Mwanamke mmoja mwenye wivu sana wa nchini Marekani amefikishwa mahakamani baada ya kuzichoma moto sehemu za siri za mpenzi wake baada ya kushuku kuwa mpenzi wake huyo ana kimada nje.
Victoria Bynes mwenye umri wa miaka 29, wa Florida nchini Marekani alichukua mafuta ya petroli na kumwagia kwenye sehemu za siri za mpenzi wake kabla ya kutumia kiberiti kuwasha moto uliozitekeza sehemu nyeti za mpenzi wake.
Wakati mpenzi wake, Andrew Williams akihangaika kuuzima moto uliokuwa ukizitekeza sehemu zake muhimu za kiume, Victoria alipanda kwenye gari lake na kuondoka bila ya kutoa msaada.
Wakati polisi walipofika walimkuta Andrew akiwa ameungua vibaya sehemu zake za siri pamoja sehemu za tumbo lake.
Sababu ya Victoria kuzichoma moto nyeti za mpenzi wake ni kumshuku kuwa ana mwanamke mwingine kwakuwa alishindwa kuwasiliana naye kwa muda wa wiki moja.
Majirani walisema kuwa Victoria alifika kwenye nyumba ya Andrew na punde walianza kulumbana kwa sauti.
Wakati wa malumbano hayo, Victoria aliitikisa chupa yenye mafuta ya petrol aliyokuja nayo na kumwagia mpenzi wake kwenye sehemu zake nyeti na kisha kuwasha moto kwa kutumia kiberiti alichokuja nacho.
Victoria akijitetea alisema kuwa alizipiga moto nyeti za mpenzi wake kwa bahati mbaya kwakuwa lengo lake lilikuwa ni kumtishia kuzichoma moto nyeti zake.
Victoria aliachiwa huru kwa dhamana ya dola 10,000 wakati uchunguzi wa kesi hiyo ukiendelea.
Andrew bado amelazwa hospitali akipatiwa matibabu kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata kwenye nyeti zake na tumboni.
Tukio hili limetokea ikiwa ni mwezi mmoja tu baada ya mwanamke mwingine naye wa Florida, kuzichoma moto sehemu za siri za mpenzi wake, baada ya kutokea mzozo kati yao.
Berlinda Dixon-Newbold alitiwa mbaroni mwezi disemba mwaka jana kwa kuzichoma moto sehemu za siri za mpenzi wake Sheldon Gonzales.
Katika tukio jingine huko huko Marekani katika jimbo la Kansas, Mwanamke mwenye umri wa miaka 42, alimpiga risasi kwenye sehemu za siri mumewe mwenye umri wa miaka 50 kutokana na malumbano ya ndani ya nyumba.
Mwanamke huyo bado anashikiliwa na polisi kwa kitendo chake hicho.
source nifahamishe
Azichoma Moto Sehemu za Siri za Mpenzi Kwa Kumhisi Anatembea Nje
Watanzania! nini kinaendeleaa........katika starehe?
kwanini watu wamezama sana kwenye burdani siku hizi, je unafikiri nini kuhusiana na hili swala? behind of the scene kuna jambo kubwa sana limejificha, wape starehe wajisahau waibie. Hili liliwakuta ndugu zetu kule Zaire enzi za Mabutu na sasa lipo hapa nyumbani, Watanzania hawajafikia uchumi wa nchi za magharibi ambapo mtu anaweza kuishi bila wasiwasi hata kama hafanyi kazi kwa maisha yake yote, na kila unapokuwa na familia kumbwa ndio maisha yako yanakuwa mazuri, utalipwa hela nyingi na kupatiwa nyumba kubwa zaidi. huhitajiki kufanya kazi. yote haya yalipatikana kwa kuiba kutoka nchi zetu changa na kupeleka uchumi wetu kwao.
Kwa kuwa baada ya uhuru unawawia vigumu kuiba kati scale ile kabla ya uhuru sasa wanakuja na staili nyengine ili kuwafanya raia wao kuishi maisha yale yale waliyozoea, hasa baada yauchumi wao na dunia kuharibika, wajitahidi kuja na mtindo wa investiment huku wakuchukua pesa kwa njia ya hisa, ili wakubane na wewe wanaweka starehe ili wewe waliyekutuma uwafanyie kazi yao uendelee kulipia kile kidogo eti unajiburudisha ili nacho wakichukue, hebu chuku mfano wewe unafanya kazi kati benki mojawapo hapo mjini mbayo inamilikiwa na hao tuliokuwa tunawaita wakoloni, wakisha kulipa mshahara wako wanugawa kati mafungu mbalimbali, mahitaji muhimu na yasio muhimu, chukulia wewe ni kujibajeti 50%/50%.
Ikifika weekend unajifanya unatoka na familia au rafiki zako kwenda kutumia, utaagiza chakula na vinywaji, wamiliki wa kampuni za vinywaji ni hao wakoloni na sasa wao wanaagiza chakula wanachokupikia toka kwao wewe unanunua kwa bei mbaya mwisho wa mwezi nusu au zaidi yamshara wako inakwenda kwao.
Je nani hapo ataendelea kuwa na maisha mazuri? vitu vingi tunavyonunua havitoki nchini kwetu je nani anatajirika, jiulize kuanzia leo kwanini wewe Mtanzania usitumie hizo pesa za ziada kuwekeza nchini kwako kama vile kilimo au ujenzi wa nyumba ukawapangisha hao wanajiita investors?
weka akiba na earn interest uone kama wataendelea kuwekeza kama wakiona hawapati kile wanachotaka, sisemi kuwa usiende kwenye starehe, jaribu sana kuangalia starehe ipi inakunufasha wewe kama Mtanzania na sio hao wengine.
Tusibweteke na starehe tunazozifanya hivi sasa tunatakiwa tufikiri sana kuhusu mustakabali wa maisha yetu sasa na vizazi vyetu baadae, Ndio maana hivi sasa watu wanashindana kuiba toka serikalini na kwengine ili kuwa nakiwango kikubwa cha akiba nje ya nchi. ndio maana watu hivi sasa wanadai madai ya katiba mpya, hili litasaidia katika uchumi wetu na sio tu kwenye siasa.
Wakoloni baada ya research ya muda mrefu wamekuja na falsafa mpya - ukitaka kumwibia Mwafrika mpe starehe, ukitaka kumuibia Mwarabu - mtishe, Ukitaka kumwibia Muhindi - invest katika sekta ya mawasiliano na sio heavy industry maana atacopy na kuanzisha yake nawe utabaki huna kitu, ukitaka kumuibia muasia kama vile Mchina Mkorea na Mjapani - Invest katika viwanda na wagomanishe ukijifanya unawalinda lakini hili walikosea kwa Mchina na wanajuta hivi sasa lakini walipatia kwa Korea na Japani.
Ndugu zangu Watanzania umefika wakati Tunatakiwa tufikirie mara mbili badala ya kujiingiza katiaka starehe kama hizo za kamari (Casino) nani anafaidika? kwanini baadhi ya watu nchini Marekani na Ulaya wamepigwa marufuku kucheza kamari?
Umefika wakati tusikubali kuibiwa kwa starehe hewa ukiamka huna kitu, mna elimu yakutosha kupambua lipi baya na zuri, wekezeni katika nchi yenu na saidianeni mafanikio yatapatikana, Ni matumaini yangu Mhariri utayapokea na kuwafikishia Watanzania wenzangu kuhusu hili, nitaendelea kuandika makala haya kwa urefu pindi ukinipa nafasi japo mara moja kwa mwezi katika makala maalumu.
source globalpublishers
11 Wafariki Wakisherehekea Mwaka Mpya Nigeria

Zaidi ya watu 11 wamefariki dunia nchini Nigeria kufuatia bomu kubwa lililolipuka kwenye baa wakati watu wakisherehekea mwaka mpya.
Zaidi ya watu 11 wamefariki dunia kufuatia bomu kubwa lililolipuka kwenye baa iliyopo karibu na kambi ya jeshi iliyopo karibu na ikulu mjini Abuja.
Eneo hilo lilikuwa likisemekana kuwa ndilo lenye usalama kuliko maeneo yote ya mji wa Abuja.
Wakati wa krismasi wiki iliyopita zaidi ya watu 80 walifariki dunia nchini Nigeria kutokana na milipuko ya mabomu katika mji wa Jos ambao umekumbwa na chuki ya kidini kati ya waislamu na wakristo.
Katika bomu lililotokea mkesha wa mwaka mpya, inakadariwa kuwa watu 30 wamepoteza maisha yao ingawa taarifa ya polisi ilithibitisha vifo vya watu 11.
Bomu hilo lilitokea muda mfupi kabla ya mwaka mpya wakati watu wakiwa wanajiburudisha baa wakisubiri kusherehekea mwaka mpya 2011.
Waziri wa ulinzi wa Nigeria amewataka watu wadumishe utulivu wakati uchunguzi mkali ukiendelea kuhusiana na milipuko ya mabomu ambayo imekuwa ikiiandama Nigeria siku za karibuni.
source nifahamishe
Auanza Mwaka Mpya Vibaya Kwa Operesheni ya Kuongeza Makalio

Mwanamke mmoja wa nchini Marekani ambaye alitaka kuingia mwaka 2011 akiwa mrembo zaidi na mwenye makalio makubwa amefariki dunia masaa matatu baada ya kufanyiwa operesheni ya kuongeza makalio.
Mwaka 2011 umeanza vibaya kwa bwana Osvaldo Vargas mkazi wa Florida, Marekani, Amempoteza mke wake ambaye operesheni ya kuongeza urembo na makalio ili aonekane mrembo zaidi mwaka 2011 ilimalizika vibaya na kupelekea kifo chake.
Lidvian Zelaya mwenye umri wa miaka 35 alitaka kuingia mwaka 2011 akiwa mrembo zaidi kwa kuamua kufanya operesheni ya kutoa nyama nyama na mafuta toka kwenye tumbo lake na kuzihamishia kwenye makalio yake ili kuyafanya yawe makubwa zaidi.
Masaa matatu baada ya operesheni hiyo, Lidvian aliwahishwa hospitali akiwa amezidiwa sana na wakati mume wake anawasili hospitali Lidvian alikuwa ameishafariki dunia.
"Amefariki akitafuta urembo, kwangu mimi alikuwa tayari ni mrembo", alisema mume wa Lidvian kwa huzuni.
"Alikuwa ni mrembo, mwenye furaha na aliyependa kudansi, nataka kujua nini kimetokea", alisema bwana Oswaldo wakati akiongea na waandishi wa habari.
"Hatumlaumu yeyote lakini tunataka kujua nini kimesababisha kifo chake", alisema Oswaldo akiwa pamoja na mwanasheria wake.
Lidvian alifanyiwa operesheni kwenye kliniki ya Strax Rejuvenation, ya Florida, hata hivyo kliniki hiyo imesema kuwa sheria zinawabana kusema chochote kuhusiana na kifo cha Lidvian.
source nifahamishe
Babu wa Miaka 83 Amuua Mkewe Kwa Kumshindilia Bisibisi Kichwani
Babu mwanablogu mzee wa nchini Taiwan mwenye umri wa miaka 83 amemuua mkewe mwenye umri wa miaka 80 kwa kumshindilia bisibisi kichwani na kisha kuweka maelezo jinsi alivyofanya mauaji hayo kwenye blogu yake.
Babu Wang Ching-hsi mwenye umri wa miaka 83 wa nchini Taiwan kutokana na huruma yake aliamua kuyamaliza maisha ya mkewe mgonjwa wa kansa kwa kuizamisha bisibisi kwenye kichwa chake.
Kabla ya kufanya mauaji hayo, Babu Wang aliandika kwenye blogu yake kuwa hali ya mkewe imezidi kuwa mbaya na amepoteza hamu ya kuendelea kuishi duniani.
Babu Wang alimpa mkewe dawa za usingi na alipopitiwa na usingizi alimuua kwa kuizamisha bisibisi kwenye fuvu lake la kichwa.
Kwa mujibu wa magazeti ya Taiwan, Wang alipiga simu polisi kuwapa taarifa kuwa amemuua mkewe na alikaa nje ya nyumba yake akiwasubiri polisi wafike.
"Kwanini nimemuua mke wangu?, majibu yote yapo kwenye blogu yangu", alisema Wang akiwaambia waandishi wa habari wakati akiingizwa kwenye karandinga la polisi.
Kwa mujibu wa taarifa zilitolewa, Wang alikubaliana na mkewe miaka kumi iliyopita kuwa kila mmoja wao afariki kwa amani muda utakapofika.
Katika makubaliano hayo, Wang alimwambia mkewe, "Muda utakapofika nitakuua".
Kumekuwa na mjadala mkubwa nchini Taiwan kuhusiana na haki ya mtu aliyechoka kuishi kusitisha maisha yake.
Mwezi juni mwaka huu, baraza la kutunga sheria la Taiwan lilipitisha sheria ya kuwaruhusu wagonjwa na ndugu wa mgonjwa aliyekuwa mahututi kwa magonjwa yaliyofikia kikomo, kusitisha kuwapa dawa au huduma za kurefusha maisha yao ili kuwaepusha na mateso wanayopata.
source nifahamishe
Jela Miaka Mitano Kwa Kusoma Email ya Mkewe

Mwanaume mmoja wa nchini Marekani ambaye alifungua email ya mkewe na kugundua kuwa mkewe alikuwa akifanya mapenzi nje ya ndoa, anakabiliwa na kifungo cha miaka mitano jela.
Leon Walker mwenye umri wa miaka 33 mkazi wa Michigan nchini Marekani anakabiliwa na kifungo cha miaka mitano jela kwa kufungua na kusoma email za mkewe.
Leon alifungua email ya mkewe, Clara Walker, kwa kutumia kompyuta waliyokuwa wakiitumia pamoja nyumbani kwao.
Kwa kutumia password yake, Leon alifungua akaunti ya Gmail ya mkewe na alisoma email zake ambapo aligundua kuwa mkewe alikuwa akitembea nje ya ndoa.
Mkewe alikasirika baada ya siri hiyo kufichuka na aliamua kufungua kesi ya madai ya talaka ambapo pia alimfungulia Leon mashtaka ya kusoma email zake.
"Hii ni kesi ya kustaajabisha, hakuna sheria inayoweka wazi suala kama hili", alisema mwanasheria Frederick Lane.
Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa hii ni mara ya kwanza sheria dhidi ya wizi wa nyaraka za siri kwenye masuala ya kibiashara inatumika kwenye masuala ya kifamilia.
Baadhi ya wanasheria wanasema kuwa huenda Leon akahukumiwa kwenda jela miaka mitano iwapo atapatikana na hatia ya kutumia password ya mkewe kusoma email zake.
Leon akiongea na waandishi wa habari alisema kuwa alichungulia email za mkewe ili aweze kujua chanzo cha mkewe kuwatelekeza watoto wao.
Kesi ya Leon itaanza kusikilizwa februari 7 mwakani.
source nifahamishe
