
Raia mmoja wa Marekani alijaribu kufanya kile ambacho serikali yake imeshindwa kukifanya kwa miaka kadhaa kwa kuamua kwenda peke yake nchini Afghanistan kumsaka na kumuua Osama bin Laden akiwa na bastola, panga na jambia.
Mmarekani Gary Brooks Faulkner mwenye umri wa miaka 52 ametiwa mbaroni nchini Pakistan akiwa kwenye misheni yake ya kumsaka na kumuua kiongozi wa Al-Qaeda, Osama bin Laden.
Faulkner alitiwa mbaroni jumapili jioni akiwa kwenye harakati za kuvuka mpaka wa Pakistan kuingia Afghanistan ili kukamilisha nia yake ya kumuua Osama ambaye inasemekana amejificha kwenye milima iliyopo kwenye mpaka wa Afghanistan na Pakistan.
Alikamatwa akiwa na bastola moja, panga, jambia na vifaa vya kumwezesha kuona nyakati za usiku. Pia alikuwa na kitabu alichoandika mistari aliyoinukuu toka kwenye biblia.
Faulkner ambaye amebatizwa jina la "American Ninja" na magazeti ya Marekani anasumbuliwa na matatizo ya figo na shinikizo la damu, alikuwa amebeba dawa zake wakati wa safari yake hiyo ya kumsaka Osama.
Faulkner aliwasili nchini Pakistan juni 2 mwaka huu kama mtalii toka California, Marekani. Alipewa mlinzi wa kuongozana naye wakati wa utalii wake lakini alitoweka ghafla jumatatu ya wiki iliyopita na kuwafanya polisi waanze msako wa kumtafuta.
Alikutwa kwenye misitu iliyopo kilomita chache toka mpakani karibu na mji wa Nuristan wa nchini Afghanistan ambao unasemekana ni ngome ya Taliban nchini Afghanistan.
Faulkner aliwaambia polisi kuwa alikuwa kwenye misheni ya kumsaka na kumuua Osama bin Laden.
Alipoulizwa kama anafikiria ana uwezo wa kumkamata Osama, Faulkner aliwaambia polisi "Mungu yuko pamoja nami, nina imani nitamuua Osama bin Laden".
Faulkner aliwaambia polisi kuwa aliamua kwenda mwenyewe kumuua Osama baada ya kuchukizwa na shambulizi la kigaidi la septemba 11, 2001.
Serikali ya Marekani imekuwa ikimsaka Osama bin Laden kwa matukio ya kigaidi duniani na kichwa cha Osama bin Laden kimetengewa zawadi ya dola milioni 25 kwa mtu atakayetoa taarifa za kufanikisha kukamatwa kwake.
source nifahamishe
Sanamu la Yesu Lapigwa na Radi, Lateketea Kwa Moto

Sanamu kubwa sana la Yesu lilikowa likijulikana kama 'Mfalme wa Wafalme' ambalo lilikuwa kivutio kikubwa cha watalii mjini Ohio nchini Marekani limepigwa na radi na kuteketea kwa moto.
Sanamu hilo maarufu lenye urefu wa mita 19 na upana wa mita 12 liliteketea kwa moto baada ya kupigwa na radi jumatatu usiku, taarifa ya polisi ilisema.
Sanamu hilo lililokuwa likijulikana kama "King of Kings" lilikuwa ni miongoni mwa vivutio vya watalii kusini magharibi mwa Ohio kuanzia mwaka 2004 lilipowekwa pembeni ya barabara ya kuu inayokatiza mbele ya kanisa la Kianglikana Monroe.
Taarifa ya polisi ilisema kuwa sanamu hilo liliteketea kwa moto jumatatu usiku kabla ya moto huo kudhibitiwa na maafisa wa zimamoto. Hakuna aliyejeruhiwa katika tukio hilo.
Sanamu hilo liligharimu dola 250,000 kulitengeneza na kutokana na ukubwa wake watu wengi wanaopita kwenye barabara ya Interstate 75 walikuwa wakisimama kwa muda mbele ya kanisa ili kupata taswira za sanamu hilo.
source nifahamishe
Zawadi ya Kiongozi Bora Afrika Yakosa Mshindi

Kwa mwaka wa pili mfululizo mshindi hajapatikana kwaajili ya zawadi ya dola milioni 5 ya kiongozi bora wa Afrika ambaye ameonyesha mfano wa uadilifu katika uongozi na serikali ya kidemokrasia.
Wadhamini wa tuzo ya kiongozi bora wa Afrika wamesema kuwa mwaka huu pia wameshindwa kumpata kiongozi wa nchi aliyeonyesha mfano wa uongozi bora na serikali ya kidemokrasia.
Washindi wa tuzo ya kiongozi bora wa Afrika hupewa zawadi ya dola milioni 5 ndani ya kipindi cha miaka 10 na baada ya miaka 10 kuisha hupewa dola laki mbili kila mwaka kwa miaka yote ya maisha yao iliyobaki.
Mo Ibrahim, mfanyabiashara bilionea aliyezaliwa nchini Sudan ndiye aliyeanzisha tuzo hizo mwaka 2006 ili kuwapa moyo viongozi wa Afrika kuongoza serikali zao kwa misingi bora ya uongozi.
Kamati huru ya watu saba ikiongozwa na katibu mstaafu wa umoja wa mataifa, Kofi Annan, ilikutana tena jumamosi lakini ilishindwa kumchagua mshindi.
Kamati hiyo pia mwaka jana ilishindwa kumchagua kiongozi yoyote wa Afrika kushinda tuzo hiyo.
Tuzo hiyo hutolewa kwa viongozi wa Afrika waliochaguliwa kidemokrasia ambao wameachia madaraka ndani ya miaka mitatu iliyopita.
"Sifa za viongozi bora zilizowekwa ziko juu na kila mwaka idadi ndogo ya viongozi wenye sifa hupatikana. Kwahiyo kuna uwezekano miaka mingine hatapatikana mshindi", alisema Mo Ibrahim.
Hadi sasa ni viongozi wawili tu wa Afrika ambao wamezawadia tuzo hiyo, rais mstaafu wa Botwana, Festus Mogae na rais mstaafu wa Msumbiji, Joaquim Chissano. Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela alipewa tuzo maalumu ya heshima mwaka 2007.
source nifahamishe
Watoto Wafariki Wakati Baba na Mama Wakiangalia Kombe la Dunia

Watoto wawili wamefariki dunia nchini Uganda kutokana na moto ulioitekeza nyumba yao wakati wazazi wao walipoenda kwa jirani mwenye televisheni kuangalia kombe la dunia.
Polisi mjini Kampala nchini Uganda wamesema kuwa watoto wawili wamefariki kutokana na moto ulioitekeza nyumba yao wakati wazazi wao walipoenda kuangalia mechi ya kombe la dunia.
Polisi nchini Uganda wamewaonya wazazi kutowaacha watoto wao peke yao ndani ya nyumba wakati wanapoenda kuangalia mechi za kombe la dunia.
Watoto wawili wenye umri wa miaka 8 na 10 walifariki kwa moto katika wilaya ya Kayunga iliyopo magharibi mwa mji wa Kampala.
Afisa wa polisi wa Kayunga, Henry Kolyanga alisema kuwa watoto hao walifariki wakati nyumba waliyokuwa wamelala iliposhika moto.
"Mama na Baba wa watoto hao waliacha mshumaa ukiwaka ndani ya nyumba na walienda kuangalia mechi ya kombe la dunia kwa jirani mwenye televisheni", alisema afisa huyo wa polisi.
"Inasemekana kuwa panya aliugonga mshumaa na mshumaa huo uliangukia kwenye meza na kukiunguza kitambaa cha mezani na kusababisha moto mkubwa ulioitekeza nyumba yote", alimalizia kusema afisa huyo wa polisi.
source nifahamishe
Miaka 10 Jela Kwa Kumuua Dada Yake Aliyepata Mimba Nje ya Ndoa

Mahakama nchini Jordan imemuondolea adhabu ya kifo aliyohukumiwa mwanaume aliyemuua dada yake baada ya kugundua amepata mimba kabla ya kuolewa. Mahakama imeamuru mwanaume huyo atumikie kifungo cha miaka 10 jela.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 24 alimuua dada yake mwenye umri wa miaka 26 kwa kumchomachoma na kisu tumboni mara 15 baada ya kugundua dada yake huyo amepata ujauzito kabla ya kuolewa.
Awali mahakama ya mjini Amman, Jordan iliamuru mwanaume huyo ahukumiwe adhabu ya kifo lakini jana mahakama iliamuru mwanaume huyo atumikie kifungo cha miaka 10 jela baada ya familia yake kumuombea msamaha mahakamani.
"Alimuua dada yake baada ya dada yake huyo kumwambia kuwa alifanya mapenzi na mwanaume ambaye alisafiri kwenda kufanya kazi nchini Saudi Arabia", alisema afisa wa mahakama ambaye hakutaka kutaja jina lake.
Taarifa ya mahakama ilisema kuwa mauaji hayo yalifanyika mwaka jana katika mji wa Karak wakati huo dada yake alikuwa na mimba ya wiki nne.
Kwa mujibu wa sheria za Jordan, mtu anayeua naye huuliwa lakini kwa mauaji yanayoitwa "Kulinda Heshima ya Familia" adhabu ya kifo huondolewa iwapo familia ya mwanamke aliyeuliwa itaiomba mahakama ipunguze adhabu kwa muuaji.
Wanawake 15 hadi 20 huuliwa kila mwaka nchini Jordan kwa staili hiyo hiyo ya kulinda heshima za familia ingawa serikali ya Jordan inafanya jitihada ya kuiondoa tamaduni hiyo potofu.
source nifahamishe
Marekani Yagundua Hazina ya Utajiri Afghanistan

Marekani imegundua hazina ya madini yenye thamani kubwa nchini Afghanistan ambayo yanakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya dola trilioni moja.
Msemaji wa Pentagon alisema kuwa utafiti wa wataalamu wa madini wa Marekani umeonyesha kuwa nchini Afghanistan kuna kiasi kikubwa sana cha madini ya thamani tofauti na ilivyokuwa ikijulikana awali.
Thamani ya madini kama vile niobium, lithium, chuma, dhahabu na kobalti ambayo yanapatikana kwa kiasi kikubwa nchini Afghanistan ni zaidi ya dola trilioni moja.
Maafisa wa Marekani waliliambia gazeti la New York Times la Marekani kuwa hazina ya madini yaliyopatikana nchini Afghanistan yanatosha kuubadilisha uchumi wa Afghanistan na kuigeuza Afghanistan kuwa mojawapo ya nchi zinazoongoza kwa uzalishaji wa madini duniani.
Rais wa Afghanistan, Hamid Karzai alisema mwanzoni mwa mwaka huu kuwa kiasi kikubwa cha madini kilichogunduliwa nchini humo kitaifanya Afghanistan itoke kwenye umaskini iwe miongoni mwa nchi tajiri duniani.
Aozeshwa Ng'ombe Aliyembaka, Azimia Wakati wa Harusi

Kijana mmoja wa nchini Indonesia ambaye alilazimishwa kumuoa ng'ombe aliyembaka, alizimia wakati wa harusi yake na ng'ombe huyo.
Kijana Ngurah Alit mwenye umri wa miaka 18 alikamatwa kwenye kijiji chake cha Yeh Embang katika kisiwa cha Bali nchini Indonesia, akiwa uchi wa mnyama akifanya mapenzi na ng'ombe.
Alit alijitetea kuwa ng'ombe huyo ndiye aliyemtongoza yeye na kumvutia kufanya naye mapenzi.
Alit alidai kuwa aliamini kuwa ng'ombe huyo alikuwa ni msichana mrembo ambaye alikuwa akimfanyia mitego mbalimbali ili afanye naye mapenzi.
Pamoja na utetezi wake, Alit alilazimishwa amuoe ng'ombe huyo na harusi ya kitamaduni iliandaliwa.
Wakati polisi wakiwaweka waandishi wa habari mbali na eneo la harusi, Alit alizimia kabla ya kukabidhiwa rasmi 'mke' wake.
Hata hivyo Alit aligeuka mjane punde baada ya harusi baada ya bi harusi wake kuzamishwa kwenye bahari kama mojawapo ya imani za kijiji hicho.
Ili kusafishika na kitendo chake, Alit aliogeshwa kwenye ufukwe wa bahari.
Mkuu wa kijiji hicho alisema baada ya harusi hiyo kuwa kijiji sasa kimesafishika baada ya tukio hilo lililoleta aibu kwenye kijiji.
source nifahamishe
