Mwanafunzi mmoja wa kike wa nchini Uingereza ameharibika sura yake kabisa kiasi cha kufanana na UFO (viumbe vinavyosemekana vinaishi angani) baada ya kutumia dawa ya kuzibadilisha rangi nywele zake ziwe nyeusi.
Abigail Colbourne mwenye umri wa miaka 15, alitumia dawa za kupaka za kubadilisha rangi ya nywele kuwa nyeusi za kampuni ya Clairol ili kuzifanya nywele zake ziwe nyeusi lakini ghafla sura yake ilianza kuvimba na macho yake yalivimba kiasi cha kushindwa kuona.
Sura yake iliharibika kabisa kiasi cha kushindwa kutambulika.
Akiongea na gazeti la The Sun la Uingereza Abigail alisema "Macho yangu yalifunga kutokana na jinsi yalivyovimba na kichwa changu pia kilivimba... nilikuwa natisha sana".
Abigail ambaye ni mkazi wa London alisema kwamba alishindwa kufanya vipimo vya aleji kabla ya kujipaka dawa hizo kama ilivyoshauriwa kwenye paketi ya dawa hizo.
Aliwahishwa hospitali ambako alipatiwa matibabu na uvimbe huo kupungua kidogo. Bado anaendelea na matibabu ya kuirudisha sura yake katika hali yake ya awali.
Mama yake Abigail, Joanna Leech alisema kuwa tukio hilo la kusikitisha lililompata mwanae liwe fundisho kwa wengine wanaotumia dawa kama hizo.
by nifahamishe.com
Busta Rymes atawasha moto katika fiesta Dar
Thursday, November 19, 2009
/
Posted by
ishak
/
comments (0)
AKON APATA SHAVU KATIKA UFUNGUZI WA KUMBE LA DUNIA
Thursday, November 19, 2009
/
Posted by
ishak
/
comments (0)
kombe la mabingwa wa barclays league lilivyotinga dar
Monday, November 16, 2009
/
Posted by
ishak
/
comments (0)
Subscribe to:
Posts (Atom)