
Mwanaume mmoja wa nchini China ambaye alikuwa akisumbuliwa na madeni mengi sana yaliyotokana na tabia yake ya kupenda kucheza kamari amejiua mwenyewe kwa kujilipua kwa bomu ndani ya basi lililokuwa limejaa abiria.
Kwa mujibu wa shirika la habari la China, Xinhua mwanaume huyo alijilipua mwenyewe ili kuepukana na madeni mengi anayodaiwa ambayo alikuwa hana uwezo wa kuyalipa.
Yang Yongshou, 42, ambaye zamani alikuwa muuza madawa ya kulevya kabla ya kuangukia kwenye uchezaji wa kamari, alijilipua kwa bomu aliloliweka chini ya kiti chake kwenye basi la abiria lililokuwa likifanya safari zake katika jimbo la Yunnan lililopo karibu na mpaka wa Vietnam.
"Yang alikuwa hana uwezo wa kulipa yuan 100,000 (Tsh. Milioni 19.8) ambazo alikuwa akidaiwa kwenye kamari", ilisema taarifa ya polisi.
Yang alifariki hapo hapo kutokana na bomu hilo huku abiria wengine 11 wa basi hilo wakipata majeraha mbalimbali.
Tabia ya watu kujilipua kwa mabomu wanapozidiwa na matatizo imekuwa ikiongezeka kwa kasi sana nchini China ambapo sababu kubwa inasemwa kuwa ni uhaba wa kazi na kuongezeka kwa tofauti ya kipato kati ya watu masikini na matajiri.
source nifahamishe

Kwa umri ana miaka miwili tu lakini kutokana na unene wake mtoto huyu wa nchini China ana uzito wa kilo 41 na bado anaendelea kunenepa.
Mtoto wa kike Pang Ya wa nchini China ingawa ana umri wa miaka miwili tu ana uzito wa kilo 41.
Uzito wa mtoto Pang ni sawa sawa na uzito wa mwanamke mtu mzima wa nchini China mwenye umbile la wastani.
Wazazi wake wamekuwa wakihangaika kutafuta tiba ya unene wa mtoto Pang ambao unatishia maisha yake.
"Madaktari hawajui nini chanzo cha unene wake hali ambayo inatufanya tuwe na hofu kubwa kuhusiana na maisha yake", alisema baba wa mtoto huyo.
Mtoto Pang ambaye anaishi na wazazi wake katika mji wa Taocun katika jimbo la Shanxi, alizaliwa akiwa na uzito wa kawaida wa kilo 3.6.
Katika takwimu za serikali ya China zilizotolewa hivi karibuni, watu milioni 60 wa nchini humo wanakabiliwa na matatizo ya unene uliokithiri.
source nifahamishe

Mvuta sigara aliyeteseka miaka mingi kutokana na magonjwa yaliyotokana na uvutaji sigara ametimiziwa matakwa yake kuwa atakapofariki jeneza lake na kaburi lake liweke maneno yanayosema 'Sigara Zimeniua'.
Jeneza la mzee Albert Whittamore lilizungushwa katika mitaa ya mji wake nchini Uingereza huku likiwa limewekewa maneno 'Sigara Zimeniua'.
Mzee Albert aliyefariki mwishoni mwa mwezi uliopita akiwa na umri wa miaka 85, aliacha wosia kuwa atakapofariki kaburi na jeneza lake liwekewe maneno hayo ili kuwaonya vijana wasije wakapoteza maisha yao kama alivyopoteza ya kwake kutokana na magonjwa yaliyotokana na uvutaji sigara.
Mzee Albert aliteseka miaka mingi sana kutokana na matatizo ya mapafu, ugonjwa uliotokana na uvutaji wake uliokithiri wa sigara enzi za ujana wake.
Bango lilitengenezwa na kuwekewa maandishi ya 'Sigara Zimeniua' kabla ya jeneza lake kuzungushwa kwenye mitaa kadhaa ya mji wa Dover uliopo kilomita 160 toka jijini London.
Kwenye kaburi lake nako kuliwekewa bango kama hilo ambalo inasemekana litakaa hapo kwa muda wa wiki moja.
Mzee Albert kabla ya kufariki alikuwa akiwausia vijana kuhusiana na madhara yanayotokana na uvutaji wa sigara.
source nifahamishe

MAZISHI YA ASKARI WA BWANA YESU KRISTO MAJOR NASSON JOHN KITUTA AMBAYE NDIYE MMOJA WA WAANZIRISHI WA JESHI LA WAKOVU HAPA TANZANIA (THE SALVATION ARMY).
MAZISHI YA ASKARI WA BWANA YESU KRISTO MAJOR NASSON JOHN KITUTA AMBAYE NDIYE MMOJA WA WAANZIRISHI WA JESHI LA WAKOVU HAPA TANZANIA (THE SALVATION ARMY)
Azikwa kifahari kama viongozi wa serikali ya Nyerere.
Mmoja wa wanzilishi wa shirika la kikristo la Salvation Army hapa nchini Major Nasson Kititu mwenye umri wa miaka 83 alizaliwa mwaka 1926 june 6 na amefariki dunia tarehe 26 februari katika hospitali ya Mikocheni, na kuzikwa katika shamba lake lililopo Kongowe Dar es Salaam,
Alipata Kujiunga na Jeshi la wokovu mwaka1948 akiwa chunya alifunga ndoa na mke wake 'Maria Kititu' mwaka 1950 katika wilaya ya chunya mkoani mbeya,mwaka wa 1951 aliitikia wito wa kumtumiki mungu kama mchungaji akamua kwenda katika chuo cha uchungaji cha jeshi la wokovu Nairobi.
Baada yakumaliza mafunzo ya uchungaji alianza kazi kama Luteni wa Jeshi la wokovu kanisa la Igunga 1952 hadi 1955
Katika mazishi yake kulikuwa na mvua nyingi ilinyesha kuashiria kuwa alikuwa mtumishi wa mungu mamia ya waumini wakiwemo majirani ndugu jamaa walihudhulia katika mazishi ambayo hakiki yalikuwa kama ya mtu mmoja wa kifahari kabisa na yenye heshima kuu kama mtumishi wa mungu yakiwa yameongozwa na COLONEL HEZEKIEL MAVUNDLA ambaye ni kiongozi wa Mkuu wa makanisa ya Salvation Army Tanzania. ambaye ni raia wa South Africa
source nifahamishe
Sugu Awatuhumu Wamarekani Na Ikulu Dar Kwa Kumuingiza Mjini

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Joseph Mbilinyi a.k.a Mr. II au Sugu ameituhumu taasisi moja ya Marekani na Ofisi ya Rais (Ikulu) ya Tanzania kwa kupora haki yake ya kuandaa tamasha la uzinduzi wa mradi wa kampeni ya kuzuia malaria mwezi uliopita.
Kwa mujibu wa gazeti moja la kila siku, Sugu alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa, tayari amewasilisha malalamiko yake makao makuu ya taasisi hiyo, New York, Marekani kwa kosa la kwenda kinyume na makubaliano ya awali.
Kampeni hiyo ambayo ilizinduliwa Februari 13 kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais Jakaya Kikwete, inalenga kuhamasisha jamii kupambana na malaria.
Sugu alisema kilichotokea ni kudhulumiwa wazo lake na Wamarekani hao ambao wameshirikiana na mkurugenzi na maofisa wengine (majina tunayo) wa Tanzania.
Alisema, baada ya kukutana na mmoja wa maofisa hao waliweza kujenga urafiki na alipomtaarifu kuhusu mpango wa asasi yao kutaka kuja nchini kuendesha kampeni kubwa ya kutokomeza malaria, hivyo yeye akamshauri atumie muziki wa Bongo Flava na wasanii wake kufikisha ujumbe.
“Kabla ya hapo, siyo huyu ofisa wala mtu yeyote kutoka kwenye asasi hiyo kule Marekani aliyekuwa akijua lolote kuhusu muziki wa Bongo Flava,” alisema Sugu.
Alisema aliandika mchanganuo na mpango mzima wa namna watakavyotekeleza na kupitishwa na bodi ya asasi hiyo yenye maskani yake Marekani.
Sugu amesema, akiwa katika matayarisho hayo mwaka jana, alilazimika kusitisha masomo yake ya elimu ya juu kwenye chuo alichokitaja kwa jina la Springfield, Massachussetts ili apate muda wa kushughulikia kampeni hiyo ya kutokomeza malaria.
“Kilichotushangaza sisi, baada ya mchakato wote kukamilika na wazo letu kukubalika na bodi ya asasi hiyo kwa miaka miwili, ghafla ulipofika muda muafaka wa kutekeleza mradi huu na kufanya uzinduzi tukajikuta tumeenguliwa,” alisema Sugu.
Mwandishi wa habari hizi alipomtafuta Mkurugenzi mmoja wa Tanzania House of Talent (THT), Rugemalira Mutahaba, alisema hawahusiki kwa lolote kuhusu mradi huo ila yeye alihusika kwa kutoa wasanii, vyombo vya muziki na kusema asihusishwe kwa lolote.
source nifahamishe
Wanafunzi Wasagana Mabwenini, Shule Yafungwa

Shule moja ya wasichana nchini Afrika Kusini imeyafunga mabweni yake na kuwalazimisha wanafunzi wote waondoke baada ya wanafunzi 27 wa shule hiyo kugundulika wanaendeleza tabia ya usagaji shuleni hapo.
Maafisa wa elimu wa nchini Afrika Kusini wanafanyia uchunguzi ripoti ya kufungwa kwa mabweni ya shule ya sekondari ya wasichana kutokana na tabia ya wanafunzi wa kike kusagana.
Wanafunzi wawili wa kike walikamatwa wakibusiana na wanafunzi wengine kadhaa inasemekana wako kwenye mahusiano ya jinsia moja.
Jumla ya wanafunzi 27 wamefukuzwa shule kutokana na tabia hiyo ya usagaji.
Watetezi wa haki za binadamu nchini Afrika Kusini wamekuja juu wakipinga uamuzi wa shule hiyo kwakuwa mahusiano ya jinsia moja yanaruhusiwa kisheria nchini Afrika Kusini.
Afrika Kusini ndio nchi pekee barani Afrika iliyoruhusu wasagaji na mashoga kujitawala kama katika nchi za barani ulaya na Amerika.
Wanafunzi waliofukuzwa shule katika shule hiyo iliyopo KwaZulu-Natal hawakutajwa majina yao kwa vyombo vya habari na jina la shule hiyo nalo liliwekwa kapuni.
Gazeti la The Star la nchini humo lilisema kwamba wanafunzi ambao walishindwa kurudi majumbani mwao walipewa hifadhi kwenye nyumba zilizo karibu na shule hiyo.
Msemaji wa kitengo cha elimu cha Afrika Kusini, Sihle Mlotshwa alinukuliwa na gazeti hilo pia akisema kuwa shule hiyo haina haki ya kuwafukuza au kuwasimamisha shule wanafunzi kwasababu ya masuala yao ya kijinsia.
source nifahamishe

Polisi nchini Marekani wanawatafuta wezi waliovamia duka moja la madini na vito vya thamani na kuiba kabla ya kukimbia na kumuacha mtoto wao.
Polisi wa Philadelphia nchini Marekani wanawatafuta wezi wawili walioiba vito vya thamani kwenye duka moja mjini humo kabla ya kukimbia na kumuacha mtoto wa kiume wa miaka minne.
Polisi walisema kuwa mwanaume na mwanamke waliingia kwenye duka la Platinum & Ice Jewelry wakiwa na mtoto na kuomba waonyeshe baadhi ya pete.
Ghafla wezi hao walichukua trei lililokuwa limejaa pete za dhahabu zenye thamani ya jumla ya dola laki moja na kukimbia nalo.
Wezi hao walimburuza mtoto huyo mita chache kabla ya kumtelekeza baada ya mmoja wa wafanyakazi wa duka hilo kuwakimbiza.
Polisi wanaendelea kuwatafuta wezi hao ambao walifanikiwa kutoweka eneo hilo na trei hilo la pete za dhahabu.
Mtoto wao amechukuliwa na kuhifadhiwa kwenye nyumba ya ustawi wa jamii.
source nifahamishe
