
Wakati China ikiendeleza kuombeleza vifo vya mamia ya watu kutokana na mafuriko na maporomoko ya udongo, mwanamke mmoja nchini humo amejaribu kujiua kwa kujirusha toka ghorofa ya 11 huku akiwa uchi wa mnyama.
Kufuatia mzozo na mumewe, mwanamke mmoja wa nchini China alijaribu kusitisha maisha yake kwa kujirusha toka ghorofa ya 11.
Katika tukio hilo lililotokea kwenye jimbo la Anhui nchini humo, mwanamke huyo alisababisha kizaazaa baada ya kuvua nguo zake zote na kupanda kwenye dirisha la nyumba iliyopo ghorofa ya 11 na kutishia kujiua kwa kujirusha chini.
Pamoja na jitihada za zimamoto na majirani kumsihi asijirushe, mwanamke huyo aliamua kujirusha ili kuhitimisha maisha yake.
Hata hivyo maisha ya mwanamke huyo yalinusurika baada ya kuangukia kwenye boya lililowekwa chini na zimamoto. Aliwahishwa hospitali kwa uchunguzi na matibabu zaidi.
Iligundulika kuwa sababu ya mwanamke kujaribu kujiua ni mzozo uliotokea usiku wa siku moja kabla ya tukio hilo.
source nifahamishe

Msichana mmoja wa nchini Hungary ambaye aliinadi bikira yake kwenye mtandao ili apate pesa za kuisaidia familia yake, amepata mteja ambaye ameinunua bikira yake sawa na Tsh. Milioni 500.
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 19 anayejiita "Miss Spring" ameamua kuiuza bikira yake kwa mwanaume raia wa Uingereza ambaye atatoa paundi 200,000.
Msichana huyo alisema kuwa aliamua kuiuza bikira yake ili aweze kulipia gharama za masomo yake na pia aweze kulipa madeni ya mama yake.
"Familia yangu ina madeni na hatuwezi kuyalipa, mama yangu alikopa pesa ambazo alishindwa kuzilipa na kupelekea tupoteze nyumba yetu, nataka nilipe madeni yote", alisema msichana huyo.
"Pesa nilizopata sio nyingi sana kwani nitapoteza nusu yake kwenye kodi", aliongeza msichana huyo.
Msichana huyo alisema kuwa anajiandaa kwenda Uingereza ili aweze kumtunuku bikira yake mdau aliyetoa dau kubwa kuliko wote.
Mnada wa bikira ya msichana huyo ulianzia kwenye mtandao wa Ebay lakini ulimalizikia kwa njia ya email baada ya Ebay kuufutilia mbali mnada huo baada ya kugundua unahusisha uuzaji wa mapenzi.
"Nilikuwa nikiwasiliana na washindi wawili, mmoja raia wa Uingereza na mwingine raia wa Ireland, nimemchagua mwanaume wa Uingereza".
"Wote wanataka kunioa na kuitunza familia yangu lakini kwa sasa sifikirii kuishi maisha ya ndoa", alisema msichana huyo.
source nifahamishe
Nyota wa Uingereza Amhonga Kahaba Paundi 800 Kwa Usiku Mmoja

Nyota wa Uingereza na timu ya Tottenham Hotspurs, Peter Crouch ameingia kwenye skendo kubwa sana baada ya kumsaliti mchumba wake na kumhonga kahaba paundi 800(Takribani Tsh. Milioni 1.8) kwa usiku mmoja.
Peter Crouch alikuwa kwenye vakesheni nchini Hispania pamoja na mchumba wake mwanamitindo, Abbey Clancy.
Siku mbili baada ya kumaliza vakesheni yake, Crouch alishindwa kujizuia kumsaliti mchumba wake kwa kununua penzi toka kwa kahaba mwenye umri wa miaka 19, anayejiita Monica Mint.
Crouch alimhonga kahaba huyo, paundi 800 ili afanye naye mapenzi mara mbili ndani ya usiku mmoja, mara moja kwenye taksi na baadae hotelini kwake.
Akitoboa siri ya tukio hilo, Monica aliliambia gazeti la News of the World la Uingereza kuwa Crouch hakujivunga hata kidogo kununua penzi lake kwa kiasi kikubwa cha pesa.
"Hakuhofia watu kutuona nyuma ya taksi, alisisitiza tufanye mapenzi ndani ya taksi wakati tukielekea hotelini", alisema Monica.
"Nilikuwa sijui kuwa ana mchumba, bado siamini amenunua penzi langu wakati ana mwanamke mrembo amemuacha nyumbani kwake", alimalizia kusema Monica.
source nifahamishe
Waziri Amla Uroda Malkia, Kuhukumiwa Adhabu ya Kifo

Waziri wa Sheria na rafiki wa karibu wa Mfalme Mswati wa Swaziland ametupwa jela na anakabiliwa na adhabu ya kifo baada ya kumla uroda mmoja wa wake wa mfalme Mswati.
Chini ya amri ya mfalme Mswati, waziri wa sheria na rafiki wa karibu wa Mfalme Mswati, Ndumiso Mamba ametupwa jela baada ya kukamatwa kitandani hotelini akimla uroda malkia wake, Nothando Dube, ambaye ni mke wa 12 wa mfalme huyo wa Swaziland.
Malkia Nothando Dube mwenye umri wa miaka 22 amewekwa ya chini ulinzi mkali nyumbani kwa mama mkwe wake huku waziri huyo mkware akiendelea kunyea debe jela.
Waziri Mamba alikamatwa na polisi kitandani akijivinjari na malkia wake kwenye hoteli ya Royal Villas mjini Mbabane.
Wadadisi wa masuala ya kisiasa nchini Swaziland walidai kwamba uhusiano wa kimapenzi kati ya malkia na waziri huyo ulikuwa ukijulikana sana kilichobaki watu walikuwa wakisubiri ushahidi.
Mamba huenda akahukumiwa adhabu ya kifo iwapo atapatikana na hatia.
Mfalme Mswati yuko nchini Taiwan kwa ziara ya kiserikali.
Dube ambaye amezaa watoto wawili na mfalme Mswati aliolewa na Mfalme Mswati akiwa na umri wa miaka 16 baada ya kuonekana kwenye dansi maalumu la kila mwaka la wasichana bikira ambapo wasichana hupita wakiwa wameacha matiti yao nje huku mfalme akijichagulia yupi amuongeze kwenye himaya zake.
Dube huenda akafukuzwa toka kwenye himaya za kifalme iwapo atapatikana na hatia.
source nifahamishe

Mwalimu mmoja nchini Uingereza ameacha kazi yake ya ualimu wa sekondari na kuamua kuanza kazi mpya ya usanii wa filamu za ngono huku akitumiwa salamu za kutakiwa mafanikio na wanafunzi wake walioziona filamu zake kwenye internet.
Liselle Bailey mwenye umri wa miaka 30 aliacha kazi yake ya ualimu wa sekondari na kuanza kazi mpya kucheza na kuongoza filamu za ngono.
Wanafunzi wa mwalimu huyo waliobahatika kuona filamu zake kwenye internet walipigwa na butwaa lakini hawakusita kumtumia salamu za kumtakia mafanikio kwenye kazi yake hiyo mpya.
Mmoja wa wanafunzi wake aliyeitwa Daniel aliandika "Mwalimu Bailey tunakupenda, nakutakia mafanikio kwenye kazi yako mpya".
Mwanafunzi mwingine aliandika maoni kwenye internet "Mwalimu bora wa kiingereza, umepata kazi bora kuliko zote, hongera".
Mwalimu Bailey alikuwa akifundisha somo la kiingereza na somo la maigizo kwenye shule ya seminari ya Grindon Hall.
"Huu ulikuwa ni uamuzi wangu wa busara", alisema Bailey na kuongeza kuwa katika mwaka mmoja wa fani yake hiyo mpya ameweza kuwa nyota wa kampuni ya Joybear Pictures.
source nifahamishe

Mwanamuziki maarufu duniani wa muziki wa Hip Hop, wa kundi la Fugees, Wycleaf Jean amejitosa kwenye siasa na atagombea urais wa Haiti katika uchaguzi utakaofanyika novemba.
Baada ya kutesa kwa muda mrefu katika anga ya muziki wa hip hop na miondoko reggae, nyota wa kundi la Fugees la Marekani, Wycleaf Jean ameamua kujitosa kwenye masuala ya siasa na atakuwa miongoni mwa wagombea urais.
Wycleaf ambaye alizaliwa nchini Haiti amesema kuwa atatangaza rasmi kugombea wa urais wa Haiti kesho alhamisi kupitia televisheni ya CNN kwenye kipindi cha Larry King Live.
Uchaguzi wa Haiti utafanyika novemba 28 mwaka huu na rais wa sasa wa Haiti, Rene Preval, hataweza kugombea tena urais kutokana na kumaliza miongo yake kisheria.
Ili aweze aweze kugombea urais Wycleaf anakabiliwa na changamoto ya kuthibitisha kuwa ameishi nchini Haiti kwa miaka mitano na hana uraia wa nchi nyingine yoyote.
Wycleaf alizaliwa nje kidogo ya mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince, lakini alilelewa Brooklyn, New York nchini Marekani.
Wycleaf ana historia ndefu ya kujihusisha na masuala ya kisiasa nchini Haiti na alikuwa miongoni mwa watu walioshiriki kuandaa tamasha la kusaidia wahanga wa tetemeko kubwa la ardhi lililotokea mwezi januari mwaka huu na kuua maelfu ya watu.
source nifahamishe

Mwanamke wa nchini Iran ambaye kutokana na kufanya zinaa alihukumiwa kupigwa mawe hadi atakapofariki, amesema kuwa anaogopa kufariki na anaomba awakumbatie watoto wake kwa mara ya mwisho.
"Kila siku kabla ya kulala huwa nafikiria nani ndio angekuwa wa kwanza kunirushia mawe", alisema Sakineh Mohammadi Ashtiani mwenye umri wa miaka 43 ambaye ni mama wa watoto wawili.
Hivi karibuni adhabu ya kuuliwa kwa kupigwa mawe ya Sakineh ilibadilishwa na kuwa adhabu ya kuuliwa kwa kunyongwa baada ya mashirika ya kutetea haki za binadamu kuishinikiza serikali ya Iran kumwachia huru mwanamke huyo.
Katika ujumbe wake alioutuma kwa watu toka jela aliyofungwa mjini Tabriz, Sakineh aliwashukuru watu waliofanya kampeni ya kutaka aachiwe huru lakini alisema kuwa anaogopa kufariki.
"Siku niliyohukumiwa kuuliwa ni siku ambayo naiona kama nilidondokea kwenye shimo refu lenye giza, nimepoteza fahamu zangu, siku nyingine kabla ya kulala huwa nafikiria nani angekuwa wa kwanza kunipiga mawe na kwa sababu ipi?, Nawaambieni nyote, Naogopa kufariki naomba nisaidieni, naomba niwakumbatie watoto wangu kwa mara ya mwisho", alisema Sakineh.
Sakineh aliendelea kusema kuwa alivunjika sana moyo siku ambayo alicharazwa bakora 99 mbele ya mtoto wake Sajad mwenye umri wa miaka 17.
Sakineh alipatikana na hatia ya kufanya mapenzi nje ya ndoa yake mwaka 2006 na alihukumiwa kuuliwa kwa kupigwa mawe lakini kutokana na kampeni za mashirika ya kutetea haki za binadamu hatimaye serikali ya Iran hivi karibuni iliibadilisha adhabu hiyo na sasa Sakineh atauliwa kwa kunyongwa.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu bado yanaendeleza kampeni za kutaka Sakineh aachiwe huru lakini serikali ya Iran imekuwa ikisisitiza kuwa adhabu iliyotolewa itatekelezwa kama inavyotakiwa.
source nifahamishe
