Obama Aweka Wazi Cheti cha Kuzaliwa

Thursday, April 28, 2011 / Posted by ishak / comments (0)Baada ya Kusakamwa Sana, Obama Ameamua kuweka Wazi Cheti cha Kuzaliwa

Baada ya kusakamwa sana kuwa hajazaliwa Marekani na hivyo hafai kuwa rais wa Marekani, Barack Obama ameamua kukata mzizi wa fitina kwa kuweka wazi cheti cha kuzaliwa.
Rais Barack Obama wa Marekani ili kumaliza majungu ya wapinzani wake kuwa yeye si Marekani ameamua kuweka wazi cheti chake cha kuzaliwa.

Wapinzani wa Obama kwa muda mrefu sana wamekuwa wakisema kuwa Obama hajazaliwa Hawaii, Marekani kama anavyodai hivyo haruhusiwi kisheria kuwa rais wa Marekani.

Ilikuwa ikidaiwa kuwa huenda Obama alizaliwa Kenya anakotoka baba yake mzee Hussein Obama au nchini Indonesia ambako Obama alikuwa huko wakati wa utoto wake.

Huku uchaguzi mkuu utakaofanyika tena mwakani ukianza kujongea, Obama ameamua kusambaza nakala za cheti cha kuzaliwa ili kumaliza gumzo la sehemu aliyozaliwa.

Akisambaza nakala za cheti chake cha kuzaliwa, Obama alisema kuwa hana muda wa kupoteza kubishana na wapinzani wake.

source nifahamishe