Radi Yaua Wanafunzi 18 Shuleni Uganda

Saturday, July 02, 2011 / Posted by ishak / comments (0)

Radi iliyopiga kwenye shule moja ya msingi nchini Uganda, imewaua watoto 18 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 50.
Radi hiyo iliyopiga kwenye shule ya msingi ya Runyanya katika wilaya ya Kiryandongo magharibi wa jiji la Kampala, imepelekea vifo vya wanafunzi 15 wa kike na watatu wa kiume.

Msemaji wa polisi, Judith Nabakooba alisema kuwa zaidi ya wanafunzi wengine 50 walijeruhiwa na radi hiyo.

“Baadhi ya wanafunzi waliojeruhiwa waliwahishwa hospitali za karibu lakini wanafunzi 15 waliojeruhiwa vibaya sana waliwahishwa kwenye hospitali kuu ya wilaya”, alisema Nabakooba.

Magazeti ya kila siku ya Uganda yaliripoti kuwa wanafunzi wengine 21 katika shule nyingine iliyopo kwenye wilaya ya Zombo, nao walijeruhiwa vibaya baada ya kuunguzwa na radi.

Wakati gazeti la The Daily Monitor likiripoti jumla ya wanafunzi 28 wameishafariki kutokana na radi tangu wiki iliyopita, msemaji wa polisi hakutoa idadi kamili ya wanafunzi waliofariki kutokana na radi katika msimu huu wa mvua zilizoambatana na radisource nifahamishe