Rais Atupwa Jela Miaka Saba Kwa Kubaka

Thursday, March 24, 2011 / Posted by ishak /



Moshe Katsav
Wednesday, March 23, 2011 1:57 AM
Hatimaye Rais wa zamani wa Israel, Moshe Katsav ambaye alikuwa akikabiliwa na kesi ya ubakaji, amehukumiwa leo kwenda kunyea debe jela kwa miaka saba.
Aliyekuwa rais wa Israel Moshe Katsav amehukumiwa kwenda jela miaka saba kwa makosa ya ubakaji na makosa mengine ya kuwashambulia wanawake.

Wakitoa hukumu ya kesi hiyo iliyochukua miaka minne, majaji watatu wa kesi hiyo walimuadhibu rais huyo mkware kwa kumuweka kwenye kundi la watu ambao hawatapata msamaha wowote wa kutoka jela katika miaka miwili ijayo.

Katsav pia alihukumiwa kumlipa fidia ya dola 27,000 mwanamke aliyemfikisha mahakamani anayejulikana kwa jina la "Aleph".

Mwezi disemba mwaka jana Katsav alipatikana na hatia ya kubaka, kufanya shambulizi la kijinsia na kuizuia sheria kushika mkondo wake.

Wakati hukumu ikitolewa mmoja wa watoto wa rais huyo wa zamani wa Israel alimsogelea baba yake ili aweze kumkumbatia na baba yake alipiga kelele kwa sauti akisema "Usihofu Hawajatenda haki".

"Uongo umeushinda ukweli, Wanajua wameongopa", Katsav aliwaambia majaji wa kesi hiyo akiwaashiria wanawake waliomfikisha mahakamani kwa ubakaji.

Mmoja wa majaji alimwambia Katsav kuwa kosa la ubakaji linaharibu utu wa mtu na hivyo lazima adhabu iwe kali.

"Mtuhumiwa ametenda kosa kubwa na kama watu wengine ataadhibiwa, Hakuna mtu aliye juu ya sheria", alisema jaji huyo.


source nifahamishe

0 comments:

Post a Comment