishe