OBAMA akutana na wakuu wa usalama wake

Wednesday, January 06, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya mkutano huo, Rais Obama amesema vyombo vya usalama nchini humo vinatambua vitisho vilivyopo vya usalama.

Wakosoaji wamekuwa wakijadili kwamba njama za kufanya mashambulio wakati wa Krismas, zimeonesha udhaifu katika mfumo wa upelelezi nchini humo, ambao ungepaswa kushughulikiwa bada ya kutokea kwa shambulio la kigaidi la Septemba 11 mwaka 2001 nchini humo.

Wakati huohuo, Ikulu ya Marekani imesema nchi hiyo itasimamisha kuwahamisha wafungwa wengine zaidi kutoka katika gereza la Guantanamo kwenda Yemen.
Rais Obama pia amesisitiza nia yake ya kulifunga gereza hilo la Guantanamo.

aliempiga aisha picha asakwa

Wednesday, January 06, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Imeelezwa na vyanzo vyetu kuwa Khumalo, aliye raia wa Afrika Kusini, ndiye anayetuhumiwa kumpeleka Aisha nchini humo ambako alimlaghai na kumpiga picha chafu kabla ya kurudi Bongo kuzisambaza.

Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka aliliambia gazeti hili kuwa picha hizo za Aisha ambaye ni mwajiriwa wake kwenye Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’, zimemfedhehesha na zimemuudhi.
Alisema, tayari analo jibu kamili la mtu aliyehusika na mchezo mzima, hivyo akaahidi kumfikisha kwenye vyombo vya sheria kabla ya kumuweka ‘ubayani’ kwa kitendo alichofanya.

Asha alisema kuwa kitendo cha Aisha kupigwa picha chafu siyo tu kwamba ni aibu, bali kimeichafua bendi yake kwa sababu ndiyo ambayo mnenguaji huyo anaifanyia kazi.
Aliendelea kusema, Khumalo ni mpenzi wa Aisha na alimpiga picha hizo wakiwa faragha, hivyo haikuwa sahihi kwa raia huyo wa Sauz, kuzisambaza kwa sababu yoyote ile.

“Mimi sijafurahishwa hata kidogo kwa maana ni kitendo cha udhalilishaji, isitoshe huyo ni bwana wake ambaye wapo naye muda mrefu, na ndiye aliyemshawishi kwenda hata huko Afrika Kusini,” alisema Asha a.k.a Iron Lady na kuongeza:
“Nilikuwa naongea sana na huyo Steven Khumalo, hata hapa nina ‘meseji’ zake kwenye simu yangu, na kama sababu ni dawa za kulevya, basi angempiga hizo halafu akazileta ofisini kwangu nimshughulikie kuliko kumpiga za utupu na kusambaza gazetini.”

Asha aliendelea: “Naongea kwa uchungu kama mlezi wa Aisha, pia kama mkurugenzi wake, nitahakikisha Steven namfungulia mashtaka na anakamatwa, asifikiri kwa sababu yeye ni mgeni ndiyo hatuwezi kumkamata.”
Meneja wa Twanga Pepeta, Abuu Semhando alisema kuwa Steven si mtu mwema kwa sababu ndiye aliyemshawishi Aisha kwenda Afrika Kusini ambako amemgeuka na kumpiga picha chafu ambazo amekuja kuzisambaza Bongo.

“Huyo Steven angetuambia sisi kuwa Aisha anavuta bangi nasi tungejua jinsi ya kumsaidia, kuliko alichokifanya kwa sababu kimetudhalilisha,” alisema Abuu a.k.a Baba Diana.
Mnenguaji mwenye jina kubwa Bongo, Lillian Tungaraza ‘Internet’, aliliambia Risasi Mchanganyiko juzi kuwa tangu alipoziona picha za Aisha, ufanisi wake umepungua kutokana na kukosa msisimko wa kazi.

Internet ambaye mashabiki humtambua kama mpinzani halisi wa Aisha jukwaani, alisema kuwa kinachomuumiza zaidi ni kuona kwamba aliyemfanyia hivyo mwenzake ni ‘bwana’ke’ wa muda mrefu.
“Sisi tulijua anakwenda kufanya kazi lakini kumbe amekwenda kumdhalilisha. Mimi naamini hizo dawa alimlisha ili aweze kumnyanyasa na kumdhalilisha,” alisema Lillian Internet.

Gazeti hili lilipompata Khumalo, alisema, anajua kuwa anasakwa na mtu anayemtafuta kwa udi na uvumba ni Asha Baraka, hivyo akasisitiza kwamba haogopi na hakuna wa kumbabaisha.
“Najua Asha Baraka ndiye anayepika kila kitu lakini mimi sibabaishwi. Hizo picha sikupiga mimi, mwenyewe nimeletewa na marafiki zangu ili kunionesha kuwa mchumba wangu hafai.

“Zimeunganishwa tofauti tofauti, sijapiga picha mimi. Kwanza mimi ndiye napaswa kulaumu kuwa nimedhalilishwa, mtu ambaye nilitarajia ningefunga naye ndoa kumbe ni mchafu kiasi hiki,” alisema Khumalo.
Aliendelea kusema: “Hivi sasa simtaki tena Aisha, nimemwambia mama ampe nauli ili arudi huku Bongo, sitaki aendelee kuwepo kule kwa sababu alikuwepo kwa sababu yangu na sasa simtaki aondoke.”

Wakati tunaelekea mtamboni, kuna habari kuwa polisi wamekwishaanza kazi ya kumsaka Khumalo, ingawa halijaelezwa aliyeshtaki ni nani.

source.globulpubliks

Jengo Refu Kuliko Yote Duniani lafunguliwa Rasmi Dubai

Wednesday, January 06, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Jengo refu kuliko yote duniani lililopo Dubai ambalo limeenda angani mita 828 toka ardhini linalojulikana kama Burj Khalifa limefunguliwa rasmi kwa sherehe kubwa iliyorushwa LIVE na televisheni nyingi sana duniani.
Jengo hilo ambalo awali lilikuwa likijulikana kama Burj Dubai kabla ya Dubai kupewa msaada wa kifedha na Abu Dhabi baada ya kuingia kwenye madeni, lilifunguliwa kwa sherehe iliyoambatana na shoo ya fataki mbali mbali.

Jengo hilo lilibadilishwa jina na kuitwa Burj Khalifa ili kumuenzi kiongozi wa Abu Dhabi aliyeipa msaada Dubai wa dola bilioni 10.

Jengo hilo lina urefu wa mita 828 na lina ghorofa 160 ambazo ni nyingi sana kulinganisha na jengo lililokuwa likijulikana awali kama ndilo refu kuliko yote duniani la Taipei lenye ghorofa 101.

Ghorofa hilo ambalo ujenzi wake ulianza mwaka 2004, mbali ya kuwa jengo refu kuliko yote duniani ndilo pia jengo lenye lifti ndefu kuliko zote duniani.

Jengo hilo pia lina msikiti ulio juu kuliko yote duniani kwenye ghorofa ya 158 na lina bwawa kubwa la kuogelea lililo juu kuliko yote duniani kwenye ghorofa ya 76.


source.nifahamishe

Kakobe na Waumini Wake Wakesha Kulinda Tanesco Wasipitishe Umeme

Wednesday, January 06, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Askofu Mkuu wa kanisa la Full Gospel Bible fellowship lililopo Mwenge jijini Dar es salaam na wauminini wake wameweka kambi nje ya kanisa hilo ili kuishinikiza Tanesco wasipitishe umeme mkubwa karibu na kanisa lao.
Kakobe na waumini wa kanisa lake wameweka kambi kwa muda usiojulikana wakiwa wamevalia sare ya tisheti zenye maneno ya kuibeza Tanesco na Serikali yenye ujumbe unaosomeka kwa mbele "Tanesco mwogopeni Mungu" na nyuma "Baada ya richmond mmegeukia kanisa!!".

Askofu mkuu wa kanisa hilo Zacharia Kakobe amesema kuwa endapo umeme huo utapitishwa pale jamii itarajie mpambano baina yao na Tanesco.

Kakobe aliwataka Tanesco kwenda kujifunza kwake masuala ya umeme kwani amesoma kuliko wao na watarajie kupata upinzani mkubwa kutoka kwa waumini hao wenye uelewa mkubwa wa athari ya ememe huo.

Alisema kinachofanya waumini hao kukesha hapo kwa muda wote ni kutokana na kutojua ni muda gani nyaya hizo zitapitishwa eneo hilo, hivyo wameona bora waendelee kuwepo kwa muda wote ili kuhakikisha hazipitishwi.

"Huu ni ufisadi unaofanyika hapa,na tutakuwa hapa mpaka kieleweke hata kama ni mwaka mzima kwani huu umeme chuo kikuu waliukataa kutokana na madhara yake hivyo sisi hatuutaki pia na tutapambana" alisema Askofu Kakobe.

Aidha alisema kuwa ujumbe katika tisheti hizo utakuwa unabadilika kulingana na matukio yatakayokuwepo kwani hawatojali gharama kwani uhuru ni gharama kubwa kuliko fedha zinazotumika kutengeneza tisheti hizo.

Aidha Askofu Kakobe aliilaumu Serikali kwa kusema kuwa imekuwa na upendeleo kwa misikiti katika operesheni zake tofauti na inavyofanyika katika makanisa ya kiroho.

"Serikali inapendelea misikiti zaidi kuliko kanisa,mfano Tabata dampo katika uvunjaji wa nyumba msikiti haukuguswa na zinatumika gharama kubwa na ushirikishwaji unakuwepo" alisema Kakobe.

Pia Kokobe aliendelea kusema kuwa hayo yanayofanyika hapo Serikali haiwezi wala kuthubutu kuyafanya katika makanisa mengine hasa kwa Kardinal Pengo.

"Huu ni ujinga mtupu,na kama angekuwa Kardinal Pengo asingethubutu kuuruhusu kufanyika kwake kamwe" alisema.

Alibainisha kuwa ni juzi tu Serikali imemuita yeye kuwa ni kichuguu tu hivyo anataka kuwadhihirishia kuwa hawawezi kumkanyaga vile wapendavyo na wasitarajie hilo kutokea kamwe.

Baadhi ya waumini waliokuwepo kanisani hapo wamesema kuwa wanaungana na Askofu wao ili kuhakikisha nyaya hizo hazipitishwi eneo hilo na watakuwepo kwa muda wote.

"Tupo tayari hata kuzolewa na tinga tinga lakini hawapitishi nyaya hizo hapa na tutakuwepo kwa masaa 24 na tutahakikisha hilo linatekelezeka" walisema waumini.

Muumini mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Jackson Mgesa alisema kuwa wapo kambini hapo kwa hali ya tahadhari na kuishinikiza Tanesco kutopitisha nyaya hizo kwani hazihitajiki kupitishwa eneo hilo kama walivyofanya chuo kikuu cha Dar es salaam.

source.nifahamishe.com

Rais wa Afrika Kusini Aoa Mke wa Tatu, Wanne Anasubiria

Wednesday, January 06, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Rais wa Afrika Kusini ameoa mke wa tatu katika sherehe za kitamaduni zilizofanyika chini ya ulinzi mkali katika mji wa KwaZulu-Natal huku taarifa zaidi zikisema kuwa ataongeza mke wa nne hivi karibuni kwa kumuoa mchumba wake mpya.
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amefunga ndoa kwa mara ya tano katika sherehe kubwa za harusi zilizohudhuriwa na wafanyabiashara, wanasiasa na watu wengi maarufu.

Rais Zuma alikuwa afunge ndoa na mchumba wake Thobeka Mabhija mwenye umri wa miaka 36 mwaka jana lakini sherehe za harusi ziliahirishwa kutokana na shuguli za kisiasa za rais Zuma.

Rais Zuma awali alioa mara nne lakini mke wake mmoja alifariki wakati mke wake mwingine aliachana naye.

Wake wa sasa wa rais Zuma ni Sizakele Khumalo, aliyemuoa mwaka 1973, na Nompumelelo MaNtuli-Zuma, aliyemuoa mwaka 2007.

Wake hao wawili wa rais Zuma walihudhuria sherehe hiyo iliyofanyika Nkandia,KwaZulu-Natal ambapo waandishi wa habari walipigwa stop kuikaribia nyumba ya rais Zuma ambako sherehe hiyo ya kitamaduni ilikuwa ikifanyika.

Ndoa za rais Zuma zimewaganya watu wengi huku vijana wa kisasa wakisema kuwa hazina nafasi katika dunia hii ya kisasa.

Kwa mujibu wa tamaduni za Zulu, wake wawili wa Zuma wanalazimika kumkubali mke mpya atakayejiunga nao na pia wanatakiwa kuhudhuria sherehe za harusi yake.

Wakati huo huo taarifa zaidi zinasema kuwa rais Zuma mwenye umri wa miaka 67 anatarajia kuongeza mke wa nne katika siku zijazo.

Wiki iliyopita mchumba wake mpya Gloria Bongi Ngema alipeleka zawadi za kitamaduni za harusi kwenye familia ya rais Zuma.

Rais Zuma ana jumla ya watoto 18.


source.nifahmishe

Drogba Aifunga, Aipongeza Taifa Stars

Wednesday, January 06, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


HUKU akiwa mfungaji wa bao pekee na la ushindi la Ivory Coast, mshambuliaji wa Chelsea Didier Drogba amesema Taifa Stars inastahili pongezi kutokana na soka ililocheza katika mchezo wao wa kirafiki uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Taifa,Dar es Salaam
Drogba alisema, awali walitahadharishwa kuhusu uwezo wa Stars lakini hawakuwa na uthibitisho wa kile walichoambiwa; “Tuliambiwa timu ni kali, lakini hatukupata nafasi ya kuangalia kumbukumbu yoyote, na ndicho kilichotokea Uwanjani.”

Katika mchezo huo, Drogba aliweza kuifungia timu yake bao pekee la ushindi kwenye dakika ya 39 kwa kichwa akiunganisha krosi ya chinichini kutoka upande wa kulia wa Uwanja.

Naye Kocha wa Ivory Coast, Vahid Halilhodžic alisema kiufundi Stars ilicheza vizuri na ni moja kati ya timu zinazoweza kuja kufanya vizuri katika siku za usoni katika soka la Afrika.

“Timu ni nzuri, ina speed nzuri, wachezaji wengi wanajua wanachokifanya Uwanjani, pia wameweza kutumia vema kucheza nyumbani,” alisema Halilhodžic.

Naye Kocha wa Taifa Stars, Marcio Maximo alisema; “Tumecheza katika kiwango cha kuridhisha, tumeonesha kwamba tunaweza kucheza na timu nyingine zaidi ya Ivory Coast.”

Ivory Coast ipo jijini Dar es Salaam kwa kambi ya muda ya mazoezi kabla ya kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika itakayofanyika kuanzia Januari 10 m waka huu.

Timu hiyo keshokutwa Alhamisi itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Rwanda ‘Amavubi’ kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

source nifahamishe.com

Kizimbani Kwa Kumtukana Mama Mkwe Wake

Wednesday, January 06, 2010 / Posted by ishak / comments (0)

MWANAMKE Salma Hamisi [28] mkazi wa Magomeni, amefikishwa katika mahakama ya mwanzo Magomeni kwa kosa la kumtukana mama mkwe wake matusi ya nguoni.
Salma alifikishwa mahakamani hapo jana majira ya saa 3 asubuhi, ili kujibu shtaka hilo linalomkabili

Ilidaiwa na Mwendesha Mashitaka, Noel kuwa, mshitakiwa alitenda kosa hilo Desemba 30, mwaka jana, majira ya jioni huko maeneo ya Magomeni Mwembechai.

Ilidaiwa kuwa mshitakiwa alifika kwa mama mkwe wake huyo na kuanza kumtukana matusi ya nguoni ya kumdhalilisha.

Moja ya matusi hayo yaliyobainishwa mahakamani hapo ni pamoja na kumwambia mama huyo kuwa alikuwa anamfatilia maisha yake kama mke mwenzake

Hakimu alipomuuliza mlalamikaji aliyefahamika kwa jina la Asha [56] kama ni kweli alitukanwa matusi na mkwe wake huyo alisema alitukanwa matusi mengi ya kumdhalilisha likiwemo kumwambia kuwa anamtaka mwanae huyo wa kiume na baadae kutaka kumpiga.

Mshitakiwa alipoulizwa alikana na kudai kuwa mama mkwe wake ana matatizo ya kuwafuatilia maisha yake yeye na mume wake hali ambayo inaonekana ni kero kubwa kwake na alikana kutaka kumpiga mama huyo.

Mshitakiwa aliachiwa huru kwa dhamana mpaka kesi hiyo itakapotajwa tena Januari 18 mwaka huu.


source.nifahamishe

Wezi Kama Hawa Hawajawahi Kutokea

Wednesday, January 06, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Polisi nchini Sweden wamewatia mbaroni wezi wa kimataifa ambao staili yao ya wizi haijawahi kutokea duniani.
Wezi hao wa nchini Sweden walikuwa wakiwasumbua wafanyabiashara wa maduka makubwa ya viatu nchini Sweden na nchini Denmark.

Kwa kuwa katika maduka ya viatu ya nchini Sweden viatu vya kushoto ndio huwekwa kwenye shoo za maduka, wezi hao walikuwa wakiiba kiatu kimoja kimoja cha kushoto nchini Sweden na kisha kwenda kuiba kiatu cha kulia nchini Denmark ambako maduka huviweka viatu vya kulia kwenye shoo za shelfu zao.

Kutokana na staili hiyo ya wizi walifanikiwa kupata pea kadhaa za viatu vya gharama ambavyo waliviuza kwa bei poa.

Wakati wanatiwa mbaroni walikutwa na viatu sita vya kushoto ambavyo pea zake huuzwa kwa dola 1,400.

Wezi hao walikuwa wakifanya wizi huo katika mji wa Malmo nchini Sweden na Copenhagen nchini Denmark.

Mji wa Malmo una maduka yapatayo 125 ya viatu na kutoka Malmo hadi Copenhagen ni mwendo wa dakika 30 tu kwa treni.Mtumie Rafiki Yako
Comments Add your Comment

Mtoa Maoni: moms016 Wednesday, January 06, 2010 00:54:39

Ni kweli mwanadamu hashikiki "ukimzibia huku anatoboa kule" lkn ndio tunarejea palepale kuwa iwapo mpanga sheria ni mwanadamu basi na mvunjaji ni huyohuyo.
BHAI uko wapi? seria kata bele na juma..
UBUGUVU endelea tu na kuvaa mapira ya gari, muhimu ni ya kwako hujamuibia mtu!
KING anatambea pekupeku!
DECLAKERS anauliza viau ni kitu gani?
Sis MINA anavaa viatu kisha soksi! Kuna kazi!

source.nifahamishe

Jeshi la Israel Lawafundisha Mbwa Kuwang'ata Wanaosema 'Allahu Akbar'

Wednesday, January 06, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Kwa mujibu wa mbunge mmoja wa Israel, jeshi la Israel limewafundisha mbwa wake kuwang'ata watu wote watakaopiga kelele za 'Allahu Akbar' (Mungu Mkubwa).
Jeshi la Israel linadaiwa kuja na silaha mpya ya kupambana na waarabu wa Palestina kwa kuwafundisha mbwa wake kuwang'ata watu wanaopiga kelele za "Allahu Akbar, Allahu Akbar".

Akiongea na shirika moja la habari la nchini Israel, mbunge mmoja wa Israel mwenye asili ya kiarabu, Ahmed Tibi, alisema kuwa jeshi la Israel limewapa mafunzo baadhi ya mbwa wake kuwang'ata watu wote wanaopiga kelele za "Allahu Akbar, Allahu Akbar".

"Mbwa wa jeshi la Israel wamefundishwa kuwashambulia waarabu wote watakaopiga kelele za Allahu Akbar", alisema Mbunge huyo.

Mbunge Tibi alisisitiza kuwa ndugu wa wanajeshi walioshuhudia shoo ya jeshi la Israel iliyofanyika jumapili, walilishuhudia tukio hilo.

Madai hayo ya mbunge Tibi yanafuatia madai ya mtangazaji wa radio ya jeshi la Israel, Carmela Menashe ambaye alisema kuwa mbwa wa jeshi la Israel wamepewa mafunzo kuwashambulia waarabu wanaopiga kelele za "Allahu Akbar".

Kwa mujibu wa gazeti la Israel la Haaretz, jeshi la Israel limekanusha madai hayo ya mbunge Tibi na kusema kuwa mbwa wao hawajapewa mafunzo hayo bali wamefundishwa kuwajua adui wakiwa wamevalia unifomu zao au nguo za kiraia.


source;nifahamishe

Ana Mimba ya Miezi Mitano Lakini Bado Bikira

Wednesday, January 06, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 14 wa nchini Uturuki amewashangaza wazazi wake na madaktari baada ya kupimwa na kukutwa ana mimba ya miezi mitano huku ingali bado ni bikira.
Mtoto huyo mwenye umri wa miaka 14 wa mji wa Aydin nchini Uturuki, alipelekwa hospitali baada ya tumbo lake kuzidi kuwa kubwa huku akilalamika kuwa na maumivu ya tumbo.

Baada ya vipimo vya madaktari ndipo hali ya kushangaza ilipojulikana kuwa msichana huyo ambaye bado ni bikira ana mimba ya miezi mitano.

"Alilalamika kusumbuliwa na maumivu ya tumbo huku tumbo lake likizidi kuwa kubwa ndipo tulipomleta hospitali", alisema mama wa mtoto huyo.

Wakati wazazi wa mtoto aliyetajwa kwa kifupi cha majina yake kama E.T wakiwa kwenye butwaa, daktari aliyemfanyia vipimo vya ujauzito mtoto huyo alitoa taarifa kwa uongozi wa hospitali ambao uliwapa taarifa polisi.

Katika mahojiano na polisi baba wa mtoto huyo aliyetajwa kama S.T alisema kuwa alifanya mapenzi na mkewe katika siku ambazo inasemekana mtoto wake alipata ujauzito.

"Baada ya kumaliza kufanya mapenzi na mama yake, nilijifuta mbegu za kiume kwa kutumia taulo ambalo nililiacha bafuni, inawezekana alilitumia taulo hilo kujifutia kwenye sehemu zake za siri", alisema baba wa mtoto huyo.

Baba huyo alisisitiza kuwa hakuna uwezekano hata kidogo wa mtoto wake kupata ujauzito kwa kufanya mapenzi na mwanaume nje ya nyumba yao kwakuwa mtoto wake bado ni bikira na ubikira wake umethibitishwa na madaktari.

Mtoto E.T anapatiwa matibabu ya kisaikolojia kwenye hospitali kuu ya mji huo.

source; nifahamishe