Picha ya Maiti ya Mandela Yazua Mzozo Afrika Kusini

Saturday, July 10, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Msanii ambaye amechora picha ya rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela akiwa amefariki maiti yake ikifanyiwa uchunguzi ameingia kwenye mzozo mkubwa na chama tawala cha ANC.
Chama tawala nchini Afrika Kusini, African National Congress (ANC) kimelaani picha hiyo ambayo imetengezwa na msanii wa nchini humo na kuwekwa kwenye shopping centre mjini Johannesburg.

ANC imesema kuwa picha hiyo inamvunjia heshima mzee Mandela kwa kuzivunja haki zake.

Picha hiyo inauonyesha mwili wa Mandela ukiwa umepasuliwa huku viongozi wakuu wa Afrika Kusini wakiwa wameuzunguka.

Katika picha hiyo, maiti ya Mandela inaonekana ikiwa imelazwa kwenye meza huku mwanaharakati wa kupambana na ukimwi, Nkosi Johnson, ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 12, anaonekana akiifanyia uchunguzi maiti ya Mandela.

Desmond Tutu, rais wa zamani wa Afrika Kusini, FW de Klerk, Thabo Mbeki na wanasiasa wengine wanaonekana wakiwa pembeni wakiangalia kinachoendelea.

Pamoja na tuhuma zote, msanii Yiull Damaso aliyechora picha hiyo amesema kuwa nia yake kubwa ni kuwakumbusha watu juu ya kifo.

"Nelson Mandela ni mtu mkubwa sana, lakini ni mtu kama watu wengine.. kifo cha Mandela ni kitu ambacho kitatokea na sote kwa pamoja kama taifa itatubidi tukipokee", alisema Damaso alipokuwa akiongea na shirika la habari la Uingereza la BBC.

Kuongelea kifo cha Mandela mwenye umri wa miaka 91 kunaonekana kama ni uchuro na huonekana kama kumvunjia heshima mzee Mandela.

Mwandishi wa habari wa BBC alisema kuwa wananchi wa Afrika Kusini hawazungumzii kabisa kifo cha Mandela kwa kuhofia ukweli kuwa siku moja wataamka mzee Mandela akiwa hayupo tena.

Uongozi wa Hyde Park Mall ambako picha hiyo imewekwa kama maonyesho, umesema kuwa umepokea malalamiko mengi kuhusiana na picha hiyo kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo ndugu wa Mandela.

Hata hivyo uongozi huo umesema utaendelea kuunga mkono Uhuru wa Kujieleza kwenye Sanaa.


source nifahamishe

Maziwa ya Watoto Yenye Sumu Yagundulika Tena China

Saturday, July 10, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Kwa mara nyingine tena serikali ya China imekamata tani 64 za maziwa ya watoto ambayo yamechanganywa na kemikali za viwandani ili kufoji ubora wa maziwa. Maziwa hayo yaliua watoto sita mwishoni mwa mwaka juzi na kuwageuza wagonjwa mamia ya watoto.
Maziwa ya watoto yenye sumu ambayo yaliua watoto sita na kuwafanya maelfu ya watoto wawe wagonjwa, yamegundulika tena nchini China.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Xinhua la nchini China, tani 64 za maziwa ya watoto ambayo yamechanganywa na kemikali za melamine zinazotumika viwandani, zimegundulika kwenye jimbo la Qinghai nchini humo.

Kemikali za melamine hutumika zaidi kwenye viwanda vya kutengeneza plastiki lakini zinapochangwa na maziwa ya watoto huyafanya maziwa yaonekane yana protini nyingi sana hivyo kuyafanya maziwa hayo yaonekane yana ubora wa hali ya juu na bei yake kuwa juu.

Taarifa iliyotolewa ilisema kuwa waandaaji wa maziwa hayo waliweka kiasi cha melamine mara 500 zaidi ya kiwango kinachokubalika kisheria.

Kemikali ya melamine iliwasababishia watoto waliotumia maziwa hayo kuwa na ugonjwa wa kidole cha tumbo na figo zao kushindwa kufanya kazi.

Watoto sita walifariki na watoto wengine 300,000 waliugua ghafla na kulazimika kupatiwa matibabu.

Mwezi novemba mwaka jana, watu wawili waliuliwa kwa kudungwa sindano za sumu nchini China kwa kujihusisha na biashara ya kutengeneza na kuuza maziwa hayo ya watoto yenye sumu.

source nifahamishe

Wachezaji wa Hispania Waingizwa Mjini Afrika Kusini

Saturday, July 10, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Wachezaji wawili wa timu ya taifa ya soka ya Hispania ambayo itacheza fainali ya kombe la dunia siku ya jumapili, wameibiwa mali zao walizoziacha kwenye vyumba vya hoteli waliyofikia nchini Afrika Kusini.
Sergio Busquets na Pedro Rodriguez waliibiwa mali zao hotelini wakati Hispania ilipokuwa ikijiandaa kucheza mechi ya nusu fainali ya kombe la dunia dhidi ya Ujerumani mjini Durban.

Vyombo vya habari vya Hispania vimeripoti kuwa vyumba vya wachezaji hao vilivunjwa na wezi walifanikiwa kuondoka na baadhi ya vitu walivyovikuta kwenye vyumba hivyo.

Busquets aliibiwa euro 800 wakati Pedro aliibiwa euro 1,000 zilizokuwa kwenye sefu yake.

"Hakuna mtu anayependa kuibiwa" alisema Busquets.

Shirikisho la soka la Hispania halijasema chochote kuhusiana na wizi huo.

Mwanzoni mwa mechi za fainali za kombe la dunia, wachezaji watatu wa Ugiriki waliibiwa pesa zao walizoziacha kwenye vyumba vyao vya hoteli mjini Durban.

Hispania itacheza na Uholanzi siku ya jumapili katika mechi ya fainali ya kombe la dunia.


source nifahamishe

Mwanamke Afariki Akiangalia Video ya Ngono

Friday, July 09, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanamke wa nchini Uingereza ambaye inadaiwa alikuwa na afya njema bila matatizo yoyote ya kiafya, amefariki dunia kutokana na shambulio la moyo lililosababishwa na msisimuko alioupata wakati akiangalia filamu ya ngono.
Nicola Paginton, 30, alikutwa amefariki kwenye kitanda chake huku toy la vibrator likiwa pembeni yake na filamu ya ngono ikiendelea kuonekana kwenye laptop yake, limeripoti gazeti la The Sun la Uingereza .

Daktari aliyeifanyia uchunguzi maiti ya Nicola alisema kuwa Nicola alikuwa fiti na mwenye afya njema kabla ya kifo chake cha ghafla.

"Hakuna kitu kwenye moyo wake ambacho naweza kukitaja kama sababu ya kifo chake cha ghafla", alisema daktari huyo.

Nicola inasemekana alifariki kutokana na shambulio la moyo lililomkumba ghafla baada ya mapigo ya moyo kuongezeka kwa kasi kutokana na msisimuko wa kingono alioukuwa akiupata.

Maiti ya Nicola iligundulika nyumbani kwake baada ya baada ya polisi kwenda nyumbani kwake kufuatia taarifa kuwa hajaonekana kazini kwa siku kadhaa.

source nifahamishe

Keki ya Bethidei Kutimiza Miaka 130

Friday, July 09, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Bibi Antisa Khvichava wa nchini Georgia ambaye alizaliwa mwaka 1880 alisherehekea siku yake ya kuzaliwa jana kwa kukata keki iliyokuwa na maandishi ya umri wake Miaka 130.
Bibi Antisa Khvichava anayeishi kwenye kijiji cha Sachire magharibi mwa Georgia, alizaliwa julai 8 mwaka 1880 na kwa mujibu wa maafisa wa Georgia, Antisa ndiye mtu ambaye ameishi miaka mingi kuliko watu wote duniani.

Maafisa wa Georgia walimtembelea bibi Antisa Khvichava ambaye alistaafu kazi yake ya kuvuna chai mwaka 1965 wakati huo akiwa na umri wa miaka 85.

Maafisa hao walimwonyesha bibi Antisa nyaraka mbili ambazo alizipoteza, moja ikionyesha tarehe yake ya kuzaliwa kama ilivyoandikwa kwenye cheti chake cha kuzaliwa ambacho amekipoteza.

Bibi Antisa alikata keki aliyoletewa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa na kutimiza miaka 130.

Bibi Antisa ambaye hutembea kwa kutumia mkongoja, ana mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Mikhail mwenye umri wa miaka 70. Mikhail alizaliwa wakati mama yake akiwa na umri wa miaka 60.

Bi Antisa ana wajukuu 10, vitukuu 12 na vilembwe sita.

source nifahamishe

PWEZA ATATABIRI TENA .........?

Thursday, July 08, 2010 / Posted by ishak / comments (2)

Wapenzi wasomaji munaonaje kuhusu pweza,final ya tarehe 11 ataleta mshindi mapema kama alivyofanya mwanzo

toa maoni yako


siku njema

Mwanamke Ajaribu Kufungua Mlango wa Ndege Ikiwa Angani

Thursday, July 08, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanamke mmoja nchini Kanada alisababisha kizaazaa ndani ya ndege iliyokuwa imebeba abiria 131 wakati alipolazimisha kufungua mlango wa ndege huku ndege ikiwa angani.
Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Barbara Loretta Morton, 47, alipelekea ndege ibadili mwelekeo wake na kutua kwa dharura baada ya kulazimisha kufungua mlango wa ndege huku ndege ikiwa angani.

Wafanyakazi wa ndani ya ndege ya WestJet ambayo ilikuwa imebeba abiria 131 walitumia nguvu za ziada kumzuia mwanamama huyo asifungue mlango wa ndege, iliripoti televisheni ya CTV News.

Ndege hiyo iliyokuwa ikitoka Calgary kuelekea Halifax, ililazimika kutua kwa dharura kwenye uwanja wa ndege wa Winnipeg.

Barbara alikamatwa na alifunguliwa mashtaka ya kuwashambulia watu, kuhatarisha maisha ya watu na kukataa kufuata maelezo ya wafanyakazi wa ndani ya ndege.

Mfanyakazi mmoja wa ndani ya ndege hiyo na abiria mmoja mwenye umri wa miaka 77 walijeruhiwa katika purukushani hiyo ya kumzuia Barbara asifungue mlango wa ndege.


source nifahamishe

Mike Tyson Aenda Makka Kuhiji

Tuesday, July 06, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Bingwa wa dunia wa zamani wa ndondi, Mike Tyson ambaye alibadili dini kuwa muislamu alipokuwa jela kwenye miaka ya 1990 yupo nchini Saudi Arabia kwaajili ya hija ndogo.
Bingwa wa dunia wa zamani wa ngumi za uzito wa juu, Mike Tyson anatembelea miji mitakatifu ya waislamu Makka na Madina kwaajili ya kuhiji.

Tyson ambaye alikuwa bingwa dunia kuanzia mwaka 1986 hadi 1990, aliwasili Madina siku ya ijumaa akiwa na maafisa wa umoja wa Daa'wa wa Kanada kwaajili ya Umrah ambayo ni hija ndogo.

Baada ya kutoka Madina, Tyson ataenda Makka na gazeti la Okaz la Saudia limeripoti kuwa Tyson ana mpango wa kutembelea pia miji mingine ya Saudia.

Tyson mwenye umri wa miaka 44 alibadili dini kuwa muislamu wakati alipokuwa jela akitumikia kifungo cha miaka 10 jela kwa kumbaka mrembo wa Marekani mwaka 1991. Hata hivyo alitumikia miaka mitatu jela na kuachiwa huru.

Baada ya kutoka jela alijaribu kurudi tena kwenye ngumi lakini hakuweza kulirudia taji lake na mwishoe aliachana na ndondi mwaka 2005.

source nifahamishe

Mama Amuua Mtoto Wake na Kuliuza Sikio Lake Kwa Mganga

Tuesday, July 06, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mama mmoja nchini Zimbabwe amemuua mtoto wake wa miezi 18 na kisha kulikata sikio lake moja na kumuuzia sikio hilo mganga wa nchini Msumbuji kwa dola 20.
Christine Hofisi mwenye umri wa miaka 21 anayeishi katika kitongoji cha Chipinge nchini Zimbabwe karibu na mpaka wa nchini Msumbiji, alimuua mtoto wake mchanga wa kiume mwenye umri wa miaka 18 na kisha kulikata sikio lake la kushoto na kumuuzia mganga anayeishi nchini Msumbiji.

Mwili wa mtoto huyo aliyepewa jina la Edmore uligunduliwa na majirani kwenye kichaka kilichopo karibu na nyumba ya mwanamke huyo.

Christine aliliuza sikio la mtoto wake kwa dola 20 kwa mganga anayeishi karibu na mpaka nchini Msumbiji anayeitwa Maheza.

Taarifa zaidi zinasema kuwa Christine alipewa dola 10 na dola 10 zilizobaki aliahidiwa kulipwa baadae.

Mganga Maheza anatafutwa na polisi akituhumiwa kwa mauji ya watu wengine kadhaa baada ya mafuvu 11 ya binadamu kukutwa ndani ya nyumba yake.

Polisi nchini Zimbabwe wamesema kuwa wanamhoji Christine kwa mauaji ya mtoto wake na wataenda nchini Msumbiji kushirikikiana na maafisa wa Msumbiji kumsaka mganga Maheza.


source nifahamishe

Ajiua Baada ya Brazil Kufungwa na Kutolewa Kombe la Dunia

Sunday, July 04, 2010 / Posted by ishak / comments (0)

Kipigo cha Brazil jana toka kwa Uholanzi kimepelekea kijana mmoja nchini Haiti ajiue mwenyewe kwa kujigongesha kwenye gari lililokuwa spidi.
Kijana mmoja nchini Haiti kutokana na huzuni za Brazil kufungwa na Uholanzi na kutupwa nje ya kombe la dunia, amejiua mwenyewe kwa kujigongesha kwenye gari.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 18 alifariki hapo hapo kwenye eneo la tukio katika kitongoji cha Nerette kilichopo nje kidogo ya mji mkuu wa Haiti.

Brazil ilitandikwa na Uholanzi mabao 2-1 kwenye mechi ya robo fainali na kutupwa nje ya kombe la dunia.

Nchini Haiti, Brazil ina washabiki wengi na Brazil ilipokuwa ikishinda mechi zake za kombe la dunia, watu walikuwa wakimiminika mitaani kushangilia.

Hali ilikuwa tofauti kidogo jana kutokana na kipigo hicho cha Brazil ambacho kimekiweka kibarua cha kocha wa Brazil, Dunga matatani.

source nifahamishe