Mgombea Ubunge Agawa Simu 800 Kwa Wananchi Musoma

Saturday, July 24, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mgombea ubunge wa jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara, Bw. Nimrod Mkono ameanza kampeni yake ya kugombea ubunge kwa kugawa simu 800 kwa wananchi wake ili apate kupita.
Malalamiko hayo yametolewa na Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM kutoka mkoa huo Bw. Anthony Mtaka wakati akizungumza na Nifahamishe.com.

Alitoa malalamiko hayo kutokana na kauli ya hivi karibuni ya mbunge Nimrod Mkono ambaye anakitetea kiti chake cha ubunge, alipokaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akikiri kugawa simu na kuahidi kuendelea kugawa zaidi.

Katika kauli yake, mbunge huyo alisema kuwa ataendelea kugawaza zaidi, kwa madai kwamba zitawasaidia wana CCM kuwasiliana na pia kuweza kukichangia chama chao.

Akasema kuwa simu hizo ambazo tayari ametoa, zimegawiwa kwa utaratibu halali ulioelekezwa na chama chake kwa kuzikabidhi kwa viongozi wa chama ili wao ndio wazitoe kwa walengwa.

Mkono alisema kuwa lengo lake ni kugawa simu zaidi ya 800 ili zitatumike kwa kile kilichokusudiwa ambapo wana CCM waliopo vijijini wataweza kutoa fedha kidogo kuchangia Chama cha Mapinduzi.

Hata hivyo, kauli hiyo ya Mkono imemsikitisha mjumbe huyo ambaye amedai kuwa jimbo la Musoma Vijijini lina matatizo mengi ambayo yanatakiwa kutafutiwa ufumbuzi na sio hizo simu anazogawa.

"Kauli ya mbunge wetu kwa kweli imenisikitikisha, nilisoma kwenye magazeti akikiri kugawa simu za mkononi huku akiahidi kuendelea kugawa na kuacha matatizo ya msingi jimboni mwake," alisema Bw. Mtaka.

Alisema kuwa jimbo hilo lina changamoto nyingi za maendeleo ambazo zinafanana na majimbo mengine hapa nchini, hivyo yanahitaji kutafutiwa ufumbuzi wa haraka na sio kugawa simu za mkononi.

Alidai tarafa zote za jimbo hilo zikiwemo za Kiagata, Makongoro na Nyanja zina matatizo mengi kama ubovu wa barabara, shule kukosa mabweni, vyoo na mengine mengi yanayohitaji ufumbuzi wa haraka.

"Badala ya kushughulikia hayo, mbunge anajigamba kwa kugawa simu za promosheni kwa wana CCM, hili kwa kweli mimi kama mwana CCM na kiongozi limenisikitisha sana," alisema.

Alisema kuwa ni vyema mbunge huyo akashughulikia matatizo ya jimbo badala ya hilo alilolifanya la kugawa simu eti zisaidie wana CCM kuchangia chama chao kabla ya uchaguzi.

Alisema kukichangia chama sio muhimu, lakini inategemea na mhusika yuko katika mazingira gani na kudai kuwa wananchi wa jimbo hilo wanakabaliwa na matatizo mengi yanayokwamisha maendeleo yao.

"Yeye kama mwana CCM mwenzangu, nimeona nimkumbushe hayo ili anapoendelea na utaratibu wa kugawa simu, atambue yapo matatizo ya msingi anayopaswa kuyapa kipaumbele," alisema.

Sakata la ugawaji simu hizo kwa sasa liko mikononi wa Takukuru mkoani humo ambao bado wanaendelea na uchunguzi wao ili kubaini uhalali wa mgawo wa simu hizo.


source nifahamishe

Fella Ageukia Qaswida

Saturday, July 24, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


MENEJA wa kundi la TMK Wanaume Family, Saidi Fella ameamua kumgeukia mungu na kukisaidia chuo cha Almadrasat Chalama Islamia kutoa albamu yake ya nyimbo za Qaswida.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana, Fella alisema kuwa ameamua kukisaidia chuo hicho ambacho kiko Mbagala Kizuiani kutoa albamu ikiwa ni harakati ya kutangaza habari za mungu kupitia Qaswida.

"Hiki ni chuo ambacho mimi nilisoma, kwa hiyo nimeona ni vyema nikawasaidia kutoa albamu hii ili waweze kufikisha ujumbe wao kwa jamii kupitia Qaswida," alisema Fella.

Fella alisema kuwa albamu hiyo ambayo tayari imeshaingia sokoni ina nyimbo nne ambazo ni Mazingira uliobeba jina la albamu, Ukimwi na Ndoa.

Alisema kuwa anaamini Qaswida kama zitapewa nafasi zinaweza kufanya vyema katika ulimwengu wa muziki na kusaidia vilivyo kuiweka jamii katika mstari ulionyyoka.

"Qaswida mara nyingi nyimbo zake ni zile ambazo haziipotoshi jamii, na ni muziki ambao wahusika wake wanatakiwa kuweka mbele huduma zaidi za kijamii ukilinganisha na gospo ambao umegeuka kuwa muziki wa kibiashara zaidi," alisema Fella.

source nifahamishe

Amuua Mkewe Baada ya Kunyimwa Unyumba

Saturday, July 24, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanaume mmoja wa nchini Uingereza ambaye alikuwa akipenda sana kuliko kawaida kupewa unyumba na mkewe, amemuua mkewe baada ya mkewe kumnyima unyumba.
Brent Mott mwenye umri wa miaka 32 alimuaa mkewe, Kate, mwenye umri wa miaka 35 baada ya mkewe huyo kulalamika kwa marafiki zake na wafanyakazi wenzake kuwa amechoka kudaiwa unyumba kila wakati na mumewe.

Kabla ya siku ya tukio hilo, Mott alikuwa amepigwa marufuku na mahakama kuingia kwenye chumba cha mkewe baada ya wanandoa hao kuamua kuivunja ndoa yao.

Mott alimuua Kate siku moja kabla ya mahakama kutoa hukumu ya kuvunja ndoa yao ambapo Mott angetakiwa ahame nyumba na kumuacha Kate na watoto wao wawili.

Siku ya tukio hilo januari 21 mwaka huu, Mott alimfuata mkewe bafuni wakati akioga na kumuomba unyumba, alipokataliwa aliamua kutumia pijama ya mkewe kumnyonga.

"Baada ya kumuua mkewe alimvalisha nguo zingine na kumuingiza kwenye gari la familia na kumpeleka kwenye eneo la mashamba ambapo aliligongesha gari hilo ili kufanya ionekane mkewe amefariki kwa ajali", alisema mwendesha mashtaka Nigel Power akiiambia mahakama mjini Liverpool.

"Siku iliyofuatia alizuga hajui mkewe alipo na kuwapigia simu wakwe zake na polisi akisema anahofia kupotea kwa mkewe", aliendelea kusema mwendesha mashtaka huyo.

Mott ambaye ni mkazi wa Merseyside, alituhumiwa kuwa alikuwa akimnyanyasa sana mkewe kwa unyumba kiasi cha kufikia kudai unyumba siku tano baada ya mkewe kujifungua mtoto kwa operesheni.

Mott amekanusha kesi ya mauaji, kesi hiyo inaendelea.


source nifahamishe

Nyie Njooni tu Mjini' - Mwana FA

Saturday, July 24, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


MSANII Hamisi Mwinjuma 'Mwana FA' amesema kuwa wimbo wao wa Usije mjini aliyouimba na swahiba wake Ambwene Yesaya 'Ay', haukulenga kuwaogopesha watu kuja mjini isipokuwa unawapa watu taswira halisi ya maisha ya mjini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Mwana FA alisema kuwa walipata wazo la kutunga wimbo huo baada ya kusikiliza nyimbo nyingi za wasanii wa Tanzania ambazo zinaelezea zaidi mambo ya party hali ambayo inawajengea taswira watu walioko vijijini kuwa maisha ya mjini ni ya raha.

"Hata ukiangalia video za wasanii wetu, utaona nyingi zinazungumzia raha na watu wanajichana kila kukicha. Sasa mtu wa kijijini akiona ama kusikia nyimbo hizo taswira inayomjia kichwani mjini kuna maisha mazuri".

"Wengine wanajikuta wanatoka mjini ambako angalau alikuwa anamudu kuendesha maisha yake na kuja kuteseka mjini. Sasa sisi tukaona kuwa kuna kila sababu ya kutoa elimu juu ya hili," alisema msanii huyo.

Akizungumzia ni wapi walipopata wazo hilo, msanii huyo alisema kuwa wazo kamili lilikuja baada ya kuona msongamano wa watu waliokuwa wanasubiri daladala eneo la Mwananyamala.

"Nakumbuka siku hiyo mimi na Ay tulikuwa kwenye matembezi yetu ya kawaida, sasa tulipofika Mwanyamala tukaona mkusanyiko wa watu wanasubiri usafiri. Tukaanza kuelezana. Wakati hali iko hivi kuna baadhi ya watu wanajipanga kukimbia vijijini na kuja mjini, wakati huku mjini watu wanateseka".

"Tukakumbuka wimbo wa jamaa fulani kutoka Kenya wanajiita Sauti Soul ambao wanazungumzia raha za maisha ya kijijini".

"Tukaona ala kama kijijini kuna raha hizi, vipi watu waendelee kuja kuteseka hapa mjini?. Tukamwaga ujumbe," alisema Mwana FA.


source nifahamishe

Inakuwaje Wanigeria Wakazaa Mtoto Mzungu?

Thursday, July 22, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Wataalamu wa vinasaba (genetic) wanaumiza vichwa kutafuta sababu imekuwaje mama mweusi na baba mweusi wote toka Nigeria wamezaa mtoto wa kizungu mwenye nywele na macho kama ya watoto wa kizungu.
Madaktari nchini Uingereza wanaumiza vichwa kujua sababu ya kuzaliwa kwa mtoto wa kizungu na mama mweusi na baba mweusi ambao wote familia zao mpaka za mababu zao hawajawahi kuchanganya damu na mzungu.

Madaktari wataalamu wamethibitisha mtoto wa kike aliyezaliwa juzi jijini London katika familia ya Benjamin Ihegboro na mkewe Angela ni mzungu na wala si ALBINO.

Mtoto huyo amepewa jina la Kinigeria la Nmachi.

Benjamin na mkewe wote wana asili ya Nigeria na wote wana ngozi nyeusi na wana watoto wengine wawili ambao wote ni weusi.

Angela mwenye umri wa miaka 35 aliliambia gazeti la The Sun la Uingereza kuwa anajivunia mtoto wake huyo ingawa awali alishangazwa sana kuzaa mtoto mzungu kiasi cha kuwauliza madaktari "Huyu ni mtoto wangu kweli?".

"Ni mtoto mrembo -- mtoto wa miujiza", alinukuliwa akisema Angela.

Mtaalamu wa genetics Dr Mark Thomas alisema kuwa kutokana na historia ya familia zao, uwezekano wa Angela na mumewe kuzaa mtoto mzungu ulikuwa ni kati ya moja kati ya mamilioni.

Wataalamu wa genetics nchini Uingereza wanamfanyia uchunguzi mtoto Nmachi ili kujua sababu ya kuzaliwa akiwa na asili ya watu wa ulaya.

Lakini hata hivyo baba yake alisema kuwa hajali sana rangi aliyozaliwa nayo mtoto huyo.

"Ni mtoto mwenye kuvutia na tunampenda", alisema Benjamin na kuongeza "Hata kama angezaliwa akiwa wa njano au wa kijani, tungeendelea kumpenda


source nifahamishe

Mwarabu Atupwa Jela Kwa Kufanya Mapenzi na Myahudi

Thursday, July 22, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanaume mmoja wa kiarabu wa nchini Israel ametupwa jela miezi 18 baada ya kugundulika kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke wa kiyahudi baada ya kumuongopea kuwa yeye ni Myahudi.
Mahakama ya wilaya ya Jerusalem imemhukumu Sabbar Kashur mwenye umri wa miaka 30 kwenda jela mwaka mmoja na nusu kwa kosa lililohesabika kama kubaka kwa kufanya mapenzi na mwanamke wa kiyahudi baada ya kumuongopea kuwa yeye ni myahudi anayetaka uhusiano wa kimapenzi wa muda mrefu.

Kashur alifanikiwa kuanza uhusiano wa kimapenzi na mwanamke huyo lakini baada ya mwanamke huyo kugundua kuwa Kashur si myahudi kama alivyodai, alienda polisi kushtaki na Kashur alitiwa mbaroni akikabiliwa na kosa la ubakaji, limeripoti gazeti la Haaretz la Israel.

"Kama angejua kuwa mtuhumiwa si myahudi anayetaka uhusiano wa kimapenzi wa muda mrefu, asingemkubalia", alisema jaji Zvi Segal wakati akitoa hukumu.

Kashur ambaye ameoa na ana watoto wawili wadogo, ameiita hukumu hiyo kuwa ni ya kibaguzi.

"Kama mimi ningekuwa ni myahudi, wala wasingeniuliza kitu, huwezi kusema nimebaka", gazeti la Haaretz lilimnukuu Kashur.

"Alikubali mwenyewe bila kulazimishwa kila kitu ambacho kilitokea".

Kutumia uongo ili kuweza kumlaghai mwanamke na kufanya naye mapenzi huhesabika ni kubaka kwa mujibu wa sheria ambayo iliwekwa mwaka 2008 nchini humo baada ya mwanaume mmoja kujifanya yeye ni afisa wa masuala ya majumba ambaye aliwaahidi kuwapatia nyumba wanawake ambao angefanya nao mapenzi.

Kuna waarabu milioni 1.3 nchini Israel ambao ni sawa na asilimia 20 ya watu wote nchini humo.


source nifahamishe

Atumia Shada la Maua Kupora Pesa Benki

Thursday, July 22, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanaume mmoja nchini Marekani alitumia njia ya aina yake baada ya kwenda benki akiwa na shada la maua na kulitumia kama silaha kupora pesa.
Mwanaume huyo wa mjini New York nchini Marekani alienda benki akiwa na shada kubwa la maua na kumkabidhi mfanyakazi wa benki kibarua ambacho kilisema kuwa yeye ni jambazi aliyekuja kupora benki.

Polisi waliliambia gazeti la New York Post kuwa wanalifanyia uchunguzi shada la maua ya rangi mbalimbali , njano, nyekundu, kijani na rangi ya machungwa. Maua hayo yaliachwa na jambazi huyo ambaye alifanya uhalifu wake wiki iliyopita.

Kamera za ulinzi zilimuonyesha mtuhumiwa akiwa amesimama mbele na shada lake la maua huku akimkabidhi mfanyakazi wa benki kibarua ambacho aliandika "Nipe pesa zote mia mia na hamsini hamsini, usijaribu kuwa shujaa".

Imeripotiwa kuwa mwanaume huyo aliondoka benki akiwa amechukua kiasi cha dola 440.


source nifahamishe

Wazisaliti Ndoa Zao, Wadondoka Toka Ghorofani Wakila Uroda

Thursday, July 22, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanaume na mwanamke wa nchini Ujerumani ambao walizisaliti ndoa zao na kula uroda kwa siri, walianguka toka ghorofani kupitia kwenye dirisha ambalo waliliegemea wakati wakipeana uroda.
Wapenzi hao waliozisaliti ndoa zao walijikuta wakiwa uchi pembezoni mwa barabara baada ya kudondoka toka ghorofa ya kwanza katika jengo lililopo kwenye mji wa Lubeck nchini Ujerumani.

Majirani walisema kuwa wapenzi hao walikuwa wakikutana mara kwa mara katika nyumba hiyo.

"Hatukuwaona wakati wakifanya mapenzi lakini tulizisikia sauti walizokuwa wakizitoa", alisema mmoja wa majirani.

Polisi walisema kwamba wapenzi hao wakware walikuwa wakifanya mapenzi wakiegemea dirisha ambapo mwanamke alidondoka na kuangukia kifudifudi huku mpenzi wake akimfuatia kwa juu.

Wapenzi hao walivunjika baadhi ya mifupa ya miili yao na walipata majeraha kichwani.

Lakini katika hali ya kushangaza, pamoja na kwamba walikutwa pembeni ya barabara wakiwa uchi, mwanamke alisisitiza kuwa hawakuwa wakifanya mapenzi bali wakifanyiana masihara.

Na katika kuleta utamu zaidi wa tukio hilo, mwanamke huyo na mpenzi wake waliwahishwa hospitali ambako huko walikutana na mume wa mwanamke ambaye naye siku hiyo hiyo aliwahishwa hospitali baada ya kudondoka toka kwenye paa la nyumba yake wakati akilifanyia marekebisho.

source nifahamishe

Waislamu Indonesia Wasali Kuelekea Afrika Badala ya Makka

Tuesday, July 20, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Waislamu nchini Indonesia wamekuwa wakisali kuelekea Afrika badala ya Makka baada ya kiongozi mmoja wa kidini kujichanga na kuwapotosha watu juu ya uelekeo wa kibla.
Bodi ya waislamu nchini Indonesia ilitoa taarifa jana kwa waislamu nchini humo kuwa ilifanya makosa katika kuwaelekeza watu uelekeo wa kibla.

Kuanzia mwezi machi mwaka huu waislamu nchini humo walikuwa wakisali kuelekea Africa baada ya bodi hiyo kusema kuwa mji mtakatifu wa Makka upo magharibi mwa nchi hiyo.

Waislamu wote duniani wanatakiwa kusali kuelekea kibla kilichopo mjini Makka nchini Saudi Arabia.

Ma'ruf Amin, mwanazuoni wa bodi ya wanazuoni wa Indonesia ULEMA alisema "Baada ya uchunguzi na utafiti wa watalaam imeonekana kuwa watu wamekuwa wakisali kuelekea kusini mwa Somalia na Kenya".

"Sasa tumejua kuwa tunatakiwa tuelekee kaskazini magharibi", alisema.

Mwanazuoni huyo alisema kuwa Waindonesia hawatakiwi kuwa na hofu juu ya kukubalika kwa sala zao kutokana na kuelekea upande tofauti.

"Mungu anajua kuwa binadamu hufanya makosa", alisema mwanazuoni huyo na kuongeza "Allah siku zote husikiliza sala za waja wake".

Indonesia ndio nchi yenye waislamu wengi kuliko nchi zote duniani.

Indonesia ina jumla ya watu milioni 237 asilimia 90 kati yao ni waislamu.


source nifahamishe

Gazeti Lamuaibisha Rais wa Ufaransa

Monday, July 19, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Gazeti moja nchini Ufaransa limeingia matatani baada ya kutengeneza picha na kuziweka kwenye ukurasa wake wa mbele zikimwonesha rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy akiwa jela kama shoga akiinamishwa kwenye machuma.
Gazeti la vichekesho la Le Monte la Ufaransa katika tokeo lake la mwezi wa saba limeingia matatani baada ya kutengeneza picha za kumuaibisha rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy.

Gazeti hilo ambalo lilitakiwa liwe sokoni hadi mwezi wa nane, litaondolewa toka madukani kesho kufuatia uamuzi wa mahakama.


Gazeti ambalo lina idadi kubwa ya wasomaji lilitengeneza picha ikimuonyesha Sarkozy akiwa jela akiwa hana nguo hata moja akiingiliwa kinyume cha maumbile na mfungwa mwingine.

Picha hizo za kutengeneza ziliambatana na kichwa cha habari "Sarkozy akiwa jela".

Sarkozy ambaye hivi sasa yupo kwenye misukosuko mikubwa ya kisiasa alifungua kesi mahakamani kulishitaki gazeti hilo.

Nayo mahakama mjini Paris ilitoa hukumu ya kesi hiyo katika kipindi kifupi sana ambapo iliamua picha hizo za Sarkozy zifutwe katika nakala mpya zitakazochapishwa au la itabidi walipe faini ya euro 100 kwa kila picha itakayoonekana.

Katika kuimaliza kesi hiyo, hakimu alitowa hukumu gazeti hilo kumpa fidia Sarkozy sawa na euro 1(moja).

source nifahamishe

Mrembo Mwenye Matiti Makubwa Kuliko Wote Duniani Apigania Maisha Yake

Monday, July 19, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanamke mwenye matiti makubwa kuliko wanawake wote duniani ametakiwa achague moja matiti hayo yaondolewe ili aweze kuishi au la afariki akiwa na rekodi yake ya matiti makubwa kuliko wanawake wote duniani.
Sheyla Hershey alipata maambukizi kwenye matiti yake wakati akifanyiwa operesheni ya kuyaongeza matiti yake ambayo yana ukubwa wa 38KKK.

Mrembo huyo wa Brazili mwenye umri wa miaka 30 aliambiwa na madaktari kuwa kuna uwezekano wa asilimia 80 ataweza kuliokoa titi lake moja. Lakini mrembo huyo amesema kuwa ni bora matiti yote yaondolewe kuliko abaki na titi moja.

"Uwezekano wa kuyaokoa matiti yake yote mawili ni mdogo sana kati ya asilimia 10 na 20", alisema Sheyla.

Sheyla alikuwa anafanyiwa operesheni nchini Marekani ili kurekebisha matiti yake ambayo yalipata maambukizi alipofanyiwa operesheni nchini Brazili mwaka jana.

Hiyo ilikuwa operesheni yake ya 10 ya kurekebisha matiti yake tangu alipojifungua mtoto mwaka jana.

Madaktari wa Marekani walikataa kuongeza ukubwa wa matiti yake kwakuwa ni marufuku nchini Marekani kuweka zaidi ya lita 4.5 za silicone kwenye matiti.

Maambukizi aliyopata yalisababisha apate tabu kupumua.

"Niko kwenye maumivu makali ambayo najaribu kuyapunguza kwa kunywa madawa, maambukizi niliyopata ni sawa sawa na kansa", alisema Sheyla.

"Njia pekee ya kuondokana na maumivu haya ni kuyaondoa matiti haya", alisema Sheyla ambaye alikuwa akijivunia sana rekodi yake ya kuwa mwanamke mwenye matiti makubwa kuliko wanawake wote duniani.


source nifahamishe

Bibi Mwenye Miaka 108 Amrudia Mumewe wa Miaka 38

Monday, July 19, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Bibi wa nchini Malaysia mwenye umri wa miaka 108 amemrudia mumewe mwenye umri wa miaka 38 ambaye alitoka jela hivi karibuni kwa matumizi ya madawa ya kulevya.
Bibi Wook Kundor mwenye umri wa miaka 108 alivuma kwenye vyombo vya habari mwaka 2006 wakati alipofunga ndoa na kijana Muhammad Noor Che Musa ambaye sasa ana umri wa miaka 38.

Wapenzi hao walirudiana siku ya alhamisi baada ya Che Musa kuruhusiwa kutoka kwenye kituo cha kurekebisha tabia ambako alitumikia miezi 12 akipatiwa tiba ya matumizi ya madawa ya kulevya.

"Nimefurahi mume wangu amerudi, nimefurahi tumeonana tena kwakuwa bado nampenda sana", alisema bibi Wook akiliambia gazeti la Utusan Malaysia ambalo liliweka picha yake akimkumbatia mumewe kwenye ukurasa wake wa kwanza.

"Tutarudia maisha yetu ya kawaida kama zamani na nitaendelea kumpa huduma kama wanawake wengine wanavyowahudumia waume zao".

Che Musa alisema kuwa mke wake huyo alimtembelea mara tano alipokuwa kwenye kituo cha kurekebisha tabia.

Bibi Wook aliripotiwa na vyombo vya habari mwaka jana kuwa yupo tayari kuolewa mara ya 23 na mwanaume mwingine kwa kuhofia Che Musa atakapotoka kwenye kituo cha kurekebisha tabia akiwa ameacha madawa ya kulevya angetafuta mwanamke mwingine wa rika lake.

"Nimemmiss sana, najua nimefanya kosa na nimejutia kosa langu, bado nampenda sana mke wangu", alisema Che Musa.

sorce nifahamishe