10 Wafariki Katika Maandamano ya Kuchomwa Kwa Quran

Sunday, April 03, 2011 / Posted by ishak / comments (0)


Saturday, April 02, 2011 6:37 PM
Wafanyakazi 10 wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan wamefariki dunia kufuatia mashambulizi toka kwa maelfu ya watu waliokuwa wakiandamana kupinga kitendo cha mchungaji wa kanisa moja la nchini Marekani kuichoma Quran.
Wafanyakazi 10 wa ofisi ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa katika mji wa Mazar-i-Sharif nchini Afghanistan, wameuliwa na waandamanaji waliokuwa wakipinga kitendo cha mchungaji wa kanisa moja la nchini Marekani kuichoma moto Quran.

Waandamanaji waliandamana jana katika miji ya Mazar-i-Sharif na mji mkuu wa Afghanistan kupinga kitendo cha mchungaji Wayne Sapp wa kanisa la Florida nchini Marekani kukichoma moto kitabu kitukufu cha waislamu, Quran.

"Watu 10 wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wameuliwa na waandamanaji, wote waliouliwa walikuwa ni raia wa kigeni", alisema msemaji wa polisi wa Afghanistan, Lal Mohammad Ahmadzai.

Mchungaji Sapp aliichoma moto Quran tarehe 21 mwezi uliopita chini ya usimamizi wa mchungaji Terry Jones, ambaye alisababisha mtafaruku mkubwa sana mwaka jana alipotishia kuichoma moto misahafu.

Aliahirisha uamuzi wake huo baada ya serikali ya Marekani na viongozi wa kimataifa kumuonya kuwa kitendo hicho kitahatarisha maisha ya Wamarekani duniani.


source nifahamishe