Mtoto Mnene Kuliko Wote Duniani

Friday, August 20, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Ana umri wa miezi 10 lakini mtoto huyu wa nchini China ana uzito zaidi ya mtoto wa miaka sita.
Mtoto wa miezi 10 wa nchini China anayeitwa Lei Lei huenda akawa ndio mtoto mnene kuliko watoto wote duniani.

Lei Lei pamoja na umri wake huo mdogo ana uzito wa kilo 20 ambao kawaida ni uzito wa mtoto kuanzia umri wa miaka sita.

Lei Lei alizaliwa akiwa na uzito wa kawaida kama watoto wengine.

Lakini mbali ya maziwa ya mama yake, Lei Lei alikuwa akibugia kila kitu kilichokuwa mbele yake,

Lei Lei ambaye anaishi na wazazi wake kwenye jimbo la Hunan, amebatizwa jina la "Mtoto wa Michelin" na majirani zake.

Lei Lei amelazwa kwenye hospitali moja mjini humo akifanyiwa uchunguzi na madaktari ili kujua sababu ya unene wake.

source nifahamishe

Miaka 25 Jela Kwa Kuiba Chakula Kanisani

Friday, August 20, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanaume mmoja wa nchini Marekani ambaye alihukumiwa kwenda jela miaka 25 baada ya kujaribu kuiba chakula kanisani, ametoka jela jana baada ya kutumikia miaka 13 jela.
Gregory Taylor, alijaribu kuganga njaa yake kwa kuzamia kwenye jiko la kanisa kwa nia ya kuiba chakula, kitendo chake hicho kiliyafanya maisha yake yaende mrama.

Taylor alikamatwa ndani ya jiko la kanisa na kufunguliwa mashtaka ya wizi ambapo alihukumiwa kwenda jela miaka 25.

Baada ya kutumikia miaka 13 jela, Taylor ameachiwa huru jana baada ya mahakama kuona kuwa adhabu aliyopewa ilikuwa kubwa sana kuliko kosa lenyewe.

Taylor alitupwa jela mwaka 1997 baada ya hakimu wa California kuitumia sheria inayosema kuwa mtuhumiwa anayekamatwa baada ya kufanya uhalifu mara tatu basi atupwe jela kuanzia miaka 25.

Kabla ya tukio la kujaribu kuiba chakula kanisani, Taylor alikuwa akikabiliwa na tuhuma za makosa mawili ya wizi, kosa la kwanza lilikuwa ni kumchomolea mtu pochi lake na kosa la pili lilikuwa ni kujaribu kumpora mtu mali zake.

Taylor alitoka kwenye jela ya wanaume ya mjini Los Angeles jana asubuhi na kulakiwa na ndugu na marafiki.

Taylor aliwaambia waandishi wa habari kuwa sasa amebadilika na anamshukuru mungu kwa kumpa chansi ya pili.

Alisema kuwa ana mpango wa kufanya kazi kwenye mgahawa wa kaka yake ili aweze kuwasaidia watu wengine wanaotafuta chansi ya pili katika maisha.


source nifahamishe

Afariki Baada ya Kulipukiwa na Simu ya Nokia

Thursday, August 19, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanaume mmoja nchini India amefariki dunia baada ya simu yake aina ya Nokia kumlipukia wakati akiwasiliana na mtu mwingine kwa kutumia simu hiyo.
Mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina la Gopal Gujjar, mwenye umri wa miaka 23, alifariki dunia baada ya kupata majeraha makubwa shingoni, mabegani na masikioni.

Taarifa zinasema kuwa Gujjar mkazi wa jimbo la Rajasthan nchini India alikuwa akiwasiliana na mtu mwingine kwa kutumia simu yake aina ya Nokia wakati mlipuko mkubwa ulipotokea.

Mwili wake ulikutwa pembeni ya mabaki ya simu yake kwenye shamba lake lililopo kwenye kijiji cha Banda, limeripoti gazeti la The Times of India.

Polisi walithibitisha kupatikana kwa mabaki ya simu aina ya Nokia 1209 ya mwaka 2008.

Gazeti la The Times of India limesema kuwa tukio hili huenda likawa tukio la kwanza nchini humo kwa mtu kulipukiwa na simu ambayo haipo kwenye umeme ikichajiwa.

Mwezi januari mwaka huu, mwanamke mmoja nchini India mwenye umri wa miaka 27 alifariki dunia baada ya kulipukiwa na simu iliyotengenezwa China wakati akiongea huku akiichaji simu hiyo kwenye umeme.

Vifo vya watu kulipukiwa na simu vimekuwa vikiripotiwa mara nyingi nchini China, Korea Kusini na Nepal.

source nifahamishe

Amuuza Binti Yake Ili Apate Pesa za Pombe

Wednesday, August 18, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanaume mmoja nchini India, anashikiliwa na polisi baada ya kumuuza binti yake mwenye umri wa miaka sita ili aweze kupata pesa za kununulia pombe.
Mwanaume huyo chapombe mwenye umri wa miaka 40 aliyetajwa kwa jina la Krishnaiah, alimuuza binti yake mwenye umri wa miaka sita ili aweze kupata pesa za kununulia pombe.

kwa mujibu wa gazeti la The Times la India, Krishnaiah alikuwa na kiu ya pombe kali lakini alipoenda kwenye duka la jirani ambalo hununua pombe siku zote, alitolewa nduki kwakuwa alikuwa akidaiwa pesa na mwenye duka.

Ili aweze kukata kiu yake ya pombe, Krishnaiah aliamua kumuuza binti yake mtaani kwa bei ya kuanzia rupia 300 ambazo ni sawa na Tsh. 8000.

Hatimaye alifanikiwa kumuuza binti yake kwa rupia 1,000 ( Tsh. 28,000).

Polisi walipewa taarifa na walifanikiwa kumuokoa binti huyo aliyeuzwa na baba yake kabla ya mnunuzi hajatoweka naye.

Katika tukio hilo lililotokea katika jimbo la Kadapa, Krishnaiah alikamatwa na kutupwa rumande.

Mnunuzi wa binti yake alifanikiwa kukimbia kabla hajatiwa mikononi mwa polisi

source nifahamishe

Atakayemuonyesha Obama Matiti Yake Kulipwa Dola Milioni 1

Wednesday, August 18, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Bilionea mmoja wa nchini Marekani ameahidi kutoa zawadi ya dola milioni moja kwa mwanamke yoyote atakayejitokeza mbele ya rais wa Marekani, Barack Obama na kisha kumuonyesha matiti yake.
Bilionea Alki David ili kuitangaza tovuti yake ya "Battlecam" ameahidi donge nono la dola milioni 1 kwa mwanamke yoyote atakayekuwa wa kwanza kujitokeza mbele ya rais Obama na kisha kumuonyesha matiti yake huku akiwa amebandika lebo ya "Battlecam" kwenye kifua chake.

Sharti ya kushinda donge hilo nono ni kwamba tukio hilo lazima lionyeshwe LIVE kwenye tovuti ya Battlecam inayomilikiwa na bilionea huyo.

Awali bilionea huyo aliahidi kutoa zawadi ya dola laki moja lakini ameamua kuiongeza zawadi hiyo iwe dola milioni 1 baada ya watu kuona dola laki moja si donge nono.

"Watu wengi wanafikiria dola 100,000 hazitoshi kumfanya mtu azionyeshe sehemu zake nyeti kwenye hadhara, lakini dola milioni 1 ni pesa za kutosha kabisa", alisema bilionea Alki.

Alki alisema kwamba hadi sasa jumla ya watu 150 wameishajiandikisha kuwania zawadi hiyo.

Bilionea huyo alidai kuwa ameamua kumchagua Obama kwakuwa Obama ndiye kiongozi mkubwa wa dunia.

Bilionea Alki alizaliwa Lagos, Nigeria lakini anaishi Los Angeles, Marekani.

Ana nyumba tatu za kifahari nchini Uingereza na alitajwa kushika nafasi ya 45 katika listi ya matajiri waliopo Uingereza kwa mujibu wa gazeti la The Times la Uingereza.

source nifahamishe