RAMANI YA BUSTANI NA MAEGESHO YA GARI DARAJAN

Thursday, March 03, 2011 / Posted by ishak / comments (0)

Miaka miwili jela kwa kuchoma msahafu

Thursday, March 03, 2011 / Posted by ishak / comments (0)

MAHAKAMA ya Wilaya yaMwanakwerekwe Mjini Zanzibar imemuhukumu kifungo cha miaka miwili jela pamoja na kulipa fidia ya shilingi 200,000/ Ramadhan Tuma (28) kwa kosa la kuchoma moto kitabu kitakatifu kiitwacho msahafu.
Hukumu hiyo imetolewa mahakamani hapo na Hakimu Khamis Ali Simai baada ya kuridhika na na ushahidi na kupatikana na hatia hiyo.

Hakimu Simai alisema kuwa,upande wa mashitaka umeweza kuthibitisha makosa hayo dhidi ya mtuhumiwa na atapewa adhabu hiyo kwa mujibu wa sheria kwa kuwa kitendo hicho ni uvunjifu wa amani kwa mujibuwa sheria za Zanzibar.

Kabla ya kutolewa hukumu hiyo mtuhumiwa aliiomba mahakama hiyo impunguziwe adhabu kwa madai kuwa ana familia inayomtegemea akiwemo mke na mtoto pia aliiambia mahakama kuwa alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya tumbo ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.



Awali ilidaiwa kuwa, Ramadhan Handa Tuma alifanya kosa hilo Novemba 16, mwaka jana, akiwa hadharani kwa makusudi alichoma moto kitabu kitakatifu cha dini ya kiislamu ‘msahafu’ pamoja na juzuu.


source nifahamishe

Jinsi ya kupima BMI yako

Sunday, February 20, 2011 / Posted by ishak / comments (0)

Tatizo hili la unene uliopitiliza kuliko inavyohitajika kiafya huwa linaletwa na kuongezeka kwa kiwango cha mafuta mwilini. Njia rahisi na inayokubalika ya kuweza kugundua kama mtu ni mnene kupita kiasi (obese) inafahamika kama kipimo cha Body Mass Index (BMI). Vipimo hivi vya BMI ndio vinaweza kukujulisha kama unene ulionao unastahili kulingana na umri, urefu na uzito wako. Vipimo hivi ni kama ifuatavyo:

CategoryBMI range – kg/m2
Emaciationless than 14.9
Underweightfrom 15 to 18.4
Normalfrom 18.5 to 22.9
Overweightfrom 23 to 27.5
Obesefrom 27.6 to 40
Morbidly Obesegreater than 40

Jinsi ya kupima BMI yako

Kanuni ya BMI hutumia uzito wa mtu pamoja na urefu wake. Uzito wa mtu hupimwa katika kilograms (kg) na urefu wake katika mita (m) au sentimita (cm). Ikumbukwe pia kuwa mita moja ni sawa na sentimita 100 na mita² = mita x mita.

BMI (kg/m2) = Uzito katika kilograms/Urefu katika meters². Maana yake ni kwamba ili kuweza kupata BMI itakayokuwezesha kujifahamu kama u mnene ama la, chukua uzito wako gawa kwa kipeo cha pili cha urefu wako.

Tatizo la Unene Uliopitiliza

Sunday, February 20, 2011 / Posted by ishak / comments (0)


Kuna mambo kadhaa yanayoweza kusababisha unene uliopitiliza. Mambo hayo ni pamoja na

  • Vyakula vya mafuta – Ulaji wa vyakula venye mafuta mengi au calories nyingi.
  • Kutofanya mazoezi – Wale wasiofanya mazoezi mara kwa mara huwa wanene tofauti na wale wanaofanya mazoezi.
  • Kurithi viashiria vya asili (genes) – Viashiria hivi vinaweza kuwa moja ya vichocheo vya kuongeza uzito kwani ndivyo huamua wapi mafuta huhifadhiwa mwilini na kwa kiwango gani. Lakini haimanishi kuwa mtu akiwa navyo basi ndio atakumbwa na tatizo hili.
  • Umri – Watu wengi huongezeka uzito au hunenepa kadri umri unavyoongezeka kwa sababu wanakuwa hawajishughulishi sana (less active) na huwa wanapungua maumbile ya miili yao (muscles mass)
  • Matatizo ya kisaikolojia – Wakati mwengine watu wenye matatizo ya kisaikolojia au msongo wa mawazo (stress) huwa na tabia ya kula sana, matokeo yake ni kunenepa.
  • Dawa – Baadhi ya dawa zenye madhara ya kuongeza unene ni kama corticosteroids, blood pressure medications, tricyclic medications na kadhalika.
  • Matatizo ya afya – Baadhi ya magonjwa yanachangia kuongezeka kwa uzito au kenenepa kama cushings syndrome, hypothyroidism, osteoarthritis na kadhalika

Vihatarishi vya tatizo la unene wa kupitiliza

Aidha yapo mambo kadhaa ambayo yanaweza kumuhatarisha mtu kupata unene wa kupitiliza. Mambo haya ni pamoja na

  • Kukua kwa uchumi wa nchi – Wananchi wengi wanaoishi kwenye nchi zilizoendelea au wenye kipato kikubwa ndio wanaopata tatizo hili kutokana na kuishi mfumo wa maisha ya kivivu na hali ya kutokufanya mazoezi (sedentary lifestyle).
  • Historia ya kuongezeka uzito uliopitiliza kwenye familia nayo yaweza kuhatarisha mtu kupata tatizo hili. Aidha, si jambo la kushangaza kuona karibu familia nzima au wengi wa wanafamilia kuwa wanene kupitiliza.
  • Kutojishughulisha na chochote (inactive).
  • Kupenda kula sana kuliko kawaida (overeating).
  • Kula vyakula vya mafuta mengi
  • Kutumia dawa zenye madhara ya kuongeza uzito uliopitiliza.
  • Kuwa na ugonjwa wa vichocheo mwilini (hormonal disorders) kama cushingsyndrome, hypothyroidism.
  • Kuwa na msongo wa mawazo au kuathirika kisaikolojia.

Magonjwa yanaoweza kuambatana na tatizo la unene uliopitiliza

  • Kisukari
  • Shinikizo la damu (hypertension)
  • Kiharusi (Stroke)
  • Magonjwa ya moyo
  • Tatizo la kutopumua vizuri wakati mtu yupo usingizini (Sleep apnea)
  • Vijiwe katika mfuko wa nyongo (Gallstones)
  • Kiwango cha juu cha lijamu kwenye damu (cholesterol ikiwemo triglycerides)
  • Ugonjwa wa mifupa kama yabisi (osteoarthritis).
  • Saratani ya matiti
  • Saratani ya tezi dume (prostate cancer)
  • Saratani ya utumbo mpana pamoja na maeneo ya haja kubwa (Colorectal cancer)
  • Matatizo ya mzunguko na mishipa ya damu kama vile kuvimba kwa vena za miguuni(varicose veins)

Tiba ya kuongezeka unene kupita kiasi

Tiba ya tatizo hili ni mhusika kujitambua ya kwamba ana tatizo na kuwa tayari kupunguza uzito. Mabadiliko ya tabia ya mhusika ni muhimu sana, mabidiliko haya yawe ndio mfumo wa maisha yake ya kila siku.

Kupungua uzito na kujilinda au kutunza uzito ulionao baada ya kupunguza uzito ni jambo la msingi sana na inahusisha mazoezi, chakula na madiliko ya tabia ya mtu.

  • Mabadiliko ya tabia - Hii inahusisha muhusika kupunguza kiwango cha chakula anachokula lakini kiwe chenye virutubisho vyote muhimu vya afya na kuongeza kiwango cha ufanyaji mazoezi.
  • Mazoezi - Mazoezi husaidia kupunguza uzito hasa kipindi cha miezi sita ya mwanzo na hutunza uzito uliokusudiwa kwa muda mrefu. Pia hupunguza mafuta ya mwilini, huongeza ufanisi wa moyo, hupunguza tatizo la shinikizo la damu (hypertension), na kuweka sukari katika kiwango kinachohitajika mwilini.

Kama hujazoea kufanya mazoezi ni vizuri uanze taratibu na ujiwekee lengo kwa kufanya mazoezi kwa muda wa nusu saa kila siku, siku tano kwa wiki,(dakika 30 kila siku kwa siku tano kwa wiki). Mazoezi mazuri ni kama kuogelea, kuendesha baiskeli, kutembea, kunyanyua vitu vizito (visiwe vyenye uzito mkubwa), mazoezi ya viungo na kadhalika. Kama mtu ni mnene sana basi ni bora kuzungumza na daktari wako kabla ya kuanza mazoezi mapya. Baada ya kuanza mazoezi kwa mara ya kwanza, mwili utakuwa na maumivu, hii ni kawaida lakini kama mtu atapata maumivu zaidi ya masaa 2 baada ya kufanya mazoezi ni vizuri kumuona daktari.

  • Dawa - Zipo dawa nyingi za kupunguza uzito lakini ikumbukwe ya kwamba hakuna tiba ya tatizo hili na dawa hizi zina madhara mengi kama kuongeza shinikizo la damu (hypertension), matatizo ya moyo, kuharisha,msongo wa mawazo (depression) na mengineyo.
  • Chakula - Msingi wa kupunguza uzito au unene ni kujua ni kiwango gani cha caloriesmwili wako unahitaji kwa siku ili uwe unakula chakula ambacho hakitazidisha au kupunguza kiwango cha calories unazohitaji kwa siku. Mlo mzuri ni ule ulio na matunda kwa wingi, mboga za majani, nafaka ambazo hazijakobolewa, mafuta kidogo (less saturated fat). Vyakula vengine ni kama mayai, nyama isiokuwa ya mafuta (lean meat), samaki, kuku na vingineyo.
  • Tiba ya upasuaji - Kuna aina nyingi za upasuaji ambao unasaidia kupunguza uzito aina hizi ni kama gastric banding, gastric bypass (Roux-en-Y-procedure), liposuction. Kabla ya kufanyiwa upasuaji, muhusika atahitaji kupimwa kisaikolojia (psychological testing) na kupewa ushauri nasaha kwani tiba hii pia ina madhara yake.

Wanawake ambao wana uzito wa kupitiliza (obese women) wakiwa wajawazito wako kwenye hatari ya kupata madhara yafuatayo;

  • Kisukari cha mimba (Gestatitional diabetes) – kisukari hiki kinatokea wakati wa ujauzito na hupotea baada ya kujifungua mtoto.
  • Shinikizo la damu (hypertension)
  • Shinikizo la damu wakati wa ujauzito pamoja na kifafa cha mimba (pre-eclampsia & eclampsia)
  • Kuzaa kwa njia ya upasuaji (caesarean section)
  • Tatizo la kiumbe kutopata hewa vizuri wakati wa ujauzito (fetal distress)

Noti mpya bandia sasa zapitia benki

Wednesday, February 16, 2011 / Posted by ishak / comments (0)

KASHFA ya kukithiri kwa noti mpya bandia inazidi kuongezeka na sasa imebainika kuwa hata baadhi ya benki nchini zinashindwa kuzibaini na hivyo kujikuta zinaziingiza kwenye mzunguko.

Hali hiyo inatokana na Karani wa Fedha wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Februari 14 kuchukua fedha benki ya CRDB tawi la Lumumba na bila kutambua hatimaye akagundua amepewa noti nyingi za Sh 10,000 zikiwa bandia.

Hata pale mmoja wa wafanyakazi wa TSN aliyepewa noti hizo alipokwenda kuweka baadhi ya noti hizo kwenye moja ya benki bila kujua kuwa ni bandia, karani wa benki hiyo alizipokea na kuzipitisha kwenye mashine na kuridhika kuwa ni halali.

Kitendo hicho kinaonesha kuwa mashine za benki hazizitambui noti hizo na hata wafanyakazi wenyewe wa benki yawezekana hawana utaalamu wa kutosha wa kutofautisha noti bandia na halali hasa za Sh 10,000.

Noti hizo ziligunduliwa na wafanyakazi waliopewa fedha hizo baada ya kuanza kuzitumia na kukataliwa mitaani ambapo jana baadhi yao walijikuta wakiwa na noti hizo.

Meneja wa Fedha wa TSN, Diana Lyatuu, alithibitisha kuchukuliwa fedha hizo kutoka benki ya CRDB tawi la Lumumba kwa kubadilishwa na hundi.

Noti nyingi ambazo zimezagaa ni zinazoishia na namba 366 na 362 ambazo ndizo wafanyakazi wengi wa TSN walikabidhiwa.

Mmoja wa wafanyakazi wa TSN, Nelly Mtema, alikamatwa na Polisi baada ya kuzitumia fedha hizo alizopewa ofisini kwa ajili ya kwenda kulipia bili ya maji katika ofisi za Kampuni ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO).

Akielezea tukio hilo, Mtema alisema Februari 15 asubuhi alikwenda Dawasco kulipia maji lakini akashangaa kuwekwa chini ya ulinzi kwa maelezo kuwa ana fedha bandia.

“Niliwakatalia kuwa si bandia kwani nililipwa ofisini, lakini nikapelekwa Polisi kituo cha Kimara,” alisema Mtema ambaye baada ya kuzichunguza noti hizo aligundua bandia zikiwa tatu za Sh 10,000.

Aliongeza kuwa baada ya sakata hilo, alilazimika kupiga simu ofisini, kufahamisha kuwa fedha alizopewa ni bandia na amekamatwa na polisi baada ya kuzitumia kulipia huduma ya maji.

“Ofisini walizungumza na polisi juu ya kuwapo tatizo hilo ndipo nikaachiwa,” alisema Mtema.
Mkurugenzi wa Masoko wa CRDB, Tully Mwambapa, alipoulizwa juu ya tatizo hilo, alisema ana uhakika asilimia 100 ya fedha hizo hazikutolewa na benki yake.

“Sisi tuna sheria inayomtaka mteja ahesabu na ahakiki fedha zake kabla ya kuondoka dirishani, itakuwaje keshia aondoke ndipo tupokee malalamiko ya kuwapo fedha bandia?” Alihoji Mwambapa.

Keshia wa TSN alipoulizwa alisema hakuona haja ya kuhakiki fedha hizo kwa vile anaiamini benki hiyo kwani amefanya nayo kazi kwa siku nyingi. Hata hivyo, Mwambapa alisema: “Benki yangu ina sera ya kutoaminiana katika mambo ya fedha.”

Alijitetea kuwa kila dirisha lina kamera inayochukua mwenendo wa matukio ya kuanzia asubuhi hadi jioni yanayofanywa na karani aliyepo kwenye dirisha husika. “Ndiyo maana nasema fedha hizo hazikutoka kwetu,” alisema

Gazeti hili lilitaka kujua ukweli kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kutokana na kukithiri kwa noti hizo bandia, lakini simu ya Gavana Benno Ndulu ilikuwa inaita bila majibu.

Baadaye Katibu Muhtasi wa Gavana alisema bosi wake alikuwa kwenye kikao muhimu na akashauri mwandishi kama ni suala hilo la noti bandia uulizwe uongozi wa benki husika kwani utakuwa na majibu ya tatizo hilo.

Katika hatua nyingine, Mbunge wa Mji Mkongwe, Ibrahim Muhamad Sanya (CUF) ametoa hadhari kwa BoT na Hazina juu ya kuzagaa kwa noti mpya bandia na kuvitaka vyombo hivyo kuchukua hatua za haraka kwa kuwa kuna hatari ya uchumi kuathirika.

Sanya alitoa hadhari hiyo na kuwasilisha noti bandia ya Sh 10,000 juzi bungeni wakati wa mjadala wa hotuba ya Rais Jakaya Kikwete, aliyoiwasilisha wakati akifungua Bunge la 10, mwaka jana.

Kwa hadhari hiyo, Spika wa Bunge Anne Makinda, aliitaka Wizara ya Fedha kuwasilisha taarifa juu ya suala hilo bungeni. Akiwasilisha noti hiyo, Sanya alisema iligundulika kuwa bandia baada ya kukaguliwa na kubainika haina picha ya Baba wa Taifa upande wa kushoto.

Alipoulizwa na Spika Makinda alikoipata noti hiyo, alisema alikabidhiwa na mfanyabiashara ndogo mjini Dodoma ambaye alidai kuipata kwa mteja aliyemwuzia bidhaa, hali ambayo ilimtia hasara kwa kuwa kiasi hicho cha fedha ni sawa na mtaji wake.

“Kijana huyo aliponiona alinikabidhi noti hii na kudai kuwa kwa sasa zimezagaa mjini hapa na kunitaka niiwasilishe bungeni ili vyombo husika vichukue hatua, kwa kuwa hali mtaani ni mbaya,” alisema Sanya.

Akipokea taarifa na noti hiyo, Makinda alimshukuru Sanya kwa kutoa taarifa hiyo, na kuitaka serikali ichukue hatua za haraka na kulitolea maelezo suala hilo bungeni.

Tangu kutangazwa kwa noti hizo mpya kumekuwa na malalamiko kadhaa kutoka kwa wananchi wakidai noti hizo hazina ubora na ni rahisi kughushiwa lakini BoT ilijitetea na kudai kuwa zina ubora wa kimataifa na si rahisi kughushiwa.


source habarileo

Ajaribu Kujiua Kwa Kukosa Matiti Makubwa

Wednesday, February 16, 2011 / Posted by ishak / comments (0)

Mrembo wa Brazil ambaye awali alikuwa akishikilia rekodi ya dunia ya kuwa na matiti makubwa kuliko wanawake wote duniani na baadae matiti hayo kukatwa ili kuokoa maisha yake, amejaribu kujiua kwa mara ya pili akisema kuwa hawezi kuishi bila ya matiti
Mrembo Sheyla Hershey wa nchini Brazil ambaye mwaka jana matiti yake makubwa yalikatwa ili kunusuru maisha yake alipopatwa na maambukizi kwenye matiti yake, amejaribu kujiua kwa mara ya pili.

Sheyla alifanya operesheni nyingi za kuongeza matiti yake ili kuvunja rekodi ya kuwa na matiti makubwa kuliko wanawake wote duniani. Alifanikiwa kuvunja rekodi hiyo lakini aliipoteza rekodi hiyo mwaka jana baada ya madaktari kuamua kuyakata matiti yake ili kuyaokoa maisha yake yalipokuwa hatarini kutokana na maambukizi.

Kutokana na kushindwa kuishikilia rekodi ya dunia ya matiti makubwa, mwezi uliopita Sheyla alijaribu kujiua kwa mara ya kwanza akisema kuwa hawezi kuishi bila ya matiti yake makubwa.

"Bila ya matiti yangu makubwa nachukiza na nakuwa sijielewi", alisema Sheyla ambaye anaishi Texas nchini Marekani.

Sheyla alishawahi kupatiwa matibabu ya kisaikolojia kutokana na lindi la mawazo la kupoteza kitambulisho chake cha mwanamke mwenye matiti makubwa kuliko wote duniani.

Jumapili wiki iliyopita, Sheyla alijaribu kujiua kwa mara ya pili kwa kumeza kiasi kikubwa cha vidonge.

Sheyla ambaye ana umri wa miaka 31 bado amelazwa hospitali tangu jumapili akiwa kwenye chumba cha watu mahututi.

"Madaktari hawajui ni wakati gani atazinduka, tunamuombea dua aweze kuzinduka", alisema mumewe.


source nifahamishe

Siri ya Mapenzi ya Michelle Obama

Wednesday, February 16, 2011 / Posted by ishak / comments (0)

Katika kusherehekea siku ya wapendanao duniani, mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama amewapa wapendanao siri ya mapenzi kuwa ni 'Si kwa wapenzi kununiana na kuwa siriasi muda wote bali ni kuchekeshana na kupeana matabasamu wakati wote.
Michelle Obama amesema kuwa siri kubwa ya mapenzi ndani ya nyumba ni kuchekeana na mpenzi wako hivyo kudumisha furaha wakati wote.

Michelle Obama amesema kuwa amekuwa akiitumia njia hiyo kuyadumisha mapenzi kati yake na rais Barack Obama na kwa kweli amefanikiwa katika hilo.

Ingawa ndoa yao imekumbwa na misukosuko mingi ya kimaisha na harakati za kisiasa, ndoa hiyo imetimiza miaka 19 sasa.

Bi Obama alisema kuwa siri kubwa ya kudumu kwa mapenzi ndani ya ndoa yao ni kuchekeshana na kupeana matabasamu wakati wote.

Katika kusherehekea siku ya wapendanao Valentine Day, Bi Obama alisema anatarajia mzee Obama atazama mfukoni na kumnunulia zawadi ya mkufu au hereni za dhahabu.

source nifahamishe