Japan earthquake: tens of thousands missing as full devastation emerges
Magari Saba Ya Kifahari Kwaajili ya Wake wa Rais
| Pamoja na kwamba ana ndege yake maalumu ya kiraisi na msururu wa magari ya serikali anayoambatana nayo katika misafara yake, rais Jacob Zuma anatafuta magari saba ya kifahari kwaajili ya wake zake. | ||
| Kamati ya ulinzi wa rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma imetangaza kutoa tenda ya kukodisha magari saba ya kifahari kwaajili ya wake wa rais Zuma . Katika miji saba ya Afrika Kusini ukiwemo mji anaotoka Jacob Zuma wa KwaZulu-Natal kutakuwepo na gari moja ambalo litakuwa tayari tayari kwaajili ya wake wa Rais Zuma. Kwa mujibu wa nyaraka za tenda ya kukodisha magari hayo, magari yanayohitajika yanatakiwa yawe ni magari mapya ya kifahari na magari hayo lazima yawe ni aidha Mercedes-Benz S600, BMW 7 series, Audi A8 au A6, Mercedes-Benz ML, BMW X5 series, Audi Q7, Toyota Prado, Toyota Land Cruiser au Nissan Pathfinder. Rais Zuma amewahi kuwaoa wanawake watano ambapo mwanamke mmoja kati yao, Nkosazana Dlamini-Zuma, alimpa talaka mwaka 1998 wakati mke wake mwingine toka Msumbiji, Kate Mantsho, alijiua mwenyewe mwaka 2000. Hivi sasa Zuma anaishi na wake zake watatu Gertrude Sizakele, Nompumelelo Ntuli (MaNtuli) na Thobeka Stacie Madiba. Zuma pia ana wachumba wawili ambao amepanga kuwaoa katika siku za karibuni. nifahamishe source | ||
RAMANI YA BUSTANI NA MAEGESHO YA GARI DARAJAN
MAHAKAMA ya Wilaya yaMwanakwerekwe Mjini Zanzibar imemuhukumu kifungo cha miaka miwili jela pamoja na kulipa fidia ya shilingi 200,000/ Ramadhan Tuma (28) kwa kosa la kuchoma moto kitabu kitakatifu kiitwacho msahafu. Hukumu hiyo imetolewa mahakamani hapo na Hakimu Khamis Ali Simai baada ya kuridhika na na ushahidi na kupatikana na hatia hiyo.
Hakimu Simai alisema kuwa,upande wa mashitaka umeweza kuthibitisha makosa hayo dhidi ya mtuhumiwa na atapewa adhabu hiyo kwa mujibu wa sheria kwa kuwa kitendo hicho ni uvunjifu wa amani kwa mujibuwa sheria za Zanzibar.
Kabla ya kutolewa hukumu hiyo mtuhumiwa aliiomba mahakama hiyo impunguziwe adhabu kwa madai kuwa ana familia inayomtegemea akiwemo mke na mtoto pia aliiambia mahakama kuwa alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya tumbo ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.
Awali ilidaiwa kuwa, Ramadhan Handa Tuma alifanya kosa hilo Novemba 16, mwaka jana, akiwa hadharani kwa makusudi alichoma moto kitabu kitakatifu cha dini ya kiislamu ‘msahafu’ pamoja na juzuu.
source nifahamishe
Tatizo hili la unene uliopitiliza kuliko inavyohitajika kiafya huwa linaletwa na kuongezeka kwa kiwango cha mafuta mwilini. Njia rahisi na inayokubalika ya kuweza kugundua kama mtu ni mnene kupita kiasi (obese) inafahamika kama kipimo cha Body Mass Index (BMI). Vipimo hivi vya BMI ndio vinaweza kukujulisha kama unene ulionao unastahili kulingana na umri, urefu na uzito wako. Vipimo hivi ni kama ifuatavyo: Jinsi ya kupima BMI yako Kanuni ya BMI hutumia uzito wa mtu pamoja na urefu wake. Uzito wa mtu hupimwa katika kilograms (kg) na urefu wake katika mita (m) au sentimita (cm). Ikumbukwe pia kuwa mita moja ni sawa na sentimita 100 na mita² = mita x mita. BMI (kg/m2) = Uzito katika kilograms/Urefu katika meters². Maana yake ni kwamba ili kuweza kupata BMI itakayokuwezesha kujifahamu kama u mnene ama la, chukua uzito wako gawa kwa kipeo cha pili cha urefu wako.Category BMI range – kg/m2 Emaciation less than 14.9 Underweight from 15 to 18.4 Normal from 18.5 to 22.9 Overweight from 23 to 27.5 Obese from 27.6 to 40 Morbidly Obese greater than 40
Kuna mambo kadhaa yanayoweza kusababisha unene uliopitiliza. Mambo hayo ni pamoja na Vihatarishi vya tatizo la unene wa kupitiliza Aidha yapo mambo kadhaa ambayo yanaweza kumuhatarisha mtu kupata unene wa kupitiliza. Mambo haya ni pamoja na Magonjwa yanaoweza kuambatana na tatizo la unene uliopitiliza Tiba ya kuongezeka unene kupita kiasi Tiba ya tatizo hili ni mhusika kujitambua ya kwamba ana tatizo na kuwa tayari kupunguza uzito. Mabadiliko ya tabia ya mhusika ni muhimu sana, mabidiliko haya yawe ndio mfumo wa maisha yake ya kila siku. Kupungua uzito na kujilinda au kutunza uzito ulionao baada ya kupunguza uzito ni jambo la msingi sana na inahusisha mazoezi, chakula na madiliko ya tabia ya mtu. Kama hujazoea kufanya mazoezi ni vizuri uanze taratibu na ujiwekee lengo kwa kufanya mazoezi kwa muda wa nusu saa kila siku, siku tano kwa wiki,(dakika 30 kila siku kwa siku tano kwa wiki). Mazoezi mazuri ni kama kuogelea, kuendesha baiskeli, kutembea, kunyanyua vitu vizito (visiwe vyenye uzito mkubwa), mazoezi ya viungo na kadhalika. Kama mtu ni mnene sana basi ni bora kuzungumza na daktari wako kabla ya kuanza mazoezi mapya. Baada ya kuanza mazoezi kwa mara ya kwanza, mwili utakuwa na maumivu, hii ni kawaida lakini kama mtu atapata maumivu zaidi ya masaa 2 baada ya kufanya mazoezi ni vizuri kumuona daktari. Wanawake ambao wana uzito wa kupitiliza (obese women) wakiwa wajawazito wako kwenye hatari ya kupata madhara yafuatayo;
KASHFA ya kukithiri kwa noti mpya bandia inazidi kuongezeka na sasa imebainika kuwa hata baadhi ya benki nchini zinashindwa kuzibaini na hivyo kujikuta zinaziingiza kwenye mzunguko.
Hali hiyo inatokana na Karani wa Fedha wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Februari 14 kuchukua fedha benki ya CRDB tawi la Lumumba na bila kutambua hatimaye akagundua amepewa noti nyingi za Sh 10,000 zikiwa bandia.
Hata pale mmoja wa wafanyakazi wa TSN aliyepewa noti hizo alipokwenda kuweka baadhi ya noti hizo kwenye moja ya benki bila kujua kuwa ni bandia, karani wa benki hiyo alizipokea na kuzipitisha kwenye mashine na kuridhika kuwa ni halali.
Kitendo hicho kinaonesha kuwa mashine za benki hazizitambui noti hizo na hata wafanyakazi wenyewe wa benki yawezekana hawana utaalamu wa kutosha wa kutofautisha noti bandia na halali hasa za Sh 10,000.
Noti hizo ziligunduliwa na wafanyakazi waliopewa fedha hizo baada ya kuanza kuzitumia na kukataliwa mitaani ambapo jana baadhi yao walijikuta wakiwa na noti hizo.
Meneja wa Fedha wa TSN, Diana Lyatuu, alithibitisha kuchukuliwa fedha hizo kutoka benki ya CRDB tawi la Lumumba kwa kubadilishwa na hundi.
Noti nyingi ambazo zimezagaa ni zinazoishia na namba 366 na 362 ambazo ndizo wafanyakazi wengi wa TSN walikabidhiwa.
Mmoja wa wafanyakazi wa TSN, Nelly Mtema, alikamatwa na Polisi baada ya kuzitumia fedha hizo alizopewa ofisini kwa ajili ya kwenda kulipia bili ya maji katika ofisi za Kampuni ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO).
Akielezea tukio hilo, Mtema alisema Februari 15 asubuhi alikwenda Dawasco kulipia maji lakini akashangaa kuwekwa chini ya ulinzi kwa maelezo kuwa ana fedha bandia.
“Niliwakatalia kuwa si bandia kwani nililipwa ofisini, lakini nikapelekwa Polisi kituo cha Kimara,” alisema Mtema ambaye baada ya kuzichunguza noti hizo aligundua bandia zikiwa tatu za Sh 10,000.
Aliongeza kuwa baada ya sakata hilo, alilazimika kupiga simu ofisini, kufahamisha kuwa fedha alizopewa ni bandia na amekamatwa na polisi baada ya kuzitumia kulipia huduma ya maji.
“Ofisini walizungumza na polisi juu ya kuwapo tatizo hilo ndipo nikaachiwa,” alisema Mtema.
Mkurugenzi wa Masoko wa CRDB, Tully Mwambapa, alipoulizwa juu ya tatizo hilo, alisema ana uhakika asilimia 100 ya fedha hizo hazikutolewa na benki yake.
“Sisi tuna sheria inayomtaka mteja ahesabu na ahakiki fedha zake kabla ya kuondoka dirishani, itakuwaje keshia aondoke ndipo tupokee malalamiko ya kuwapo fedha bandia?” Alihoji Mwambapa.
Keshia wa TSN alipoulizwa alisema hakuona haja ya kuhakiki fedha hizo kwa vile anaiamini benki hiyo kwani amefanya nayo kazi kwa siku nyingi. Hata hivyo, Mwambapa alisema: “Benki yangu ina sera ya kutoaminiana katika mambo ya fedha.”
Alijitetea kuwa kila dirisha lina kamera inayochukua mwenendo wa matukio ya kuanzia asubuhi hadi jioni yanayofanywa na karani aliyepo kwenye dirisha husika. “Ndiyo maana nasema fedha hizo hazikutoka kwetu,” alisema
Gazeti hili lilitaka kujua ukweli kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kutokana na kukithiri kwa noti hizo bandia, lakini simu ya Gavana Benno Ndulu ilikuwa inaita bila majibu.
Baadaye Katibu Muhtasi wa Gavana alisema bosi wake alikuwa kwenye kikao muhimu na akashauri mwandishi kama ni suala hilo la noti bandia uulizwe uongozi wa benki husika kwani utakuwa na majibu ya tatizo hilo.
Katika hatua nyingine, Mbunge wa Mji Mkongwe, Ibrahim Muhamad Sanya (CUF) ametoa hadhari kwa BoT na Hazina juu ya kuzagaa kwa noti mpya bandia na kuvitaka vyombo hivyo kuchukua hatua za haraka kwa kuwa kuna hatari ya uchumi kuathirika.
Sanya alitoa hadhari hiyo na kuwasilisha noti bandia ya Sh 10,000 juzi bungeni wakati wa mjadala wa hotuba ya Rais Jakaya Kikwete, aliyoiwasilisha wakati akifungua Bunge la 10, mwaka jana.
Kwa hadhari hiyo, Spika wa Bunge Anne Makinda, aliitaka Wizara ya Fedha kuwasilisha taarifa juu ya suala hilo bungeni. Akiwasilisha noti hiyo, Sanya alisema iligundulika kuwa bandia baada ya kukaguliwa na kubainika haina picha ya Baba wa Taifa upande wa kushoto.
Alipoulizwa na Spika Makinda alikoipata noti hiyo, alisema alikabidhiwa na mfanyabiashara ndogo mjini Dodoma ambaye alidai kuipata kwa mteja aliyemwuzia bidhaa, hali ambayo ilimtia hasara kwa kuwa kiasi hicho cha fedha ni sawa na mtaji wake.
“Kijana huyo aliponiona alinikabidhi noti hii na kudai kuwa kwa sasa zimezagaa mjini hapa na kunitaka niiwasilishe bungeni ili vyombo husika vichukue hatua, kwa kuwa hali mtaani ni mbaya,” alisema Sanya.
Akipokea taarifa na noti hiyo, Makinda alimshukuru Sanya kwa kutoa taarifa hiyo, na kuitaka serikali ichukue hatua za haraka na kulitolea maelezo suala hilo bungeni.
Tangu kutangazwa kwa noti hizo mpya kumekuwa na malalamiko kadhaa kutoka kwa wananchi wakidai noti hizo hazina ubora na ni rahisi kughushiwa lakini BoT ilijitetea na kudai kuwa zina ubora wa kimataifa na si rahisi kughushiwa.
