Mwanaume mmoja nchini China anashikiliwa na polisi baada ya kumuua mtoto wa miaka 11 na kisha kuula ubongo wake akidai kuwa aliambiwa kuwa tiba ya kifafa ni ubongo wa mtoto.
Polisi nchini China wanamshikilia mwanaume aliyemuua mtoto wa miaka 11 na kisha kuula ubongo wake akidai kuwa mke wake wa zamani aliwahi kumwambia kuwa ubongo wa mtoto ni tiba bora ya ugonjwa wa kifafa.
Wang Chaoxu, wa kijiji cha Qixian katika jimbo la Yunnan, kusini mwa China alitiwa mbaroni jumatano baada ya polisi kukuta mwili wa mtoto wa kiume wa miaka 11, Li Xuetang ukiwa umezikwa kwenye kichaka.
Kichwa cha mtoto huyo kilikuwa kimepasuliwa na sehemu ya ubongo wake ilikuwa imenyofolewa.
Mama wa mtoto huyo, Yu Chaohu alisema kuwa alipatwa wasiwasi mkubwa baada ya mtoto wake kutoweka ghafla majira ya jioni.
"Giza lilikuwa likiingia na sikuweza kumuona mtoto wangu, niliwaomba wanakijiji wanisaidie kumtafuta na hata nilimuomba mkuu wa kijiji apeleke tangazo redioni", alisema mama wa mtoto huyo kwa uchungu.
Mama wa mtoto Li hakuruhusiwa kuiona maiti ya mwanae kutokana na jinsi ilivyokuwa imeharibika vibaya sana.
Wakati Wang alipotiwa mbaroni alisema kuwa alikuwa akiamini kuwa kwa kula ubongo wa mtoto uliochangwanya na minyoo na sisimizi, ugonjwa wake wa kifafa ungeondoka.
Polisi pia wanaendelea kufanya uchunguzi kujua kama Wang anahusika na kifo cha mtoto wa kike wa miaka mitatu ambaye mwili wake ulipatikana siku hiyo hiyo huku kichwa cha mtoto huyo nacho kikiwa kimepasuliwa na ubongo wake ukiwa umenyofolewa
source nifahamishe
Mgonjwa wa Kifafa Ala Ubongo wa Mtoto Akidai ni Tiba ya Kifafa
Mwanaume mmoja nchini Marekani ameiaga dunia baada ya kuangukiwa na ndege ndogo ya injini moja wakati alipokuwa akitembea pembeni mwa ufukwe wa bahari.
Ndege ya injini moja imemua mwanaume aliyekuwa akifanya mazoezi ufukweni, baada ya kumuangukia wakati ilipopata hitilafu angani.
Ndege hiyo ilipata hitilafu kwenye injini yake wakati ikipaa kuelekea Virginia toka Florida.
Ndege hiyo ilitakiwa itue kwa dharura kwenye uwanja wa ndege wa South Carolina lakini ikiwa njiani ilipata tatizo jingine la kuvuja kwa mafuta ya ndege kabla ya injini yake kuzimika kabisa.
Rubani wa ndege hiyo aliamua kunusuru maisha yake na ya abiria mmoja aliyekuwa ndani ya ndege hiyo kwa kutua kwa dharura kwenye ufukwe uliopo kwenye mji huo.
Ilikuwa ni wakati huo, ndege hiyo ilipomgonga mwanaume aliyekuwa akifanya mazoezi kwenye ufukwe huo kabla ya kuserereka na kwenda kusimama kwenye maji.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, kwakuwa injini ya ndege hiyo ilikuwa imezimika, ndege hiyo haikuwa ikitoa kelele yoyote hali ambayo ilisababisha kugongwa kwa mwanaume huyo.
Majina ya mwanaume aliyefariki na majina ya rubani wa ndege hiyo ya abiria wanne hayakupatikana mara moja.
source nifahamishe
Sindano Iliyomuua Michael Jackson Kupigwa Mnada
Sindano ambayo iliripotiwa kuwa Michael Jackson aliitumia kujidunga dozi kubwa ya madawa yaliyopelekea kufariki kwake, itapigwa mnada na inategemewa kununuliwa kwa dola milioni 5.
Kwa mujibu wa gazeti la The Telegraph la Uingereza, sindano hiyo inapigwa mnada mjni Las Vegas ikichukuliwa kama mojawapo ya kumbukumbu muhimu za Michael Jackson.
Vyanzo vya habari vilisema kuwa sindano hiyo inatarajiwa kununuliwa kwa dola milioni tano na huenda ikapata mnunuzi wakati wa mnada mkubwa utakaofanyika juni 25 wakati wa kuadhimisha mwaka mmoja tangia alipofariki mfalme huyo wa muziki wa Pop.
Familia ya Michael Jackson inasemekana kuwa inazo taarifa za mnada wa sindano hiyo na imekasirishwa sana na mawazo ya watu wanaotaka kunufaika na kifo cha Michael Jackson.
"Hili ni mojawapo ya matukio kadhaa ya kusikitisha", alisema mdau mmoja wa familia ya Jackson.
"Sindano hiyo haihitajiki kwenye kesi ya mauaji aliyofunguliwa daktari wa Michael Jackson, Dr Murray, lakini inasikitisha kuona kuna watu wasio na utu hata kidogo", alisema mdau huyo wa familia ya Jackson ambaye hakutajwa jina lake.
Mwanaume aliyeitia mikononi sindano hiyo amekuwa akiwasiliana na wanasheria wake kuhakikisha kuwa hakuna mtu atakayejitokeza kumnyang'anya sindano hiyo wala hatakaliwa kuipiga mnada sindano hiyo.
Michael Jackson alifariki mwezi juni mwaka jana kutokana na matatizo ya moyo kufuatia tabia yake ya kutumia dozi kubwa za madawa ya kupunguza maumivu.
source nifahamishe
Mlowezi wa kiingereza nchini Australia ameingia kwenye rekodi za dunia kwa kuwa mtu wa kwanza kutambulika kisheria kuwa hana jinsia yoyote si ya kiume wala ya kike.
Norrie May-Welby mwenye umri wa miaka 48, Muingereza anayeishi nchini Australia amekuwa mtu wa kwanza duniani kutambulika kisheria kuwa hana jinsia yoyote.
Madaktari nchini Australia walishindwa kumuweka Norrie kwenye fungu la wanawake au wanaume kutokana na hali yake ya kutokuwa na viungo vyovyote vya siri.
Norrie alizawaliwa kama mwanaume lakini alifanya operesheni ya kubadilisha jinsia yake kuwa mwanamke mwaka 1990 wakati huo akiwa na umri wa miaka 28.
Lakini baada ya kutokuwa na furaha katika hali yake mpya ya uanamke, Norrie aliamua kufanya operesheni nyingine na kuondoa uke alioupandikiza ili asiwe na jinsia yoyote.
Katika pasipoti yake mpya kama raia wa Australia, ilibidi maafisa wa serikali waongeze fungu jingine la watu wasio na jinsia baada ya madaktari kusema kuwa wanashindwa kuthibitisha Norrie ni jinsia gani.
"Mimi si mwanaume wala mwanamke, mimi nimeona bora nisiwe na jinsia yoyote", alisema Norrie.
Kutokana na uamuzi huo wa maafisa wa Australia, Norrie amekuwa mtu wa kwanza duniani kutambulika kisheria kuwa hana jinsia yoyote.
source nifahamishe
Mpemba kortini kwa kulawiti watoto wanne kwa mpigo
SELEMANI RASHIDI mkazi wa mtaa wa Utete Ilala jijini Dar es Salaam, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashitaka ya kulawili watoto wanne wenye umri wa miaka kumi .
Mshitakiwa huyo mwenye asili ya kipemba, alifikishwa mahakamani hapo mwishoni mwa wiki iliyopita akikabiliwa na mashitaka hayo.
Alifikishwa Mbele ya Hakimu Mkazi Genevitus Dudu, na upande wa Mashitaka ulikuwa ukisimamiwa naWakili wa Serikali, Abubakar Mrisho wote wa maakma hiyo.
Ilidaiwa kuwa, mshitakiwa alilawiti watoto hao wanne huku akijua ni kosa kisheria. Na amekwenda kinyume cha kifungu cha 154(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kama ya mwaka 2002.
Ilidaiwa kuwa, Februari 15 mwaka huu, majira ya saa nane mchana, huko Mtaa wa Kilwa na Utete, Ilala nyumba namba 1, kwa mshitakiwa aliwalawiti watoto wanne wenye umri kati ya miaka minane na kumi.
Mshitakiwa huyo alikana shitaka hilo na wakili wa kujitegemea Mabere Marando aliiomba mahakama impatie mteja wake dhamana kwa kuwa mashitaka yanayomkabili yanadhaminika kisheria.
Hata hivyo, Hakimu Mkazi Dudu alisema hakuwa kwenye nafasi nzuri ya kutoa masharti ya dhamana, hivyo akaamuru mshitakiwa apelekwe rumande hadi Machi 17 mwaka huu, siku ambayo atatoa masharti ya dhamana.
Hivyo mshitakiwa alirudishwa rumande na atarudishwa tena kesho kwa kutajwa na atakwua nje wka dhamdana endapo hakimu atatoa masharti ya dhamana.
source nifahamishe
Mwanamke Ajitesa Ili Avunje Rekodi ya Dunia
Mwanamke ambaye alivunja rekodi ya dunia kwa kuwa mwanamke mnene kuliko wote duniani kujifungua mtoto, anakula chakula cha kuwatosha wanawake sita kila siku ili aweze kuvunja rekodi ya dunia ya kuwa mwanamke mnene kuliko wote duniani.
Donna Simpson,toka New Jersey,Marekani hivi sasa ana uzito wa kilo 273 lakini ametangaza nia yake ya kula sana ili uzito wake ufikie kilo 450 ndani ya miaka miwili.
Donna ambaye ana umri wa miaka 42 tayari anashikilia rekodi ya kuwa mwanamke mnene kuliko wote duniani kujifungua mtoto. Alijifungua mtoto wa kike mwaka 2007 wakati huo akiwa na uzito wa kilo 241.
"Ningependa kutimiza kilo 450... ingawa ni vigumu, kumkimbiza kimbiza mtoto wangu kunanifanya nisiongezeke uzito kwa kasi", alisema Donna alipokuwa akifanya mahojiano na gazeti la Daily Mail la Uingereza.
Donna ambaye anahitaji scotter kumwezesha kutembea, hula kiasi kikubwa cha chakula kila siku ambacho kingeweza kuwatosha wanawake sita.
Donna ambaye anapewa kampani na mumewe kutimiza rekodi hiyo, hujitahidi asitembee umbali mrefu ili kalori za vyakula anavyokula zisipotee.
Donna anatumia dola 815 kila wiki kwaajili ya kununulia chakula. Donna hujiingizia pesa anazotumia kwa matumizi yake kwa kutumia tovuti yake aliyoifungua ambapo wanaume hulipa pesa kumuangalia yeye akifakamia vyakula vyake.
source nifahamishe
Mtu Mfupi Kuliko Wote Duniani Afariki Dunia
He Pingping mbaye alikuwa kitambulika kama mwanaume mfupi kuliko wote duniani akiwa na urefu wa sentimeta 74.61 amefariki dunia jumamosi kutokana na matatizo ya moyo.
He Pingping, amefariki dunia nchini Italia akiwa na umri wa miaka 21.
He alikuwa nchini Italia kwaajili ya kushiriki kwenye shoo ya kwenye luninga lakini alisumbuliwa na maumivu makali kwenye kifua na alipowahishwa hospitali wiki mbili zilizopita alifariki siku ya jumamosi kutokana na kile kinachoaminika kuwa ni matatizo ya moyo.
He alizaliwa nchini China akiwa na ugonjwa unaomfanya awe mfupi sana. Baba yake He Yun aliwahi kusema kuwa He alipozaliwa alikuwa mdogo sana kiasi cha kuenea kwenye viganja vyake vya mikono.
He alitambulika rasmi kama mtu mfupi duniani na kuingizwa kwenye kitabu cha rekodi za dunia, Guinness mnamo mwaka 2008.
Akiwa na taji lake hilo, He alisafiri nchi mbalimbali duniani kutangaza rekodi yake hiyo akiwa na watu wengine waliovunja rekodi za dunia.
Mwezi septemba mwaka 2008, He alienda mjini London, Uingereza na kupiga picha na mwanamke mwenye miguu mirefu kuliko wanawake wote duniani, Svetlana Pankratova.
Mwanzoni mwa mwaka huu, He alisafiri kwenda Istanbul,Uturuki ambapo alikutana na mtu mrefu kuliko wote duniani Sultan Kosen mwenye urefu wa sentimeta 246.5.
Guinness World Records wamesema kuwa mrithi wa taji la He atatangazwa katika siku zijazo.
Hata hivyo, Khagendra Thapa Magar, 18, toka Nepal ndiye anayeonekana kuwa mtu atakayenyakua taji hilo kwani ni mfupi kuliko He akiwa na urefu wa sentimeta 51 tu.
source nifahamishe
WANAUME wawili wamejikuta wakipeana dozi ya ngumi baada ya kukerwa na adha ya usafiri iliyofanya mmoja ashikwe na hasira baada ya mmoja kumuumiza mke wake.
Wanaume hao wamejikuta wakirushiana maneno na mmoja wao kushikwa na hasira kali na kujikuta akimrushia ngumi mwenzake baada ya kukerwa na kuumizwa kwa mke wake ndani ya dalalada hiyo.
Hali hiyo ilitokea mwishoni mwa wiki, maeneo ya Kariakoo katika mabasi yaendayo Mbezi.
Mtafaruku huo ulitokea baada ya mume wa dada huyo kuingia ndani ya daladala na kuwahi siti mbili ili nyingine aje kukalia mke wake ambaye hakuweza pulukushani ya kuingia mlangoni kuwahi siti.
Hivyo katika hali ya kawaida jijini Dares Salaam utaratibu huo wa kuwekeana siti ndani ya daladala huwa watu wengi watumiao usafiri huo huwa hawaukubali kutokana na shida ya usafiri na hasa nyakati zajioni kila mmoja huwa amechoka na kutaka kukalia siti.
Kwa kuwa dada huyo alichelewa kuingia ndani ya basi hilo na watu wengine waliona siti hiyo imewekwa handbag kumaanisha kuwa kuna mtu amewahi ilihali yuko chini baba mmoja alimtaka atoe handabag hiyo akalie hiyo siti.
Mume wa dada huyo alianza kumwambia kuwa alimuweke mkewe ambaye yuko chini atakuja kukalia, kutokana na jibu hilo mtu aliyetaka kukalia siti hiyo hakumuelewa na kumuona mpuuzi na kutoa handbag hiyo na kukalia siti hiyo.
Alianza kumwambia atoke na mke wake akalie siti hiyo mtu huyo aliendaelea kumuona mpuuzi na mume wa dada huyo kumuamrisha mke wake amkalie baba huyo hivyohivyo kwa kuwa alikuwa mbishi.
Kabla dada huyo hajafanya kama mumew ake alivyomwambia baba huyo aliyekalia hiyo siti alimsukumiza dada huyo na kuanguka upande mwingine.
Hivyo kutokana na hali hiyo mtafarufku ndipo ulipoianzia hapo na kuanza kutupiana maneno hali iliyofanya kuzuke kwa zaogo ndani ya basi hilo bila sababu za msingi.
BAadhi ya abiia walionekana kumsaidida mume wa dada huyo na baadhi walimsaidia aliyekalia siti hiyo na kumtetea kuwa utaratibu wa kuwekeana siti kikawaida hautumiki unatumika kwa mabasi yanedayo mikoani.
Kwa kuwa mtu aliyekalia siti hiyo aliendelea na msimamo wake wa kutotoka mume wa dada huyo alishikwa na jazba na kuanza kumpiga ngumi na Yule hakukubali na kuanza kuzichapa.
Hali hiyo ilitulia baada ya dereva kuamrisha kuwa akifika Magomeni ataingiza gari polisi awaache watu hao kwa kuleta adha ndani ya daladala.
Matukio hayo hutokea mara kwa mara katika mabasi ya usafiri wa daladala, na kadri siku zinavyozidi kusogea usafiri huo wa daladada unazidi kuwa washida na mgumu mno kwa kusemekana kila siku idadi ya watu wengi kuingia jijini Dar es Salaam wakitokea mikoani na kufanya usafiri huo kuzidi kuwa mgumu katika njia zote jijini.
source nifahamishe
Kahaba Aenda Mahakamani Kupinga Kufukuzwa Kazi
Ingawa ni kinyume cha sheria kufanya ukahaba, Kahaba mmoja nchini Afrika Kusini ameenda mahakamani kupinga kusimamishwa kazi isivyo halali kwenye danguro moja lililopo mjini Cape Town.
Kahaba huyo anayejulikana kwa jina la Kylie alisimamishwa kazi kutokana na tabia yake ya kuchagua wateja na kutumia muda mwingi na mpenzi wake ambaye alikuwa hataki kulipa kwa huduma ya ngono anayopewa.
Jaji wa kesi alishikwa na butwaa akisema kuwa haamini inakuwaje mtu anayefanya kazi haramu akaenda mahakamani kuitetea kazi haramu anayofanya.
Hata hivyo wanasheria wa Kylie wanasema kuwa kesi ya Kylie si kuhusiana na kufanya kwake ukhaba ambao ni kinyume cha sheria bali ni kufukuzwa kwake kazi isivyo halali.
Mahakama kadhaa za nchini Afrika Kusini zimekataa kuisikiliza kesi hiyo zikisema kuwa kufanya ukahaba ni kinyume cha sheria, vimeripoti vyombo vya habari vya Afrika Kusini.
Majaji watatu wa mahakama ya kazi wanakuna vichwa vyao kujua kama waisikilize kesi hiyo au la.
"Wakati unaposimamishwa kufanya kitu haramu.. haiingii akilini kusimama na kupigania watu wakurudishe kufanya kazi ya haramu", alisema rais wa majaji, Raymond Zondo.
Kylie amekuwa akipigania kurudishwa kwenye kazi yake haramu kwa miaka saba sasa tangia aliposimamishwa kazi mwaka 2003
source nifahamishe
Sura ya Yesu Yadaiwa Kuonekana Kwenye Kikaangio
Picha yenye sura ya Yesu imedaiwa kuonekana kwenye kikaangio cha mwanaume mmoja wa nchini Uingereza ambaye aliunguza mapishi yake ya nyama ya nguruwe kwenye kikaangio hicho wakati alipopitiwa na usingizi wakati anapika.
Toby Elles, 22, anadai kugundua sura ya Yesu kwenye kikaangio baada ya kuunguza chakula alipopitiwa na usingizi wakati anapika.
Toby anadai kuwa baada ya kuziokoa nyama zake za nguruwe ambazo zilikuwa zikiungua kwenye kikaangio hicho, hakuamini macho yake alipoona sura kama ya Yesu kwenye kikaangio.
"Sura yake inaonekana wazi, pua, macho na ndevu zake zote zinaonekana wazi", alisema Toby.
"Nilipitiwa na usingizi wakati nakaanga nyama ya nguruwe, iliungua na ndipo sura hii ya Yesu ilipotokea, ni kama miujiza vile", alisema Toby mwenye umri wa miaka 22 ambaye ni mfanyakazi wa benki ya Halifax nchini Uingereza.
Toby anasema kwamba hatakiosha kikaangio hicho na badala yake atakiweka ukutani kimlinde yeye na nyumba yake.
"Nafikiria kutengeneza fremu ya kioo nikiweke hiki kikaangio, kimekuwa gumzo kwa kila anayeingia nyumbani kwangu".
source nifahamishe
Amfumania Mkewe na Wanaume Wawili, Awaua Wote
Mwanaume mmoja wa nchini Marekani ambaye aliingia nyumbani kwa mpenzi wake na kumkuta mpenzi wake akifanya mapenzi na wanaume wawili kwa mpigo, anashikiliwa na polisi kwa kumuua mpenzi wake na wanaume hao wawili aliowafumania nao.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 50 mkazi wa Brooklyn, New York aliingia kwenye nyumba ya mpenzi wake na bila kutarajia alimkuta mpenzi wake akifanya mapenzi na wanaume wawili kwa wakati mmoja.
Mwanaume huyo alimuachia ujumbe wa sauti rafiki yake kuwa amemuua mpenzi wake mwenye umri wa miaka 51 baada ya kumfumania akifanya mapenzi na wanaume wawili kwa mpigo.
Polisi walipewa ujumbe huo wa sauti na kuwahi kwenye nyumba ya mwanamke huyo na kumkuta mwanaume huyo akiizunguka maiti ya mpenzi wake.
Mwanaume huyo alikiri mbele ya polisi kuwa alishikwa na hasira sana baada ya kumfumania mpenzi wake akiliwa mtungo na wanaume wawili, alimuua mpenzi wake na wanaume hao wawili na kisha kuikatakata vipande vipande miili ya wanaume hao na kwenda kuitupa kwenye vichaka.
Jirani mmoja wa mwanaume huyo alisema kuwa mwanaume huyo hakuonekana kutetereka wala kujutia mauaji aliyoyafanya, aliinamisha kichwa chake chini wakati alipokuwa akipandishwa kwenye karandinga la polisi, liliripoti gazeti la New York Post.
Polisi wanaendelea kumshikilia mwanaume huyo na uchunguzi wa kesi yake unaendelea.
source nifahamishe
Wakati mwanafunzi wa chuo kikuu kimoja nchini China alipoweka tangazo kwenye ubao wa shule kuwa anatafuta mpenzi, alitarajia wanaume wawili watatu wangejitokeza lakini kwa mshangao wake maelfu ya wanaume wa chuo kikuu hicho walijitokeza mbele ya chumba chake.
Ilikuwa ni siku ya wasichana kwenye chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha mjini Chengdu nchini China. Chuo hicho kina wanaume wengi sana kuliko wanawake. Uwiano wa wanaume 25 kwa mwanamke mmoja.
Kila mwanafunzi wa kike alipewa karatasi nyeupe akitakiwa aandike chochote anachotaka na karatasi hiyo itabandikwa kwenye ubao wa matangazo wa chuo hicho.
Msichana wa mwaka wa kwanza Zhang Mengqian kwa upande wake aliandika kwenye karatasi hiyo kuwa yeye ni mrembo sana lakini hana bahati ya kupata mpenzi, alitaka mwanaume anayetaka kuwa na uhusiano naye asimame mbele ya bweni lake kati ya saa 12:30 na 12:50 ya siku ya alhamisi ambayo ilikuwa machi 11 mwaka huu na kisha aite jina lake kwa sauti. Zhang alisema atachungulia kwenye dirisha lake kumuangalia mwanaume anayemuita, kama akipendezewa naye atashuka chini.
Zhang alitarajia mwanaume mmoja au wawili wangejitokeza, lakini siku hiyo ilifika na kwa mshangao mkubwa maelfu ya wanaume walijazana mbele ya bweni lake na kuanza kuita jina lake.
Kutokana na idadi kubwa sana ya watu waliojitokeza, Zhang alishindwa hata kuchungulia chini kuwaangalia wanaume waliojitokeza na kuamua kujifungia chumbani kwake.
Wanaume hao walisubiria kwa muda bila ya matumaini ya kuonana na Zhang na hatimaye waliamua kuondoka.
source nifahamishe
Migahawa Kupigwa Marufuku Kuweka Chumvi Kwenye Chakula
Wapishi katika jiji la New York nchini Marekani wako kwenye hatihati ya kupigwa faini ya dola 1,000 iwapo wataweka chumvi kwenye vyakula wanavyopika.
Manispaa ya New York imepokea muswada wa sheria ambao utawapiga marufuku wapishi kwenye migahawa yote ya mjini humo kuweka kiasi chochote kile cha chumvi kwenye vyakula wanavyoviandaa.
Muandaaji wa muswada huo Felix Ortiz alisema kuwa muswada huo ukipitishwa itakuwa ni hatua nzuri sana ya kuokoa maisha ya maelfu ya watu wanaofariki kutokana na magonjwa ya moyo.
Muungano wa wapishi wa New York umeupinga muswada huo na kuuita ni wa kipuuzi.
Tom Colicchio, mmiliki wa mgahawa wa Craft ambaye pia ni nyota wa mapishi kwenye televisheni za Marekani alisema "Iwapo watapiga marufuku chumvi kwenye chakula, hakuna atakayekuja hapa kula".
Kwa mujibu wa muswada huo, Migahawa haitaruhusiwa kuweka kiasi chochote cha chumvi kwenye vyakula vyao lakini chumvi itawekwa kwenye meza kwa mteja kujiwekea mwenyewe.
Jumla ya wakazi milioni 1.5 wa New York wanakabiliwa na matatizo ya moyo na shinikizo la damu.
Inakakadiriwa kuwa hatua ya kupunguza matumizi ya chumvi itasaidia kuokoa maisha ya watu 100,000
source nifahamishe