Wanamgambo wa kundi la Al Shabab la nchini Somalia wamemkata mkono wa kulia mwanaume aliyekamatwa akiiba simu.
Wanamgambo wa kundi la Al Shabab la nchini Somalia wameukata kwa kutumia jambia mkono wa kulia wa mwanaume mwenye umri wa miaka 30 aliyekamatwa akiiba simu.
Yusuf Sheikh Ahmed alikamatwa akiiba simu kwenye mji wa Merka ambao unatawaliwa na kundi la Al Shabab.
Yusuf alikamatwa mkono wake wa kulia mbele ya mamia ya watu waliokusanyika kushuhudia adhabu hiyo.
"Adhabu hii ni mojawapo ya juhudi zetu za kutokomeza uhalifu kwa sharia za kiislamu, mtu yoyote atakayeiba atakatwa mkono wake", alisema Sheikh Isa Mohamed, ambaye ni mmoja wa maafisa wa Al Shabab.
Jaji wa mahakama ya kiislamu ya mji huo aliamuru Yusuf akatwe mkono wake wa kulia baada ya Yusuf mwenyewe kukiri kosa lake la kuiba simu.
Yusuf aliwahishwa hospitali kwa matibabu zaidi baada ya kukatwa mkono wake.
Wakati huo huo wanaume wengine ambao walikamatwa wakiwa wamelewa pombe na madawa ya kulevya walicharazwa bakora kati ya 40 na 80.
Kundi la Al Shabab linashikilia maeneo ya kusini na katikati mwa Somalia.
source nifahamishe
Msanii wa Marekani aliyeiweka picha hii ya mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama kwenye ukurasa wake wa Twitter imembidi aombe ulinzi toka FBI baada ya mamia ya watu kumtumia vitisho vya kumuua.
Scott Baio msanii wa Marekani aliyetamba kwenye series za komedi za Happy Days na Charles in Charge ametumiwa vitisho kibao vya maisha yake baada ya kuweka picha mbaya ya mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Baio aliiweka picha hii ya Michelle Obama kwenye ukurasa wake wa Twitter ikiwa na maneno "Wow, Obama anaamshwa namna hii kila siku asubuhi".
Picha hii pamoja na maelezo yake ilichukuliwa na watumiaji wengine wa Twitter kama ubaguzi wa rangi.
Haukupita muda mrefu Baio alianza kuandikiwa maoni kwenye ukurasa wake wa Twitter akiambiwa kuwa ni mbaguzi wa rangi na ameweka picha hiyo kumdhalilisha bi Michelle Obama.
Baio alitumiwa vitisho vingi vya maisha yake kiasi cha kumfanya aripoti vitisho hivyo FBI.
"Ni rahisi kuijua nyumba yako Baio na kukumaliza", Mtoa maoni mmoja aliandika huku mwingine akitishia kumdhuru Baio, Mkewe na mtoto wake.
Hata hivyo Baio aliendelea kusisitiza kuwa alikuwa na nia ya kufanya masihara na sio kama ambavyo watu wengine walivyoichukulia picha na maandishi aliyoyaweka.
Baio aliandika pia kwenye ukurasa wake baadhi ya vitisho vya maisha yake alivyotumiwa.
Katika kuonyesha kwamba yeye sio mbaguzi wa rangi Baio aliweka picha yake akiwa pamoja na mwanamke mweusi ambaye ni rafiki wa mke wake.
"Mimi sio mbaguzi wa rangi kwa kuweka picha ya Michelle Obama, rafiki mkubwa wa mke wangu ni Mmarekani mweusi", alisema Baio.
Baio aliandika ujumbe pia kwenye Twitter akiwafahamisha watu kuwa ameisharipoti vitisho alivyotumiwa FBI.
source nifahamishe
HATIMAYE Pascal Mnaku, mlinzi wa kampuni ya Ultimate Security aliyepambana na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kwenye mashine ya kuchukulia fedha (ATM) jijini Dar es Salaam, amefukuzwa kazi na muajiri wake huyo.
Mnaku alijikuta kwenye mpambano mkali na waziri huyo baada ya kumtaka asogee pembeni ya mashine hiyo ya Standard Chartered ili kupisha wateja wengine baada ya Ngeleja kuonekana akitumia muda mwingi kuongea na simu akiwa ndani ya chumba cha mashine hiyo.
Kwa mujibu wa habari tulizozipata kutoka Ultimate na kuthibitishwa na Mnaku, uamuzi wa kumfukuza kazi ulitolewa mara baada ya kikao cha nidhamu cha kampuni hiyo kilichofanyika jana kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi jioni kwenye ofisi za Ultimate.
"Ni kweli nimefukuzwa kazi na hivi ninavyoongea na wewe ndio nimetoka katika kikao cha nidhamu na uamuzi uliofikiwa ndio huo,"alisema mlinzi huyo ambaye hakutetereka wakati Waziri Ngeleja alipohoji kama anamfahamu ni nani wakati akitakiwa kutoka kwenye ATM.
"Na hii ni kutokana na kitendo changu cha kumtaka Waziri Ngeleja awapishe wateja wengine kwenye ATM," alilalamika Mnaku.
Jana jioni Mnaku aliliambia Mwananchi kuwa anatakiwa aende kuchukua barua yake ya kutimuliwa kazini Januari 30.
Hata hivyo, mara baada ya gazeti hili kuripoti sakata hilo, Ngeleja alikiri kutokea kwa mtafaruku huo na kujitetea kuwa Mnaku ndiye aliyekuwa chanzo cha mtafaruku huo uliotokea kwenye mashine ya fedha iliyo kwenye jengo la Harbour View (zamani JMall).
Mwananchi iliripoti kuwa waziri huyo alikaribia kuzichapa na mlinzi huyo kwenye baada ya kuombwa asogee pembeni kupisha wateja wengine.
source mwananchi
Sala ya Myahudi Yasababisha Kasheshe Kwenye Ndege
Myahudi aliyeamua kusali ndani ya ndege nchini Marekani alizua hofu kwa abiria wengine kiasi cha kuifanya ndege itue kwa dharura.
Myahudi aliyeamua kutoa zana zake za kusalia ndani ya ndege ya Marekani na kuanza kusali kwa sauti, alisababisha hofu ya bomu na kupelekea ndege hiyo ibadili mwelekeo na kutua uwanja wa ndege wa karibu.
Myahudi huyo alikuwa kwenye ndege ya Chautauqua Airlines iliyokuwa ikitokea New York kuelekea Louisville, Kentucky.
Ndege hiyo ilibadili mwelekeo na kutua kwa dharura kwenye uwanja wa ndege wa Philadelphia International Airport baada ya Myahudi huyo kutoa viboksi viwili vyeusi na kujifunga mkononi na kichwani kabla ya kuanza kusali kwa sauti.
Katika sala za kiyahudi, viboksi viwili vidogo vyeusi vyenye mikanda hufungwa kichwani na mkononi kabla ya sala kuanza.
Abiria katika ndege hiyo ambao hawajawahi kuona sala za kiyahudi zinavyofanyika walidhania viboksi hivyo ni mabomu na myahudi huyo ndio alikuwa akijiandaa kujilipua.
"Alikuwa akisali kwa sauti huku akiwa amevaa viboksi vyake vyeusi, lugha aliyokuwa akiongea hakuna aliyekuwa akiielewa", alisema abiria mmoja.
Magari 12 ya polisi na timu ya wataalamu wa mabomu walikuwepo kwenye uwanja wa ndege wa Philadelphia wakati ndege hiyo ilipotua kwa dharura.
Myahudi huyo alikamatwa na kuhojiwa wakati wataalamu wa mabomu wakiisachi ndege nzima kuangalia kama kuna bomu lolote.
Myahudi huyo alichiwa huru baada ya kugundulika kuwa viboksi vyake vyeusi havikuwa mabomu bali ni vifaa vinavyotumiwa katika sala za kiyahudi.
Ulinzi katika masuala ya anga umeimarishwa zaidi nchini Marekani tangia disemba 25 mwaka jana baada ya kijana wa Kinigeria kufeli jaribio lake la kujipua kwenye ndege iliyokuwa ikielekea Marekani.
source niffahamishe
KALI YA MWAKA - Mtangazaji wa Italia Amfedhehesha David Beckham
Mtangazaji mwanamke wa televisheni moja ya nchini Italia alimuacha nyota wa soka wa Uingereza David Beckham akiuma meno kwa hasira na fedheha baada ya mtangazaji huyo kuyakamata makende yake akiwa na nia ya kujua ukubwa wake.
Huku akipiga kelele kwa kitaliano "E piccolo, Beckham" ("Beckham kumbe ni Mdogo") mtangazaji huyo alizolewa msobe msobe na walinzi wa David Beckham baada ya kuyakamata makende yake.
Mtangazaji huyo wa televisheni moja ya nchini Italia aliyejulikana kama Elena Di Cioccio alikuwa na nia ya kujua ukweli kama mali za siri za David Beckham ni kubwa kama zinavyoonekana kwenye tangazo la chupi za Armani ambalo David Beckham alishiriki.
"Nilitaka kujua ukubwa wa makende yake", alisema Elena.
Beckham alikuwa akiongea na waandishi wa habari nje ya hoteli moja mjini Milan wakati tukio hilo lilipotokea na kumwacha Beckham akiwa hajui la kufanya akibaki anamwangalia mtangazaji huyo kabla ya walinzi wake kumuondosha.
Mtangazaji huyo alipanga tukio hilo mapema na kuongozana na timu yake ya wapiga picha hadi kwenye eneo ambalo David Beckham alikuwa akiongea na waandishi wa habari.
Huku akiwa amevaa gloves za njano, mtangazaji huyo alijipenyeza na kumsogelea kwa karibu Beckham kabla ya kuzikamata nyeti zake na kuanza kupiga kelele za "Beckham kumbe mdogo".
Beckham alishiriki kwenye matangazo ya nguo za ndani za mwanamitindo maarufu duniani Giorgio Armani. Katika picha za tangazo hilo Beckham anaonekana akiwa ameshehena mzigo kwenye sehemu zake nyeti ambao mkewe Victoria Beckham aliubatiza jina la "Golden Balls".
Hivi karibuni Cristiano Ronaldo alichukua nafasi ya Beckham katika matangazo hayo ya viwalo vya ndani vya Armani.
source nifahamishe
Mtoto wa miaka miwili, mvuta sigara mdogo zaidi duniani
SOTE tunafahamu kwamba mvulana mwenye umri wa miaka miwili ni dhahiri atakuwa bado anakunywa maziwa au ameanza kula vyakula vya watu wazima. Lakini, mvulana mmoja wa Kichina ameanza kuvuta sigara wakati akiwa na umri wa miezi 18...Mtoto huyo huvuta paketi moja ya sigara kila siku na hushikwa na hamaki iwapo hapewi kiburudisho chake hicho.
Mtoto huyo, Tong Liangliang, alifundishwa jinsi ya kuwasha sigara na baba yake ambaye aliamini kwamba uvutaji ungempunguzia maumivu ya ugonjwa wa ngiri (hernia).
‘Baba-mtu hakujua jinsi tabia hiyo ingekolea kwa kitoto chake hicho hadi pale alipong’amua kwamba idadi ya sigara kilichokuwa kinavuta kila siku ilikuwa imeongezeka,” kilitangaza kituo cha China Radio International.
Tong alianza kuvuta sigara yake ya kwanza akiwa na umri wa miezi 18 katika jitihada za kupunguza maumivu ya ngiri yaliyokuwa yanamsumbua. Hili lilifanyika kwa kutambua kwamba mtoto huyo alikuwa ni mdogo mno kiasi cha kutoweza kufanyiwa opasuaji.
Hata hivyo, hii ni “rekodi ya dunia isiyokuwa rasmi” kwa vile kuingizwa kwake katika Kitabu cha Rekodi za Guiness (Guinness Book of Records) kama mvutaji mdogo zaidi wa sigara duniani, kutakataliwa kwa madai kwamba kitendo hicho kilichochea tabia yenye madhara kwa watoto.
source globalpublisher
KUNDI la watu ambao hawakuhitajika kuwa katika chakula cha mchana kilichoandaliwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi kwa ajili ya kuwapa chakula cha mchana walemavu wa aina zote nchini walivamia katika ukumbi na kufanya fujo n
Watu hao ambao hawakuwa na chembe ya hata ulemavu walivamia katika ukumbi wa Diamond Jubilee katika sherehe hizo za 16 za kila mwaka ambapo Mengi alikuwa akiwakutanisha walemavu na kuwapa chakula cha mchana kwa pamoja.
Watu hao waliodiriki kufanya fujo mbele ya mgeni rasmi Waziri Mkuu Pinda na kuvamia majofu yaliyokuwa na vinyaji na kugombania vinyaji hivyo kwa fujo hali iliyofanya kuharibu mandhari ya ukumbi mzima katika sherehe hizo.
Katika hali ya kushangaza watu hao ambao walisemekana ji wahuni wa mitaani waliingia kwenye ukumbi huo na kuvamia majokofu hayo na kufanya fujo hizo na hatimaye baadhi ya walemavu nao kuingia katika fujo hizo na wao wakionekana kugombania vinywaji hivyo.
Vinywaji vilivyokuwa vikigombaniwa ni pamoja na bia za kopo aina zote pamoja na soda za kop ambazo ziliandaliwa kwa ajili ya shuhuli hiyo.
Kufuatia hali hiyo askari polisi walikuwa wachache ukumbini hapo na kuzidiwa na kundi huilo la wahuni na hatimaye vinywaji hivyo kutkidhi haja ya wageni waliohudhuria sherehe hizo naw ahuni hao kujazad viroba walivyokuja navyo na kuondoka na vinywaji hivyo.
Risala, hotuba walizokuwa wakitoa wageni rasmi ukumbini humo zilikuwa zikisikika kwa tabu kutokana na makelele yaliyokuwa ukumbini humo hali iliyofanya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kushanga hali hiyo mbele ya macho yake.
Hali hiyo ilisababisha hadi Pinda wakati anataka kuondoka nje ya ukumbi huo kuondoka kwa shida kutokana na kukosekana kwa njia iliyotokana na vurugu hizo za kugombea vinywaji.
Watu walisukumana na kupigana kwenye maeneo yaliyopangwa kwa ajili ya kutoa huduma ya vinywaji.
Baadhi ya wafanyakazi wa IPP waliiambia NIFAHAMISHE kuwa "wanashangazwa na vurugu hizo kwa sababu vinywaji vilikuwepo vya kutosha kwa ajili ya watu hao, lakini wakaongeza kuwa watu ambao hawakukusudiwa kwa hafla hiyo, ndio waliovamia na kufanya vurugu hizo kwa kuwa hali kama hiyo haijawahi kutokea katika miaka yote ambayo Mengi huandaa chakula cha mchana.
Katika hafla hiyo iliyokutanisha watu wenye ulemavu tofauti, na walemavu wapatao 4000 walikutanishwa katika ukumbi huo klwa ajili ya chakula hicho ambapo sherehe hizo hufanyika wka mwaka mara moja.
Katika chakula hicho viongozi mabalimbali walihuduria akiwemo na askofu wa KKKT Askofu Malasusa, Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa Majeshi nchini.
Pia wabunge wawakilishi wa walemavu bungeni walihudhuria sherehe hizo.
Sherehe hizo zilifanyika Jumapili mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamondi Jubilee.
Pia wasanii mbalimbali walijumuika katika sherehe hizo kutumuiza walemavu akiwemo, TID, MARLOW,DIAMOND, DULLY SYKES, WANAUME TMK, na MWASITI
source nifahamishe
MWanajeshi aua mkewe na kisha mwenyewe kujinyonga
ASKARI mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kepteni Deogratius Chache (60), amuua mkewe kwa kumkata kichwa na kisha na yeye kujinyonga hadi kufa huko Tarime Mkoani Mara.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime, Costastino Masawe, amesema tukio hilo lilitokea Januari 16 mwaka huu, saa 2 usiku, katika kijiji cha Kiterere Mara.
Alisema askari huyo ambaye ni ofisa mstaafu wa JWTZ alimkata mkewe Aloidia Kambunga [47] na panga sehemu za kichwani na kisha na kuutenganisha mguu wake wakulia kulia na kupatikana kifo hca mma huyo.
Kamanda Masawe alisema kuwa baada ya ofisa kufanya kitendo hicho alitoka eneo la nyumbani kwake kama mita 20 kisha na yeye kwenda kujinyonga kwenye mti kutokana na hasira alizokuwa nazo.
Kamanda Masawe aliviambia vyombo vya habari kuwa, kabla ya tukio hilo kutokea marehemu hao walikuwa na ugomvi siku nyingi kati ya wana ndoa uliopelekea kila mmoja kulala katika chumba chake.
Alisema kuwa ofisa huyo alikuwa akimkanya mkewe ambaye alikuwa ni muuguzi katika Hospitali ya Kitega kuhusiana na tabia ya kutoka nje ya ndoa lakini aliona hakuna maeleweno na baadae waliamua wajitenge vyumba.
Aliongeza kuwa chanzo cha mauaji hayo yalisemekana ni kutokana na wivu wa kimapenzi
Katika tukio la lingine la mauaji mwanaume mmoja anashikiliwa na polisi wilayani Bunda kwa tuhuma za kumpiga mkewe na kumsababishia kifo.
Kamanda wa Polisi mkoani Mara, Robert Boaz, alisema mtuhumiwa huyo ni Chacha Magoki, mkazi wa Kijiji cha Kihumbu wilayani Bunda.
Kamanda Boaz alisema mwanaume huyo alitiwa mbaroni juzi asubuhi akiwa anasafirisha mwili wa marehemu huyo kutoka hospitalini ili ukazikwe katika kijiji cha Kihumbu.
Ilidaiwa kuwa mwanaume huyo alimpiga mke wake Ester Werema kutokana na kukasirishwa na kitendo cha mke wake kumpa chakula shemeji yake.
Ilidaiwa mume wake kutokana na wivu wa kimapenzi alikuwa akimkanya kitendo cha kuwa karibu na shemeji yake huyo na alikuwa akimpiga mara kwa mara.
Polisi wamesema mwanaume huyo atafikishwa mahakamani wakati wowote kujibu mashitaka ya mauaji.
sourrce nifahamishe
Daktari Anayetumia Limao Kusafishia Vidonda Aua Watu Saba
Daktari wa Ujerumani ambaye alikuwa akitumia maji ya limao kusafishia majeraha ya operesheni amefunguliwa mashtaka baada ya kupelekea vifo vya watu saba.
Dokta Arnold Pier amehukumiwa kifungo cha nje cha miezi 15 baada ya njia yake ya kusafisha majeraha kwa kutumia maji ya limao kusababisha vifo vya watu saba.
Kwa mujibu wa gazeti la Ujerumani la Bild, katika kubana matumizi katika zahanati yake Dr. Pier badala ya kutumia madawa ya kusafishia vidonda na majeraha alikuwa akitumia maji ya malimao kusafishia vidonda.
Mwanamke mmoja alifariki baada ya kupata maambukizi baada ya majeraha yake baada ya operesheni kusafishwa kwa kutumia maji ya limao.
Dr Pier ambaye ni mmiliki wa zahanati ambayo vifo hivyo vilitokea, anatuhumiwa pia kuwafanyia wagonjwa operesheni zisizo za lazima ili kujiingizia pesa zaidi.
Hospitali ya Dr. Pier ilikuwa katika hali ngumu ya kiuchumi wakati Dr. Pier alipobuni mbinu za kubana matumizi ikiwemo njia ya kutumia majji ya malimao kusafishia majeraha.
Akitoa hukumu ya kesi hiyo, Jaji Lothar Beckers alisema kuwa njia ya kutumia maji ya malimao mbali ya kuwasababishia maambukizi wagonjwa iliwasababishia maumivu makali zaidi.
Dr Pier pamoja na madaktari wenzake watatu wamefunguliwa mashtaka 64 ya kudhuru mwili kuhusiana na wagonjwa 18.
source nifahamishe
Daktari Anayetumia Limao Kusafishia Vidonda Aua Watu Saba
Daktari wa Ujerumani ambaye alikuwa akitumia maji ya limao kusafishia majeraha ya operesheni amefunguliwa mashtaka baada ya kupelekea vifo vya watu saba.
Dokta Arnold Pier amehukumiwa kifungo cha nje cha miezi 15 baada ya njia yake ya kusafisha majeraha kwa kutumia maji ya limao kusababisha vifo vya watu saba.
Kwa mujibu wa gazeti la Ujerumani la Bild, katika kubana matumizi katika zahanati yake Dr. Pier badala ya kutumia madawa ya kusafishia vidonda na majeraha alikuwa akitumia maji ya malimao kusafishia vidonda.
Mwanamke mmoja alifariki baada ya kupata maambukizi baada ya majeraha yake baada ya operesheni kusafishwa kwa kutumia maji ya limao.
Dr Pier ambaye ni mmiliki wa zahanati ambayo vifo hivyo vilitokea, anatuhumiwa pia kuwafanyia wagonjwa operesheni zisizo za lazima ili kujiingizia pesa zaidi.
Hospitali ya Dr. Pier ilikuwa katika hali ngumu ya kiuchumi wakati Dr. Pier alipobuni mbinu za kubana matumizi ikiwemo njia ya kutumia majji ya malimao kusafishia majeraha.
Akitoa hukumu ya kesi hiyo, Jaji Lothar Beckers alisema kuwa njia ya kutumia maji ya malimao mbali ya kuwasababishia maambukizi wagonjwa iliwasababishia maumivu makali zaidi.
Dr Pier pamoja na madaktari wenzake watatu wamefunguliwa mashtaka 64 ya kudhuru mwili kuhusiana na wagonjwa 18.
source nifahamishe
Walinzi wa Kivita Kuzilinda Timu Zitakazoshiriki Kombe la Dunia
Baada ya basi la wachezaji wa Togo kushambuliwa kwa risasi nchini Angola wakati wakiwasili kwaajili ya kombe la mataifa ya Afrika, timu zitakazoshiriki kombe la dunia nchini Afrika Kusini baadae mwaka huu zinakusudia kukodisha walinzi wa kivita toka nchini Iraq na Afghanistan.
Timu nyingi zitakazoshiriki kombe la dunia baadae mwaka huu nchini Afrika Kusini zimepanga kuwakodisha walinzi toka makampuni ya ulinzi katika sehemu zenye vita za nchini Iraq na Afghanistan.
Walinzi hao wakiwa na silaha za kivita watawalinda wachezaji na maafisa wa timu zitakazoshiriki kombe la dunia.
Taarifa zilizopatikana zilisema kwamba baadhi ya vyama vya soka katika nchi za barani Ulaya na Kusini mwa Amerika tayari zimeishawakodisha walinzi wa kivita ili kuwalinda wachezaji wao na familia zao muda wote watakaokuwa nchini Afrika Kusini.
Walinzi hao wakitumia silaha za kivita, magari yasiyopitisha risasi watawalinda wachezaji masaa 24 na kuwaepusha na matukio ya utekaji.
Hatua hiyo imechukuliwa kufuatia hofu ya usalama nchini Afrika Kusini ambapo matukio ya uhalifu yamekuwa yakitokea kwa kiwango kikubwa sana kila siku.
Hata hivyo shirikisho la soka duniani limezihakikishia usalama nchi zitakazoshiriki kombe la dunia kutokana na hatua ya serikali ya Afrika Kusini kuwaandaa polisi 41,000 kwaajili ya ulinzi wakati wa michuano hiyo.
source nifahamishe
Mwanasiasa Zambia Atishia Kumbaka 'Mande' Mpinzani wa Rais
Kiongozi wa umoja wa vijana wa chama tawala nchini Zambia ametishia kuwa vijana wa chama hicho watambaka 'mande' mwanasiasa mwanamke anayeonyesha upinzani wa sera za rais wa Zambia.
Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama tawala nchini Zambia cha MMD bwana Chris Chalwe ametishia kumbaka mwanansiasa mwanamke Bi. Edith Nawakwi ambaye amekuwa akiukosoa sana uongozi wa rais Rupiah Banda.
"Tutambaka mande (mtungo) Nawakwi iwapo ataendelea kumshambulia rais", alisema Chalwe kuuambia umati wawati uliokusanyika kwenye mkutano wa kisiasa.
Chalwe alitoa kitisho hicho katika kumlinda rais Banda ambaye anajiandaa na uchaguzi mkuu mapema mwaka ujao.
Nawakwi ambaye ni kiongozi wa FDD alimuunga mkono Banda wakati wa uchaguzi mwaka 2008 lakini sasa amekuwa akimkosoa kuwa uongozi wake umefeli.
"Rais amechaguliwa na watu wa Zambia hivyo anastahili heshima toka kwa wananchi wote na mtu yoyote atakeyemkosoa tutambaka mande", aliongeza Chalwe.
Chalwe anajulikana kwa ukorofi wake na hivi sasa anakabiliwa na kesi mahakamani ya kumpiga mwandishi wa habari aliyekuwa akiripoti rais Banda kurudi nyumbani toka Uganda alipofanya ziara mwezi julai mwaka jana.
Akiongelea tukio hilo la kutishiwa kubakwa, bi Nawakwi alisema kuwa jambo lolote litakalomtokea basi rais Banda ndiye atakayekuwa wa kulaumiwa.
Bi Nawakwi aliongeza kuwa amewasiliana na wanasheria wake kuhusiana na tishio hilo ambalo alisema halitoki kwa Chalwe pekee bali linatoka kwa serikali ya rais Banda kwa kuwa Chalwe na vijana wa MMD wanapata sapoti toka serikalini.
source nifahamishe
Safari ya Kuzamia Italia Ndani ya Begi.
Raia wa Afghanistan mwenye umri wa miaka 15 amenaswa na maafisa wa uhamiaji wa Italia akizamia nchini humo akiwa amejificha ndani ya begi.
Maafisa wa uhamiaji wa Italia walipigwa na butwaa baada ya kulisimamisha gari dogo aina ya Peugeot 207 na kumkuta kijana wa Kiafghanistan mwenye umri wa miaka 15 akiwa amejificha ndani ya begi lililokuwa limewekwa kwenye buti la gari hilo.
Raia wa Ugiriki Alexandros Lepesiotis, 42, aliyekuwa akiliendesha gari hilo anashikiliwa na polisi kwa makosa ya kujaribu kuwaingiza kinyemela nchini Italia, kijana huyo na kaka yake mwenye umri wa miaka 17 ambaye naye alikutwa kwenye buti la gari hilo akiwa amefunikwa na mablanketi.
Polisi walilisimamisha gari la Lepesiotis katika taratibu za kawaida za polisi za kukagua magari yanayoingia Italia toka Ugiriki lakini walishangazwa na jinsi Lepesiotis alivyokuwa akionyesha wasiwasi gari lake lilipoanza kukaguliwa.
Taarifa zilisema kuwa vijana hao wa Kiafghanistan walimlipa dereva huyo wa Kigiriki euro 2600 ili awaingize kinyemela nchini Italia.
Vijana hao walipata pesa hizo kutokana na kazi za kuosha vyombo kwenye migahawa ya Ugiriki.
Vijana hao wamehifadhiwa katika mji wa Bari nchini Italia wakati taratibu za kuwasiliana na wazazi wao zikifanyika na pia kuangalia kama wapewe haki ya ukimbizi au la.
source nifahamishe
Mama Afanya Mapenzi Mara 200 na Mtoto wa Miaka 12
Mama mmoja nchini Uingereza alifanya mapenzi mara 200 na mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 12 na alikuwa akiweka alama kwenye daftari lake kila alipomaliza kufanya naye mapenzi.
Angela Sullivan mwenye umri wa miaka 36 anakabiliwa na kifungo cha miaka mingi sana jela kwa kufanya mapenzi takribani mara 200 na mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 12 .
Angela alikuwa akiweka alama ya nyota katika daftari lake kila anapomaliza kufanya mapenzi na mtoto huyo.
Katika kipindi cha miezi 10 cha uhusiano wa Angela na mtoto huyo, daftari lake lilikutwa likiwa na alama za nyota 191 kuonyesha siku walizofanya mapenzi.
Taarifa zaidi zilisema kwamba Angela alimnunulia zawadi ya viatu mtoto huyo baada ya kufanya naye mapenzi kwa mara ya 100.
Mahakama iliambiwa kuwa Angela alianza uhusiano na mtoto huyo kwa kumlewesha pombe na kisha kuzichezea sehemu zake za siri.
Hatimaye walianza uhusiano wa kimapenzi ambao ulidumu kwa miezi 10 hadi uhusiano wao ulipogundulika kufuatia uvumi kwenye shule ya mtoto huyo kuwa Angela amepata ujauzito.
Wapelelezi waligundua pia kuwa mtoto huyo ambaye hakutajwa jina lake kwasababu za kisheria, alikuwa akijigamba kwa rafiki zake kwenye internet kuhusiana na uhusiano wake wa kimapenzi na Angela.
Mahakama iliambiwa kuwa Angela alikuwa akifanya mapenzi na mtoto huyo kwenye nyumba yake katika mji wa Middlesbrough na kabla ya kuwasili kwa mtoto huyo alikuwa akimpeleka kwa bibi yake mtoto wake pekee wa kiume aliyekuwa akiishi naye.
Alipotiwa mbaroni, Angela alikanusha kufanya mapenzi na mtoto huyo lakini alishindwa kuelezea vizuri alama katika daftari lake ambazo ziliambatana na maneno kama vile "Angela anampenda ..[jina la mtoto huyo]..".
Alipofikishwa mahakamani jana, Angela alikiri makosa yake ya kufanya mapenzi na mtoto na alifunguliwa mashtaka 10, kosa moja kwa kila mwezi mmoja wa uhusiano wake na mtoto wake.
Kesi yake imeahirishwa hadi mwezi ujao huku Angela akirudishwa rumande wakati uchunguzi ukiendelea.
Angela huenda akatupwa jela maisha ili kunusuru maisha yake kutokana na hasira za wananchi.
Madirisha ya vioo vya nyumba yake yalivunjwa kwa mawe tangia siku alipotiwa mbaroni.
source nifahamishe
Vibonge Kuanza Kulipishwa Nauli za Watu Wawili Kwenye Ndege
Mashirika ya ndege ya KLM na Air France yataanza kuwalipisha nauli za watu wawili, watu wanene ambao wanashindwa kujibana kwenye siti moja.
Watu wanene ambao hawaenei kwenye siti moja ya kwenye ndege watalazimika kulipa nauli za watu wawili iwapo watasafiri kwenye ndege za KLM na Air France.
Msemaji wa mashirika hayo, Monique Matze, alisema kuwa watu wanene sana ambao hawatoshi kwenye siti moja watalazimika kulipia asilimia 75 ya nauli ya siti ya pili.
Matze alisema kuwa uamuzi huo unatokana na sababu za kiusalama.
"Inatubidi tuhakikishe kuwa mtu anaweza kujisogeza vizuri na abiria wote wanafunga mkanda ipasavyo kwenye ndege", alisema Matze.
Watu ambao hawaenei kwenye siti moja watalazimika kufunga mkanda kwa kuunganisha mikanda ya siti mbili.
Watu wanene wasiotosha kwenye siti moja watahakikishiwa kutengewa siti mbili watakazotakiwa kuzilipia wakati wa kununua tiketi.
Sheria hiyo mpya itaanza kutumika kuanzia februari moja mwaka huu.
Kiti cha ndege kawaida huwa na unene wa sentimeta 43 na kwa ndege za masafa marefu huwa na unene wa sentimeta 44.
source nifahamishe
Bei ya samaki wa Magufuli sasa ni mguu wako
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ameitaka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kuhakikisha kuwa hadi kesho ugawaji wa samaki waliovuliwa kwa njia haramu katika fukwe za bahari eneo la Tanzania uwe umekamilika
Pinda alisema ikiwezekana samaki hao wagawiwe kwa mtu yeyote atakayehitaji ili kumaliza zoezi la ugawaji na kupisha shughuli nyingine za kimaendeleo
Pinda alitoa agizo hilo jana alipotembelea kiwanda cha kuhifadhia samaki hao cha Bahari Foods Ltd kilichopo Mwenge jijini Dar es salaam
Hata hivyo hadi jana tani kati ya za samaki waliohifadhiwa katika kiwanda hicho zilishapangwa kutolewe kwa taasisi mbalimbali
Katika msako uliofanywa kwa ushirikiano baina ya Tanzania na nchi zilizo ukanda huu wa Bahari ya Hindi mwaka jana jumla ya tani za samaki zilikutwa kwenye meli ya Tawaliq ya Vietnam iliyokutwa ikifanya uvuvi haramu
Pinda alisema samaki hao wamehifadhiwa katika eneo hilo kwa muda mrefu, hivyo kuwataka watendaji wanaohusika kuwagawa hata kurudia mara ya tatu kwa taasisi zilizokwisha chukua na ikiwezekana apewe yeyote
"Natoa siku mbili leo jana na kesho leo wote waliokuwa wameomba samaki hao wajitokeze kuchukua na wakisuasua kujitokeza hadi Jumatatu ikifika apewe yeyote ili waishe na tuachane na kazi hiyo" alisema Waziri Pinda.
Katika ugawaji huo pia wapo samaki aina ya vibua ambao walikuwa wakitumika kama chambo ya kuvua samaki aina ya Tuna na mchele ambavyo vyote vimedaiwa kugawiwa kwa taasisi zinazolea watoto yatima Waziri Mkuu alisisitiza kuwa endapo sekta za mifugo uvuvi na kilimo zitapuuzwa wimbo wa umaskini nchini hautaisha.
"Tukipuuza sekta hizo tutaendelea kuimba umaskini hadi mwisho kwani maeneo mengi tunang¡¦ang¡¦ania mipango ni mibovu hakuna mawazo ya maendeleo kila mahali kumejaa urasimu hali ambayo haitatutoa sehemu moja kwenda kwingine
Hivyo inabidi tujipange ili kujikwamua kupitia sekta hizo"¡¦ alisema Pinda.
Katika hatua nyingine Waziri Pinda alisema serikali italipa deni la zaidi ya Sh milioni inazodaiwa na kiwanda hicho kutokana na kuhifadhi samaki hao baada Mkurugenzi wa Kiwanda hicho Harko Bhagat kulalamikia kutokulipwa fedha licha ya Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kulipa zaidi ya bilioni kama fedha za awali.
Awali Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Bhagat aliilalamikia serikali kuwa inachelewesha kulipa kiasi hicho cha fedha.
Alisema kitendo hicho kinakwamisha biashara zao za uhifadhi wa samaki kutoka katika maeneo mengine wakiwemo wa kutoka ziwa Victoria.
"Inatupa wakati mgumu kibiashara lakini kwa kuwa ni serikali tumelazimika kutofuatilia hata mkataba wetu ambao ulitutaka kutokuruhusu kugawa samaki hao hadi kulipwa kwanza kwa gharama za uhifadhi ndipo tutoe, lakini tumetoa kwa kujali nchi na uzalendo hivyo ni vyema taratibu zikifanywa ili kiasi kilichobaki kikalipwa"alisema Bhagat.
Akizungumza katika ziara hiyo Waziri wa Mifugo na UvuviÆ’z Dk John Magufuli alisema fedha za kulipa uhifadhi huo ni suala mtambuka ambalo limehusisha wizara na taasisi mbalimbali likiwemo jeshi la polisi.
Nyingine kuwa ni Wizara ya Ardhi mahakama hadi ugawaji hivyo, fedha hizo wasiachiwe wizara yake pekee kuzilipa badala yake,zilipwe na wizara ya fedha kwa kuwa ndiyo yenye dhamana ya fedha nchini.
"Suala hilo sikupenda kulizungumzia muda mrefu kwa kuwa mtambuka ambalo hata hivyo nimeshawasiliana na wizara husika ili ziweze kutekeleza malipo, lakini wizara ya fedha ndiyo inayotakiwa kulishughulikia suala la ulipaji wa fedha hizo na hata bilioni tulizotoa kwa ajili ya gharama za awali tunapaswa kurudishiwa kwa kuwa suala hili ni la serikali na si Wizara yangu peke yake" alisema Dk Magufuli akimweleza waziri mkuu/
Magufuli alisisitiza kuwa baada ya kumaliza kuwagawa samaki haoÆ’z oparesheni nyingine itafanyika ili kukamata meli nyingine zinazoendelea na uharamia huo.
source mwananchi
CCM Zanzibar sasa washiriki maandamano ya CUF
CHAMA cha Wananchi(CUF) jana kilifanya maandamano makubwa yaliyowashirikisha wanachama wa CCM mjini Zanzibar, kuunga mkono maridhiano yaliyofikiwa kati ya Rais wa Serikali ya Mapindizi (SMZ), Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad Novemba 5, mwaka jana.
Maandamano hayo yalianza saa 2:00 asubuhi katika Viwanja vya Maisara na kuishia Uwanja wa Demokrasia Kibanda Maiti Mkoa wa Mjini Magharibi, yalipambwa na rangi za bendera za vyama vya CCM na CUF pamoja na picha za Maalim Seif na Rais Karume.
Katika maandamano hayo baadhi ya wanachama wa vyama hivyo walibeba mabango yenye ujumbe mbalimbali mengine yakisomeka "Ahsante Rais Karume, ahsante Maalim Seif, tumesamehe na tutasahau, kwa maslahi ya wazanzibari tupo tayari kwa lolote, asiyeitakia mema Zanzibar ni hasidi wa Wazanzibari."
Mengine yalikuwa na ujumbe uliosema: "Kujiamulia sio kuamuliwa, maslahi ya Zanzibar ni makubwa kuliko chama, Zanzibar ni moja ya Waunguja na Wapemba, Zanzibar ipo juu ya CCM na CUF, kuungana sio kutengana, hatima ya Wazanzibari itaamuliwa na Wazanzibari wenyewe zama za giza zimekwisha tukishirikiana, pasipo na mapenzi hakuna maendeleo na viongozi tusipoteze nafasi ya kuwaunganisha Wazanzibari."
Vile vile, ngoma ya mpwaka choka (beni) ya wana CCM kutoka Miembeni na Jang'ombe Mitaa yenye wanachama wengi wa CCM ilichangamsha maandamano hayo. Hii ni mara ya kwanza kwa wana CCM kushiriki maandamano ya CUF tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi nchini.
Kabla ya maridhiano hayo, wafuasi wa vyama hivyo walikuwa wakiishi kwa uhasama na mara nyingi zilitokea vurugu baina yao zilizoambatana na umwagaji damu.
Mbali ya ngoma hiyo, zumari likiongozwa na Kikundi cha Mji Mkongwe ambako ndio ngome kubwa ya CUF, walipita huku wakionesha manjonjo yao kwa Maalim Seif na wimbo wao maarufu wa 'Yaa Habibi Seif'.
Wimbo maalumu wa taarabu uliotungwa hivi karibuni kwa ajili ya maridhiano ulioimbwa na Mzanzibari Abdallah Issa (Super Star) nao uliibua shangwe kubwa kutoka kwa maelfu ya watu waliohudhuria maadamano hayo.
Kufanyika kwa maandamano hayo kumetokana na kongamano lililofanywa juzi la CUF ili kujadili mustakabali wa hali ya kisiasa na kujenga Zanzibar mpya yenye maridhiano.
Nguvu ya mshikamano visiwani humo tangu kufikiwa kwa maridhiano ya viongozi hao wawili, ilionekana pia Ijumaa wiki hii katika sala ya pamoja ambapo mamia ya Wazanzibar walijitokeza kutoka vyama vyote.
Akisoma risala ya mikoa mitatu ya Unguja, katika maandamano hayo, Mohammed Kombo alisema maridhiano yaliyofikiwa yanaweza kutoa suluhisho la viongozi kuliko uchaguzi ambao wanaamini umechafuliwa.
"Aliyeanzisha maridhiano ndio aendelee nayo, asipewe mtu mwingine kwani anaweza kuacha njiani au kuyaharibu kwa makusudi kwa lengo la kuwaacha Wazanzibari katika giza kama miaka ya nyuma," alisema Kombo.
Akizungumza katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif alisema yeye na Rais Karume hawatarudi nyuma katika kuwaangusha Wazanzibari kwa kuwa wana nia safi juu ya suala hilo na kwamba, Wazanzibari wamejenga matumaini makubwa kwao.
"Mimi ni CUF kindakindaki na mheshimiwa Karume ni CCM kindakindaki; lakini tumeamua kufanya maridhiano kwa maslahi ya Wazanzibari na haturudi nyuma," alisema Maalim Seif. Alisema kutokana na maridhiano hayo kumekuwepo na mbinu za watu fulani aliowaita wasioitakia mema Zanzibar ambao wanataka kutumia nafasi ya kuwagawa Wazanzibari kwa vyama vyao vya siasa, jambo ambalo alisema halitawezakana na kuwataka wananchi hao wakatae kugawanywa kwa kuwa wametoka mbali katika misukosuko ya kisiasa.
Alisema kwa kuwa Rais Karume ndiye muasisi wa maridhiano anapaswa kuendelea nayo kwa hali yoyote na asijaribu kumuachia mtu mwengine ambaye anaweza kuyaharibu njiani kwa maslahi yake na kuongeza kwamba, Rais Karume akubali maombi ya Wazanzibari.
"Rais Karume ndiye uliyeanzisha maridhiano haya, tena unataka tumpe mtoto nani? Tumpe mwanga? Atamuua…sisi wenyewe tunapaswa kumlea mtoto huyu, hatuwezi kuwapa hawa watu wenye kutia tia maneno; eti wanataka urais.
Hapana ni sawa na wanga watamuua…rekebisha katiba tupate kumlea mtoto wetu," alisema Maalim.
Seif alisema kutokana na maridhiano hayo Watanzania wote kwa ujumla wangefurahi na kuunga mkono kama alivyoonyesha Rais Kikwete.
Alisema ameshangazwa na watu wenye kutilia shaka na kuanza kuleta chokochoko za kutaka kuwagawa Wazanzibari.
"Namshukuru Rais Kikwete, amefahamu na ametuunga mkono na ameahidi kuwa atatumia njia zote kutusaidia katika kuyaunga mkono maridhiano haya.
Mimi nawashangaa hawa wengine ambao wameanza maneno, mimi nilidhani watu wenye akili wote watayaunga mkono; lakini bahati mbaya wanatumia vyama kutaka kutugawa tena, tusikubali kurudi huko tulipotoka jamani," alisisitiza Maalim Seif.
Baadhi ya wanasiasa wakiwamo wasomi kutoka Tanzania bara wameibuka kupinga mapendekezo ya Rais Karume kuongezewa muda yaliyotolewa wiki hii na Maalim Seif.
Juzi Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba alionyesha wasiwasi kuhusu mshikamano unaozidi kukua kati ya Maalim Seif na Rais Karume na akayaponda mapendekezo kumwongezea muda rais wa Zanzibar.
Pia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati alipinga mapendekezo hayo na kusema rais anayekuja ataendeleza maridhiano yao.
Maalim Seif aliwaomba wananchi kuunga mkono kusogezwa mbele uchaguzi wa Zanzibar ili kuweka mazingira mazuri ya kuingia katika uchaguzi katika hali ya amani na maridhiano hasa kwa kuzingatia chaguzi zote zinazofanyika huwa zinakumbwa na malalamiko na misuguano isiyo ya lazima ambayo matokeo yake husababisha chuki, uhasama na mauaji.
"Uchaguzi ni sumu ya umoja wa Wazanzibari, uchaguzi ni farka ya kutufarakanisha na yeyote anayetaka uchaguzi sasa hatutakii mema anataka kutuua tunakwenda katika uchaguzi tunapigana, tunauana hiyo ni kwa faida ya nani? Hapana tunataka tukifanya uchaguzi uwe safi" alisema Maalim.
source mwananchi
Mbwa huyo aliyekuwa akiitwa Otto, na aliyekuwa na umri wa miaka 20 alikufa siku ya ijumaa, mwili wake utachomwa na majivu yake kuzikwa.
Mmiliki wa mbwa huyo, mwanamke Lynn Jones, 54, kutoka Shrewsbury, Shropshire, Uingereza, alisema: "Nililia siku nzima tangu asubuhi. Kwangu hili ni balaa kubwa.
"Alikufa saa nne na dakika kumi asubuhi siku ya ijumaa. Hapa nilipo naona kama nimepoteza mkono wangu wa kulia. Kwangu alikuwa kama mtoto wangu wa kiume.
“Ninafurahi tu kwamba hateseki tena na maumivu, lakini nilitaka kuwa naye milele.”
Bi Jones na mumewe Peter, 68, walimpeleka Otto kwenye kituo cha tiba za wanyama ili akauawe baada ya hali yake kuwa mbaya zaidi.
"Tuligundua alikuwa na uvimbe mkubwa tumboni. Hakuweza kukaa au kulala kwa raha. Hivyo tulimpeleka kwa madaktari wa wanyama akauawe ili kuyamaliza mateso yake,” alisema Jones.
Otto, ambaye angekuwa na umri wa miaka 21 tarehe 14 Februari mwaka huu, ndiye mbwa mzee zaidi aliyetajwa katika kitabu cha Guinness Book of Records mwezi Oktoba mwaka jana.
source.globulpublisher
MZEE WA MIAKA 100 AELEZEA SIRI YA MAZOEZI YAKE
Mtu huyo, Georgina Easter, amesema siri kubwa ni kula chakula chenye lishe kamili.
"Siri yenyewe ni kuachana na vyakula ambavyo havijengi chochote mwilini,” alisema mwanamke huyo kutoka Chaddesden, Derby, Uingereza.
"Isitoshe huwa ninafanya kazi kwenye bustani yangu, napika chakula changu kila siku. Pia napenda kula maini yaliyokaangwa na vitunguu.”
Mwanamke huyo alizaliwa wakati Mfalme Edward wa Saba wa Uingereza alikuwa anashikilia taji na wakati ambapo ujenzi wa meli maarufu ya Titanic ulikuwa umefikia nusu.
Easter amewazidi kwa wastani wa miaka 30 wenzake ambao anafanya nao mazoezi ya kujiweka katika afya njema.
Freda Notley, 64, mmoja wa watu wanaofanya mazoezi na Georgina, anasema ni vigumu kuamini uwezo ambao bado anao katika mazoezi bibi huyo.
Mfanya mazoezi mwingine, Jean Bell, 71, anamsifia Georgina kwa ukakamavu wake ikiwa ni pamoja na kufanya shughuli zingine nyumbani kwake.
source.globalpublisher
Rais Abdoulaye Wade alisema watu wa Haiti ni wana wa Afrika kwani Haiti ilianzishwa na watumwa waliochukuliwa kutoka Afrika na baadhi wakiaminika kutoka Senegal.
“Rais anatoa fursa hiyo kwa watu wa Haiti watakaokubali kwa hiari yao kurejea katika shina lao,” alisema msemaji wa rais, Mamadou Bemba Ndiaye.
Jumanne iliyopita makumi ya maelfu ya watu waliuawa na wengine kukosa makazi baada ya nchi hiyo kukumbwa na tetemeko la ardhi.
Majengo yameteketea na utoaji wa misaada unakwenda taratibu mno huku watu wakiondoka katika mji mkuu wa nchi hiyo, Port-au-Prince, ambao umeharibiwa vibaya.
“Senegal iko tayari kuwapatia ardhi na hata maeneo makubwa zaidi. Hii itategemea ni watu wangapi wa Haiti watakaoamua kuja,” alisema Ndiaye.
source.globalpublish
Tolu wa Dunia Alipokutana na Mtu Mfupi wa Dunia
Mtu mrefu kuliko wote duniani na mtu mfupi kuliko wote duniani kwa mara ya kwanza walifanikiwa kukutana mbele ya waandishi wa habari nchini Uturuki.
Wanaume hao wawili wanaoshikilia rekodi za dunia za kitabu cha Guinness, walikutana kwa mara ya kwanza katika ufunguzi wa mashindano ya wazi ya kuvunja rekodi za dunia yaliyofunguliwa nchini Uturuki.
Mturuki Sultan Kosen mwenye umri wa miaka 27 ambaye kwa urefu wake wa mita 2.46 ndiye mtu mrefu kuliko wote duniani alikutana na Mchina He Pingping mwenye umri wa miaka 21 ambaye yeye urefu wake ni sentimeta 74 tu.
"Nilikuwa nikisubiria kwa hamu kukutana na Pingping tangia nilipotambulishwa rasmi kama mtu mrefu kuliko wote duniani, nimefurahi amkuja Uturuki kwenye ufunguzi wa mashindano haya ya Guinness World Records Live,", alisema Kosen.
"Nasubiria kwa hamu kumtembeza auone mji wetu mzuri wa Istanbul".
Mashindano ya The Guinness World Records live yanafanyika katika shopping Mall kubwa kuliko yote barani ulaya la "Forum Istanbul" ambapo wakazi wa Istanbul wanapewa nafasi ya kujitokeza na kujaribu kuandika majina yao kwenye rekodi za dunia.
Baada ya wiki sita katika jiji la Istanbul, mashindano hayo yatahamishiwa katika miji mingine saba ya Uturuki.
Pingping toka China ufupi wake unatokana na ugonjwa unaojulikana kama "Primordial Dwarfism" ambapo kwa mujibu wa baba yake alipozaliwa alikuwa na umbile dogo sana kiasi cha kujaa kwenye viganja vya baba yake.
Kosen kwa upande wake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa pituitary gigantism ambapo alikuwa na uvimbe uliomsababishia aendelee kukua muda wote, Baada ya operesheni kadhaa za kuuondoa uvimbe huo, Kosen aliacha kukua mwaka 2008.
Mbali ya rekodi ya kuwa mtu mrefu kuliko wote duniani, Kosen pia anashikilia rekodi ya dunia ya kuwa na mikono na miguu mikubwa kuliko watu wote duniani.
Chini ni VIDEO na Picha za tukio la kukutana kwa Tolu wa dunia na mtu mfupi kuliko wote duniani.
source nifahamishe
Hali ilivyo Nchini Haiti ni Mfano wa Jahanamu
Hali iliyopo nchini Haiti baada ya tetemeko kubwa la ardhi inatisha sana hakuna tena utawala wa sheria mwenye nguvu anamuonea mnyonge ili apate chochote cha kukaganga njaa, maiti zimezagaa kila kona kiasi cha kwamba zinatumiwa kama vizuizi vya barabarani.
Jinsi siku zinavyozidi kwenda mbele mamia ya watu wanazidi kufariki kutokana na njaa na maradhi mbali mbali huku maelfu ya watu wakiwa wamezikwa hai chini ya vifusi vya majengo yaliyoporomoka kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililotokea nchini Haiti.
Tetemeko hilo la ardhi lenye ukubwa wa 7.0 limeuharibu kwa asilimia 90 mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince.
Majengo mengi sana likiwemo jengo la ikulu na jengo la Umoja wa mataifa nchini Haiti yameporomoka na kuwafukia maelfu ya watu.
Hadi sasa jumla ya watu 50,000 wameishatibitishwa kufariki na idadi kamili ya watu waliofariki inakisiwa kuwa zaidi ya watu 200,000.
Maiti zimezagaa kila kona kiasi cha kwamba watu ambao walishindwa kupata msaada ulioletwa na mataifa ya nje waliamua kuzikusanya maiti na kuzijaza barabarani kuonyesha hasira zao.
Wezi nao wameongezeka kila kona, mwizi mmoja ambaye alikamatwa akimuibia mmoja wa wahanga wa tetemeko hilo la ardhi aliuliwa na kisha maiti yake kuburuzwa barabarani kabla ya kuchomwa moto.
Kwa hali iliyopo sasa nchini Haiti, kila mtu anajiangalia mwenyewe. Watu wenye nguvu wamekuwa wakitumia silaha zao kama vile visu na silaha nyinginezo kuwatishia watu wengine ili waweze kuwanyang'anya mali zao.
Misaada toka mataifa mbali mbali duniani imesaidia kuokoa maisha ya baadhi ya watu lakini bado haitoshi na haijawafikia watu wengi kutokana na kuharibika kwa njia zote za mawasiliano.
Hospitali zote zimefurika wagonjwa na maiti zimezagaa pia kila kona kiasi cha kwamba zimekuwa zikikusanywa na kulundikwa pamoja maiti za wanyama vile.
source nifahamishe
Mtoto wa Miaka 11 Aruhusiwa Kuendesha Gari, Aitekeza Familia Yake
Mtoto mwenye umri wa miaka 11 wa nchini Marekani ambaye aliruhusiwa kuendesha gari na wazazi wake, alisababisha ajali iliyosababisha kifo chake, mama yake na dada yake.
Polisi nchini Marekani wanafanya uchunguzi kujua ni kwanini mtoto wa kiume Jose Manuel Silva Covarrubias mwenye umri wa miaka 11 aliruhisiwa kuendesha gari lililopata ajali baada ya dereva hiyo mtoto kushindwa kusimama kwenye mataa.
Gari lililokuwa likiendeswa na mtoto Jose likiwa limembeba mama yake, dada yake na mwanaume mwingine mwenye umri wa miaka 34 liligongwa na gari jingine aina ya Ford baada ya kukatiza kwenye mataa huku taa nyekundu zikiwa zimewaka.
Polisi wanachunguza ilikuwaje Jose aliruhusiwa kuendesha gari aina ya Honda na kupelekea kutokea kwa ajali hiyo katika kitongoji cha Porterville, California.
Polisi wanatarajia kumhoji mtu pekee aliyenusurika katika ajali hiyo rafiki wa familia hiyo, Froylon Gonzalez mwenye umri wa miaka 34 aliyekuwa amekaa siti ya pembeni ya dereva huyo mtoto.
Gonzalez alinusurika kwakuwa alikuwa amevaa mkanda wakati mama wa mtoto huyo Maria Covarrubias, 30 na dada wa mtoto huyo Elizabeth Silva Covarrubias,6, walifariki baada ya kurushwa toka siti za nyuma kwakuwa hawakuwa wamevaa mkanda.
Kaka wa majeruhi aliyenusurika maisha yake alisema kuwa familia hiyo ilikuwa ikitoka kwenye mazoezi ya soka ya Jose na pia alisema kuwa hakuwahi kumuona Jose akiendesha gari kabla ya siku ya ajali hiyo.
source.nifahamishe
Mchezaji Mweusi wa Marekani Abadili Rangi ya Ngozi Yake
Mmarekani mweusi Sammy Sosa ambaye aliwika sana enzi zake kwenye mchezo wa Baseball amebadili rangi ya ngozi yake kutoka nyeusi kuwa nyeupe kama mzungu.
Mchezaji maarufu wa zamani wa Baseball, Sammy Sosa mwenye umri wa miaka 41 amejibadilisha rangi ya ngozi yake kuwa mweupe kama mzungu kwa kutumia krimu za kujichubua.
Sosa alianza kujichubua kuanzia mwaka 2007 na wiki iliyopita alionekana kwenye tuzo za Latin Grammy jijini Las Vegas akiwa hana tena rangi yake nyeusi ya kuonyesha asili yake ya Afrika.
Sosa alionekana mweupe kama mzungu na kwa watu ambao hawamfahamu ni vigumu kuamini alikuwa mweusi 'tii' zamani.
Sosa amesema kuwa nia yake kubadili rangi ya ngozi yake ni kutokana na mapenzi yake mwenyewe na si kumuiga marehemu mfalme wa muziki wa Pop, Michael Jackson.
Sosa amekiri pia kubadilika kwa rangi hakutokani na maradhi yoyote ya ngozi bali ni kutokana na krimu anayoitumia ambayo alisema ataipigia kampeni za kibiashara.
Hivi karibuni idadi ya watu weusi wanaojichubua nchini Marekani ili wakubalike katika soko la wazungu imezidi kuongezeka na wataalamu wa ngozi wanaonya kuwa matumizi ya krimu kujichubua ni hatari kwa afya.
Magonjwa mengi ya ngozi kama vile kansa ya ngozi yamekuwa yakihusishwa na madawa na krimu za kujichubua.
source.nifahamishe
Aibu Yamkumba Mkaguzi wa Silaha wa Umoja wa Mataifa
Mkaguzi wa silaha wa zamani wa Umoja wa Mataifa aliyepewa madaraka wakati huo kuzikagua silaha za aliyekuwa rais wa Iraq, Saddam Hussein amekumbwa na fedheha kubwa ya ngono za watoto ambapo alijipigisha punyeto mbele ya msichana wa miaka 15 na huenda akatupwa jela miaka saba.
Mpelelezi Scott Ritter mwenye umri wa miaka 48 ambaye alikuwa mkaguzi wa silaha wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq kabla ya kujiuzulu mwaka 1998, anakabiliwa na mashtaka ya ngono za watoto baada ya kunaswa akimtongoza msichana mwenye umri wa miaka 15.
Ritter ambaye anaishi na mkewe, bila kufahamu kuwa alikuwa akichunguzwa kuhusiana na ngono za watoto, alikuwa akiwasiliana kwa njia ya internet na msichana aliyejitambulisha kwa jina la Emily mwenye umri wa miaka 15.
Ukweli ni kwamba Emily hakuwa msichana mwenye umri wa miaka 15 bali ni afisa wa polisi Ryan Venneman aliyekuwa akimchunguza Ritter kuhusiana na ngono za watoto kwenye internet.
Ritter alianza kumwagia sera zake Emily kuanzia mwezi februari mwaka jana akitaka kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi.
Katika kipindi cha miezi tisa bila kufahamu kuwa anachunguzwa, Ritter aliendea kumwaga sera zake na kuna wakati alidiriki hata kujipigisha punyeto live huku akijionyesha kwa kutumia webcam.
Jina la Ritter lilisikika sana wakati wa utawala wa rais George Bush alipotakiwa kukagua silaha za sumu nchini Iraq ambazo mpaka Saddam Hussein ananyongwa mwaka 2006 zilikuwa bado hazijapatikana.
Ritter alishawahi kuingia matatani kwa kosa kama hili la kujihusisha na ngono za watoto mwaka 2001 lakini kesi yake ilifutwa baada ya kukosekana ushahidi wa kutosha.
Safari hii maafisa wa polisi wamesema kuwa wana ushahidi wa meseji za simu na webcam kumtia hatiani Ritter.
Ritter amefunguliwa kesi mjini Pennsylvania na kesi yake itaanza kusikilizwa mwezi machi. Iwapo atapatikana na hatia anaweza kutupwa jela miaka saba.
source.nifahamishe