Video ya Ngono Yamfikisha Mahakamani 50 Cent

Saturday, February 27, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Nyota wa muziki wa Hip Hop wa Marekani 50 Cent amefunguliwa kesi mahakamani kutokana na video ya ngono ya mwanamke mmoja wa nchini humo ambayo 50 Cent ameiweka kwenye tovuti yake.
Mwanamke mmoja wa Florida, Marekani amemfikisha kizimbani 50 Cent kwa kuiweka video yake ya ngono kwenye tovuti yake.

Kwa mujibu wa nyaraka zilizowasilishwa mahakamani wiki hii, mwanamke aliyetambulika kwa jina la Lastonia Leviston alisema kuwa mwezi juni 2008 alirekodi video wakati akifanya mapenzi na mpenzi wake wa zamani lakini mpenzi wake huyo wa zamani alimuuzia 50 Cent video hiyo mwezi machi mwaka jana.

Taarifa zinasema kuwa 50 Cent aliinunua video hiyo na kuiweka kwenye tovuti yake katika njia zake za kuendeleza vita kati yake na rapa Rick Ross.

Taarifa zaidi zilisema kuwa Lastonia alikuwa ni mmoja wa wapenzi wa zamani wa Rick Ross.

50 Cent ambaye jina lake halisi ni Curtis James Jackson aliinunua video hiyo na kuifanyia marekebisho kwa kujifanya na yeye alikuwemo kwenye video hiyo akiwa amevaa wigi.

Video hiyo awali iliwekwa kwenye tovuti ya 50 Cent ya Thisis50.com kabla ya kusambaa kwenye tovuti kadhaa ikiwemo tovuti ya YouTube.

Video hiyo hadi sasa imeishaangaliwa na mamilioni ya watu duniani na Lastonia anamshitaki 50 Cent kwa kulitumia jina lake na video yake bila ya idhini yake.

Msemaji wa 50 Cent alipoulizwa kuhusiana na suala hilo alikataa kusema chochote.

source nifahamishe

Mtu Mwenye Nywele Ndefu Kuliko Wote Duniani Afariki

Saturday, February 27, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanaume wa nchini Vietnam aliyekuwa akitambulika kama mtu mwenye nywele ndefu kuliko watu duniani amefariki dunia huku nywele zake zikiwa na urefu wa mita 6.8.
Tran Van Hay aliingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia mwaka 2004 wakati huo alikuwa na nywele zenye urefu wa mita 5.6 lakini hadi wakati anafariki juzi nywele zake zilikuwa na urefu wa mita 6.8.

Hay alianza kuzifuga nywele zake miaka 50 iliyopita kwakuwa alikuwa akiumwa sana kila alipokuwa akizikata nywele zake, gazeti moja la nchini Vietnam lilimnukuu mke wake, Nguyen Thi Hoa akisema.

Vyombo vya habari viliripoti kuwa Hay alikuwa akiishi maisha ya kawaida tu akifanya kazi ya kuuza dawa za mitishamba lakini siku zote nywele zake zilikuwa zikimzuia kufanya baadhi ya mambo.

Hakuna taksi ya pikipiki iliyokuwa tayari kumbeba Hay kwakuwa alikuwa hawezi kuvaa Helmet kutokana na ukubwa wa nywele zake.

Hay alipenda kuzikusanya nywele zake na kutengeneza kitu kama ndoo juu ya kichwa chake.

Hay alifariki juzi nyumbani kwake katika mji wa Kien Giang uliopo kusini mwa Vietnam.


source nifahamishe

Watoto Watumiwa Kama Waganga na Wanajeshi wa Jamhuri ya Kongo

Saturday, February 27, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Wanajeshi wa waasi wanaopambana na majeshi ya serikali katika jamhuri ya Kongo wanatuhumiwa kuwateka watoto wadogo na kuwatumia kama waganga.
Makundi ya kutetea haki za binadamu yamesema kuwa watoto wenye umri mdogo katika jamhuri ya Kongo wanatekwa na kutumiwa kama waganga kwenye maeneo ya vita ya mashariki mwa Jamhuri ya Kongo.

Katika ripoti ya makundi ya kutetea haki za binadamu iliyotolewa ijumaa, wanamgambo wa kundi la Mai Mai wamekuwa wakiwatumia watoto kama waganga kwa imani kuwa watoto kwakuwa wengi wao huwa hawajui na hawajihusishi na mambo ya mapenzi, huwa na nguvu kubwa za uchawi.

Katika ripoti hiyo Umoja wa mataifa umetakiwa kuwanyang'anya silaha wanamgambo wa Mai Mai na kuwaachia huru watoto wanaoshikilia mateka ambao wamegeuzwa kuwa waganga.

Mashariki mwa Kongo kumekuwa na vurugu tangia vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipotokea nchini Rwanda mwaka 1994.

Kundi la Mai Mai ni mojawapo ya makundi mengi yaliyojikita mashariki mwa Kongo ambapo wapiganaji wake mara nyingi hutumia mishale na mapanga.


source nifahamishe

Vijana Waliofanya Mapenzi na Mbuzi, Kuozeshwa Mbuzi

Saturday, February 27, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Vijana wawili wa nchini Msumbiji ambao walikamatwa wakifanya mapenzi na mbuzi wamefikishwa mahakamani lakini mmiliki wa mbuzi huyo anaitaka mahakama iamuru vijana hao walipe mahari na waozeshwe mbuzi huyo.
Gazeti la serikali la nchini Msumbiji limeripoti kuwa vijana wawili wanaotuhumiwa kufanya mapenzi na mbuzi watapandishwa kizimbani kwa makosa ya jinai lakini mmiliki wa mbuzi huyo anataka taratibu za kimila zifanyike na wanaume hao waozeshwe mbuzi.

Vijana hao wawili ambao majina yao wala umri wao haukutajwa, walikamatwa na polisi wakifanya kitendo hicho katika mji wa Mbucuta uliopo ukanda wa kati wa Msumbiji.

"Mmoja wa vijana hao alikuwa uchi akikishikilia kichwa cha mbuzi wakati kijana mwingine alikuwa akifanya mapenzi na mbuzi huyo", alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Mario Creva alipokuwa akiongea na radio Msumbiji.

Mwendesha mashtaka wa serikali amesema kuwa vijana hao wawili watapandishwa kizimbani hivi karibuni.

Lakini mmiliki wa mbuzi huyo anaweza akafungua kesi nyingine akitaka vijana hao waozeshwe mbuzi huyo.

Mmiliki wa mbuzi huyo anataka vijana hao walipe fidia kwa uharibifu wao na kisha waanze taratibu za kitamaduni kwa kulipa mahari kabla ya kuozeshwa mbuzi huyo.



source nifahamishe

Mchungaji Atumia Pesa za Kanisa Kufanya Ukahaba

Saturday, February 27, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mchungaji mmoja nchini Hispania ametimuliwa baada ya kutumia pesa za kanisa kujitangaza kwenye internet kuwa yeye ni kahaba wa kiume na alizitumbua pesa zaidi za kanisa kwa kupiga simu za ngono na kutembelea tovuti za kulipia za video za ngono.

Skendo hilo kubwa la mchungaji wa makanisa mawili ya katoliki katika mji wa Toledo, mchungaji Samuel Martin Martin, 27, limetawala magazeti ya Hispania ambapo magazeti mengi yalichapisha tangazo la kutafuta wateja la mchungaji huyo kahaba.

Mchungaji Martin aliweka tangazo hilo likiambatana na picha yake akiwa amevaa chupi ya kahawia akisema kuwa yuko tayari kufanya mapenzi na mwanamke yoyote kwa malipo ya euro 120 kwa lisaa limoja.

"Niko tayari kwa mapenzi ya staili zote, napatikana masaa 24 ukitaka nyumbani kwako au hotelini. Hautazijutia pesa zako, nitakupa raha ambayo hujawahi kuipata", lilisema tangazo la mchungaji Martin.

Mchungaji huyo ambaye alijitambulisha online kwa jina la Hector alijitamba kuwa ana mzee mwenye urefu wa sentimeta 15 ambaye yuko tayari kutoa uroda na furaha.

Mchungaji Martin aliwaomba radhi waumini wa makanisa hayo akisema kuwa alizitumia vibaya pesa za michango ya kanisa.

Anatuhumiwa kutumia euro 17,000 kwenye mitandao ya simu za mambo ya ngono na tovuti za video za ngono.

Skendo la Martin limeibuka wakati kanisa katoliki nchini Hispania linapigania kuwavuta waumini makanisani kutokana na kupungua kwa idadi ya watu wanaoenda makanisani.

Mchungaji Martin ametoweka tangia skendo hilo lilipoibuliwa magazetini na ameahidi kuzirudisha pesa alizoziiba kwenye michango ya kanisani


source nifahamishe

Madaktari Wapigana Hospitalini, Mtoto Afariki

Saturday, February 27, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Madaktari wawili wa nchini Brazili walitwangana makonde kwa zaidi ya nusu saa badala ya kumhudumia mwanamke mjamzito aliyekuwa akiwasubiria wamalize kupigana ili wamzalishe.
Madaktari wawili wa nchini Brazili waliacha kazi ya kumzalisha mwanamke na kuanza kutwangana makonde mbele ya mwanamke mjamzito aliyetakiwa kuzalishwa kwa njia ya operesheni.

Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Gislaine Santana, 32, aliingia kwenye leba na kusubiria kuzalishwa kwa njia ya operesheni wakati ngumi zilipozuka ghafla kati ya madaktari wawili ambao walitakiwa kumfanyia operesheni hiyo.

Kwa mujibu wa gazeti la Folha de Sao Paulo la Brazili, madaktari hao walitwangana makonde mazito na kugaragazana kwenye sakafu za wadi ya uzazi huku mwanamke huyo mjamzito akipiga kelele akitaka waache kupigana.

Daktari wa tatu alikuja dakika 90 baada ya tukio hilo na kumzalisha mwanamke huyo lakini mtoto wa kike aliyezaliwa alikuwa ameishafariki.

"Sitaki kusema chochote, lakini mpaka mke wangu anaingilia leba, mtoto wangu alikuwa bado yu hai na mwenye afya njema", alisema mume wa mwanamke huyo.

Mamlaka husika za nchini Brazili zimewafukuza kazi madaktari wote wawili waliodundana na wameanzisha uchunguzi kuhusiana na kifo cha mtoto huyo.



source nifahamishe

Waziri kizimbani kwa deni la Mil. 90

Friday, February 26, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


WAZIRI WA KILIMO, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam kwa tuhuma za kudaiwa shilingi milioni 90.
Kesi hiyo ilifikishwa na kusikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo.

Ilidaiwa kuwa Wasira anadaiwa deni hilo na Andrew Ngai ambae ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Cargo Building.

Shitaka la pili katika kesi hiyo ilidaiwa kuwa Wasira alimdhalilisha na kumsumbua mkurugenzi huyo.

Hakimu alipomtaka waziri huyo kujitetea mahakamani hapo alidai, alishangazwa na uwepo wa kesi hiyo, na kusema yeye ndio mwenye haki ya kumdai mkurugenzi huyo.

“Nashangaa kusikia mimi nashitakiwa wakati mimi ndio nimepata hasara ya vigae vyangu 600 vilivyokuwa kwenye kampuni yake kupotea”

Katika kesi hiyo ya madai yenye namba 24/2008, ilidaiwa na Wakili kuwa mwaka 1999 Waziri huyo aliagiza vigae 2,000 kutoka nchini Afrika Kusini na kumkabidhi Ngai anayeelezwa kuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Cargo Building amuhifadhie.

Wakili wa mshitakiwa aliiambaia mahakama kuwa, mteja wake alitumia vigae 1,400 na kubakiza 600 vilivyoelezwa kupotea na baadae Wasira kufungua kesi ya madai dhidi ya Ngai kutaka kulipwa shilingi milioni sita kama gharama za vigae 600 vilivyopotea lakini alishindwa katika kesi hiyo kesi.

Hivyo ilidaiwa kuwa baada ya kushindwa kwa kesi hiyo NGai alifungua kesi nyingine baada waziri huyo kushindwa mahakamani na kutaka kulipwa shilingi milioni 90 kama fidia ya usumbufu na kudhalilishwa kwa kampuni yake.

Hata hivyo Mahakamani iliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 12 itakaporudi tena.


source nifahamishe

7 wakamatwa kwa ujambazi Dar

Friday, February 26, 2010 / Posted by ishak / comments (0)

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwakamata watu saba wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wa kutumia silaha katika eneo la Mbezi kwa Yusuph
Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Charles Kenyella, aliviuambia vyombo vya habari kuwa, jeshi hilo limewakamata watu hao kwa kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema ambapo waliwagundua wakati wakijiandaa kwenda kufanya uhalifu.

Alisema mara baada ya kupata tarifa hiyo askari waliwafatilia mara moja majambazi hao na kufanikiwa kuwaona ambapo walikuwa wakitembelea gari dogo aina ya Baloon wakielekea maeneo ya Mbezi.

Alisema kutokana na uzoefu wa askari hao walifanikiwa kuwatia mbaroni na katika pulukushani jambazi mmoja alitaka kutoroka lakini walifanikiwa kumkamata baada ya kumfyatuliwa risasi mguuni.

Alisema majambazi hao walikuwa na silaha zikiwemo mapanga, mabomu yaliyotengenezwa kienyeji, betri na vifaa maalumu vya kujikinga na mabomu.

Hivyo majambazi hayo yanaendelea kushikiliwa na polisi huku upelelezi ukiendelea.


source nifahamishe

Sala Kuwafufua Wachungaji Waliofariki Kwa Ajali Kenya

Wednesday, February 24, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Waumini wa kanisa la Pentekoste nchini Kenya wamegoma kuwazika wachungaji wawili waliofariki kwa ajali ya gari wiki moja iliyopita na waumini hao wamekuwa wakikesha wakisali wakiamini wachungaji hao watafufuka kama YESU.
Waumini wa kanisa moja la Pentekoste magharibi mwa Kenya wamegoma kuwazika wachungaji wawili wa kanisa hilo waliofariki kwa ajali ya gari wiki moja iliyopita na wamekuwa wakisali mbele ya majeneza yao muda wote wakiamini kuwa watafufuka kama alivyofufuka YESU.

Mchungaji Patrick Wanjohi na mchungaji Francis Kamau Ndekei, walifariki februari 15 mwaka huu kutokana na ajali mbaya ya gari lakini waumini wao wamekuwa wakiamini kuwa wachungaji hao wamelala tu na wala hawajafariki.

"Hatutawazika kamwe, kwakuwa hawajakamilisha misheni zao hapa duniani, tunawahitaji warudi duniani kumalizia majukumu yao kwani bila ya wao kanisa litakufa", alisema mmoja wa waumini hao.

Awali uongozi wa kanisa hilo ulisema kuwa wachungaji hao watafufuka siku ya jumamosi na kuwafanya maelfu ya watu washinde kwenye mvua kubwa sana wakisubiria wachungaji wao wafufuke. Hata hivyo siku ya jumamosi ilimalizika bila wachungaji hao kufufuka.

Mamia ya waumini bado wanaendelea kusali masaa yote mbele ya majeneza ya wachungaji hao wakisubiria miujiza ijitokeze na wachungaji hao wafufuke.

source nifahamishe

Mwizi Anapojitafutia Balaa Mwenyewe

Wednesday, February 24, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwizi huyu wa nchini Brazili alijiingiza mwenyewe matatani baada ya kufeli kwa misheni yake ya kuiba kwenye mgahawa mmoja nchini humo. Alilazimika kupiga kelele za kuomba msaada mwenyewe.
Mwizi huyu ilibidi aombe msaada mwenyewe wa kunusuru maisha yake baada ya kunasa katikati ya kuta za jiko la mgahahawa mmoja nchini humo.


source nifahamishe

Mwanamke Aliyesingizia Kubakwa Atupwa Jela

Wednesday, February 24, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanamke wa nchini Marekani aliyemsingizia mwanaume asiye na hatia kuwa amembaka na kusababisha mwanaume huyo atupwe jela, amehukumiwa kwenda jela baada ya kutubu kanisani kuwa aliongopa kubakwa na mwanaume huyo.
Biurny Peguero mwenye umri wa miaka 27 mkazi wa jiji la New York nchini Marekani amehukumiwa kwenda jela kati ya mwaka mmoja na miaka mitatu baada ya kukiri kumsingizia mwanaume asiye na hatia kuwa amembaka.

Mwaka 2005, Biurny alimsingizia mwanaume huyo kuwa alimtishia na kisu kabla ya kumbaka. Mwanaume huyo alihukumiwa kwenda jela miaka minne.

Mwaka jana Biurny alienda kutubu madhambi yake kanisani na kukiri mbele ya mchungaji kuwa alimsingizia mwanaume asiye na hatia kuwa amembaka.

Hatua hiyo ilisababisha polisi wapewe taarifa ambapo mwanaume huyo aliachiliwa huru muda mfupi baadae.

Akisomewa hukumu yake, Biurny alihukumiwa kwenda jela kutumikia kifungo cha kati ya mwaka mmoja na miaka mitatu.

source nifahamishe

Mjerumani Aponzwa na Mbwa Wake

Wednesday, February 24, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mjerumani aliyekuwa akiwakimbia polisi na kujificha kwenye kabati ndani ya nyumba yake, aliponzwa na mbwa wake aliyewaongoza polisi hadi kwenye sehemu aliyojificha.
Mwanaume mmoja wa nchini Ujerumani aliponzwa na mbwa wake mwenyewe baada ya kuwakimbia polisi waliofika nyumbani kwake na kwenda kujificha kwenye kabati la nguo.

Wakati polisi walipogonga mlango wa nyumba yake iliyopo kwenye kitongoji cha Euskirchen karibu na mji wa Cologne, mlango ulifunguliwa na mwanaume mwingine ambaye alisema hajui mwanaume anayetafutwa ameenda wapi.

Lakini mwanaume huyo alipomuachia mbwa aliyekuwa amemshikilia, mbwa huyo moja kwa moja alienda kwenye kabati alilojificha mmiliki wake na kuanza kutingisha mkia.

Kitendo hicho kiliwashtua polisi ambao waliamua kulisachi kabati hilo lenye unene wa mita moja na urefu wa sentimeta 80.

Polisi walipolifungua kabati hilo, Mwanaume huyo alikutwa amejikunja ndani yake. Walimkamata na kumtia mbaroni.

Polisi hawakusema walikuwa wakimtafuta mwanaume huyo kwa kosa gani na walikataa kutaja umri wala jina la mtuhumiwa huyo.

source nifahamishe

Mahakamani kwa kudhalilisha

Wednesday, February 24, 2010 / Posted by ishak / comments (0)

KIJANA Ali Othumani [26] amefiksihwa katika mahakama ya Mwanzo Kariakoo kwa tuhuma za kumdhalilisha Fatuma Bakari [22] kwa kumshika maungo ya mwilini pasipo ridhaa.
Ilidaiwa kuwa February 20, mwaka huu, majira ya mchana, huko maeneo ya Mtaa wa Mkunguni Kariakoo, mshitakiwa alianza kumdhalilisha malalmikaji kwa kumshika maungo yake ya mwilini pasipo ridhaa kutoka kwake.

Ilidaiwa mshitakiwa alishika matiti ya mlamikaji na kuchezea maungo yake ya mwilini pasipo ridhaa yake mbele ya hadhara ya watu na kumtia aibu kubwa.

Alipotakiwa kujibu tuhuma hizo mahakamani alipatwa na kigugumizi na kutaka hakimu amsamehe na hatorudia tena kitendo hicho.

Hakimu alimuuliza alikuwa anatambua kwamba wakati anafanya vitendo hivyo na huku mwenyewe akimkatalia alijua kama anamdhalisha?.

Alijibu kuwa hakutambua kwa kuwa alikuwa anajua kama anamtania .

Hakimu alimtaka Ali aende rumande kwa muda wa siku tatu ili aweze kupata adabu akirudi uraiani.

Hivyo amepelekwa rumande kwa muda wa siku tatu ili aweze kujirekebisha na atatolewa kwa dhamana siku hizo tatu zikikamika

Hakimu amefanya hivyo na amekataa kumpa dhamana ili kukomesha vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake nchini

source nifahamishe

Mwanamke Abadilishana Watoto Wawili Kwa Kasuku

Wednesday, February 24, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanamke mmoja wa nchini Marekani ametupwa jela miezi 30 na kufanyishwa kazi ngumu baada ya kukiri kubadilishana watoto wawili kwa ndege aina ya Kasuku Kishungi.
Donna Louise Greenwell mwenye umri wa miaka 52 alipatikana na hatia ya kufanya biashara ya kuuza watoto wawili kwa kubadilishana kwa ndege aina ya Kockatoo (Kasuku Kishungi) pamoja na pesa dola 175.

Donna amehukumiwa kwenda jela miaka 15 pamoja kazi ngumu kwa kila kosa moja alilokiri la kuuza watoto na ataanza kutumikia adhabu yake machi 25 mwaka huu.

Donna anatuhumiwa kuwauza watoto wawili mmoja wa kike mwenye umri wa miaka minne na mwingine wa kiume mwenye umri wa miaka mitano.

Donna aliwauza watoto hao baada ya kukubali kupokea malipo ya kasuku kishungi mmoja na pesa kiasi cha dola 175.

Watoto hao walikuwa si wa Donna. Wazazi halisi wa watoto hao walimuachia Donna watoto hao awalee.


source nifahamishe

Babu wa Miaka 97 Ashinda Bahati Nasibu

Wednesday, February 24, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Babu aliyepigika na umaskini maisha yake yote ameuaga umaskini akiwa na umri wa miaka 97 baada ya kushinda bahati nasibu ya mamilioni ya pesa.
Babu mmoja wa nchini Vitenam aliyeteseka na maisha ya umaskini miaka nenda miaka rudi, amegeuka tajiri ghafla baada ya kushinda bahati nasibu na kujipatia dola 400,000 (Zaidi ya Tsh. Milioni 500).

Taarifa zimesema kuwa muda mfupi baada ya babu huyo kushinda bahati nasibu mzozo mkubwa umezuka baina ya ndugu zake wanaowania angalau urithi wa mali zake.

Jirani mmoja wa babu huyo wa mji wa Ho Chi Minh kusini mwa Vietnam alisema kuwa ilimbidi aingilie kati kumzuia babu huyo asiendelee kuzigawa pesa zake kwa mamia ya watu waliojazana kwenye nyumba yake.

Pesa zake zote zilizobakia zilipelekwa kuhifadhiwa benki, liliripoti gazeti la Thanh Nien la Vietnam.

Mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina la Nguyen Van Het alishinda bahati nasibu hiyo baada ya kununua tiketi ya bahati nasibu kwa kutumia pesa alizopewa siku ya mwaka mpya kama zawadi.

Het amejishindia kiasi cha dong za Vietnam bilioni 7.6 ambazo ni sawa na dola za kimarekani laki nne.

Afisa mmoja wa serikali ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema kuwa ilibidi wazizuie pesa za Het na kumwekea benki baada ya mamia ya ndugu na jamaa kujazana kwenye nyumba yake wakiomba pesa.

"Tutasubiria wiki kadhaa ili aweze kutulia ndipo tutakapomuuliza anataka kuzifanyia nini pesa zake", alisema afisa huyo.

source nifahamishe

Angalia Sinema Hii Ujishindie Tsh. Milioni 13

Wednesday, February 24, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Watengeneza filamu wa India wanawapima watu imani kwa kuahidi kutoa zawadi ya dola 10,000 kwa mtu yoyote atakayeweza kuangalia filamu mpya ya kutisha peke yake kwenye ukumbi wa sinema.
Nyota maarufu wa kutengeneza filamu za Kihindi Bollywood ameahidi kutoa zawadi ya dola 10,000 (Takribani Tsh. Milioni 13) kwa mtu yoyote atakayeweza kuangalia sinema mpya ya kutisha kuanzia mwanzo mpaka mwisho akiwa peke yake kwenye ukumbi wa sinema.

Filamu hiyo iliyotengenezwa na Ram Gopal Varma inayoitwa "Phoonk 2", ambayo ni sehemu ya pili ya filamu kama hiyo iliyotolewa mwaka jana, inaelezea mashetani wanavyozitesa familia.

"Mtu yoyote anayedai hawezi kutishika na sinema ya kutisha, atawekwa peke yake kwenye ukumbi wa sinema", alisema Varma alipokuwa akiitangaza filamu hiyo kwa waandishi wa habari mjini Mumbai.

Varma alisema kuwa mtu atakayejitokeza atawekewa nyaya za kupima mapigo ya moyo wake na pia atawekewa kamera ili kuhakikisha hafungi macho yake wakati wote wa filamu hiyo.

Matokeo ya vipimo vya mapigo ya moyo wake yataonyeshwa LIVE kwenye televisheni itakayowekwa nje ya ukumbi wa sinema. Mtu atakayefanikiwa kuangalia filamu hiyo toka mwanzo hadi mwisho atajipatia rupia za India 500,000.

Varma aliandaa shindano kama hilo kwenye filamu yake ya kwanza "Phoonk" ambapo ilitangazwa kuwa mtu aliyejitokeza aliweza kuangalia nusu saa tu kabla ya kukimbia.

Katika kumuonyesha Varma kuwa amechemsha mwanaume mmoja wa mji wa Bangalore alinunua tiketi za ukumbi mzima wa sinema na kuangalia filamu hiyo hiyo peke yake kuanzia mwanzo hadi mwisho huku mlinzi akiwa nje ya ukumbi.
source nifahamishe

Mwanamieleka wa Marekani Apigwa na Mkewe

Wednesday, February 24, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanamieleka maarufu wa Marekani Ric Flair amejuruhiwa baada ya kushambuliwa na mkewe nyumbani kwake.
Mwanamieleka maarufu wa Marekani, Ric Flair ilimbidi awaite polisi baada ya kushambuliwa na mkewe kwenye nyumba yao iliyopo North Carolina.

Katika taarifa aliyoitoa kuhusiana na tukio hilo, Ric Flair ambaye anajulikana sana kwa manjonjo yake ulingoni, alisema kuwa kutokuelewana na mkewe ndio sababu ya mtafaruku huo na kwamba yeye hakufanya kosa lolote.

Mamlaka husika zilisema kuwa polisi waliitwa kwenye nyumba ya Ric Flair ambapo Flair alilamika kuwa mkewe alikuwa akimshambulia.

Ric Flair alionekana akiwa na majeraha kutokana na kichapo hicho toka kwa mkewe lakini alikataa kupatiwa matibabu na watu wa ambulansi.

Polisi walimtia mbaroni mkewe wa Flair bi Jacqueline Beems mwenye umri wa miaka 41, walimtupa jela kwa muda na kumuachia huru masaa machache baadae.

Flair mwenye umri wa miaka 60 bado anaendeleza kucheza mieleka kupitia TNA baada ya kutumia miaka mingi sana ya kipaji chake chake cha mieleka kwenye WWE.

source nifahamishe

Waliohusishwa na Uchinjaji wa Watu 17 Wafikia 10

Monday, February 22, 2010 / Posted by ishak / comments (0)

JESHI la Polisi Mkoa wa Mara tayari limefanikiwa kuwakamata watu kumi wanaohusishwa na mauaji ya kinyama ya watu 17 wa ukoo mmoja katika Manispaa ya Musoma yaliyotokea mwanzoni mwa wiki iliyopita na kuacha historia ya pekee mkoani humo.
Hadi kufikia jana mchana, jeshi la polisi nchini limefanikiwa kukamata watu 10 mkoani Mara wanaohusishwa na mauaji ya watu 17 wa ukoo mmoja.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Robert Boaz, amesema hadi sasa watu hao wameshakamatwa na msako mkali unaendelea ili kuhakikisha watu wote waliohusika katika kufanya unyama huo wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Kamanda Boaz alisema watu hao walikamatwa katika maeneo tofauti ndani na nje ya mkoa huo baada ya kupata taarifa za uhakika kutoka kwa raia wema ambazo zimekuwa zikifanyiwa kazi na jeshi lake.

Pia amewataka wananchi kuzidi kutoa taarifa kwa siri kuhusiana na watu hao.

Amesema timu kubwa ya askari wake wamesambazwa kila kona ya mkoa wa Mara na nje ya mkoa ili kuwasaka watu hao wauaji na kusema kazi hiyo itafanikiwa kwa jeshi hilo.

Amesema utaratibu wa kisheria utakapokamilika watu hao wanatarajiwa kupandishwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa.

source nifahamishe

Mume Akutana na Mkewe Kwenye Taarabu, Amshushia Kipigo

Monday, February 22, 2010 / Posted by ishak / comments (1)


Mwanaume mmoja jina halikuweza kupatikana mara moja, alianza kumpa kichapo cha nguvu mkewe baada ya kumkuta katika ukumbi wa starehe akijivinjari kwa kuwa hakutegemea kumkuta mahali hapo usiku huo.
Sakata hilo lilitokea mwishoni mwa wiki, majira ya usiku, katika ukumbi wa Travetine Magomeni wakati Jahazi Taarabu ilipokuwa ikifanya onyesho ukumbini hapo.

Mwanaume huyo alifika ukumbini hapo huku akijua kwamba mke wake hatakuwa mahali hapo kwa kuwa alidai alimuaga anakwenda kwenye harusi ya ndugu yake na wakati akipapasa macho huku na huko alimuona mke wake akicheza ukumbini humo.

Hivyo alimuacha aendelee na kucheza na mziki ulipoisha mke wake huyo alirudi kukaa kwenye kiti na mume huyo ndipo alipomfuata alipokaa na kumtaka atoke nje ya ukumbi waondoke nyumbani.

Mwanamke huyo kwa vile alipania kuhudhuria shoo hiyo alimjibu mume wake huyo hatoki ukumbini na amuache hadi atakaporidhika na kuamua kuondoka yeye mwenyewe.

Kutokana na majibu hayo ya mkewe, mume huyo alichukua uamuzi wa kuanza kumshambulia kwa kumkata vibao vya nguvu mkewe hali iliyofanya kuzuke zogo kubwa mahali hapo na mwanamke huyo kuendelea kung’ang’ania kwenye kiti akiashiria haondoki mahali hapo.

Hali hiyo ilizua mtafaruku mkubwa hali iliyofanya mabaunsa kuingilia kati sakata hilo.

Mwanamke huyo alizidi kuonyesha msimamo wake na kuwaambia mabaunsa kuwa haondoki kwa kuwa alilipia na mabaunsa kumtaka atoke nje ya ukumbi kwa kuwa mumewe alikuwa anafanya fujo ukumbini hapo.

Mwanamke huyo alipoonekana ni king’ang’anizi ilibidi mabaunsa wamnyanyue na kiti alichokalia ili amani irudi mahali hapo kwa wengine waliokaa mahali hapo.
mwanamke huyo alivyopakizwa kwenye gari ndogo na kuondoka huku wakirushiana maneno ya hapa na pale na mumewe huyo.
source nifahamishe

Sinema ya Ngono za Mashoga Yaonyeshwa Kanisani

Monday, February 22, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mchungaji wa nchini Uganda anayepigania sheria kali zipitishwe dhidi ya mashoga nchini humo, amewaonyesha waumini wake kanisani sinema ya ngono wanaume wakiwaingilia kinyume cha maumbile wanaume wenzao.
Waumini zaidi ya 300 waliojazana kwenye kanisa la mchungaji Martin Ssempa la mjini Kampala nchini Uganda, walishuhudia sinema ya ngono kanisani wanaume wakiwainamisha na kuwaingilia kinyume cha maumbile wanaume wenzao.

"Angalia mwanaume huyu anakula uume wa mwanaume mwenzake", alisema mchungaji Ssempa akitoa maelezo juu ya kipengele kimoja cha video hiyo.

"Je ni haya kweli Obama anataka kutuletea barani Afrika?", alisema mchungaji huyo kufuatia kauli ya Obama kupinga sheria kali dhidi ya mashoga nchini Uganda na kutaka mashoga nao wapewe haki zao.

Mchungaji huyo aliamua kuionyesha sinema hiyo kanisani katika kutafuta kuungwa mkono juhudi zake za kutaka sheria kali dhidi ya mashoga nchini Uganda.

Sinema hiyo ilionyeshwa siku ya jumatano na kuangaliwa na waumini wengi baada ya polisi nchini Uganda kuyafuta maandamano ya watu milioni moja yaliyokuwa yafanyike kuuunga mkono muswada wa kuwahukumu kifungo cha maisha mashoga.

"Tulikuwa tumepanga wanaume na wanawake milioni moja tuandamane kwenye jiji la Kampala lakini tuliambiwa kuwa hatuwezi kuandamana kutokana na sababu za kiusalama", mchungaji Ssempa aliwaambia waumini wake.

"Hivi mnajua ni vitu gani wanavyofanya mashoga wanapokuwa kwenye vyumba vyao?", alisema mchungaji huyo na kuanza kuwaonyesha waumini wake picha za ngono za mashoga.

Mchungaji huyo aliweka video ya picha zinazoonyesha wazi wazi jinsi wanaume wanavyowaingilia wanaume wenzao.

Serikali ya Uganda imekuwa ikipata upinzani mkubwa toka nchi wafadhili ambazo baadhi zimetishia kusitisha misaada yake iwapo Uganda itapitisha muswada wake wa kuwabana mashoga na wasagaji.

Katika mojawapo ya vipengele vya muswada huo, watu wanaowakodisha nyumba mashoga na wasagaji nao pia watakumbana na sheria na watafikishwa mahakamani.

Baadhi ya mashoga watahukumiwa adhabu ya kifungo cha maisha cha maisha na wengine adhabu ya kifo kama muswada huo utapitishwa.

source nifahamishe

Tunastahili Kuadhibiwa Baada ya Kuzini'

Monday, February 22, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Wanawake watatu wa nchini Malaysia ambao walicharazwa bakora kwa kufanya mapenzi kabla ya kuolewa wamesema kuwa walistahili adhabu waliyopewa ili kuwawezesha kutubu madhambi yao.
Wanawake watatu ambao wamekuwa wanawake wa kwanza kucharazwa bakora nchini Malaysia kutokana na kufanya zinaa, wamesema kuwa walistahili adhabu waliyopewa.

Wanawake hao walicharazwa bakora wiki iliyopita baada ya kuhukumiwa na mahakama ya sheria za kiislamu kwa kufanya mapenzi kabla ya ndoa.

Kucharazwa bakora kwa wanawake hao kulisababisha hasira za makundi ya kutetea wanawake lakini wanawake hao wamejitokeza na kuzitetea adhabu walizopewa wakisema kuwa walistahili adhabu hizo kwa kosa kubwa la zinaa walilofanya.

Wanawake hao watatu wenye umri kati ya miaka 17 na 25 walijipeleka wenyewe kwenye mahakama za sheria za kiislamu wakisema kuwa wanajisikia vibaya baada ya kufanya mapenzi na wapenzi wao kabla ya kuoana na kupelekea wapate ujauzito.

Mmoja wa wanawake hao ambaye ana umri wa miaka 17 aliwaambia waandishi wa habari kuwa alijisalimisha mwenyewe kwenye mamlaka za kiislamu baada ya kufariki kwa mtoto aliyemzaa kabla ya muda wake wa kuzaliwa kufika. Hivi sasa mwanamke huyo anatumikia kifungo cha miezi sita jela.

"Najua nimefanya dhambi, nastahili kuadhibiwa, najua kucharazwa bakora ni mateso makubwa lakini nimeona kuwa ni njia bora ya mimi kutubu madhambi yangu na kurudi kwenye njia sahihi", alisema mwanamke huyo.

Mwanamke huyo tayari ameishafunga ndoa na mpenzi wake ambaye naye alicharazwa bakora na kisha kutumikia kifungo jela kwa kufanya kosa hilo la zinaa kabla ya ndoa.

Wanawake wengine wawili ambao wote wana mtoto mmoja mmoja, nao wanatarajia kufunga ndoa na wapenzi wao pindi watakapotoka jela.

Wanaume zao nao walicharazwa bakora na kutupwa jela kwa kosa hilo hilo la kufanya mapenzi kabla ya ndoa.

Wanawake wote watatu wanawashauri watu wengine wasifanye makosa ya kufanya zinaa na ambao wameishatenda dhambi hiyo wajitokeze kutubu dhambi zao.

source nifahamishe

Apigania Atambulike Kuwa Yeye Ndiye Mtu Mfupi Duniani

Monday, February 22, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanaume mwenye urefu wa sentimeta 56 tu toka nchini Nepal ameondoka nchini kwake na kuanza safari za kuzunguka nchi kadhaa akitaka atambulike kuwa yeye ndiye mtu mfupi kuliko wote duniani.
Khagendra Thapa Magar ameanza safari za kutembelea nchi za ulaya kupiga kampeni za kuingizwa kwenye kitabu cha rekodi za dunia cha Guinness kuwa yeye ndiye mtu mfupi kuliko wote duniani.

Khagendra alituma maombi yake kwenye ofisi za London nchini Uingereza akitaka aingizwe kwenye rekodi za dunia pindi afikapo umri wa miaka 18 mwezi oktoba mwaka huu.

Hata hivyo, Khagendra amesema kuwa hajapata majibu yoyote toka kwenye ofisi hiyo.

Awali Khagendra alituma maombi yake ya kuingizwa kwenye rekodi za dunia alipokuwa na umri wa miaka 14 lakini maombi yake yalitupiliwa mbali kwasababu hajatimiza umri wa miaka 18 wa kumwezesha ahesabike kama mtu mzima huku ikihofiwa kuwa anaweza kurefuka.

Madaktari nchini Nepal wameshindwa kuelezea sababu zinazomfanya Khagendra awe mfupi kiasi hicho.

"Tunaenda Italia kujaribu kuingiza jina lake kwenye kitabu cha rekodi za dunia cha Guinness " alisema baba yake Rup Bahadur Thapa Magar, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kabla ya kuanza safari toka mjini Katmandu.

Baada ya kutoka nchini Italia ambako watashiriki kwenye shoo moja kwenye Televisheni ya Italia, Khagendra na kambi yake wataamua nchi gani nyingine ya kwenda.

Mamia ya wapenzi wa Khagendra walijitokeza jana kumuaga na kumkabidhi mashada ya maua.

Hivi sasa He Pingping wa nchini China, ndiye anayeshikilia rekodi ya dunia ya mtu mfupi kuliko wote duniani akiwa na urefu wa sentimeta 73.

source nifahamishe

Akasirishwa na Gredi ya Masomo Yake, Amuua Mwalimu Wake

Monday, February 22, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanafunzi mmoja nchini Ujerumani aliyekasirishwa na gredi ya masomo yake, ameivamia shule yake na kuwashambulia walimu wake na kumuua mwalimu wake mmoja kwa kumcharanga na kisu.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea kwenye shule yenye wanafunzi 3200 ya Technik II katika maeneo ya Mundenheim ya mji wa Ludwigshafen nchini Ujerumani.

Mtuhumiwa aliyejulikana kwa jina la Florian K mwenye umri wa miaka 23 alirudi tena kwenye shule hiyo ambayo alihitimu masomo yake mwaka 2004 akiwa na kisu kikubwa na bastola kwa nia ya kufanya mauaji makubwa ya walimu wake.

Mwalimu Rudolf B. mwenye umri wa miaka 58 ambaye alimfundisha somo la hisabati Florian alifariki kwenye eneo la tukio baada ya kuchomwachomwa na kisu na Florian ambaye alikamatwa muda mfupi baada ya kufanya mauaji hayo.

Taarifa zaidi zinasema kuwa Florian alikuwa amepanga kufanya mauaji makubwa sana kwenye shule, alikutana na mwalimu Rudolf kwenye ngazi na ndipo alipotimiza azma yake hiyo.

Florian ambaye alikuwa akipiga risasi hovyo aliwajeruhi walimu watatu kabla ya kuwekwa chini ya ulinzi na timu maalumu ya polisi iliyoitwa kwenye shule hiyo yenye walimu 130.

Florian alikiri kuwa alikuwa amepanga kuwaua walimu wote waliosababisha amalize shule akiwa na gredi ya chini.

Taarifa zaidi zilizotolewa zilisema kuwa Florian aliacha ujumbe kwenye internet kuhusiana na mipango yake ya kuwaua walimu wake aliweka video za mazoezi yake ya kutumia bunduki kwenye tovuti moja ya video ya Ujerumani.

Pia Florian aliandika katika tovuti moja kuwa mwaka wake wa kufariki ni mwaka 2010 na siku yake ya kufariki ni ndiyo siku hiyo ambayo alifanya mashambulizi hayo.

source nifahamishe

Member's Login Username Password Not a member? Sign Up Sign Out Afariki Kutokana na Moto wa Sigara

Monday, February 22, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanaume mmoja wa nchini Marekani amefariki dunia baada ya sigara aliyoiwasha kusababisha pombe kali aina ya Vodka aliyojimwagia kulipuka na kumuunguza.
Paul MacClymont, wa New Jersey nchini Marekani, aliungua vibaya na moto baada ya sigara aliyokuwa akivuta kuangukia kwenye nguo zake alizovaa ambazo alizimwagia pombe kali aina ya Vodka.

Paul mwenye umri wa miaka 40 alijibiringisha kwenye sakafu kwa nia ya kuuzima moto huo kabla ya kupoteza fahamu na kuzinduka baada ya masaa sita.

Huku akiwa na majeraha makubwa ya moto, Paul aliweza kuwapigia simu polisi ambao ilibidi wauvunje mlango wake ili kuweza kumfikia.

Paul aliungua asilimia 75 ya mwili wake na alifariki hospitalini siku ya ijumaa.

Kabla ya kufariki Paul aliwaambia polisi kuwa alikuwa akinywa Vodka siku nzima siku hiyo na kuna wakati pombe hiyo ilimwagikia kwenye suruali yake aliyovaa.

Wakati alipokuwa akiwasha sigara, sigara hiyo ilimuunguza mkono wake na yeye alilazimika kuiachia na ndipo ilipoangukia kwenye nguo alizovaa ambazo zilikuwa zimelowa pombe hiyo.

Moto ndipo ulipozuka na kuanza kumuunguza na kusababisha kifo chake.

source nifahamishe

Msikiti waanguka na kujeruhi 50

Sunday, February 21, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


WATU zaidi ya 50 wamejeruhiwa vibaya baada ya msikiti kuanguka nchini Morocco siku ya Ijumaa walipokuwa wakijiandaa na sara ya Ijumaa.
Kuta za msikuti huo uliojengwa katika karne ya 16 uliopo kaskazini mwa mji wa Meknes ulianguka wakati waumini hao walipokuwa wakijiandaa kuanza swala.
Msemaji wa mamlaka ya mji huo Al-Elwi al-Ismaili amesema uokoaji bado uandelea ambapo majeruhi wote walikimbizwa hospitali ya karibu ya Bab Baradein.
Mapema kituo cha Pan-Arab al-Jazeera kiliripoti kuwa watu saba wamefariki dunia na 47 kujeruhiwa vibaya katika tukio hilo.

source gblp

Mambo ya wachina

Sunday, February 21, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Polisi wa Jimbo la Xinhua nchini China, wamelazimika kumpigia magoti mwanamke mmoja wakimuomba kufuta uamuzi wake wa kujirusha kutoka juu ya nyumba yenye urefu wa ghorofa saba, kufuatia mzozo aliotokea nyumbani kwake baina yake na mumewe.Kwa mujibu wa habari kutoka jimboni humo, mwanamama huyo Chan Bao, aliamua kuchukua uamuzi huo wa kupanda juu ya ghorofa ili kujitupa chini, kufuatia mumewe Cheng Dong kuondoka nyumbani kimya kimya bila ya kumtakia ‘Birthday njema’ wakati akijua fika kuwa siku hiyo ilikuwa ni siku yake ya kuzaliwa.

Kitendo cha mumewe kuondoka kimya kimya hakikumpendeza Chan, hali iliyomfanya ahisi amedharauliwa, jambo lilompandisha hasira na kufikia uamuzi wa kutaka kujirusha kutoka juu ya ghorofa. Hata hivyo dhamira ya mwanamke huyo haikutimia kwani baada ya polisi kuona haelewi, waliamua kumfuata hukohuko juu na kumteremsha chini kwa nguvu.

source globalp