Kuna mashindano mengi yameibuka duniani kutafuta vipaji kama vile Pop Star, Bongo Star Search na mengineyo lakini huko nchini Malaysia yameanza mashindano ya aina yake kutafuta imamu bora.
aada ya mashindano ya Popstar, American Idol, The X Factor na mengineyo kuibuka sehemu mbalimbali duniani, mashindano ya kwanza ya aina yake yameanza nchini Malaysia yakienda kwa jina la "Imam Star".
Mashindano hayo ambayo nchini Malaysia yanajulikana kwa jina la "Imam Muda", yanawashindanisha vijana wa kiislamu ili kumpata imamu bora kati yao.
Vijana wenye umri kati ya miaka 19-27 wamewekwa nyumba moja ambapo kwa kipindi cha miezi mitatu na watakuwa wakishindana kumpata imamu bora kati yao.
Vijana hao watashindana kusoma azana, kusalisha, kutoa khutba, kuosha maiti na kuongoza mazishi.
Maiti zitakazotumika katika mashindano hayo ni maiti zilizopo monchwari ambazo hazijatambuliwa na ndugu zao.
Mshindi wa mashindano hayo hatapewa zawadi ya pesa kama yalivyo mashindano mengine. Atapewa schorlaship ya kusoma mambo ya dini katika chuo kikuu cha al-Madinah University cha nchini Saudi Arabia. Mshindi pia atapewa kazi ya kusalisha misikiti mikubwa ya mjini Kuala Lumpur na pia atakuwa akilipiwa gharama zote za kuhiji Makka.
Mashindano hayo yamekuwa gumzo nchini Malaysia yakivunja rekodi ya watazamaji. Yamebakiza mwezi mmoja kuisha.
source nifahamishe
Mashindano ya Maimamu 'Imamu star' Yaanza Malaysia
'Michael Jackson Asingefariki Kama Angekuwa Muislamu'
Katika kuadhimisha mwaka mmoja tangia alipofariki, kaka yake Michael Jackson, amesema kuwa anaamini kaka yake angekuwa hai hadi leo kama angebadili dini kuwa muislamu.
Akiongea na shirika la habari la Uingereza la BBC katika mahojiano ambayo yatarushwa hewani leo, kaka yake Michael Jackson, Jermaine Jackson amesema kuwa anaamini kaka yake angekuwa hai hadi leo hii kama angefanikiwa kubadili dini kuwa muislamu.
Jermaine alisema kuwa kama Michael angebadili dini kuwa muislamu basi maisha yake yangebadilika na asingekuwa na maisha ambayo yalipelekea kifo chake.
"Naamini kama Michael angekuwa muislamu, angekuwa hai hadi leo, nasema hivi kwasababu nyingi sana", alisema Jermaine ambaye yeye alibadili dini kuwa muislamu miaka mingi sana iliyopita.
"Sababu ni kwamba mtu unapokuwa muislamu na ukafahamu kwa asilimia 100 sababu ya wewe kuwepo duniani na sababu ya watu waliokuzunguka kuwepo duniani, basi maisha hubadilika na kuwa mazuri", alisema Jermaine.
Jermaine aliongeza kuwa alimnunulia Michael vitabu vingi vya kiislamu toka Saudi Arabia na Bahrain.
"Alisoma vitabu vingi vya kiislamu", alisema Jermaine na kuongeza kuwa Michael hakuwa akiupinga uislamu.
"Walinzi wake wote walikuwa waislamu kwa kuwa aliuamini Uislamu, aliwaamini kwakuwa waislamu hujaribu kuwa watu wazuri kadri wawezavyo, si kwaajili ya Michael Jackson bali kwaajili ya Mungu".
"Wakati unapozungukwa na watu kama hawa unajua kwamba Mwenyezimungu atakulinda", alimalizia kusema Jermaine.
Michael Jackson alifariki akiwa na umri wa miaka 50, juni 25 mwaka jana kutokana na shambulizi la moyo lililotokana na matumizi makubwa ya madawa ya kupunguza maumivu.
Washabiki wake wanajiandaa kuadhimisha mwaka mmoja wa kifo chake siku ya ijumaa kwa kufanya shughuli mbalimbali za kukumbuka kazi zake za muziki.
source nifahamishe
Achomwa Kisu Kwa Kulalamikikia Miguno ya Ngono ya Jirani
Mwanaume mmoja nchini Marekani amechomwa kisu na jirani yake baada ya kulalamikia sauti kali za ngono anazozitoa anapofanya mapenzi na mpenzi wake.
Mwanaume mwenye umri wa miaka 40 aliyejulikana kwa jina la Russell Willis Shepherd Jr. amefunguliwa mashtaka ya kumshambulia jirani yake mwenye umri wa miaka 58 ambaye alikuwa akilalamika miguno ya kimahaba aliyokuwa akiitoa.
Katika tukio hilo lililotokea South Carolina nchini Marekani, jirani wa Russel alirudi nyumbani kwake na kumkuta Russel akitoa sauti kali wakati akifanya mapenzi na mpenzi wake mwenye umri wa miaka 39.
Kuepuka kelele hizo aliamua kwenda nje kuvuta sigara, aliporudi na kukuta kelele hizo zikiwa ndio zimepamba moto, aliamua kumgongea mlango Russel na kumwambia apunguze kelele za ngono anazozitoa.
Russel alikasirishwa na kitendo hicho, alichukua kisu na kuanza kumshambulia jirani yake huyo mpaka alipofanikiwa kuchoropoka na kuomba msaada toka kwa jirani.
Russel almefunguliwa mashtaka ya kufanya shambulizi la kudhuru mwili na ametupwa jela akisubiri kufikishwa mahakamani.
source nifahamishe