Mtangazaji wa Iraq ambaye alitupwa jela baada ya kumrushia viatu vyake rais wa zamani wa Marekani George Bush wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari nchini humo, ametoka jela jana huku akiwa amepoteza meno mawili kutokana na mkong'oto aliokuwa akipewa jela.
Muntazer al-Zaid mtangazaji wa televisheni ya Iraq ambaye alimfanya rais wa zamani wa Marekani, George Bush apige mbizi mara mbili kuvikwepa viatu vyake namba 10 alivyomrushia wakati akiongea na waandishi wa habari, ametoka jela jana huku akilalamika kuwa aliteswa sana alipokuwa jela.
Zaid amesema kuwa mkong'oto aliokuwa akipewa jela ulipelekea meno yake mawili yang'oke.
Zaid amesema kuwa maafisa wa jela walikuwa wakimtesa kwa kumpa adhabu mbali mbali kama vile kumpiga shoti za umeme, kumchapa kwa kutumia nyaya za umeme na mabomba ya chuma na adhabu zingine mbali mbali za kumtesa.
"Hivi sasa nipo huru lakini nchi yangu haipo huru, mimi sio shujaa lakini nina uwezo wa kuelezea maoni yangu" alisema Zaid na kuongeza "Najihisi kunyanyasika ninapoiona nchi yangu ikitaabika, Baghdad ikichomwa moto na ndugu zangu wakiuliwa" alisema Zaid muda mfupi baada ya kutoka jela.
Zaid alilakiwa na mamia ya ndugu na marafiki zake ambao walimuandalia sherehe kubwa nyumbani kwake na kumchinjia kondoo kusherehekea kurudi kwake nyumbani.
Akiongea kwenye studio za mwajiri wake wa zamani, Zaid alimtaka waziri mkuu wa Iraq, Nouri al-Maliki amuombe radhi kwa adhabu alizopewa na pia alisema atawataja maafisa wa serikali na jeshi waliokuwa wakimtesa jela.
Maisha ya Zaid yamebadilika tangia alipotoka jela kwani bosi wake amemnunulia nyumba mpya kwa ujasiri wake aliouonyesha pamoja na kuifanya televisheni yao iwe maarufu duniani.
Zaid ameahidiwa na wafanyabiashara wa kiarabu magari ya kifahari pamoja na pesa huku wanawake wengi wa Baghdad na ukanda wa Gaza wametangaza kuwania kuolewa naye.
Wakati huo huo taarifa iliyotolewa na familia ya Zaid imesema kuwa Zaid ameondoka jana jioni nchini Iraq kwenda Syria kwa ndege binafsi ambako atakaa kidogo kabla ya kuelekea nchini Ugiriki kwa matibabu ya afya yake.
source.nifahamishe.com
Aliyemrushia Bush Viatu Atoka Jela Akiwa Hana Meno Mawili
Mtaalamu wa Mapenzi Atamba Kulala na Wanaume 1,500
Mwanamke huyu wa nchini Uingereza anayejiita mwenyewe Mtaalamu wa mambo ya mapenzi, amefanya mapenzi na wanaume zaidi ya 1,500 walioenda kwake kutafuta ushauri wa kimapenzi.
Katika wateja wake zaidi ya 10,000 walioenda kwake kutafuta ushauri wa kimapenzi katika kipindi cha miaka 23, mwanamke huyu anayejitamba kuwa yeye ndio mtaalamu wa masuala ya kitandani, amefanya mapenzi na wanaume 1,500 kati yao.
Mare Simone mwenye umri wa miaka 54 mkazi wa kitongoji cha Chelsea, jijini London amejiajiri mwenyewe na ana ofisi yake jijini humo akitoa ushauri wa mambo ya kimapenzi kwa wanawake na wanaume.
Baada ya kuachana na mumewe, Mare aliamua kuisomea rasmi taaluma hiyo ya mapenzi na kisha kufungua ofisi yake ambapo hadi sasa ametoa somo la mapenzi kwa zaidi ya wateja 10,000 waliofika kwenye ofisi yake katika kipindi cha miaka 23.
Mare amesema kuwa hadi sasa ameishafanya mapenzi na wanaume zaidi ya 1,500 katika wateja wake ambao miongoni mwao ni waume au wapenzi wa wanawake wengine.
Mare anasema kuwa hafikirii hata kidogo kuwa anafanya kosa lolote kinyume cha sheria kutembea na waume za watu.
"Najipatia kipato changu kwa kulala na waume au wapenzi wa wanawake wengine. Lakini mimi sifanyi ukahaba kwakuwa taaluma ya mapenzi inaruhusiwa kisheria na mapenzi yanafanyika katika mazingira ya tiba" alisema Mare.
"Watu wananilipa kwa ushauri ninaowalipa na kwa kutibu matatizo yao hawanilipi kwasababu ya ngono".
"Nasaidia kuimarisha na kubadilisha maisha ya kimapenzi ya maelfu ya wanaume na hivyo nakuwa nimesaidia kuimarisha maisha ya kimapenzi ya wake zao au wapenzi wao"
"Wanawake wengine wanabeba mimba za wanawake wengine kwasababu wanataka kuwasaidia wanawake wasio na uwezo wa kupata mimba. Hali hiyo ni sawa na mimi kwani nawasaidia watu kuwa na maisha mazuri ya kimapenzi".
Mare alielezea kuifurahia kazi yake na huwa na furaha zaidi wateja wake wanapoondoka kurudi majumbani mwao wakiwa na matumaini mapya kwenye maisha yao ya kimapenzi.
Mare kwa siku anatoa vipindi vitano vya masuala ya mapenzi na anasema wateja wake ni watu wa rika mbali mbali. "Wateja wangu ni watu wa rika zote, jinsia zote, maumbile tofauti na wafanyakazi wa vitengo tofauti tofauti".
"Wanaume mara nyingi hunifuata kwa sababu ya matatizo ya kutosimama vyema kwa uume na kufika kileleni mapema kabla ya wapenzi wao wakati wengine huambiwa waje wanione na wake zao kwakuwa hawawaridhishi kitandani".
"Kabla hawajaniona huwa wote wanapimwa magonjwa ya zinaa na lazima watumie kondomu iwapo nitalala nao" alisema Mare.
"Kwa wanawake mara nyingi hunifuata wakiwa na matatizo ya kutofika kileleni au wanapoona wapenzi wao hawajui jinsi ya kuwaridhisha kitandani".
"Huwa nawafundisha jinsi ya kujipa raha wao wenyewe na kuipenda miili yao" alimalizia Mare.
source.nifahmishe.com
Bibi mwenye umri wa miaka 107 wa nchini Malaysia ambaye alishaolewa na kuachika mara 21 amesema yuko tayari kuolewa na mwanaume mwingine kwa mara ya 23 kwasababu anahofia kuwa mume wake wa 22 anayeishi naye hivi sasa anaweza kumkimbia na kutafuta mwanamke mwingine mwenye umri mdogo.
Baada ya kuolewa na wanaume 21 na kuachika, bibi mwenye umri wa miaka 107 wa nchini Malaysia amesema kuwa anahofia kukimbiwa na mume wake wa 22 anayeishi naye hivi sasa ambaye miezi miwili iliyopita alikamatwa akitumia madawa ya kulevya.
Bibi Wook Kundor alipata umaarufu duniani baada ya kuolewa kwa mara ya 22 na mwanaume ambaye amemzidi jumla ya miaka 70.
Hivi sasa bibi Wook hana imani kabisa na mumewe Muhammad Noor Che Musa mwenye umri wa miaka 37 ambaye hivi sasa yuko kwenye kituo cha kurekebisha tabia akipatiwa matibabu ya kuacha utumiaji wa madawa ya kulevya.
Bibi Wook ameishaanza kusaka mume wa 23 kwani anahofia Muhammad akishatoka kwenye kituo hicho na kuacha tabia yake ya kutumia madawa ya kulevya anaweza kumkimbia na kutafuta mwanamke mwingine wa rika lake.
"Katika siku za hivi karibuni kuna hofu imeniingia" alisema bibi Wook huku akiwa ameshikilia picha yake.
"Najua kwamba mimi ni mwanamke niliyezeeka. Sina umbile la kuvutia tena na kwa umri wangu siwezi kumvutia mwanaume yoyote"
"Nia yangu ya kuolewa tena ni kuepuka upweke na si kwa sababu yoyote ile" alisema Wook na kuongeza kuwa anajihisi mpweke sana wakati huu ambao mumewe yuko mbali.
Bibi Wook alisema kuwa angependa kusherehekea sikukuu ya Eid el-Fitr wiki ijayo akiwa pamoja na mumewe.
Wook alisema kuwa ana mpango wa kumtembelea Muhammad kwenye kituo chake cha kurekebisha tabia jijini Kuala Lampur iwapo majirani zake watampeleka huko kwa gari.
Muhhamad alifunga ndoa na bibi Wook miaka mitatu iliyopita akisema kuwa urafiki wa karibu na heshima uligeuka kuwa mapenzi ya kweli.
source nifahamishe.com
Zaidi ya waombelezaji 150 katika msiba mmoja nchini Zambia, wamelazwa hospitali baada ya kula chakula kinachohisiwa kuwa na sumu.
Waombelezaji 153 katika msiba mmoja nchini Zambia waliwahishwa hospitali wakiwa hoi taabani baada ya kula chakula kwenye msiba kinachohisiwa kuwa na sumu.
Afisa mmoja wa wizara ya afya wa Zambia alisema kuwa waombelezaji hao walikula ugali wa unga wa mahindi unaoitwa "Nshima" na kunywa pombe ya mahindi inayoitwa "Munkoyo".
Tukio hilo lilitokea kwenye mji wa Luanshya uliopo kilomita 250 toka mji mkuu wa Zambia Lusaka na jumla ya waombelezaji 153 waliwahishwa hospitalini siku ya jumamosi na kulazwa kutokana na sumu iliyokuwemo kwenye vyakula hivyo.
Wagonjwa hao waliwahishwa kwenye hospitali mbili za jirani na wengi wao walilazwa kwenye sakafu za hospitali hizo kutokana na upungufu wa vitanda, taarifa iliyotolewa na shirika la habari la Zambia (ZANIS) ilisema.
"ZANIS ilipotembelea hospitali zote mbili ilikuta wagonjwa wakiwa wamelazwa chini wakiwa wamewekewa dripu na walikuwa wakilalamika kuharisha, kutapika na kuhisi kizunguzungu".
Msemaji wa wizara ya afya, Reuben Mbewe alisema kuwa chakula walichokula inahisiwa kilikuwa na sumu.
"Inabidi tusubiri kukamilika kwa uchunguzi" alisema msemaji huyo wa wizara ya afya.
source.nifahamishe.com
Bi Harusi Mtarajiwa Atoweka Kabla ya Harusi, Maiti yake Yakutwa Ndani ya Ukuta
Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Yale cha nchini Marekani ambaye alikuwa aolewe jana alitoweka siku chache zilizopita kabla ya harusi yake na maiti yake imekutwa jana ikiwa ndani ya ukuta wa chuo hicho.
Mwili wa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Yale University, Annie Le mwenye umri wa miaka 24, ambaye alitoweka siku chache kabla ya harusi yake umepatikana ukiwa umefichwa ndani ya ukuta wa maabara ya chuo chake.
Mwili wake ulikutwa ndani ya ukuta ambao ndani yake kuna uwazi na nyaya za umeme na mabomba ya maji yanapita toka ghorofa moja kwenda nyingine.
Annie Le alikuwa ametoweka kwa zaidi ya siku sita kabla ya polisi kuanza msako mkali wa kumtafuta.
Awali ilidhaniwa kuwa Le alitoweka ili kukwepa kufunga ndoa na mchumba wake.
Lee alionekana siku ya jumanne asubuhi akiingia kwenye jengo la ghorofa tano ambalo ndani yake kulikuwa na maabara ambayo alikuwa akifanya kazi huku akisoma.
Kutoweka kwake kuliwashangaza polisi kwani video kamera za ulinzi zilionyesha jinsi alivyokuwa akiingia kwenye jengo hilo kwenye majira ya saa nne asubuhi lakini kulikuwa hakuna kamera iliyomuonyesha wakati akitoka pamoja na kwamba kulikuwa na jumla ya video kamera za ulinzi 75 zinazolinda eneo hilo.
Zaidi ya polisi 100 na wapelelezi walikuwa wakilifanyia uchunguzi jengo hilo kwa siku kadhaa kuitafuta maiti yake kabla ya jana kufanikiwa kuiona.
Taarifa zilisema kwamba, mwanzoni mwa mwaka huu Le aliandika makala kuhusiana na usalama katika kampasi ya chuo hicho.
Makala yake ilichapishwa kwenye jarida la chuo hicho mwezi februari ikiwa na kichwa cha habari kinachosema "Crime and Safety in New Haven".
Le na mchumba wake Jonathan Widawsky aliyehitimu shahada ya kwanza katika chuo kikuu cha Columbia University walikuwa wafunge ndoa jana jijini New York.
Awali polisi walisema kuwa Widawsky si miongoni mwa watu wanaoshukiwa kufanya mauaji hayo na alikuwa akishirikiana vyema na polisi.
Polisi hawajasema kama kuna mshukiwa yeyote wa mauaji hayo aliyepatikana hadi sasa.
source.nifahamishe.com
Hauwezi Kuolewa Kwasababu Huna Akili, Hujui Maana ya Ndoa
Yalikuwa yamebaki masaa 48 kabla ya harusi kufungwa na sherehe kubwa za harusi kuanza, wakati bibi harusi ambaye alikuwa tayari ni mjamzito alipoambiwa kuwa wewe huwezi kuolewa kwasababu huna akili hujui nini maana ya ndoa.
Kerry Robertson, ambaye ana kichwa kigumu kuelewa, mkazi wa Fife, Scotland aliambiwa kuwa harusi yake imefutwa masaa 48 kabla ya kuvaa shela lake la harusi kufunga ndoa na mchumba wake Mark McDougall.
Kerry mwenye umri wa miaka 17 alikuwa ameishanunua gauni lake la harusi, yeye na mchumba wake walikuwa wameishanunua pete za harusi na sherehe kubwa baada ya kufungishwa ndoa kanisani ilikuwa imeandaliwa kufanyika jumamosi iliyopita.
Lakini siku mbili kabla ya harusi, maafisa wa ustawi wa jamii walimwambia bibi harusi kuwa harusi yao imefutwa kwasababu "haelewi chochote kuhusiana na maisha ya ndoa".
Kerry ambaye ana ujauzito wa miezi mitano alitoa malalamiko yake jana akisema kuwa uamuzi uliotolewa wa kuifutilia mbali harusi yake ni wa kikatili.
"Bado nina huzuni sana, najua ndoa nini. Ni wapenzi wawili kuamua kutumia maisha yao yote wakiishi pamoja. Nampenda Mark na nataka kuwa mke wake" alisema Kerry.
Kerry alikuwa akilelewa na bibi yake tangia alipokuwa na umri wa miaka 9 baada ya wazazi wake kushindwa kumtunza vyema, na gharama zote za matunzo yake zilikuwa zikitolewa na ofisi ya ustawi wa jamii.
Mwezi januari mwaka huu, Kerry alikutana na McDougall mwenye umri wa miaka 25 na kuanza uhusiano wa kimapenzi. Kerry alipopata mimba waliamua kufunga ndoa.
McDougall alisema kuwa balaa hilo lilianza alhamisi iliyopita wakati maafisa wawili wa ustawi wa jamii walipofika kwenye nyumba yao waliyokuwa wakiishi pamoja na kuwaambia kuwa ndoa yao ni kinyume cha sheria kwakuwa Kerry ana upungufu wa akili na hana uwezo wa kujiamulia mambo mwenyewe.
"Kerry aliangua kilio hapo hapo". "Pamoja na kujibishana nao sana tukiwaambia kuwa tunapendana na tusingependa mtoto wetu azaliwe wazazi wake tukiwa hatujaoana, hawakutaka kutuelewa na walishikilia uamuzi wao huo", alisema McDougall.
Kwa mujibu wa sheria za Scotland, afisa wa serikali anayefungisha ndoa, anaweza kuivunja harusi kama ataona kuwa mmoja wa maharusi au wote wawili wana upungufu wa akili na hawajui chochote kuhusiana na ndoa.
source.nifahamishe.com
Mtoto Mapacha Azaliwa bila Kichwa Afghanistan
Mwanamke mmoja wa nchini Afghanistan amejifungua watoto wawili mapacha walioungana kwenye kifua huku pacha mmoja akiwa hana kichwa.
Mwanamama mmoja wa nchini Afghanistan amejifungua watoto wawili mapacha wa kiume walioungana kwenye sehemu za kifua pekee huku pacha mmoja wapo akiwa hana kichwa.
Pacha ambaye hana kichwa alizaliwa akiwa amekamilika viungo vyote vingine vya binadamu kasoro kichwa tu.
Alikuwa na kiwiliwili cha juu, mikono, miguu na viungo vingine isipokuwa kichwa pekee ndicho kilichokosekana.
Mapacha hao walizaliwa siku ya alhamisi katika hospitali moja kaskazini mwa Afghanistan.
"Kwa siku chache za mwanzo pacha ambaye hakuwa na kichwa alikuwa hai na alikuwa akiisogeza sogeza mikono na miguu yake, lakini hivi sasa amefariki" alisema Dr Homayoun Khamoosh wa hospitali ya mji wa Kunduz walikozaliwa mapacha hao.
"Hii ni mara ya kwanza tunaona mapacha kama hawa kwenye mji huu wa Kunduz" alisema Dr Homayoun.
Dr Khamoosh alisema kuwa mapacha hao wanahitaji kufanyiwa operesheni ya kuwatenganisha haraka iwezekanvyo ili kuokoa maisha ya pacha aliyezaliwa akiwa amekamilika viungo vyote.
"Madaktari wameamua kufanya operesheni ya kuwatenganisha mapema kabla ya mwili wa pacha ambaye hana kichwa aliyefariki haujaanza kuharibika", alidokeza Dr Khamoosh.
Mama wa mapacha hao mwenye umri wa miaka 35 ambaye ana watoto wengine wanne, alijaribu kuficha sura yake kwa waandishi wa habari na alikataa kutaja jina lake.
source.nifahamishe.com
MFANYABIASHARA maarufu na mdau mkubwa wa michezo na burudani nchini, Mohamed Mpakanjia amefariki dunia jana katika hospitali ya jeshi la Lugalo jijini Dar es Salaam ambako mkewe wa zamani Amina Chifupa alifariki.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana katika hospitali hiyo ambayo pia alifikia aliyekuwa mkewe Amina Chifupa, Mpakanjia alifariki dunia katika hospitali hiyo majira ya saa saba mchana.
Chanzo chetu cha habari kilichopo katika hospitali hiyo kilisema kuwa mfanyabiashara huyo alifikishwa hopitalini hapo jumamosi iliyopita kutokana na kusumbuliwa na homa ya mapafu.
"Aliletwa hospitalini hapa jumamosi akisumbuliwa na matatizo ya homa ya mapafu. Wakati analetwa alionekana mwenye afya njema lakini hali yake ilibadilika ghafla leo na mauti kumfika," kilisema chanzo hicho cha habari.
Katika uhai wake Mpakanjia alikuwa ni miongoni mwa watu waliotoa mchango mkubwa katika maendeleo ya michezo na burudani hasa kutokana na kusaidia wasanii, wanamuziki na bendi nyingi za muziki hapa nchini.
Alikuwa mfadhili mkuu wa bendi ya DDC Mlimani Park 'Sikinde', Tanzania One Theater 'TOT Plus'.
Pia alidhamini albamu za pamoja za wanamuziki Ramadhani Masanja 'Banza Stone', Ally Choki na kiongozi wa Msondo iitwayo 'Sisi ndiyo Sisi' ya mwaka 2005.
Kwa upande wa sanaa alitoa mchango mkubwa kwa kuwasaidia wasanii wengi wa sanaa ya filamu na maigizo kwa kuwawezesha kifedha kukamilisha kazi zao hizo.
Mungu ailaze roho yake pema peponi.
source.nifahamishe.com
Ukimwona ni mrembo sana na anavutia kwa wanaume wengi lakini aliamua kuacha wanaume wote wa umri wake na kuanza kazi ya kumsaka mtoto wake wa kiume ambaye alimgawa kwa familia nyingine imlee muda mfupi baada ya kumzaa.
Aimee Louise Sword 35, mkazi wa Michigan nchini Marekani alitumia internet kumtafuta mtoto wake huyo ambaye hakuwa na mawasiliano naye kwa zaidi ya miaka 10 tangia alipomgawa kwa familia hiyo.
Hatimaye kwa kutumia internet Aimee alifanikiwa kujua mtoto wake alipo na baada ya kukutana naye alianza uhusiano naye wa kimapenzi.
Waendesha mashtaka walisema kuwa mtoto wake ambaye jina lake halikutajwa kwasababu za kisheria na umri wake kuwa mdogo, alikuwa hajui kuwa mwanamke anayefanya mapenzi ni mama yake mzazi.
Msako wa kumtafuta Aimee ulianza baada ya polisi kupewa taarifa za uhusiano huo wa mama huyo na mwanae.
Aimee alikamatwa na kufunguliwa mashtaka matatu ya jinai baada ya kujisalimisha mwenyewe kwenye kituo cha polisi kufuatia polisi kupewa waranti tatu za kumkamata.
Aimee alikanusha mashtaka aliyofunguliwa na yuko nje kwa dhamana.
by nifahamishe.com