Ndoa ya rais wa Marekani, Barack Obama na mkewe Michelle iliwahi kupitia misukosuko mikubwa ambayo ilitishia kuvunjika kwake. Miongoni mwa vitu vilivyokuwa vikisababisha kutokuelewana ni Obama kuvuta sana sigara na kukoroma sana usiku wakati Obama alikuwa akichukizwa na tabia ya Michelle kumsema sema sana kila wakati.
Wakati Obama alikuwa hapendi jinsi Michelle alivyokuwa akichonga sana na kumkosoa mara kwa mara, Michelle alikuwa akichukizwa na tabia ya Obama kukoroma sana wakati wa kulala na kuvuta sana sigara kiasi cha kwamba alikuwa akinuka sigara muda wote.
Mwaka 2007 wakati akifanya mahojiano na jarida la Glamour la Marekani, Michelle alisema kuwa Obama alikuwa ananuka sana sigara na kukoroma sana kiasi cha kwamba watoto wao walikuwa hawataki kulala naye.
Michelle pia alikuwa akichukizwa sana na Obama kujihusisha zaidi na siasa kuliko kuiangalia familia yake.
Mara kwa mara Michelle alimwambia Obama "Unajifikiria mwenyewe tu, sikuwahi kufikiria kwamba nitakuja kuilea familia peke yangu, sikuolewa kwaajili hii".
Michelle pia aliwahi kumwambia Obama wakati huo wakiwa na mtoto mmoja kwamba baada ya miaka minane ya ndoa yao, siku za ndoa yao zilikuwa zikihesabika na wakati wowote ingevunjika.
Kwa upande wake Obama alimwambia bibi yake Madelyn 'Toot' Dunham, ambaye alimlea alipokuwa Hawaii kwamba "Nampenda sana Michelle, lakini ni mkali sana na wakati wote ana hasira".
Maisha ya Obama na mkewe yameongelewa kwenye kitabu cha "Barack And Michelle: The Love Story " cha mwandishi wa habari wa Marekani na mtunzi wa vitabu, Christopher Andersen, ambacho kimeingia madukani wiki hii.
Historia ya Obama inaanzia Honolulu, Hawaii alikozaliwa kutokana na mama Mmarekani na baba 'Cha Pombe' (Mlevi sana) toka Kenya aliyekuwa mwanafunzi nchini Marekani.
Obama alilelewa na mama yake nchini Marekani na Indonesia wakati huo baba yake alirudi Kenya na kuoa mke mwingine.
Obama Alikutana na Michelle Robinson baada ya kumaliza mwaka wake wa kwanza kwenye chuo cha Harvard Law School, na kwenda kufanya field yake wakati wa likizo kwenye kampuni kubwa ya sheria inayoitwa Sidley Austin.
Michelle ambaye alikuwa akifanya kazi kwenye kampuni hiyo ndiye aliyepewa majukumu ya kumsimamia Obama wakati wa field yake kwenye kampuni hiyo.
Obama alivutiwa na Michelle baada ya kutambulishwa na alimwambia rafiki yake baadae kwamba "Michelle ni mrembo sana, nitatumia uchawi wangu wote kumnasa".
Ili kumwingiza kwenye mitego yake, Obama alianza kumtumia Michelle maua na barua za kimapenzi pamoja kumpigia simu mara kwa mara mpaka alipokubali mwaliko wake baada ya kumsikia akitoa hotuba kwenye mkutano wa vijana weusi wa Marekani.
Hatimaye Obama alifanikiwa kumnasa Michelle na alifunga naye ndoa ilipofika oktoba 3 mwaka 1992.
Ndani ya miaka minne ya ndoa yao huku Obama akiwa amejikita zaidi kwenye siasa na kuchaguliwa kuwa seneta wa jimbo la Illinois, matatizo yalianza kujitokeza kwenye ndoa yao.
Michelle alikuwa akichukizwa na tabia ya Obama kutofanya usafi na kutozihifadhi vizuri soksi na chupi zake kwani baada ya kuzivua alikuwa akizitelekeza kwenye sakafu.
Michelle alichukizwa pia na tabia ya Obama kutofanya kazi yoyote ya nyumbani na kuacha mataulo yaliyolowa kwenye sakafu bafuni na pia kuacha vyombo vichafu kwenye sinki baada ya kula.
Hakuna kitu ambacho Michelle alikuwa akikichukia zaidi kama uvutaji wa sigara wa kupindukia wa Obama. Michelle alikuwa akilalamika nyumba yao ilikuwa ikinuka sigara na mazulia yao yote yalikuwa na matobo kutokana na moto wa sigara.
Wakati Michelle alikuwa akiingia kulala saa nne usiku ili awahi kuamka kuwahi kwenye kazi yake aliyokuwa akilipwa pesa nyingi sana, Obama alikuwa akiingia kitandani kulala mida ya saa nane usiku.
Mbali na kuingia kitandani kulala mida hiyo, Obama alikuwa akimsumbua Michelle kwa kukoroma sana.
Kuzaliwa kwa binti yao wa kwanza Malia, julai 4 mwaka 1998 hakukusaidia kuiimarisha ndoa hiyo badala yake kuliifanya ndoa hiyo iwe hatarini.
Obama alikuwa akitumia siku nne hadi tano akiwa mji mwingine kwenye bunge la Seneti na hali hiyo ilimfanya Michelle ajihisi ametelekezwa.
Michelle alifikiria kwamba Obama alikuwa akipoteza muda kwenye siasa badala ya kufanya kazi kama mwanasheria na kulipwa pesa nyingi zaidi.
Misuko suko kwenye ndoa ya Obama ilipungua wakati binti yake wa pili Natasha ambaye anajulikana zaidi kama Sasha alipopata ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo (Meningitis) mwaka 2001 wakati huo akiwa na umri wa miezi mitatu.
Sasha aliwahishwa hospitali na ilimbidi Obama na mkewe wapokezane kukaa naye hospitali kwa masaa 72 wakati alipolazwa kwa matibabu zaidi.
Baada ya hapo utulivu ulirudi kwenye ndoa yao na mambo yote yalikaa sawa baada ya Obama kushinda uchaguzi wa urais wa Marekani.
Hatimaye mwezi novemba mwaka jana katika mji wa Chicago familia ya Obama ilitambulishwa rasmi kuwa familia namba moja ya Marekani.
"Nisingesimama hapa bila ya msaada wa rafiki yangu wa miaka 16, nguzo ya familia yangu, mke wangu Michelle Obama" alisema Obama.
Hivi sasa familia ya Obama imesahau yaliyopita na imekuwa ikitolewa mifano kama mojawapo ya familia bora duniani.
Obama Alikuwa Akikoroma Sana, Michelle Alikuwa Akichonga Sana
Nyota wa Brazili, Ronaldo de Lima ametakiwa na mahakama nchini Brazili afanye vipimo vya DNA ili kuondoa mzozo wa kubambikiwa mtoto na mwanamke raia wa Brazili anayeishi nchini Singapore.
Tangia Ronaldo aliporudi Brazili mwaka 2008 toka timu ya AC Milan ya Italia, amekuwa akikumbwa na maskendo mbali mbali kama vile kuanikwa kwenye magazeti baada ya kulala na mashoga hotelini na kisha kukataa kuwalipa baada ya huduma.
Safari hii Ronaldo amekumbwa na skendo jingine akidaiwa kuzaa na mwanamke raia wa Brazili anayeishi nchini Singapore na kisha kumkataa mtoto wake.
Ronaldo ambaye hivi sasa anaichezea timu kongwe ya Brazili ya Corinthians ametakiwa na mahakama nchini humo kufanya vipimo vya DNA ili kumaliza mzozo wa mwanamke anayedai Ronaldo ni baba wa mtoto wake mwenye umri wa miaka minne.
Taarifa toka jiji la Rio de Janeiro zinasema kwamba mwanamke huyo anayejulikana kama Michele Umrazu mwenye umri wa miaka 27, awali kabla ya kudai amezaa na Ronaldo alikuwa akidhania mtoto wake mwenye umri wa miaka minne ni wa mpenzi wake wa zamani raia wa Marekani.
Lakini baada ya vipimo vya DNA kufanyika na kugundulika kuwa mtoto huyo si wa huyo Mmarekani, Michele aligeuza kibao na kudai kuwa mtoto huyo ni wa Ronaldo.
"Nywele zake, macho yake mpaka pua vyote vinafanana na Ronaldo" alisema Michele.
Mama yake Michele alidai kwamba Ronaldo ambaye aliwahi kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa dunia mara tatu, alikutana na Michele kwa mara ya kwanza mwaka 2002 wakati wa kombe la dunia nchini Japan.
Walikutana tena mwezi wa nane mwaka 2004 ikiwa ni miezi tisa kabla ya kujifungua mtoto huyo.
Kutokana na Ronaldo kumkataa mtoto huyo, mzozo ulifika mahakamani na sasa mahakama imemtaka Ronaldo afanye vipimo vya DNA ili kumaliza mzozo huo.
Ronaldo ambaye alitimiza miaka 33 siku mbili zilizopita ana watoto wengine wawili Ronald, mwenye umri wa miaka tisa na Maria Sofia mwenye umri wa miezi tisa.
Ronaldo alithibitisha mwezi uliopita kuwa anatarajia mtoto wa tatu mwanzoni mwa mwaka ujao.
source.nifahamishe.com
Atumia Staili za Mike Tyson Kunyofoa Sikio la Mpenzi Wake
Mwanaume mmoja wa nchini Ujerumani mwenye wivu wa ajabu baada ya mpenzi wake kuamua kuvunja uhusiano wao, kwanza alimshushia kipigo cha nguvu na kisha kutumia staili ya Mike Tyson kwa kumng'ata sikio lake na kunyofoa kipande cha sikio lake
Mike J. mfanyakazi wa kampuni ya ujenzi nchini Ujerumani alitumia staili ya wajina wake Mike Tyson kumng'ata sikio mpenzi wake aliyeamua kuvunja uhusiano wao.
Mike mwenye umri wa miaka 29 alipata hasira za ajabu baada ya mpenzi wake aliyetajwa kwa jina moja la Stephanie mwenye umri wa miaka 19, mwanafunzi wa sekondari nchini humo kumtamkia wazi kuwa hataki kuendelea na uhusiano wao wa kimapenzi wa miaka miwili.
"Mike ana wivu wa ajabu, muda mfupi baada ya kutamka maneno mazuri ya kimapenzi hubadilika ghafla na kuanza kunipiga, baada ya kubusiana naye huanza kuonyesha hasira zake", alisema Stephanie anayetoka mji wa Jessen.
"Baada ya kushauriana na rafiki zangu niliamua kuvunja uhusiano wetu" aliendelea kusema Stephanie.
Stephanie alisema kwamba baada ya kumtamkia wazi Mike kuwa hataki kuendelea na uhusiano wao wa kimapenzi, Mike hakuridhia na alimfuata siku hiyo hiyo nyumbani kwake mida ya usiku.
"Aliponigongea mlango nilidhani anakuja tuongee naye kuhusiana na uhusiano wetu lakini alipoingia ndani moja kwa moja alinirukia na kunipiga na kisha kuning'ata sikio na kunyofoa kipande cha sikio langu na kisha kukitema chini, kila sehemu ilijaa damu" alisema Stephanie.
Stephanie alidokeza kwamba alifanikiwa kukipata kipande cha sikio lake kilichonyofolewa lakini madaktari walishindwa kukiunga tena.
Mike alifikishwa mahakamani na alihukumiwa kifungo cha nje cha mwaka mmoja pamoja na kulipa faini ya euro 1600.
Mike alipinga hukumu hiyo na alidai atakata rufaa.
Tukio hili limekumbushia tukio la bingwa wa zamani wa ndondi Mike Tyson kumng'ata sikio Evander Holyfield wakati wa pambano lao lililofanyika juni 28 mwaka 1997.
source.nifahamishe.com