Makahaba Kuvaa Vizibao Vya Njano Ili Waonekane Vizuri

Thursday, October 28, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Makahaba wa nchini Hispania wanaowinda wanaume pembeni ya barabara wameanza kuvaa vizibao vya njano vinavyoakisi mwanga ili waweze kuonekana vizuri.
Ili kuepuka faini ya euro 40, makahaba katika mji wa Els Alamus kaskazini mwa Hispania wameanza kufuata masharti ya serikali ya kuvaa vizibao vya njano vinavyoakisi mwanga.

Meya wa mji huo aliamuru makahaba wote wanaosimama pembeni ya barabara kuwinda wanaume wavae vizibao hivyo ili kuwafanya waonekane vizuri na hivyo kuepusha kutokea kwa ajali.

Taarifa ya meya wa mji huo ilisema kuwa baadhi ya makahaba wameanza kuvaa vizibao hivyo baada ya polisi kuanza kuwatoza faini ya euro 40 makahaba wanaosimama pembeni ya barabara kuu kuwinda wateja.

Nchini Hispania kuna jumla ya wanawake laki tatu wanaofanya biashara ya ukahaba. Mwanamke anaruhusiwa kisheria kufanya ukahaba nchini Hispania ingawa kujinufaisha kwa kuwatafutia makahaba wateja ni kinyume cha sheria.

Ni jambo la kawaida katika miji mbalimbali nchini Hispania kuwaona wanawake wanaovaa nguo fupi sana wakiwa wamesimama pembeni ya barabara wakitafuta wanaume.

Utafiti uliofanywa hivi karibuni nchini Hispania ulionyesha kuwa mwanaume mmoja kati ya wanne nchini Hispania ameishawahi kununua penzi toka kwa kahaba.

source nifahamishe

Apata Mimba Sita Nje ya Ndoa, Awaua Watoto na Kuficha Maiti

Thursday, October 28, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanamke wa nchini Marekani ambaye alipata mimba sita nje ya ndoa bila ya mume wake kujua, aliwaua watoto wake na kuzificha maiti zao kwenye sanduku.
Michele Kalina mwenye umri wa miaka 44 mkazi wa Pennsylvania nchini Marekani, alizificha mimba sita alizozipata kwa kufanya mapenzi nje ya ndoa na aliwaua watoto wote waliotokana na mimba hizo na kuzificha maiti zao kwenye masanduku.

Matokeo ya DNA yalionyesha kuwa mifupa ya binadamu iliyokutwa kwenye sandaku lililotiwa kufuli ilikuwa ni mifupa ya watoto watano ambapo wanne kati ya watoto hao walizaliwa wakiwa hai wakati mmoja alizaliwa akiwa tayari ameishafariki.

Kalina na mumewe wa ndoa, Jeffrey walifanikiwa kupata watoto wawili, mmoja wa kike mwenye umri wa miaka 19 na mwingine wa kiume ambaye aifariki dunia mwaka 2003 akiwa na umri wa miaka 13.

Mahakama ilithibitisha kuwa watoto wanne kati ya sita Kalina alizaa na kibuzi chake nje ya ndoa.

Mume wa Kalina na binti yake waligundua mifupa ya watoto wachanga ikiwa imefichwa kwenye maboksi ndani ya sanduku mwezi wa nane mwaka huu ambapo waliripoti polisi na Kalina alitiwa mbaroni.

Mume wa Kalina aliwaambia polisi kuwa ni mara moja tu alihisi mke wake alikuwa mjamzito lakini hakuwa na uhakika.

Mwanaume aliyekuwa akijiiba na Kalina ambaye jina lake liliwekwa kapuni, aliwaambia polisi kuwa Kalina alimwambia kuwa alikuwa na uvimbe tumboni uliolifanya tumbo lake liwe kubwa na uvimbe huo ulikuwa ukimtokea mara kwa mara.

Mwanaume huyo naye alisisitiza kuwa hakugundua kama Kalina alikuwa mjamzito.

Kalina ametupwa jela akikabiliwa na makosa ya mauaji na kuficha maiti za watoto wake.

Kesi ya Kalina itaanza kusikilizwa wiki hii.

source nifahamishe

Mamba Aiangusha Ndege Kongo, 20 Wafariki

Sunday, October 24, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Watu 20 wamepoteza maisha yao nchini Kongo baada ya ndege waliyokuwamo kuanguka toka angani baada ya mamba aliyeingizwa kinyemela ndani ya ndege hiyo kuchoropoka na kuleta kizazaa kikubwa ndani ya ndege.
Abiria aliyetaka kumsafirisha mamba wake kinyemela kwa kumficha mamba huyo ndani ya begi na kuingia nalo ndani ya ndege amesababisha vifo vya watu 20.

Ni mtu mmoja tu kati ya watu 21 waliokuwemo ndani ya ndege huyo ndiye aliyenusurika maisha yake.

Kwa mujibu wa abiria huyo aliyeponea chupu chupu kupoteza maisha yake, mamba huyo aliyekuwa amefichwa ndani ya begi na kuingizwa kinyemela ndani ya ndege nchini Kongo alisababisha mtafaruku mkubwa ndani ya ndege na kupelekea ndege kuanguka.

Mamba huyo alichoropoka toka kwenye begi wakati ndege ndogo ya abiria iliyotengenezwa nchini Czech aina ya Let 410 ilipokuwa angani ikitoka mji wa Kinshasa kuelekea Bandundu.

Ilikuwa ni patashika nguo kuchanika wakati mamba huyo alipoanza kuranda randa ndani ya ndege na kupelekea abiria waviache viti vyao kusalimisha maisha yao.

Wahudumu wa ndani ya ndege walikimbilia ndani ya chumba cha marubani na kufuatiwa na baadhi ya abiria ambao nao waliamua kuitumia nafasi hiyo kusalimisha maisha yao.

Inasemekana kuwa ndege hiyo ilianguka toka angani kutokana na uzito ndani ya ndege kuelemea upande mmoja.

Ndege hiyo iliangukia kwenye nyumba iliyopo maili chache toka kwenye uwanja wa ndege ambao ndege hiyo ilipanga kutua.

Mamba aliyesababisha ajali hiyo alitoka salama salimini toka kwenye mabaki ya ndege hiyo lakini aliuliwa kwa kuchomwachomwa na kisu na watu waliojitokeza kuwaokoa majeruhi wa ajali hiyo.

source nifahamishe