Mtoto Anusurika Kimiujiza, Watu 103 Wafariki

Wednesday, May 12, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Watu 103 wamefariki dunia baada ya ndege ya Libya kulipuka wakati ikitua kwenye uwanja wa ndege nchini Libya huku mtoto wa miaka minane akiwa ndiye mtu pekee aliyetoka hai kwenye ajali hiyo mbaya.
Ndege ya shirika la ndege la Libya Afriqiyah Airways, iliyokuwa imebeba abiria 104 toka nchini Afrika Kusini ililipuka wakati wa kutua kwenye uwanja wa ndege wa mjini Tripoli, Libya.

Abiria wote walifariki hapo hapo lakini mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka minane raia wa Uholanzi ndiye aliyenusurika maisha yake kimiujiza.

Abiria wengine 61 ambao nao walikuwa ni raia wa Uholanzi walifariki kwenye ajali hiyo

Waziri wa usafiri wa Libya, Mohamed Zidan, alisema kwamba uchunguzi unafanyika kujua chanzo cha ndege hiyo aina ya Airbus A330 kulipuka na kugawanyika vipande vipande wakati wa kutua.

"Kulikuwa na watu 104 ndani ya ndege, abiria 93 na wafanyakazi wa ndani ya ndege 11", alisema Zidan na kuongeza kuwa maiti za watu 96 zimeishatambulika.

"Kuna mtu mmoja tu aliyenusurika naye ni mtoto wa miaka minane raia wa Uholanzi ambaye anaendelea kupatiwa matibabu hospitali", alisema waziri huyo wa usafiri.

Wizara ya mambo ya nje ya Uholanzi imesema kuwa mtoto huyo amelazwa hospitalini mjini Tripoli akipatiwa matibabu baada ya mifupa yake kadhaa kuvunjika.

Tukio hili linakumbushia ajali ya ndege ya shirika la ndege la Yemen, Yemenia Airways mwaka jana ambapo mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 12, Bahia Bakari alinusurika maisha yake baada ya ndege kudondoka baharini kwenye visiwa vya Komoro na kuua watu wengine wote 152 waliokuwemo kwenye ndege hiyo.

source nifahamishe

Wanafunzi SUA wasakwa kwa mauaji

Wednesday, May 12, 2010 / Posted by ishak / comments (0)

JESHI la POLISI Mkoani Morogoro linawasaka wanafunzi sita wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mlinzi wa anayelinda chuoni hapo Jafari Thabiti [38] wa Kampuni ya Moku.Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Thobias Andengenye alisema wanafunzi hao walifanya shambulio hilo Mei 8, mwaka huu, majira ya saa 12:00 jioni chuoni hapo.

Alisema mlinzi huyo alishambuliwa na wanachuo hao na alipata majeraha sehemu ya kichwani na sehemu nyingine za mwili baada ya kumtuhumu kusababisha upotevu wa simu ya mkononi katika bweni la wanafunzi wa kike wa chuo hicho.


Kamanda aliendelea kusema kuwa, mlinzi huyo alifariki siku mbili baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.

Wanafunzi wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo ni sita na wanasakwa na jeshi hilo kwa uhalifu huo


source nifahamishe

MWANAUME mmoja aliyetambulika kwa jina la Msepele Salum, mkazi wa Kigamboni, amefariki dunia mara baada ya kuanguka kutoka ghorofa ya nne wakati akiwa

Wednesday, May 12, 2010 / Posted by ishak / comments (0)

JESHI la POLISI Mkoani Morogoro linawasaka wanafunzi sita wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mlinzi wa anayelinda chuoni hapo Jafari Thabiti [38] wa Kampuni ya Moku.Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Thobias Andengenye alisema wanafunzi hao walifanya shambulio hilo Mei 8, mwaka huu, majira ya saa 12:00 jioni chuoni hapo.

Alisema mlinzi huyo alishambuliwa na wanachuo hao na alipata majeraha sehemu ya kichwani na sehemu nyingine za mwili baada ya kumtuhumu kusababisha upotevu wa simu ya mkononi katika bweni la wanafunzi wa kike wa chuo hicho.


Kamanda aliendelea kusema kuwa, mlinzi huyo alifariki siku mbili baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.

Wanafunzi wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo ni sita na wanasakwa na jeshi hilo kwa uhalifu huo

source nifahamishe

Fundi Apoteza Maisha Baada ya Kuanguka Toka Ghorofa ya Nne

Wednesday, May 12, 2010 / Posted by ishak / comments (0)

MWANAUME mmoja aliyetambulika kwa jina la Msepele Salum, mkazi wa Kigamboni, amefariki dunia mara baada ya kuanguka kutoka ghorofa ya nne wakati akiwa katika shughuli za ujenzi maeneo ya katikati ya jiji.
Tukio hilo lilitokea jana majira ya mchana, katika makutano ya barabara ya Indiragand na Bridge wakati akiwa katika ujenzi wa ghorofa mali ya shirika la nyumba la Taifa.

Mashuhuda waliokuwa eneo la tukio ambao ni mafundi wenzake walidai kuwa, marehemu alikuwa akiendelea na ujenzi katika ghorofa ya nne ambapo yeye alikuwa ni fundi wa kujenga na wengine walikuwa ni mafundi rangi na mafundi wengine wa aina mbalimbali.

WAlisema kuwa wao wakiwa katika gorofa ya tatu walisikia kishindo kikubwa chini na walidharau na kuendelea na shughuli zao, ndipo mmoja wao alipoamua kushuka chini na kumkuta mwenzao huyo ameanguka chini na alikuwa tayari ameshakufa.

Ndipo walipotoa taarifa kituo cha polisi na maafisa wa polisi kuja kupima eneo hilo ili kuthibitisha kifo cha marehemu huyo, na wakati wakiwa katika upimaji huo marehemu aligundulika alifariki papohapo kwa kuwa alipoanguka kichwa chake kilipasuka.

Hata hivyo katika uchunguzi wa kina ulibainika kuwa mafundi hao walikuwa wakiendela na shughuli za ujenzi bila ya kuwa na vifaa maalum vya kuwakinga na maafa, na tayari ilishadaiwa kuwa toka ujenzi huo uanze tayari mafundi zaidi ya wawili walishaanguka mahali hapo.

Hata hivyo juhudi zakumsaka mkandarasi anayeendesha ujenzi mahali hapo hazikuzaa matunda na hakupatikana kwa kuwa hakujulikana.

source nifahamishe

Uingereza imepata waziri mkuu mpya David Cameron toka chama cha Conservative baada ya chama cha Labour kupigwa mwereka kwenye uchaguzi mkuu. Kiongozi

Wednesday, May 12, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Hizi ni picha za kusikitisha za mwanaume mwenye umri wa miaka 25 wa nchini Uingereza ambaye alipewa kipigo na kisha kumwagiwa tindikali baada ya kutuhumiwa anamchukua mke wa mtu.
Awais Akram alijeruhiwa vibaya baada ya kumwagiwa tindikali na hata baada ya matibabu makubwa mwili wake umebaki na majeraha yanayotisha kuanzia kichwani mpaka miguuni.

Sura ya Akram imeharibika vibaya sana wakati nywele zale zinamea kwenye sehemu ya mbele tu ya kichwa chake ambayo ilinusurika na tindikali.

Majeraha zaidi ya tindikali yapo pia sehemu mbalimbali za mwili wake kama vile kifuani, tumboni, mgongoni, miguuni na mikononi.

Yote haya yaliyomkumba Akram yalisababishwa na mwanamke mwenye umri wa miaka 24 aliyefahamiana naye kwenye FaceBook aliyejulikana kwa jina la Sadia Khatoon.

Kaka yake Sadia aliyeitwa Vakas aligundua uhusiano wao baada ya kuwaona pamoja mitaani na alipogundua wanawasiliana kwa kutumia mtandao wa FaceBook alithibitisha kuwa dada yake anaisaliti ndoa yake.

Mume wa Sadia, Shakeel Abassi na yeye alipogundua uhusiano wa Akram na mkewe kwenye FaceBook, alikula njama na kaka yake Sadia wamteketeze Akram kwa kuingilia ndoa za watu.

Sadia alilazimishwa na kaka yake aliyeshirikiana na mumewe amlaghai Akram afike kwenye eneo ambalo wao walipanga kufanya shambulizi lao.

Akram naye bila kujua hili wala lile alijitosa kwenye eneo la tukio akijua anaenda kukutana na Sadia.

Alipofika kwenye eneo la tukio, Akram alijikuta akipewa kipigo cha nguvu kabla ya kumwagiwa tindikali iliyomuunguza sehemu kubwa ya mwili wake.

Akram alinusurika maisha yake lakini hadi leo bado anaendelea kupatiwa matibabu.

Sadia na mumewe walifanikiwa kutoroka Uingereza na kukimbilia kwao Pakistan ambako inasemekana wanaendelea kujificha huko.

Kaka yake Sadia, Vakas alikamatwa na jana ndio ilikuwa hukumu yake kwenye mahakama ya Old Bailey jijini London.

Vakas alipatikana na hatia ya kufanya jaribio la kuua mtu na alihukumiwa kwenda jela miaka 30.


source nifahamishe

Uingereza Yapata Waziri Mkuu Mpya

Wednesday, May 12, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Uingereza imepata waziri mkuu mpya David Cameron toka chama cha Conservative baada ya chama cha Labour kupigwa mwereka kwenye uchaguzi mkuu.
Kiongozi wa chama cha Labour, Gordon Brown alitangaza kujiuzulu jana jioni na hivyo kumaliza zengwe la uchaguzi wa Uingereza uliofanyika alhamisi ambapo hakuna chama kilichoshinda uchaguzi huo.

Vyama vikuu vitatu vya Uingereza vilishindwa kupata kura za kutosha kuwawezesha kuingia madarakani hivyo kuwepo kwa ulazima wa serikali ya mseto au ufanyike uchaguzi mwingine kama wote wakishindwa kuafikiana.

Hatimaye chama cha Liberal Democrats kilichoshika nafasi ya tatu kwa wingi wa viti bungeni kilifanikiwa kuafikiana na chama cha Conservative kilichoshika nafasi ya kwanza na hivyo kuunda serikali ya mseto ambayo inaing'oa serikali ya Labour iliyokaa madarakani kwa miaka 13.

David Cameron, mwenye umri wa miaka 43, alienda kwanza kukutana na malkia wa Uingereza kwenye jumba lake la Buckingham Palace na kupewa rasmi pendekezo la kuunda serikali.

Katika serikali ya mseto iliyoundwa, Cameron amewapa chama cha Liberal nafasi tano za uwaziri wakati kiongozi wa chama cha Liberal Democrats, Nick Clegg ndiye atakayekuwa naibu waziri mkuu.

source nifahamishe

Wanawake Wengi Wanaojiuza Maeneo ya Manzese ni Wake za Watu

Wednesday, May 12, 2010 / Posted by ishak / comments (0)

IMEDAIWA kuwa wanawake wengi wanaofanya biashara ya kuuza miili yao katika maeneo ya Manzese jijini Dar es Salaam ni wake za watu na imegundulika kuwa wanaagizwa na waume zao wakafanye biashara hiyo ili wapate pesa za kujikimu.
Hayo yamegundulika katika utafiti wa kina uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Madawa Afrika [AMREF]

Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki na Meneja wa Mradi wa Haki za Wananchi wa taasisi hiyo, Michael Kimaryo, wakati wa semina iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa habari za Ukimwi (AJAAT) kwa kushirikiana na taasisi hiyo.

Kimaryo alisema walibaini hali hiyo wakati walipokuwa wakifanya ufuatiliaji kuhusu mradi huo uliolenga kuwaelimisha wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya afya ya ukimwi na mambo mengine katika maeneo ya Manzese, Tandale na Kiwalani, Vingunguti na kwingineko

Alisema wanawake hao wamejiingiza katika biashara hiyo ambayo waume zao majumbani wanatambua hali hiyo na huwaruhusu ili waweze kujipatia kipato cha siku cha kujikimu na familia zao.

Mradi huo wa AMREF ulianzishwa mwaka 2008 ukiwa na lengo la kuwakomboa wananchi katika nyanja mbalimbali, kuwaelimisha kuhusiana na ugonjwa wa ukimwi na jinsi ya kujikinga na walioathirika kujifunza njia za kuepuka kuwaambukiza wengine.

Mradi huo ulilenga zaidi maeneo ya Manzese na Tandale.


source nifahamishe

Uchungu wa Mwana Aujuaye ni....

Wednesday, May 12, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Siku zote husemekana kuwa akina mama kutokana na uchungu kwa watoto wao huwa tayari kuyatoa maisha yao kwaajili yao, lakini pia akina baba nao si wa kubeza kama baba huyu wa nchini Australia ambaye alitumia mwili wake kama ngao ya kumlinda mtoto wake na mzinga mkubwa wa gari.
Andrew Leach alikuwa amebeba mtoto wake wa miezi minne akitembea pamoja na familia yake pembeni ya barabara wakati gari lililokuwa likiendeshwa na bibi lilipopoteza muelekeo na kumgonga.

Ajali hiyo mbaya ilitokea magharibi mwa jiji la Sydney kwenye kitongoji cha Penrith.

Video za kamera ya ulinzi zililinasa tukio hilo ambapo Leach alitumia mwili wake kama ngao ya kumlinda mtoto wake na mzinga mkubwa wa gari uliotokea.

"Wakati wa ajali nilifikiria, kama gari lingenigonga mgongoni, lingenivunja mguu au kiungo chochote kile ningeweza kupona lakini kama lingemgonga mtoto wangu asingepona", alisema Leach.

Leach alimshikilia mtoto wake kifuani na aliendelea kumshikilia wakati wa gari lilipomgonga na kumburuza kwenye kiambaza cha ukuta wa duka huku miguu yake ikiwa imebanwa ukutani.

Mtoto wake alinusurika kwenye ajali hiyo na hakupata jeraha lolote lile.

Leach alivunjika miguu yake yote miwili wakati wazazi wake aliokuwa akitembea nao wakati wa ajali, walijeruhiwa vibaya sana lakini hivi sasa hali zao zinaendelea vizuri.

Ajali hiyo ilitokea mwaka 2008 lakini habari kuhusiana na ushujaa wa Leach kumuokoa mwanae zimetolewa wiki hii na televisheni ya 9 TV ya Australia.


source nifahamishe

Madaktari Wapagawishwa na Mtu Ambaye Hajala Miaka 70

Tuesday, May 11, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Madaktari wa jeshi la India wameshindwa kuamini macho yao baada ya babu Prahlad Jani ambaye anadai hajala chakula kwa miaka 70, alipomaliza siku 15 walizomweka chini ya ulinzi mkali bila kula wala kunywa chochote wala kwenda chooni.
Madaktari na wanasayansi duniani wamekiri kuwa hawajui ni kitu gani kinamwezesha babu Prahlad Jani mwenye umri wa miaka 82, aweze kuishi siku nyingi bila kula wala kunywa chochote na bila kwenda haja.

Babu Jani aliwekwa kwenye chumba chenye kamera za ulinzi kibao akifuatiliwa kila anapokwenda kwa masaa yote 24 kwa siku zote 15 ambazo wanasayansi waliona zinatosha kuthibitisha kama ni kweli madai ya babu Jani kuwa hajala chakula chochote kwa miaka 70 sasa.

Madaktari wamethibitisha kuwa kwa siku 15 ambazo wamekuwa wakimfanyia uchunguzi babu Jani hajala chakula chochote wala kunywa kinywaji cha aina yoyote kile.

Babu Jani ni mfuasi wa mungu wa kihindi Amba ambaye Jani anaamini ndiye aliyempa nguvu zote hizo alizo nazo za kuweza kuishi miaka mingi bila kula wala kunywa chochote.

Kitu ambacho madaktari wanashindwa kukielewa ni jinsi Jani alivyoweza kuishi siku zote hizo bila ya kwenda haja.

Afya ya Jani ilipofanyiwa uchunguzi imeonyesha kuwa babu Jani ni mtu mwenye afya njema kuliko hata baadhi ya watu wenye nusu ya umri wake.

Jani hana matatizo ya akili na ubongo wake umeonekana kuchapa kazi kama kijana wa miaka 25.

Akiongea baada ya kutoka hospitali, Jani alitamba mbele ya waandishi wa habari kwa kusema "Niko fiti na mwenye nguvu leo mpaka madaktari wamekubali, wamenifanyia kila aina ya vipimo wanavyovijua kwa siku zote 15 na wamethibitisha kuwa sihitaji chakula ili kuishi".

"Nina nguvu na mwenye afya kwakuwa mungu ndivyo alivyotaka niwe", alisema Jani.

Madaktari wa India wanaamini kuwa jibu la kitu gani kinachomwezesha Jani kuishi siku nyingi bila kula, litawawezesha wanasayansi kubuni njia za kuokoa watu kwenye majanga ya asili kama vile matetemeko ya ardhi.

source nifahamishe

Aiba Mguu wa Maiti toka Kaburini

Tuesday, May 11, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Kijana mmoja wa Kimarekani ametiwa mbaroni na polisi baada ya kuiba mguu wa maiti ya msichana wa kiyahudi toka kwenye makaburi ya wayahudi nchini Marekani.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 18 aliyetambulika kwa jina la Daniel Wayne Staley, alitiwa mbaroni ijumaa alfajiri akiwa ameubeba mguu wa binadamu aliouiba toka kwenye makaburi ya wayahudi mjini Dallas.

Polisi waliwasili kwenye eneo la tukio majira ya saa tisa na nusu usiku baada ya kupewa taarifa na mtu aliyeshuhudia tukio hilo.

Daniel alikamatwa akiwa amebeba mfuko wa rambo ambao ndani yake kulikuwa na mguu wa binadamu.

"Nilifukua kaburi na kuuchukua mguu wa maiti ya msichana ya kiyahudi kwakuwa nilikuwa nikitaka mguu", Daniel aliwaambia polisi.

Daniel amefunguliwa mashtaka ya wizi wa maiti ya binadamu na huenda akatupwa jela mwaka mmoja na kupigwa faini ya dola 4,000, limeripoti gazeti la The Dallas Morning News.

Daniel hakusema mguu huo alikuwa akiuhitaji kwa shuguli zipi.

source nifahamishe

Uchovu wa Mume Kitandani Wamponza

Monday, May 10, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanamke wa nchini Marekani ambaye hakuridhishwa na pafomansi ya mumewe kitandani anashikiliwa na polisi kwa kumjeruhi mumewe kwa mkasi.
Michelle Thomas, 26, alikamatwa jumanne wiki iliyopita baada ya polisi kuitwa kwenye nyumba yao kwenye majira ya saa saba usiku.

Tukio hilo lilitokea Texas, Marekani wakati Michelle alipokasirishwa na uwezo mdogo ulioonyeshwa na mumewe kitandani siku hiyo.

Mume wa Michelle aliwaambia polisi kuwa Michelle alipatwa na hasira baada ya gemu la malavidavi kuisha bila ya Michelle kuridhishwa kimapenzi.

Alisema kuwa Michelle alichukua mkasi na kuutumia kumkatakata kwenye sehemu mbalimbali za mwili wake.

Polisi walimkuta mume wa Michelle akiwa na majeraha makubwa kifuani, mkononi na miguuni.

Michelle amefunguliwa mashtaka ya kudhuru mwili kwa kutumia silaha hatari ingawa mumewe hakutaka kufungua kesi dhidi yake, liliripoti gazeti la Lufkin Daily News.

Michelle huenda akatupwa jela miaka 20 iwapo atapatikana na hatia.


sou
rce nifahamishe

Gaidi wa Nigeria Akifanya Mazoezi na Al-Qaeda

Sunday, May 09, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Video imetolewa ikimuonyesha mwanafunzi wa Nigeria anayetuhumiwa kujaribu kuilipua ndege ya Marekani siku ya krismasi, akifanya mazoezi na wenzake kwenye kambi ya Al-Qaeda nchini Yemen.
Video hiyo inamuonyesha Umar Farouk Abdulmutallab na wanaume wengine wakifanya mazoezi ya kulenga shabaha kwenye kambi ya kundi la Al-Qaeda nchini Yemen linalojulikana kama "Agap".

Umar anakabiliwa na mashtaka ya kujaribu kuiangusha ndege ya Marekani kwa kutumia mabomu aliyoyaficha kwenye chupi yake.

Jaribio lake lilifeli na Umar alibaki na majeraha ya kuungua na moto kwenye sehemu zake za siri.

Alikanusha madai ya kesi zote alizofunguliwa lakini shirika la ujasusi la Marekani limesema kuwa anaonyesha ushirikiano kwa maafisa wa upelelezi.

Umar mwenye umri wa miaka 23 aliwaambia wapelelezi wa Marekani kuwa alipewa mafunzo nchini Yemen. Alipewa vifaa vyenye uwezo wa kusababisha mlipuko mkubwa na kuambiwa nini anatakiwa afanye.

Umar aliwaonya Wamarekani kuwa mamia ya vijana kama yeye wapo wengi nchini Yemen wakipatiwa mafunzo na wako tayari kufanya mashambulizi wakati wowote.

Katika video iliyotolewa, Umar anaonekana akiwa ameshika bunduki na mwishoni mwa video anaonekana akitoa ujumbe katika lugha ya kiarabu.

Haijajulikana ni lini video hii ilitengenezwa na kama ni feki au la.


source nifahamishe

Nani Kasema Mapenzi Hayana Umri?

Sunday, May 09, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Mwanamke mwenye umri wa miaka 28 wa nchini Marekani anashikiliwa na polisi baada ya kutumia fimbo ya kutembelea ya mpenzi wake mwenye umri wa miaka 77 kumtandika nayo na kumjeruhi vibaya sana.
Kristina N. Pongracz mwanamke mwenye umri wa miaka 28 wa Bedford County, Virginia nchini Marekani anashikiliwa na polisi kwa kumjeruhi mpenzi wake babu mwenye umri wa miaka 77.

Babu William Herchenrider alikutwa nyumbani kwake kwenye dimbwi la damu akiwa amejeruhiwa vibaya sana huku mkongoja wake ukiwa pembeni.

Taarifa zilisema kuwa Kristina alitumia mkongoja wa babu William kumtandika nao na kumjeruhi vibaya sana kabla ya kuanza kunywa pombe na kupitiwa na usingizi pembeni yake.

Polisi walifika kwenye eneo la tukio baada ya kupewa taarifa za kelele toka kwenye nyumba ya babu William.

William aliwahishwa hospitali kupatiwa matibabu huku mpenzi wake akitupwa mahabusu kwenye jela ya Blue Ridge mjini Bedford.


source nifahamishe

Matiti Yenye Uzito wa Kilo 12 Yamlaza Kitandani

Sunday, May 09, 2010 / Posted by ishak / comments (0)


Wanawake wengi siku hizi hufanya operesheni kuongeza ukubwa wa matiti yao lakini hali ilikuwa tofauti kwa mama wa watoto wanne wa nchini Peru ambaye ugonjwa wa ajabu ulisababisha matiti yake yawe makubwa sana kiasi cha kufikia uzito wa kilo 12.
Julia Manihuari [29] mama wa watoto wanne wa nchini Peru alisumbuliwa na ugonjwa wa ajabu ambao uliyafanya matiti yake yawe makubwa sana na kufikia ukubwa wa saizi N.

Matiti yake yalikuwa na uzito wa kilo 12 hali iliyomfanya ashindwe kuendelea na shughuli zake za kila siku na kutumia muda mwingi kitandani.

Julia alianza kuona mabadiliko kwenye matiti yake baada ya kujifungua mtoto wake wa tatu miaka saba iliyopita. Matiti yake yalizidi kuwa makubwa siku hadi siku.

Alipojifungua mtoto wa nne, matiti yake yalizidi kuwa makubwa zaidi, titi la kushoto lilikuwa na uzito wa kilo tano wakati la kulia lilikuwa na uzito wa kilo saba.

Wakati alipokuwa akisimama matiti yake yalikuwa yakimzidia uzito na alipokuwa akilala uzito wa matiti yake kifuani ulimfanya apumue kwa tabu.

Kwa miaka kadhaa Julia aliendelea kuteseka na hali hiyo kwakuwa yeye na mumewe ni wakulima maskini na hawakuwa na uwezo wa kulipia gharama za matibabu.

Julia hatimaye alifanikiwa kupata tiba mwaka huu baada ya wafadhili kujitokeza baada ya habari kuhusiana na mateso yake zilipotolewa kwenye magazeti.

Madaktari nchini Peru walifanikiwa kuyafanyia operesheni matiti yake na kuyapunguza kufikia ukubwa wa saizi B.

Julia hivi anaishi maisha ya furaha baada ya kuondokewa na uzito wa matiti yake uliomtesa kwa miaka mingi sana.


source nifahamishe