Picha ya Yesu Akinywa Pombe Yazua Kasheshe India

Saturday, February 20, 2010 / Posted by ishak / comments (1)


Serikali ya India imelazimika kuvikusanya vitabu vyote vya shule za msingi vilivyochapishwa na kampuni moja nchini humo vikiwa na picha ya Yesu akinywa pombe huku akiwa ameshikilia sigara.
Serikali ya India katika jimbo la Meghalaya inavikusanya vitabu vipya vilivyochapishwa kwaajili ya shule za msingi nchini humo vikiwa na picha ya Yesu akiwa ameshikilia kopo la bia mkono mmoja huku mkono mwingine akiwa ameshikilia sigara.

Vitabu hivyo vilianza kutumika kwenye shule za msingi na picha hiyo ya Yesu imesababisha kasheshe kubwa katika jimbo hilo la Meghalaya ambalo asilimia 70 ya wakazi wake ni wakristo.

Waziri wa elimu wa jimbo hilo Ampareen Lyngdoh amesema kuwa taratibu za kisheria zimeanza kuandaliwa dhidi ya kampuni iliyochapisha vitabu hivyo.

"Tunajiandaa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya kampuni ya Skyline Publications ambayo imechapisha vitabu vilivyozua mtafaruku," alisema waziri Mr Lyngdoh.

Picha hiyo ya Yesu ilikuwa kwenye kava la vitabu vya mazoezi ya kuandika kwa shule za msingi.

Waziri Lyngdoh amesema kuwa vitabu hivyo vilianza kutumika kwenye shule za msingi za binafsi na serikali ya India imeamua kuvikusanya vitabu vyote vyenye picha hiyo toka kwenye mashule yote ya India na kwenye maduka ya vitabu.

Kampuni ya Skyline Publications yenye makazi yake mjini New Delhi haijasema chochote kuhusiana na tukio hilo.

source nifahamishe

Oh Mapenzi Kweli Yanachanganya Akili!

Saturday, February 20, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Oh mapenzi mapenzi, wakati mwingine mapenzi hutufanya tufanye mambo mengi ya ajabu tusiyotarajia kuyafanya, mapenzi hayo hayo ndiyo yaliyomfanya mwanaume mmoja wa nchini Ujerumani awe anaruka ukuta kuingia jela kumfuata mpenzi wake aliyetupwa jela, alifanya hivyo si mara moja ni kila siku usiku mpaka siku aliponaswa akiruka ukuta.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 33 wa mji wa Bielefeld nchini Ujerumani aliyetambulika kwa jina la Daniele E. alijikuta na yeye akitupwa jela kwa kosa la kuruka ukuta na kuingia jela.

Kwa mujibu wa gazeti la kila siku la mji huo Westfalen-Blatt, Daniele amepatikana na hatia ya kuzamia jela na kesi yake itaanza kusikilizwa mwezi ujao.

Taarifa zilisema kuwa Daniele alikuwa akiruka ukuta kila siku usiku kuingia kwenye jela ya wanawake yenye ulinzi mdogo ili kumfuata mpenzi wake aliyetupwa jela baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya.

Daniele alisema kuwa alikuwa anashindwa kuishi mbali na mpenzi wake aliyesema alimvalisha pete ya uchumba kabla ya kukamatwa na kutupwa jela.

Mambo yalikuwa moto moto kwenye selo namba 13 ya jela hiyo ambayo haikutajwa jina, Daniele alisababisha kero kwa wafungwa wengine wanawake kutokana na kelele za mapenzi walizokuwa wakizitoa usiku yeye na mpenzi wake.

Baadhi ya wafungwa wanawake walilamika kuwa Daniele alikuwa akiwakosesha usingizi huku wafungwa wengine wakiwa na matumaini siku moja Daniele atawatimizia na wao hamu zao za kimapenzi.

Baada ya malalamiko kufikishwa kwa maafisa wa jela hiyo, kamera za ulinzi ziliwekwa kuzunguka ukuta wa jela hiyo na ndipo novemba 8 mwaka jana Daniele aliponaswa akiruka ukuta kuingia kwenye jela hiyo.

Daniele alitupwa jela ya wanaume akisubiri hukumu ya kesi hiyo pamoja na kesi zingine za kupora pesa kwenye vituo kadhaa vya mafuta zilizogundulika baada ya kukamatwa kwake.

Kwa mujibu wa sheria za jela hiyo, Daniele na mpenzi wake wangeweza kupewa ruhusa ya kutembeleana mara kwa mara ili kuokoa uhusiano wao lakini tatizo ni kwamba mpenzi wa Daniele aliandika jina la mwanaume mwingine kama mpenzi wake siku aliyotupwa jela kutumikia kifungo chake.

source nifahamishe

Kikwete ziarani Jordan, Uturuki

Thursday, February 18, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


RAIS Jakaya Kikwete hayuko nchini na ameanza ziara ya mwaliko nchini Uturuki na Jordan kwa mwaliko wa viongozi wa nchi hizo mbili.

Rais Kikwete aliyeondoka nchini jana aliyeongozana na mkewe Salma wakiwemo na wafanyabiashara mbalimbali wa Tanzania.


Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, ilisema jana kuwa Rais Kikwete alipokea na kukubali mwaliko wa kutembelea Uturuki Februari mwaka jana wakati Rais Gul alipotembelea Tanzania kwa ziara ya pili, kwa mwaliko wa Rais Kikwete.

Katika ziara hiyo Rais Kikwete anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake, na pia Waziri Mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan.

Rais Kikwete pia atakutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Chama cha Wafanyabiashara wa Uturuki, pamoja na mabalozi wa Afrika wanaoziwakilisha nchi zao katika nchi hiyo.

Tanzania na Uturuki zinatarajiwa kutiliana saini mikataba sita ya ushirikiano na pia Rais Kikwete atatunukiwa shahada ya juu (PHD) ya heshima na Chuo Kikuu cha Faith cha Fatih, mjini Istanbul.

Rais Kikwete anatarajiwa kuondoka Uturuki Jumapili, Februari 21, 2010, kwenda Jordan kwa ziara ya siku tatu kwa mwaliko wa Mfalme Abdullah wa Pili.
source nifahamishe

Mwanajeshi amcharanga mkewe kwa visu

Thursday, February 18, 2010 / Posted by ishak / comments (0)

MWANAJESHI Mstaafu wa Jeshi la JWTZ, Mang'eng'e Matiko, amemchoma kisu mkewe baada ya kutopatikana kwa maelewano katika ugomvi wa ardhi.

Ilidaiwa kuwa mwanajeshi huyo alimchoma kisu mkewe katika sehemu mbalimbali za mwili wake na kupelekea kuanguka ghafla baada ya mwanamke huyo kukataa kuuzwa kwa ardhi waliyokuwa wakiimiliki wote kwa pamoja.

Mume huyo alitaka kuuza ardhi hiyo lakini mwanamke huyo alipinga kuuzwa kwa ardhi hiyo kwa kudai ingewasaidia baadae kwa kuwa walikuwa na watoto.

Hivyo baada ya mabishano hayo mwanajeshi huyo alichukua uamuzi wa kumchoma kisu mkewe na kupelekea majeruhi hayo.


Majirani wa familia hiyo walidai kuwa alichukua uamuzi wa kumchoma visu katika sehemu za mwili wake na aliweza kuokolewa baada ya mwanamke huyo kupiga kelele na majirani kufika nyumbani kwao hapo na kumkuta wmanamke huyo anatoka damu nyingi na ghafla alipoteza fahamu.


Walidai kuwa mwanamke huyo hali yake ilikuwa mbaya na alipelekwa katika kituo cha Polisi Karakata baaada ya polisi kufika eneo hilo na kutumia gari la polisi lililokuwa na namba T 481 AER aina ya Land Rover Defender na kukimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.

source nifahamishe

Aanguka toka ghorofa ya tisa

Thursday, February 18, 2010 / Posted by ishak / comments (0)

FUNDI ujenzi aliyefahamika kwa jina moja la Ally, amekufa baada ya kuanguka kutoka ghorofa ya tisa wakasti akiwa katika shughuli za ujenzi katika ghorofa hiyo.

Fundi huyo alikuwa katika ya nyumba ya Shubas Patel iliyokuwa na ghorofa 12 na alianguka wakati akiwa kazini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, amesema ajali hiyo ilitokea jana, saa 10 jioni, Mtaa wa Sewa na Zanaki Ilala jijini Dar es Salaam.

Alisema fundi huyo, akiwa na wenzake wakiendelea na kazi kwenye ghorofa ya tisa, ghafla alidondoka hadi ghorofa ya tatu ambapo alinasa kwenye kizuizi cha mabati.

Alisema alipata majeraha kwenye paji la uso pamoja na kuvunjika mkono wake wa kushoto.

Hata hivyo wenzake walimkimbiza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu na alikufa muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini hapo.


source nifahamishe

17 wa ukoo mmoja wauawa kinyama Mara

Thursday, February 18, 2010 / Posted by ishak / comments (0)

WATU 17 wa ukoo mmoja kutoka familia tatu wameuawa kikatili kwa kwa kuchinjwa kama kuku kwa kukatwakatwa mapanga na watu wasiojulikana katika mtaa wa Bhugharanjabho Kata ya Buhare huko mkoani Mara.
Mbali na kuwanjinjaw atu hao pia waharifu hao walifanya uharibifu kuuwa mifugo ya marehemu hao walikatakata ng’ombe na mbuzi na kuacha mizoga katika mji huo.

Tukio hilo la kihistoria na la kutisha na la kwanza kutokea mkoani Mara, lilitokea usiku wa kuamikia jana, majira ya saa 8 usiku katika kata hiyo.

Familia ya kwanza iliyochinjwa katika tukio hilo ni ile ya Kawawa Kinguye ambapo mke na watoto wake watano waliuawa, familia ya pili ni ile ya mdogo wake Kinguye aitwae Moris Mgaya iliweza kupoteza watu sita, familia ya tatu ni ile ya binamu yao aliyetambulika kwa jina la Mgaya Nyarukende pia watu watano waliuawa katika familia hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Mstaafu Enos Mfuru.aliliagiza Jeshi la Polisi mkoani humo kufunga ofisi zao mara moja na kuanza msako mkali na kwa gharama yoyote dhidi ya watu waliofanya mauaji hayo ili wafikishwe katika vyombo vya sheria haraka iwezekanavyo.

Na kuwataka wananchi waishio maeneo hayo kutoa ushirikiano wa kutosha kuwasaka wauaji hao ambao utafanikisha kutiwa mbaroni watuhumiwa hao haraka.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Robert Boaz, alisema tayari kikosi kikubwa cha askari wake kisambazwa kila kona kuanza msako huo ili kuhakikisha watu wote waliohusika wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Ilidaiwa kuwa tukio hilo linavyosemekana ni la visasi, taarifa ambazo zilipatikana jana katika eneo la tukio zilidai kuwa huenda tukio hilo likahusishwa na ulipishaji kisasi kutokana na marehemu Kawawa kuwahi kutuhumiwa kuua watu wawili waliodhaniwa ni wezi wa mifugo, lakini baadaye ikabainika kuwa walikuwa wameua na nungunungu.

Mwaka 2006 baada ya Kawawa kuachiwa, watu wasiojulikana walivamia boma lake na kuua mama na dada yake Kawawa na kuahidi kuwa wangerudi tena na kuhisiwa huenda tukio hilo ni wale watu walioahidi wangerudi.

Taarifa hizo ziliendela kusema kuwa, marehemu Kawawa aliachiwa huru na Mahakama Kuu baada ya kuonekana hana hatia na kukuta ndugu zake hao walikwisha kuuawa na watu hao na kwamba tangu wakati huo aliendelea kuishi eneo hilo hadi hapo jana nay eye yalipomkuta umauti.

Hadi jana saa 12 jioni polisi walikuwa wakizifanyia uchunguzi maiti hizo katika eneo la tukio kutokana na kuwa katika hali mbaya, kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Musoma Geofrey Ngatuni, miili ya watu hao inatarajiwa kuzikwa leo endapo uchunguzi huo utakamilika.

source nifahamishe

Watano wafariki kwa kufunikwa na kifusi –Dodoma

Tuesday, February 16, 2010 / Posted by ishak / comments (0)

WATU watano wamefariki dunia papo hapo jana, baada ya kufukiwa na kifusi wakati wakiwa wanachimba kokoto huko katika kijiji cha Ntyuka, mkoani Dodoma
Waliofariki katika tukio hilo ni wanawake watatu na watoto wawili ambao walikuwa na mama zao eneo la tukio.

Wanawake hao ni Monica Chizumi na mwanawe Porina Chizumi mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu, Mwajuma Mnubi na mtoto wake, Jonas Mnubi wa mwaka mmoja na miezi 8 na Mbeleje Ndingomo

Mbali na waliokufa dunia watu wengine wawili ambao ni Beatrice Chizumi na Noel Lazaro alijeruhiwa na walikimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma baada ya kunusurika katika tukio hilo.

Tukio hilo la kusikitisha lililotokea jana majira ya saa 7 mchana kijijini humo.


source nifahamishe

Mwanamke Atupwa Jela Miaka 25 Kwa Kumuua Mbakaji Wake

Tuesday, February 16, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanamke mmoja nchini Afrika Kusini amehukumiwa kwenda jela miaka 25 kwa moyo wa ukatili aliouonyesha wa kumuua mbakaji wake na kisha kuifukia maiti yake kabla ya kuifukua na kuwalisha mamba maiti hiyo.
Michelle Nadasen mama wa mtoto mmoja wa nchini Afrika Kusini ametupwa jela miaka 25 kwa kumuua mbakaji wake na kisha kuwalisha mamba maiti yake.

Michelle mwenye umri wa miaka 23 alimuua mwanaume aliyemnyanyasa kijinsia na kisha kuizika maiti yake mbele ya nyumba yake.

Siku ya nne baada ya kuizika maiti hiyo, Michelle kwa kushirikiana na mpenzi wake waliifukua maiti hiyo na kuitupa kwenye mto wenye mamba wengi.

Akisomewa hukumu katika mahakama kuu ya mji wa Pietermaritzburg, jaji wa kesi hiyo alisema kuwa Michelle ameonyesha moyo wa kikatili na usio na utu kwa kulala siku nne katika nyumba ambayo maiti ya mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina la Gansen Gounden ilikuwa imefukiwa.

Michelle alikiri kosa lake na kuelezea jinsi yeye na mpenzi wake walivyoizika maiti ya Gounden katika shimo la futi chache walilochimba chini ya mwembe uliopo nyuma ya nyumba yao.

Michelle pia aliielezea mahakama jinsi alivyosaidiana na mpenzi wake kuitupa maiti ya Gounden kwenye mto Enseleni wenye mamba wengi.

source nifahamishe

Amuua Mpenzi Wake Baada ya Kuambiwa Hayawezi Majambozi

Tuesday, February 16, 2010 / Posted by ishak / comments (0)

Mwanaume mmoja nchini Uingereza amefikishwa mahakamani kwa kumuua mpenzi wake aliyemkebehi kuwa ana uume mdogo sana hivyo hawezi kumtosheleza hamu zake za kimapenzi.
Peter Ling, 50, aliiambia mahakama kuwa alishindwa kuzitawala hasira zake baada ya kipenzi chake Linda Casey kumwambia kuwa hana kiungo cha siri kikubwa cha kuweza kumtosheleza hamu zake za kimapenzi, limeripoti gazeti la Daily Mail la Uingereza.

Ling, aliandaa sehemu ya starehe jijini London kwaajili ya kukutana na Linda akiwa na nia ya kumuuliza kama Linda ana mwanaume mwingine pembeni.

Baada ya kukutana na baadae kufanya naye mapenzi, Ling alimgeukia Linda na kuanza kumhoji kuhusiana na emails alizozituma zinazohusiana na tovuti za kutafuta wachumba na pia kama ana mwanaume mwingine pembeni.

Wakati wa mabishano yaliyozuka wakati huo, Linda aliongelea masuala ya viungo vya siri vya Ling akimuambia kuwa uume wake ni mdogo sana kuweza kumtosheleza.

"Nilikuwa ni kama bomu lililokuwa likisubiria kulipuka wakati wowote, alipotoa maoni hayo moja kwa moja yalizama kwenye akili zangu", Ling aliiambia mahakama.

"Siku zote nimekuwa nikiushuku ukubwa wa uume wangu", aliongeza Ling.

Baada ya Linda kutoa maoni hayo, Ling alianza kumshushia kipigo Linda mpaka alipofariki.

Ling anaitaka mahakama iamue kesi hiyo kama mauaji bila kukusudia badala ya kesi ya mauaji ya kukusudia aliyofunguliwa.


source nifahamishe