antivirus song-song of MR. Two a.k.a sugu.wmv
Waziri Mkuu Mwanamke Afunga Ndoa na Mwanamke Mwenzie
Baada ya bunge la Iceland kuipitisha sheria ya kuruhusu watu wa jinsia moja kuoana, waziri mkuu wa Iceland ambaye ni mwanamke amefunga ndoa na mwanamke mwenzake.
Waziri mkuu wa Iceland, bi Johanna Sigurdardottir amefunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi ambaye pia ni mwanamke.
Siku chache baada ya bunge la Iceland kupitisha sheria ya kuruhusu watu wa jinsia moja kuoana, bi Johanna amefunga ndoa na mpenzi wake Jonina Leosdottir.
Bi Johanna amekuwa akiishi na Jonina kwa muda mrefu na walifunga ndoa juzi jumapili.
Sheria ya kuruhusu wanaume kuoa wanaume wenzao na wanawake kuoa wanawake wenzao ilipitishwa juni 11 mwaka huu bila ya upingamizi wowote.
Bi Johanna mwenye umri wa miaka 66 alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Iceland mwaka jana baada ya migomo iliyosababishwa na kutetereka kwa uchumi kupelekea serikali iliyokuwepo kuondolewa madarakani.
Bi Johanna ndiye waziri mkuu wa kwanza barani ulaya kujitangaza wazi kuwa yeye ni msagaji. Ndoa yake inaonekana itakuwa ni changamoto kwa jumuiya zinazounga mkono ndoa za jinsia moja.
source nifahamishe
Mji wa Luanda Angola Ndio Mji Wenye Maisha Ghali Afrika
Mji wa Luanda nchini Angola ndio mji ambao gharama za maisha ni kubwa kuliko miji yote barani Afrika, kwa duniani mji huo unashika nafasi ya tatu baada ya miji ya Tokyo, Japan na Oslo, Norway.
Kwa mujibu wa takwimu za gharama za maisha katika miji mbalimbali duniani kwa mwaka huu wa 2010 zilizotolewa na ECA International, mji wa Luanda nchini Angola unashika nafasi ya tatu duniani kwa gharama za maisha.
Katika takwimu za mwaka jana, mji wa Luanda ndio uliokuwa ukishika nafasi ya kwanza mbele ya miji mingi mikubwa duniani.
Katika takwimu za mwaka huu, mji wa Tokyo Japan unashika nafasi ya kwanza ukifuatiwa na mji wa Oslo, Norway.
Mjini Luanda nchini Angola, chakula cha mchana katika mgahawa wa saizi ya kati, kinagharimu dola 47, kopo moja la bia ni dola 1.62, kilo moja ya mchele ni dola 4.73 na dazani moja ya mayai hugharimu dola 4.75. Ukitaka kwenda sinema na mpenzi wako basi jiandae kutoa dola 13 kwa kichwa kimoja.
ECA imetoa listi ya miji 65 duniani ambayo ndiyo inayoonekana ina gharama kubwa za maisha kwa kuangalia gharama za chakula, nguo, vifaa vya umeme na burudani.
Katika listi ya miji 65 iliyolewa mji wa New York unashika nafasi ya 29 wakati jiji la Dar es Salaam limeshindwa kuingia kwenye orodha hiyo.
Chini ni orodha ya miji iliyomo kwenye top 10.
1:Tokyo
2:Oslo
3:Luanda
4:Nagoya
5:Yokohama
6:Stavanger
7:Kobe
8:Copenhagen
9:Geneva
10:Zurich
source nifahamishe
Amuua Mtoto Wake Kwa Hasira za Marekani Kufungwa na Ghana
Mwanaume mmoja nchini Marekani anashikiliwa na polisi baada ya kumpiga mpaka kumuua mtoto wake aliyekuwa akilia sana wakati yeye akiangalia mechi ya kombe la dunia kati ya Marekani na Ghana ambayo Marekani ilifungwa 2-1 na kuliaga kombe la dunia.
Hector Castro mwenye umri wa miaka 28 alimpiga sana na kisha kumuua kwa kumziba pumzi mtoto wake wa kambo wa kike mwenye umri wa miaka miwili.
Baada ya kumuua mtoto huyo ili kuficha ukweli, Castro aliididimiza bisibisi kwenye shingo ya mtoto huyo ili kufanya kifo cha mtoto huyo kionekane kuwa ni cha ajali.
Castro aliita ambulansi akidai mtoto wake amepata ajali wakati akicheza na bisibisi imezama kwenye shingo yake.
Hata hivyo mchezo wake uligundulika muda mfupi baada ya madaktari waliokuja na ambulansi kugundua kuwa mtoto huyo alifariki kutokana kupigwa na kuvunjwa mbavu kadhaa na wala si bisibisi.
Castro alitiwa mbaroni kwa tukio hilo lililotokea jumamosi wakati wa mechi ya kuwania kuingia robo fainali kati ya Marekani na Ghana.
Castro alijitetea kuwa alishikwa na hasira kutokana na mtoto huyo kulia sana bila kunyamaza wakati yeye akiangalia mechi hiyo ya Marekani na Ghana ambayo iliisha kwa Marekani kufungwa mabao 2-1.
Kutokana na umri mdogo wa mtoto aliyeuliwa, Castro huenda akahukumiwa adhabu ya kifo iwapo atapatikana na hatia.
source nifahamishe
Nyota wa muziki wa Pop wa Marekani, Chris Brown aliangua kilio jukwaani wakati wa shoo ya kumkumbuka mfalme wa muziki wa Pop, Michael Jackson.
Akipanda jukwaani kufanya shoo yake ya kwanza kubwa baada ya kuingia matatani kwa kumpiga mpenzi wake zamani, Rihanna, Chris Brown aliangua kilio jukwaani wakati akiimba nyimbo ya Michael Jackson.
Brown alipanda jukwaani kufanya shoo ya kumuenzi Michael Jackson wakati wa tamasha la kutoa tuzo za muziki za Black Entertainment Television.
Brown alianza kwa kuwachengua watazamaji kwa shoo ya dansi akiigiza staili mbalimbali za Michael Jackson.
Alipoanza kuimba wimbo wa Michael Jackson "Man In The Mirror" uliotamba sana mwaka 1988, Chris Brown alianza kuangua kilio jukwaani na kushindwa kuendelea kuimba hali iliyopelekea watu waliohudhuria shoo hiyo kuungana naye kuimba nyimbo hiyo.
Pamoja na hisia alizozionyesha jukwaani kuhusiana na kifo cha Michael Jackson, Chris Brown amekumbwa na tuhuma kuwa alizuga kujiliza jukwaani ili watu waanze kumsapoti tena baada ya kashfa ya kumpiga Rihanna mwaka jana.
Chris Brown kutokana na kumpiga Rihanna alipoteza washabiki wengi na baadhi ya wadhamini wake na alihukumiwa kufanya kazi za kuitumikia jamii kwa miezi sita.
Maoni mengi katika tovuti ya MTV.com yalimponda Chris Brown kwa kuonyesha hisia za uongo ili kupata huruma za watu.
Watu wengi wamekuwa wakijiuliza kama hisia za Chris Brown zilikuwa za kweli au la.
source nifahamishe
HOSPITALI ya Wilaya ya Ilala Amana ya Dar es Salaam, imemkabidhi Martin [35] mtoto Alphonce Martin aliyekuwa akilelewa hapo kwa takribani siku 11 baada ya uthibitisho wa kina kuwa ni mwanae halali
Martin Melicyori mkazi wa Pugu Kinyamwezi, akifuatana na ndugu zake aliweza kukabidhiwa mtoto huyo kwa kuwasilisha barua ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa anapoishi kuthibitisha kuwa ni mwanae na kufafanua maswali aliyopewa hospitalini hapo.
Mbali na kuwasilisha maelezo hayo pia aliweza kutoa ushahidi mwengine mbalimbali ikiwemo picha mbalimbali na kufafanua vizuri maswali aliyokuwa akihojiwa.
Martin alidai kwa kweli hakuwa na habari kabisa kama mkewe alifikishwa hospitalini hapo kwa kuwa siku ya mwisho mkewe alimuaga kwenda kutafuta huduma za uzazi wa mpango akiwa na jirani yake.
Alisema kuwa majira ya jioni jirani yake huyo alifika nyumbani kwake na kumuulizia mke wake kama alikuwa amerudi na kumshanga kwa kuwa waliondoka wote na kutoa taarifa kituo cha polisi.
Alisema alijitahidi kufika hospitali mbalimbali hadi Muhimbili na kuambiwa hakuna jina la la mgonjwa kama huyo na hadi juzi walipoona taarifa hiyo kwenye gazeti.
KAtika maelezo yake alisema kuwa Alphonce ni motto wake wa tatu kuzaliwa kati ya watoto watatu ikiwa ni pamoja na Sweet (9) na Samson (4.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Dk. Meshark Shimwela, baada ya kuridhika na maelezo hayo pia ndugu hao waliruhusiwa kuja kuchukua mwili wa marehemu ambao ulikuwa umehifadhiwa hospitalini hapo ilipowasiliana na uongozi wa hospitali hiyo ulidai kuwa mwili huo utachukuliwa leo kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Tabata.
Watu 11 wamefariki nchini Senegal na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya jengo walilojazana kuangalia mpira kuporomoka.
Polisi nchini Senegal wamesema kuwa watu 11 wamefariki dunia wakiangalia mechi ya kombe la dunia wakati jengo walilokuwemo lilipobomoka na kuwafunika.
Kundi kubwa la watu lilikusanyika kwenye nyumba ya mkuu wa kampuni ya umeme katika mji wa Matam kaskazini mwa Senegal ili kuangalia mechi ya kombe la dunia.
Polisi walisema kuwa jengo hilo lilibomoka wakati wakati wa mechi ya jumamosi mchana kati ya Uruguay na Korea.
Senegal haikufanikiwa kufuzu kushiriki fainali za kombe la dunia lakini fainali za kombe za dunia zinazoendelea nchini Afrika Kusini zimekuwa zikifuatiliwa kwa ukaribu sana nchini humo.
Mamia ya watu walimiminika mitaani jumamosi usiku kushangilia ushindi wa Ghana wa mabao 2-1 dhidi ya Marekani.
Ghana ndio wawakilishi pekee wa Afrika waliobaki kwenye kombe la dunia na wataingia uwanjani ijumaa kumenyana na Uruguay ili kuwania tiketi ya nusu fainali.
source nifahamishe
Afukua Maiti Toka Kaburini na Kufanya nayo Mapenzi
Kijana mwenye umri wa miaka 20 wa nchi ya kusini mwa Amerika ya Guyana amewashangaza watu wengi kwa kitendo chake cha kufukua maiti ya bibi wa miaka 75 na kisha kufanya nayo mapenzi.
Kijana huyo aliyetajwa kwa jina la Roopram Bacchus ambaye hufanya kazi ya kuokota taka, alipandishwa kizimbani ijumaa kujibu mashtaka yanayomkabili.
Bacchus alikiri mashtaka aliyofunguliwa ya kufanya mapenzi na maiti.
Kijana huyo alikiri kulifukua kaburi la bibi mwenye umri wa miaka 75 na kisha kufanya mapenzi na maiti yake.
Bacchus alijitetea kuwa ana matatizo ya kupenda sana pombe ambayo ndiyo iliyompelekea akafanya kitendo hicho.
Jaji aliamuru afanyiwe uchunguzi wa akili zake na alimuamuru alipe faini ya dola 200 za Kimarekani. Atatupwa jela mwaka mmoja kama akishindwa kulipa faini hiyo.
Kamanda wa polisi wa eneo hilo, Steve Merai alisema kuwa Bacchus alilifukua kaburi la bibi huyo siku moja baada ya bibi huyo kuzikwa.
"Bacchus alilivunja jeneza, aliitoa maiti toka kwenye jeneza na alifanya nayo mapenzi", alisema kamanda huyo wa polisi.
Kamanda huyo wa polisi aliongeza kuwa Bacchus na familia ya bibi huyo walikuwa ni majirani.
source nifahamishe