Obama Aweka Wazi Cheti cha Kuzaliwa

Thursday, April 28, 2011 / Posted by ishak / comments (0)



Baada ya Kusakamwa Sana, Obama Ameamua kuweka Wazi Cheti cha Kuzaliwa

Baada ya kusakamwa sana kuwa hajazaliwa Marekani na hivyo hafai kuwa rais wa Marekani, Barack Obama ameamua kukata mzizi wa fitina kwa kuweka wazi cheti cha kuzaliwa.
Rais Barack Obama wa Marekani ili kumaliza majungu ya wapinzani wake kuwa yeye si Marekani ameamua kuweka wazi cheti chake cha kuzaliwa.

Wapinzani wa Obama kwa muda mrefu sana wamekuwa wakisema kuwa Obama hajazaliwa Hawaii, Marekani kama anavyodai hivyo haruhusiwi kisheria kuwa rais wa Marekani.

Ilikuwa ikidaiwa kuwa huenda Obama alizaliwa Kenya anakotoka baba yake mzee Hussein Obama au nchini Indonesia ambako Obama alikuwa huko wakati wa utoto wake.

Huku uchaguzi mkuu utakaofanyika tena mwakani ukianza kujongea, Obama ameamua kusambaza nakala za cheti cha kuzaliwa ili kumaliza gumzo la sehemu aliyozaliwa.

Akisambaza nakala za cheti chake cha kuzaliwa, Obama alisema kuwa hana muda wa kupoteza kubishana na wapinzani wake.

source nifahamishe

Shakira Aingizwa Mjini na Kibaka

Saturday, April 16, 2011 / Posted by ishak / comments (0)


Shakira

Mwanamuziki maarufu duniani wa muziki wa Pop, Shakira ambaye anajulikana sana kwa kunyonga kiuno chake, ameibiwa pete yake ya thamani wakati alipokuwa akiwasalimia kwa kuwapa mkono washabiki wake waliohudhuria shoo yake nchini Mexico.
Shakira mwenye umri wa miaka 34, alikuwa akipafomu kwenye shoo yake katika chuo kikuu cha University of Monterrey kilichoko kwenye mji wa Monterrey, Mexico siku ya alhamisi wakati kibaka mmoja alipofanikiwa kuivua pete ya nyota huyo wa muziki wa Pop.

Shakira ambaye alikuwa akiwasalimia kwa kuwapa mkono washabiki wake, aligundua muda mfupi baadae kuwa pete yake ameishavuliwa.

Tukio hilo la wizi lilinaswa live na mpiga picha za video katika shoo hiyo hata hivyo Shakira hakukatisha shoo yake na wala hakumkamata mwizi wake.

Hakuna mtu aliyekamatwa hadi sasa kutokana na tukio hilo.

Wakati huo huo, mpenzi wa Shakira, nyota wa soka beki wa timu ya Barcelona ya Hispania, Gerard Pique amesema kuwa ingawa anafurahia kuwa kwenye mahusiano na Shakira lakini bado hajazoea maisha ya kufuatiliwa kila kona na paparazzi ambao wamekuwa wakimfuatilia nyota huyo wa soka tangu ilipojulikana kuwa anatoka na Shakira.

"Huwa wanakuja kundi kubwa, inabidi kuzoea hali hii ya kufuatwa mitaani kila kona", alisema Pique.


source nifahamishe

Mbunge Anayepiga Vita Sinema za Ngono Anaswa Akiangalia Ngono Bungeni

Saturday, April 16, 2011 / Posted by ishak / comments (0)


Arifinto akipiga chabo video za ngono ndani ya Bunge

Mbunge wa nchini Indonesia ambaye alijipatia umaarufu kwa kusimama kidete kushinikiza sheria kali zipitishwe kama vile kutupwa jela miaka 15 kwa kushiriki kwenye video za ngono, mbunge huyo amelazimika kujiuzulu baada ya kunaswa akiangalia ngono bungeni.
Arifinto, mwanasiasa wa nchini Indonesia ambaye alikuwa mstari wa mbele katika kupigania sheria za kupinga video na picha za ngono, amenaswa akiangalia video ya ngono ndani ya kikao cha bunge.

Arifinto alilazimika kujiuzulu ubunge baada ya picha zake kusambaa kwenye vyombo vya habari zikimwonyesha akiwa bize kwenye laptop yake akiangalia video ya ngono.

Arifinto alikuwa miongoni mwa wanasiasa walioshinikiza na hatimaye kupitishwa kwa sheria ya kupinga picha, video na vitendo vya ngono hadharani.

Sheria hiyo iliyopitishwa mwaka 2008 inaweka wazi kuwa adhabu ya kutupwa jela hadi miaka 15 au kupigwa faini itamkumba mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya kubusiana hadharani au kuangalia picha au video za ngono.

Kuzionyesha, kuzimiliki au kuzihifadhi video au picha za ngono ni marufuku kwa mujibu wa sheria hiyo.

Arifinto mwenye umri wa miaka 51 ambaye pia ni baba wa watoto watano, alikuwa ndio msemaji mkubwa wa kushinikiza kupitishwa kwa sheria hiyo.

Arifinto aliitisha kikao na kutangaza mbele ya waandishi wa habari kuwa anajiuzulu ubunge wake mara moja.

"Huu ni uamuzi wangu, hakuna mtu aliyenishinikiza kufanya hivyo", alisema Arifinto ambaye kama raia wengine wa Indonesia anajulikana kwa jina moja tu.

Indonesia, ni nchi ya kidemokrasia yenye jumla ya watu milioni 237, ndiyo nchi yenye waislamu wengi kuliko nchi zote duniani.


source nifahamishe

10 Wafariki Katika Maandamano ya Kuchomwa Kwa Quran

Sunday, April 03, 2011 / Posted by ishak / comments (0)


Saturday, April 02, 2011 6:37 PM
Wafanyakazi 10 wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan wamefariki dunia kufuatia mashambulizi toka kwa maelfu ya watu waliokuwa wakiandamana kupinga kitendo cha mchungaji wa kanisa moja la nchini Marekani kuichoma Quran.
Wafanyakazi 10 wa ofisi ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa katika mji wa Mazar-i-Sharif nchini Afghanistan, wameuliwa na waandamanaji waliokuwa wakipinga kitendo cha mchungaji wa kanisa moja la nchini Marekani kuichoma moto Quran.

Waandamanaji waliandamana jana katika miji ya Mazar-i-Sharif na mji mkuu wa Afghanistan kupinga kitendo cha mchungaji Wayne Sapp wa kanisa la Florida nchini Marekani kukichoma moto kitabu kitukufu cha waislamu, Quran.

"Watu 10 wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wameuliwa na waandamanaji, wote waliouliwa walikuwa ni raia wa kigeni", alisema msemaji wa polisi wa Afghanistan, Lal Mohammad Ahmadzai.

Mchungaji Sapp aliichoma moto Quran tarehe 21 mwezi uliopita chini ya usimamizi wa mchungaji Terry Jones, ambaye alisababisha mtafaruku mkubwa sana mwaka jana alipotishia kuichoma moto misahafu.

Aliahirisha uamuzi wake huo baada ya serikali ya Marekani na viongozi wa kimataifa kumuonya kuwa kitendo hicho kitahatarisha maisha ya Wamarekani duniani.


source nifahamishe

MAALIM SEIF AREJEA NYUMBANI

Friday, March 25, 2011 / Posted by ishak / comments (0)

MAKAMO wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akishuka kutoka kwenye ndege wakati alipowasili katika Uwanja wa kimataifa wa Abeid Karume akitokea nchi za nje alipokuwa katika ziara ya kiserikali pamoja na matibabu.
MAKAMO wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akivishwa shada la maua alipowasili nyumbani

MAKAMO wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiwapungia mkono wananchi pamoja na viongozi waliokuwepo uwanjani ambapo Dufu pia lilikuwepo kumkaribisha uwanjani hapo
MAKAMO wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari alipowasili katika Uwanja wa Zanzibar. Kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa shirika la utangazaji Zanzibar, Hassan Mitawi.


source othmanmapara

Jela Maisha Kwa Kumpachika Mimba Binti wa Miaka 9

Friday, March 25, 2011 / Posted by ishak / comments (0)


Fede Datilus
Saturday, March 26, 2011 2:42 AM
Mwanaume mmoja wa nchini Marekani amehukumiwa kwenda jela maisha kwa kumpachika mimba mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 9.
Fede Datilus wa Florida nchini Marekani amehukumiwa kwenda jela maisha kwa kumpachika mimba msichana mwenye umri wa miaka 9 raia wa Haiti.

Datilus lipatikana na hatia ya kumbaka msichana mwenye umri chini ya miaka 12 kosa ambalo aliadhibiwa kifungo cha maisha.

Datilus alipatikana na hatia ya kosa jingine la kumpachika mimba msichana mwenye umri wa miaka 9 kosa ambalo alihukumiwa kwenda jela miaka mitano.

Msichana aliyepachikwa mimba alikuwa ni raia wa Haiti amabye alihamia Marekani pamoja na wazazi wake miaka miwili iliyopita.

Baba wa msichana huyo aligundua mtoto wake ni mjamzito mwezi machi mwaka jana baada ya kumpeleka kliniki alipokuwa akiumwa.

Msichana huyo ambaye jina lake halikutajwa kwa sababu za kisheria alifanikiwa kumtambua Datilus kuwa ndiye mwanaume aliyembaka.

Msichana huyo alijifungua salama mwa huu akiwa amefikisha umri wa miaka 10.

Datilus mwenye umri wa miaka 33, alihukumiwa kwenda kuyamalizia maisha yake yaliyobakia jela.


source nifahamishe

Mchezaji wa Manchester City Atupwa Jela

Friday, March 25, 2011 / Posted by ishak / comments (0)



Kelvin Etuhu

Mshambuliaji wa Manchester City, Kelvin Etuhu ametupwa jela miezi minane kwa kumpiga mtu mtaani na kumvunja taya.
Mshambuliaji wa timu tajiri ya nchini Uingereza Manchester City, Kelvin Etuhu ametupwa jela miezi minane kwa kumpiga mtu mtaani na kumvunja taya lake.

Etuhu ambaye alisomewa mashtaka yake katika mahakama ya mjini Manchester alipatikana na hatia ya kufanya shambulizi la kudhuru mwili na kufanya vurugu.

Etuhu mweye umri wa miaka 22 baada ya kupata ulabu alimshambulia mwanaume mmoja aliyekuwa akizozana naye ndani ya baa mwaka jana, Etuhu alionekana kwenye CCTV akiendelea kumshushia kipigo mwanaume huyo baada ya kumtandika ngumi iliyomdondosha chini.

Etuhu ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Nigeria, amehukumiwa kwenda jela miezi minane.

source nifahamishe