Nyota wa muziki wa R&B wa Marekani Rihanna amekanusha uvumi uliozagaa nchini Barbados alikozaliwa kuwa alimhonga penzi mkongwe wa hip hop Jay-Z ili apate umaarufu alio nao sasa.
Nyota wa muziki wa R&B wa Marekani aliyetamba na nyimbo yake ya "Umbrella" ameelezea kuchukizwa na uvumi uliozagaa wakati alipoanza kuwika kwenye anga ya muziki kuwa alimhonga penzi Jay-Z ili ampe tafu kwenye masuala ya kimuziki.
Kipaji cha muziki cha Rihanna kilivumbuliwa kwenye visiwa vya Barbados na Jay-Z ambaye aliamua kumpa tafu Rihanna kuandaa albamu yake ya kwanza.
Lakini Rihanna anasema kuwa uvumi ulizagaa kila kona kwenye visiwa hivyo kuwa alimpa uroda Jay-Z ili ampe tafu kimuziki.
Rihanna anasema kuwa hata marafiki zake wa karibu waliamini kuwa alilala na Jay-Z ili apewe tafu.
Rihanna amekanusha uvumi huo na kusema kuwa hakuwahi kuwa na uhusiano wowote wa kimapenzi na Jay-Z.
"Uvumi huu ulinifanya nijisikie vibaya wakati wote na nilishindwa hata kumuangalia machoni Jay-Z", alisema Rihanna.
"Siku moja Jay-Z aliniita na kuniambia nisisikilize watu wanachovumisha, nisiishi kwa kufuatisha maneno ya watu", alisema Rihanna.
source.nifahamishe.com
BUSTA RYMES ALIVYOKAMUA NDANI YA FIESTA 2009
Sunday, November 22, 2009
/
Posted by
ishak
/
comments (0)
Subscribe to:
Posts (Atom)