Noti za Plastiki Kuchukua Nafasi ya Noti za Karatasi

Monday, March 08, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Kidogo kidogo noti za karatasi zinaanza kutoweka duniani na nafasi yake inachukuliwa na noti za plastiki, Kanada imekuwa nchi ya nane duniani kubadilisha pesa zake na kuanza kutumia noti za plastiki.
Noti za karatasi kidogo kidogo zinaelekea kuwa historia na nafasi yake inachukuliwa na noti za plastiki ambazo hazipitishi maji hivyo hata ukizisahau kwenye nguo zako wakati wa kuzifua hazitapata madhara yoyote tofauti na noti za noti za karatasi ambazo huchanika kirahisi zinapolowa maji.

Kanada inakuwa nchi ya nane duniani kubadilisha noti zake na kuanza kutumia noti za plastiki. Kanada itaanza kuziondoa noti za karatasi kidogo kidogo kuanzia mwishoni mwa mwaka ujao.

Noti za plastiki zinatumia plastiki aina ya polymer biaxially-oriented polypropylene (BOPP) na zimeambatanishwa na vionjo vingine vya ulinzi ili kuzifanya noti hizo ziwe si rahisi kufojiwa.

Noti za plastiki hazichaniki wala kuharibika kirahisi hivyo kuziokoa pesa za serikali zinazotumika kuchapisha noti mpya kila baada ya muda.

Faida nyingine ya noti za plastiki ni kwamba hazibebi uchafu mwingi na bakteria kama zilivyo noti za karatasi. Mfano mzuri ni noti za dola ya Kimarekani asilimia kubwa ya noti hizo zina uchafu wa madawa ya kulevya kutokana na kutumiwa zaidi na wauzaji wa madawa ya kulevya.

Australia ndio iliyokuwa nchi ya kwanza kutumia noti za plastiki. Ilianza kutumia noti hizo tangia mwaka 1992.

Nchi zingine zinazotumia noti za plastiki ni Bermuda, Brunei, New Zealand, Papua New Guinea, Romania na Vietnam.

source nifahamishe

Mizimu Iliyowekwa Kwenye Vichupa Yapigwa Mnada

Monday, March 08, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mizimu miwili iliyokamatwa na kuingizwa kwenye chupa wanapigwa mnada kwenye internet na mamia ya watu wamejitokeza kuinunua mizimu hiyo.
Mwanamke wa nchini New Zealand, Avie Woodbury anawapiga mnada mizimu waliokuwa wakimsumbua kwenye nyumba yake ambao walikamatwa na mchungaji wa kanisa moja nchini humo na kuingizwa kwenye vichupa viwili vidogo.

Avie ameweka tangazo kwenye internet akivipiga mnada vichupa viwili ambavyo anasema vina mizimu iliyokuwa ikimsumbua kwa muda mrefu.

Avie alisema kuwa mizimu hiyo ilikamatwa na kuwekwa kwenye vichupa vidogo vyenye maji matakatifu.

"Maji matakatifu yanawafanya mizimu waishiwe nguvu na kuwafanya walale muda wote", alisema Avie.

Avie ameweka tangazo lake kwenye tovuti ya minada inayoitwa TradeMe. Hadi sasa dau kubwa alilopata ni paundi 1,000.

Avie amedai kuwa tangia mizimu hiyo ilipowekwa kwenye chupa mwezi julai mwaka jana hajapata usumbufu wowote kwenye nyumba yake kama ilivyokuwa zamani.

Mmoja wa mizimu hiyo anadaiwa kupenda kuviangusha vitu na kuzima na kuwasha vitu vya umeme. Mzimu mwingine unadaiwa kupenda kuwatisha watu.

Ili kuizindua mizimu hiyo Avie amesema kuwa ameambiwa kuwa ayamimine maji yaliyomo kwenye vichupa hivyo kwenye dishi na ayaache maji hayo yayeyuke ndani ya nyumba anayotaka mizimu hiyo ikae.

Chupa za mizimu hiyo zimewekewa majina maalumu ili wanunuzi wajue wanamnunua mzimu yupi.

Mnada wa mizimu hiyo umevuta watu wengi na umebakiza siku mbili kabla ya mshindi mwenye dau kubwa kuondoka na vichupa vyenye mizimu hiyo

source nifahamishe

http://www.nifahamishe.com/NewsImages/4193402.jpg

Monday, March 08, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mtoto aliyezaliwa kabla ya muda wake ambaye alikuwa mwepesi sana kiasi cha kwamba kopo dogo la cocacola lilikuwa zito kulinganisha na uzito wake, amemaliza minane akiwa hai pamoja na hofu ya madaktari kuwa asingeweza kuishi siku nyingi.
Mtoto huyo alizaliwa nchini Ujerumani akiwa na umbile dogo sana na uzito wa gramu 275 tu kiasi cha kwamba aliingia kwenye rekodi za kuwa mtoto wa kiume aliyezaliwa akiwa na uzito mdogo kuliko wote.

Kwa jinsi alivyokuwa na umbile dogo karatasi ya daftari yenye ukubwa wa A4 iliweza kumfunika kuanzia kichwani hadi miguuni.

Uzito wake ulikuwa ni robo tatu ya uzito wa kopo la Cocacola ambalo huwa na uzito wa gramu 350.

Awali madaktari walisema kuwa ni vigumu sana kwa mtoto anayezaliwa akiwa na uzito chini ya gramu 350 kuishi muda mrefu.

Lakini mtoto huyu amefanikiwa kumaliza miezi kadhaa akiwa hai kutokana na matunzo ya kitaalamu aliyokuwa akipewa.

Habari za kuzaliwa kwa mtoto huyo hazikutangazwa kutokana na hali mbaya ya kiafya aliyokuwa nayo wakati alipozaliwa.

Madaktari wameamua kutoa taarifa za kuzaliwa kwa mtoto huyo baada ya kuthibisha sasa kuwa afya yake imekuwa njema na maisha yake hayako hatarini tena.

Mtoto huyo alizaliwa mwezi juni mwaka jana wakati mimba ya mama yake ilipokuwa imetimiza wiki 25.

Alitumia miezi sita akipewa huduma maalumu hospitalini kabla ya wazazi wake kuruhusiwa kuondoka naye mwezi disemba mwaka jana wakati uzito wake ulipoongezeka na kufikia kilo 3.7.

Taarifa ilisema kuwa madaktari wa Ujerumani walizipitia rekodi za watoto wa kiume waliozaliwa kabla ya muda wao katika nchi mbali mbali duniani lakini hakupatikana mtoto hata mmoja aliyezaliwa akiwa na uzito mdogo kama wa mtoto huyo.

source nifahamishe

Makahaba 40,000 Kwenda Afrika Kusini Wakati wa Kombe la Dunia

Monday, March 08, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Makahaba wapatao 40,000 toka nchi mbalimbali duniani wanatarajiwa kuingia nchini Afrika Kusini wakati wa kombe la dunia litakalofanyika nchini humo baadae mwaka huu.
Wanawake wapatao 40,000 wanatarajiwa kuingia nchini Afrika Kusini kufanya kazi ya ukahaba wakati wa mwezi mmoja wa kombe la dunia ambalo litafanyika baadae mwaka huu nchini humo.

Afrika Kusini inaongeza ulinzi kwenye mipaka yake ili kuzuia wimbi hilo la makahaba ambao wengi wao wanatarajiwa kutoka nchi za ulaya mashariki.

Zaidi ya watu 450,000 toka nchi mbali mbali duniani wanatarajiwa kuingia nchini Afrika Kusini kwaajili ya kombe la dunia.

Akiongea katika kikao na umoja wa mataifa kuhusiana na vita dhidi ya madawa ya kulevya na uhalifu nchini humo, David Bayever, ambaye ni makamu mwenyekiti wa mamlaka ya kupambana na madawa ya kulevya nchini Afrika Kusini alisema kuwa maafisa wa Afrika Kusini wanahofia wimbi kubwa la wanawake wanaotarajiwa kuingia nchini humo kwaajili ya biashara ya ukahaba.

"Tumepewa taarifa na waandaaji wa kombe la dunia kuwa wamepata taarifa kuwa wanawake 40,000 wameajiriwa kuja kufanya ukahaba wakati wa kombe la dunia", alisema.

"Hali inatisha sana kutokana na kwamba asilimia 16 ya idadi ya watu wana maambukizi ya virusi vya ukimwi", alisema.

Bayever alisema kuwa wamehakikishiwa na idara ya uhamiaji kuwa ulinzi utaongezwa kwenye mipaka na ukaguzi wa pasport utaimarishwa.

source nifahamishe

Auliwa Kwasababu ya Picha Kwenye Facebook

Sunday, March 07, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanaume mwenye wivu aliyekuwa akiishi nchini Trinidad na Tobago alisafiri umbali mrefu hadi Uingereza na kumuua mpenzi wake baada ya kuona picha yake kwenye Facebook akiwa na mwanaume mwingine.
Paul Bristol, 25, alisafiri toka Trinidad and Tobago hadi Uingereza kumfuata mpenzi wake ambaye alipata mpenzi mwingine baada ya kufika Uingereza.

Paul alifanya safari hiyo kutokana na wivu aliokuwa nao baada ya kuona picha ya mpenzi wake huyo kwenye mtandao wa Facebook akiwa na mwanaume mwingine aliyemtambulisha kama mpenzi wake.

Paul alimuua kwa kumchoma choma na kisu Camille Mathurasingh, 27, ndani ya nyumba aliyokuwa akikaa mashariki mwa jiji la London.

Paul ambaye ni fundi wa vifaa vya umeme, alisafiri kwenda Uingereza ndani ya wiki mbili baada ya kuiona picha hiyo kwenye Facebook.

Paul amepandishwa kizimbani nchini Uingereza na alikanusha mashtaka ya mauaji aliyofunguliwa.

Mahakama iliambiwa kuwa Paul na Camille walikuwa wapenzi kwa miaka mitatu nchini Tobago lakini Camille alivyofika Uingereza alipata mpenzi mwingine na kuamua kuuvunja uhusiano wake na Paul kimya kimya.

"Inavyoonekana mpenzi wake alitaka kuuvunja uhusiano wao kimyakimya bila ya kumwambia kuwa amepata mpenzi mwingine", alisema mwendesha mashtaka wa kesi hiyo.

"Aligundua uhusiano wao baada ya kuziona picha zao kwenye Facebook".

Paul alikamatwa na polisi wakati alipokuwa akikimbia baada ya kufanya mauaji huku akiwa na damu usoni na kwenye nguo zake.

Hukumu ya Paul itatolewa baadae mwezi huu.

source nifahamishe.

Mwanamieleka wa Sumo Ainyofoa ATM na Kukimbia Nayo

Sunday, March 07, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanamieleka wa Sumo wa nchini Urusi ametiwa mbaroni baada ya kuinyofoa mashine ya kutolea fedha toka kwenye ukuta wa duka moja nchini humo na kisha kuibeba mabegani na kukimbia nayo.
Mwanamieleka wa mchezo wa Sumo wa nchini Urusi ametiwa mbaroni baada ya kuing'oa mashine ya kutolea fedha toka kwenye ukuta wa duka moja mjini Moscow na kisha kuanza kukimbia nayo.

Polisi wa nchini Urusi walisema kuwa mwanamieleka huyo baada ya kuing'oa mashine hiyo yenye uzito wa kilo 90, aliiweka mabegani na kuanza kukimbia nayo.

Polisi waliendelea kusema kuwa mwanamieleka huyo alifika kwenye eneo la tukio akiwa na wenzake wawili na kuing'oa mashine hiyo iliyokuwa na kiasi cha pesa za kirusi roubles 25,000 sawa na Tsh. Milioni 1.2.

Mfanyakazi wa duka hilo aliyeshuhudia tukio hilo alipiga simu kuwaita polisi ambao waliwahi kufika na kuwakamata washirika wawili wa mwanamieleka huyo.

Mwanamieleka huyo alikamatwa na kushikiliwa na polisi baada ya kukiri kosa lake

source nifahamishe

Polisi Mwanamke Mwenye Pepo la Ngono Asimamishwa Kazi

Sunday, March 07, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Afisa mmoja wa polisi mwanamke wa nchini Australia amesimamishwa kazi kutokana na usumbufu anaowapa maafisa wa polisi wa kiume kwa kuwabembeleza afanye nao mapenzi.
Afisa wa polisi Jessica Parfrey mwenye umri wa miaka 19, amesimamishwa kazi kutokana na usumbufu anaowapa maafisa wenzake wa kiume kwa kuwataka afanye nao mapenzi.

Ndani ya siku chache za kuanza kazi kama afisa wa polisi wa mjini Sydney nchini Australia, Jessica alimtongoza bosi wake akimwambia kuwa "Kila mtu anajua kuwa unatakiwa uwe na uhusiano wa kimapenzi na mfanyakazi mwenzako".

Mwezi mmoja baada ya kuona bosi wake hana dalili zozote za kukubali, Jessica alimfuata na kumwambia "Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 19, unaonaje tukifanya mapenzi tu, hivi wewe una matatizo gani?"

Mahakama ya mambo ya kazi iliambiwa pia kuwa Jessica alifanya mapenzi na afisa mwingine wa polisi kwenye choo cha baa.

Jessica hakuishia hapo, alimsumbua afisa mwingine mwanaume wa polisi kwa kumpigia simu mara 12 na kumtumia meseji sita kabla ya kumuahidi kumsaidia afisa huyo kwenye mtihani wake wa mambo ya polisi. Jessica alimwambia afisa huyo kuwa kwa kila swali moja atakalopata basi yeye atasaula nguo yake moja. Afisa huyo alikataa dili hilo.

Awali Jessica alisimamishwa kazi mwishoni mwa mwaka 2007 lakini alikata rufaa akisema kuwa matukio ya yeye kuwataka maafisa wenzake yalitokea wakati wakiwa baa nje ya muda wa kazi.

Mahakama ya kazi ya mjini Sydney ilitoa uamuzi wake juzi na kuitupilia mbali rufaa ya Jessica.

Mahakama hiyo iliunga mkono hukumu iliyotolewa awali ya kumfukuza kazi Jessica kwa kukiuka maadili ya kazi na kuwasumbua maafisa wenzake.

source nifahamishe